Vincent Nyerere ampa Mkapa vidonge stahiki

Vincent Nyerere ampa Mkapa vidonge stahiki

mbona alilitolea ufanunuzi mda mrefu,Mkapa atafute gazet la RAIA MWEMA limewai fanya mahojino nae akasema ajaziliwa na Julias nyerr
nazan mkapa na yeye ni mvivu wa Kujisomea!!!
Iwa mwema
Wakatabahu
Adharusi
 
Tumekuwa tukisoma hapa JF kuwa mzee aliuawa . Hakuna aliyetaja ni nani , na jinsi mambo yalivyo sasa ndani ya CCM huyu jamaa ndio mhusika na ndiye aliyeweka presidence kwa mauaji mengine yanayoendelea hivi sasa katika Tanzania Politique. Another title for CCM "" Serial Killer" Mkapa njoo ukanushe haya tena. d
 
Mbona CCM hawaeleweki kwa mambo wanayofanya! Kwenye vikao walivyofanya Dodoma hivi karibuni waliamua kuwa wazee wapumzike kufanya shughuli nzito za chama ikiwa ni pamoja na kuwaondoa kwenye CC. Inakuwaje wazee hao hao ambao walisema wapumzike wanawatwisha jukumu zito la kwenda kusimama majukwaani kuwaombea watu kura? Na inakuwaje mtu mzima kama Mkapa tena babu anasimama jukwaani kuanza kujadili ubini wa watu wengine, ama ndivyo alivyoagizwa na CCM. Tusishangae pale akina Ruksa, Tingatinga na Kingunge nao wakafurushwa huko walikojikalia kwenda kumwombea mjukuu/mtoto wao kura! Ila kama ni kutaka majibu Vicent amemjibu vizuri huyo babu wa watu.
 
Mbona CCM wamemwaga damu nyingi tu za wasio na hatia lakini bado wanapeta? au nikutajie uwakumbuke? DR. Juma, Kolimba, Sokoine,

hivi kweli jamani umenikumbusha. wakati Sokoine anakufa nilikuwa na miaka 6. ila kila nikisoma ajali yenyewe ilitokeaje mpaka leo sielewi! hebu naomba kwa faida ya wengi mtu anayejua ajali ya Sokoine ilikuwaje hebu atukumbushe basi ili na sisi hansad zetu vichwani zikae sawa tafadhali!
 
VITA ya maneno, vijembe na kejeli kati ya Chama cha Mapinduzi (CCM) na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), katika kampeni za uchaguzi mdogo wa ubunge katika Jimbo la Arumeru Mashariki, mkoani Arusha imeanza. Baada ya juzi Rais mstaafu, Benjamin Mkapa, kufanya uzinduzi wa kampeni za CCM na kuipiga vijembe CHADEMA, chama hicho jana kilijibu mapigo kupitia kwa Mbunge wa Msoma Mjini, Vincent Nyerere, ambaye ni Naibu Meneja wa Kampeni wa CHADEMA. Akizungumza katika mikutano ya kampeni maeneo mbalimbali, mbunge huyo alishusha tuhuma nzito juu ya kile alichokiita ‘utata’ wa kifo cha Mwalimu Nyerere huku akihusisha na maamuzi ya Mkapa kung’ang’ania Mwalimu aende kutibiwa Uingereza baada ya kuanza kumkosoa juu ya sera za ubinafsishaji. Nyerere ambaye ni mmoja wa wanafamilia wa hayati Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere, akiwa amekulia katika familia hiyo, aliwaambia wananchi wa maeneo hayo kuwa umefika wakati sasa Mkapa atoke hadharani afafanue alikuwa na nia gani kumlazimisha Mwalimu Nyerere akatibiwe Uingereza wakati mwenyewe alikuwa amekataa, akisema kuwa ugonjwa uliokuwa unamsumbua tayari ulikuwa unajulikana na daktari wake, Profesa David Mwakyusa, alikuwa tayari akimhudumia vizuri bila tatizo. “Jana katika hotuba yake ametumia muda mwingi sana kuisema CHADEMA na akanisema mimi kwa jina moja kwa moja, sasa ‘kanibipu’ na mimi nimeamua kumpigia, tunamtaka kama anaweza arudi hapa Arumeru, aje ajibu maswali ya msingi juu ya ufisadi unaomwandama. Alianza kwa kuuza mashirika ya umma, akauza viwanda, ukienda leo miji mikubwa kama Dar es Salaam na kwingineko, vijana wengi wamegeuka kuwa waokota makopo kwa sababu hakuna ajira, viwanda viliuawa wakati wa Mkapa. “Kwa kupitia sera yake ya ubinafsishaji akauza kila kitu, akauza viwanda, wawekezaji walionunua nao wakafanya ufisadi wamegeuza viwanda hivyo kuwa maghala ya kutunzia vitu vyao, viwanda ambavyo vingeweza kuajiri vijana Watanzania vikauzwa kiholela kwa bei ya kutupa, vingine wakajiuzia wao wenyewe. Misingi iliyowekwa na Mwalimu yote ikabomolewa badala ya wao kujenga nyumba juu ya misingi hiyo. “Mashirika yaliyokuwa yakifanya kazi vizuri au ambayo yalihitaji usimamizi tu mzuri ili yafanye vizuri yakauzwa kiholela, yakauzwa kifisadi, tena mkumbuke alianza kwa kuuza benki. Mwalimu kuona hivyo akashtuka, akaanza kumhoji na kumkosoa hadharani juu ya sera yake hiyo, jamaa (Mkapa) kuona hivyo akaona huu sasa ni usumbufu, akaanza kumshawishi Mwalimu aende akatibiwe Uingereza, Mwalimu alikataa kabisa akisema kuwa ugonjwa unaomsumbua tayari daktari wake anamhudumia vema,” alisema Nyerere na kuongeza: “Mwalimu alikuwa akihoji inakuwaje reli inakufa, yeye amekazana tu na ubinafsishaji, Mwalimu akahoji inakuwaje anatoza kodi kibao na kutunza pesa, kumbe Mkapa tayari alikuwa anaandaa pesa za EPA ambazo baadaye ndizo mlizisikia kupitia kashfa maarufu ya mabilioni ya EPA. Mkapa akamng’ang’ania Mwalimua akatibiwe Uingereza, akasema naye ni mmoja wa wanafamilia yetu, basi tukakubali, lakini mnajua kuwa Mwalimu alikwenda anatembea akarudi amenyamaza ndani ya jeneza? “Sasa Mkapa atuambie ukweli juu ya hili, aje ajibu maswali yote haya, nitakuja na vigongo vingine, lazima tupambane na ufisadi hadi mwisho. Ilifikia mahali hata taarifa za ugonjwa akawa anatoa yeye Mkapa, oooh mara Mwalimu amepatwa na mkanda wa jeshi, mara oooh leo imekuwa hivi, badala ya daktari wake. Baada ya Mwalimu kufariki dunia, wakamwambia yule daktari wake agombee ubunge watampatia uwaziri, ndivyo ilivyotokea,” alisema Nyerere. Aliongeza kusema kuwa pamoja na uhakika wa maisha yake baada ya kustaafu ambapo anagharimiwa kila kitu kwa kodi za Watanzania, bado Rais Mkapa alijimilikisha mgodi wa Kiwira ambao baada ya kelele nyingi za nguvu za umma, zikiongozwa na CHADEMA bungeni na nje ya Bunge, hatimaye umerudishwa kwa umma. Alimtaka Rais Mkapa kujibu tuhuma juu ya ufisadi katika ununuaji wa ndege, wakati tayari serikali ilikuwa na ndege nyingine mbili, moja ikinunuliwa wakati wa Mwalimu na ina uhakika wa kufanya kazi kwa miaka 100 iwapo ingefanyiwa matengenezo kadiri inavyotakiwa. Pia akamtaka kujibu hoja za Watanzania juu ya ufisadi wa rada, ambao hata Waingereza wanaupigia kelele, baada ya yeye na wenzake serikalini kufanya ‘dili’ kujinufaisha wao badala ya kuongoza wananchi. Nyerere aliongeza tuhuma kwa Mkapa akisema kuwa pia anatakiwa kujibu hoja juu ya mauaji ya Zanzibar ya mwaka 2001, ambapo kwa mara ya kwanza Tanzania mbali ya serikali kuua raia wake kwa risasi, ilizalisha wakimbizi kwenda nchi za Kenya na Somalia. Akifafanua tuhuma za ufisadi dhidi ya Rais Mkapa, mbunge huyo alisema kuwa kama Mkapa anataka kueleweka mbele ya Watanzania wenye uchungu na nchi yao, anatakiwa kujibu hoja za msingi juu ya tuhuma hizo za ufisadi zinazomwandama tangu akiwa madarakani hadi anastaafu. Mbunge huyo ambaye alikuwa akihutubia mamia ya wakazi wa maeneo ya Lenguruki, Poli, Sing’isia na Nkoaranga, alisema kuwa rais huyo mstaafu anapaswa kuwa mmoja wa watu wa mwisho kusimama mbele za watu kwani hali inayolikabili taifa kwa sasa, ikiwamo ufisadi uliotapakaa ndani ya chama chake na serikali ya CCM, iliasisiwa tangu wakati wa utawala wake, kwa kuanzia na sera za ubinafsishaji zilizoua misingi ya viwanda iliyowekwa na Mwalimu Nyerere. Kwa upande wake, mgombea wa CHADEMA Joshua Nassari, alisema kuwa amegombea kwa nia ya kubeba ‘mizigo’ ya wana wa Arumeru kwani anaitambua, hivyo yuko tayari kuibeba kwenda nayo bungeni Dodoma na katika Halmashauri ya Wilaya ya Meru, kuwasemea na kuiwajibisha serikali ili iwajibike kwa wananchi. Joshua alionekana kuwagusa wananchi wa maeneo hayo pale alipokuwa akizungumzia kero za kila eneo husika, kama vile ardhi, maji, afya na elimu na namna ambavyo wanaweza kushirikiana pamoja na mbunge wao katika kuyatatua, iwapo watamchagua yeye ambaye amezaliwa na kukulia katika maeneo hayo na yuko tayari kuwatumikia akiwa anaishi katika maeneo ambayo wanaishi wao pia. Aliwataka watu wa Meru wasidanganyike na maneno ya Mkapa kuwa atakwenda kumshauri Rais Jakaya Kikwete ashughulikie matatizo ya ardhi katika wilaya hiyo, kwani alishindwa kufanya hivyo wakati akiwa na mamlaka ya urais, hawezi kuifanya kazi hiyo kwa sasa kwani rais ana hiari ya kukubali au kukataa ushauri wa mtu yeyote kwa mujibu wa katiba yetu mbovu. “Kwa mujibu wa katiba yetu mbovu ambayo tunataka tuiandike upya, rais halazimiki kuchukua ushauri wa mtu yeyote, hivyo Kikwete anaweza kukataa ushauri wake huyo Mkapa, aje ajibu hoja hapa kwa nini alishindwa kutatua matatizo ya ardhi kwa watu wa Arumeru wakati akiwa madarakani?” alihoji Nyerere.CHANZO: Tanzaniadaima 14 Machi, 2012.
 
Angeweza tu kusema Mkapa hawezi kujua wanafamilia wote wa mwalimu kwani si mmoja wa wanafamilia. angelenga zaidi kuthibitisha kwa umma ukweli wa undugu wake na mwalimu nyerere kila mtu ana hamu ya kujua jambo hilo nikiwemo mimi.
 
Haijawahi kusemwa hata siku moja kua Vincent ni mtoto wa Julius,na inajulikana wazi watoto wa Julius walikua kina nani,kinachoeleweka ni kua Vincent ni mtoto wa Josephat ambae ni kaka wa Julius,sasa hapo hakuna undungu?huyu mzee Mkapa naona kachanganyikiwa sasa,hoja alizotoa ni za kitoto mno na hazikua na mantinki kwa wana Arumeru!pili Vincent kitu alichoeleza ni sahihi kabisa!huyu Mkapa ndie aliyeiingiza nchi hii kwenye matatizo yote haya!uwa nasema siku zote,aliua viwanda na mashirika ya umma akitegemea nchi iendelee vp?yeye ndio chanzo cha watu wachache kulijilimbikizia mali na yeye ndio muasisi wa mikataba mibovu ili kuitia nchi hasara na pia ndie muasisi wa ufisadi wote!huyu mzee si wakumsamehe hata kidogo!
 
Unaongea kishabiki bila kutafuta taarifa sahihi. Vicent amikiri huko sing'isi kwamba yeye siyo mtoto wa Julius Nyerere bali ni mtoto wa josephat nyeree ambae ni kaka wa julius. ulitaka akujibu hoja gani hasa uridhike?
Ninashauku ya kupata majibu yaliyojitosheleza kutoka kwa Vicent Nyerere kuhusu tuhuma kwamba yeye si mtoto wa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere. Vicent hajajibu hoja hiyo matokeo yake ameishia kumtuhumu Mkapa kwamba ndiye muasisi wa ufisadi na kwamba alimuua Mwalimu bila kueleza kwa kiina uhusiano wake na Mwalimu.
 
Mshaurini Vicent Nyerere aachane na hizo siasa. Hoja kuu ambayo alitakiwa kuisimamia ni kwamba Vicent Nyerere hajawahi ku-claim mahali popote pale kwamba yeye ni mtoto wa Marehemu Mwalimu Nyerere. Kwa hiyo, claim ya Mkapa ilikuwa baseless na haiwezi ku-hold maji na hizo ndio siasa za maji taka, watu wanaacha hoja halafu wanakijita kwenye kuzua vijambo na vijimambo.

Discussion za chanzo cha kifo cha Mwalimu Nyerere kwa sasa haziwezi kuwasaidia CHADEMA ili washinde huko Arumeru Mashariki. Mjadala huo kwa sasa hauna msaada wowote kwa wananchi wa Arumeru ambao wana matatizo ya Ardhi na Maji, pamoja kukosekana kwa ajira kwa vijana.

Focus ya Kampeni ya CHADEMA iwe ni kwenye kero za wananchi wa Arumeru. Ili kumgonga vilivyo Mkapa na Chama chake, matatizo ya maji na ardhi hayajaanza leo wala juzi, yapo kwa miaka mingi sasa. Je, Mkapa akiwa Rais ina maana hakuyajua hayo matatizo, kama aliyajua, kwanini hakuyashughulikia? Kikwete yuko madarakani mwaka wa 7 sasa, je hajapelekewa hayo matatizo au hajui hayo matatizo? Je, wananchi watakuwaje na imani kwamba Mkapa akienda kumwambia Kikwete matatizo ya maji na adhi atayatatua na ilihali amekuwa madarakani kwa miaka 7 na matatizo yako pale pale?

Iwapo Mzee Sumari (RIP) alishindwa kusaidia kutatua matatizo ya Arumeru Mashariki akiwa Naibu Waziri wa Fedha (sehemu ya serikali ya chama tawala), je leo hii mwanae ndio ataweza kuyatatua? CCM kimebaki kuwa ni chama cha kuweka ahadi hewa bila kutimiza. Hapo ndio CHADEMA inatakiwa kusimamia kwa kuwa ndo ukweli wenyewe na wananchi wanajionea. Wakumbusheni kwamba hata Igunga ambako CCM walishinda uchaguzi mdogo, zile ahadi zote za CCM zilizotolewa kwa wana Igunga ikiwemo ya kujengewa daraja hazijatimizwa hata moja!

Keil Nakushukuru sana!
Ni kweli kuwa wananchi wa Arumeru Mashariki wanahitaji kujua kero zao zitatatuliwa vipi na nani na kwa muda gani.
Ni ukweli usiopingika kuwa CCM wameshindwa kutatua matatizo ya wanajimbo hili kwa muda sasa. Zimebakia kuwa ahadi ambazo hazitekelezeki.
Nitatofautiana na wewe kidogo! Vicent kuamua kumjibu Mkapa ni sahihi kabisa! Kwa nini nasema hivi! Mkapa ametumia jukwaa hili la siasa hasa wakati huu wa kampeni kumtuhumu kuwa yeye sio mtoto wa Nyerere. Kimsingi hakuna pahali popote Vicent amesema yeye ni mtoto wa Julius! Kama alimaanisha hivyo! Vicent ni mtoto wa Josephat na ubin wao ni Nyerere kuna kosa hapo? Vicent akinyamaza bila kutoa ufafanuzi watu wanaweza kuchukulia vingine! Imebidi atumie jukwaa hili hilo kumjibu huyo huyo aliyatamka hayo! Wanasema UKIACHA UONGO UENDELEE KUSEMWA SANA HUGEUKA KUWA UKWELI! Sasa unapomua kuchafua wenzako hakikisha kuwa wewe nawe ni msafi! Kama unajua we sio msafi basi usipende kuchafua wenzako. Yanamkuta Mkapa kwa kuwa anapenda kuchafua wenzake! Kauli za Mkapa ni za kitoto maana mtu mzima kama yule hawezi kusimama na kusema watu wazima kama yeye tena wengine wamemzidi kwa kila kitu kuwa eti wapinzani ni wajinga sijui wapuuzi. Sikutarajia kauli toka kwa kiongozi kama huyo.
Ajifunze kuwa na staha kama Mzee Mwinyi ili aheshimiwe! angalia sasa anaanza kunyooshewa kidole kuhusu kifo cha Mwalimu! Mtu mwenye busara huchagua cha kuongea na sio kupayuka hovyo!
 
Vincent Nyerere ni mtoto wa nje wa mdogo wake Nyerere, Familia ya Nyerere hawamtambui kabisa mdogo wake Nyerere alizaa na mwanamke mmoja pale Makoko.

Hamna shida. Kwani mtoto wa nje sio mtoto? DNA hazitasema? awe wa nje au wa ndani ni mtoto. na Kwa sababu umri wa Vicent Nyerere hauitaji msaada wa kutunzwa (wala utetezi wa ustawi wa jamii) haitatushinda kwenda kucheki DNA lakini sio hapa Bongo!
 
Ninashauku ya kupata majibu yaliyojitosheleza kutoka kwa Vicent Nyerere kuhusu tuhuma kwamba yeye si mtoto wa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere. Vicent hajajibu hoja hiyo matokeo yake ameishia kumtuhumu Mkapa kwamba ndiye muasisi wa ufisadi na kwamba alimuua Mwalimu bila kueleza kwa kiina uhusiano wake na Mwalimu.

Umejuaje kuwa hajajibu? Na hiyo habari ya Kumtuhumu Mkapa kuhusika na kifo cha JKN umeipata wapi?
 
Huyu Vincent anaonekana amekosa malezi mazuri...Kuna vitu vya kuhoji, but hili la kifu cha nyerere lilikuwa lipo wazi kabisa!
Kwa hili ametokota!

Rejao, umenikumbusha lile onyo la Mtume Paulo kwa Waefeso 6:4, "NANYI AKINA BABA, MSIWACHOKOZE WATOTO WENU; BALI WALEENI KTK ADABU NA MAONYO YA BWANA."
Ktk hili Mkapa anastahili majibu ya Vincent Nyerere, Mkapa hakuwa na haki ya kuingilia Familia ya Nyerere, angewaomba kina Makongoro, Chief Wanzagi nk alitaka kumdhibiti Vincent.
 
naomba STIDE, de levis, na feedback niwape hecko hapa naona circumstantial evidance
 
Angeweza tu kusema Mkapa hawezi kujua wanafamilia wote wa mwalimu kwani si mmoja wa wanafamilia. angelenga zaidi kuthibitisha kwa umma ukweli wa undugu wake na mwalimu nyerere kila mtu ana hamu ya kujua jambo hilo nikiwemo mimi.

Mama P hilo mbona amelijibu? Amesema yeye ni mtoto wa Joseph Nyerere mdogo wake na Julius. I used to think Mkapa is smart lakini kumbe I was very wrong. Inawezekanaje mtu smart akaomba kura (of course wao wanomba kula) kwa kujadili koo za watu? Watu wa Arumeru hawana maji, matibabu ya kueleweka etc, hayo ya koo yanawasaidia nini? Shame on you Ben.
 
Back
Top Bottom