Vincent Nyerere ampa Mkapa vidonge stahiki

Vincent Nyerere ampa Mkapa vidonge stahiki

Mshaurini Vicent Nyerere aachane na hizo siasa. Hoja kuu ambayo alitakiwa kuisimamia ni kwamba Vicent Nyerere hajawahi ku-claim mahali popote pale kwamba yeye ni mtoto wa Marehemu Mwalimu Nyerere. Kwa hiyo, claim ya Mkapa ilikuwa baseless na haiwezi ku-hold maji na hizo ndio siasa za maji taka, watu wanaacha hoja halafu wanakijita kwenye kuzua vijambo na vijimambo.

Discussion za chanzo cha kifo cha Mwalimu Nyerere kwa sasa haziwezi kuwasaidia CHADEMA ili washinde huko Arumeru Mashariki. Mjadala huo kwa sasa hauna msaada wowote kwa wananchi wa Arumeru ambao wana matatizo ya Ardhi na Maji, pamoja kukosekana kwa ajira kwa vijana.

Focus ya Kampeni ya CHADEMA iwe ni kwenye kero za wananchi wa Arumeru. Ili kumgonga vilivyo Mkapa na Chama chake, matatizo ya maji na ardhi hayajaanza leo wala juzi, yapo kwa miaka mingi sasa. Je, Mkapa akiwa Rais ina maana hakuyajua hayo matatizo, kama aliyajua, kwanini hakuyashughulikia? Kikwete yuko madarakani mwaka wa 7 sasa, je hajapelekewa hayo matatizo au hajui hayo matatizo? Je, wananchi watakuwaje na imani kwamba Mkapa akienda kumwambia Kikwete matatizo ya maji na adhi atayatatua na ilihali amekuwa madarakani kwa miaka 7 na matatizo yako pale pale?

Iwapo Mzee Sumari (RIP) alishindwa kusaidia kutatua matatizo ya Arumeru Mashariki akiwa Naibu Waziri wa Fedha (sehemu ya serikali ya chama tawala), je leo hii mwanae ndio ataweza kuyatatua? CCM kimebaki kuwa ni chama cha kuweka ahadi hewa bila kutimiza. Hapo ndio CHADEMA inatakiwa kusimamia kwa kuwa ndo ukweli wenyewe na wananchi wanajionea. Wakumbusheni kwamba hata Igunga ambako CCM walishinda uchaguzi mdogo, zile ahadi zote za CCM zilizotolewa kwa wana Igunga ikiwemo ya kujengewa daraja hazijatimizwa hata moja!

Very well said. Maneno kama haya wafikishiwe wapiga kampeni wa CHADEMA.
 
na ex president anaacha mambo ya maana kwenye kampeni na kuanza kuzungumzia mtoto wa fulani wakati hata yeye mkewe alizaa na bwana mwingine ujue tumekwisha kisera!!
sijui ni kiongozi gani Tanzania ambaye hana mtoto wa nje! mahita ameonesha njia - jamani ninyi wote mliozalishwa na viongozi wetu hebu jitokezeni! sipati picha mtoto wa nje wa mkapa awe amefanana na baba yake sasa sijui atakuwa na umbo gani mtumeeee! halafu na yeye awe na kipara kama baba yake! uuuwi!
 
-Watanzania tutaendelea kubaki kuwa wajinga Period kwa kuependa na kushabikia siasa za maji taka.

-Nilijua CDM wameamua kuachana nazo kwa sasababu hazileti tija ila zinaendeleza siasa za kizamani ambazo hazilisaidii Taifa.


1.Kama vicent alijua wazi kuwa Mkapa na Serikali yake ndiyo waliomumaliza JKN,alikuwa wapi kusema zamani?huu ni unafiki mkubwa..Haiwezekani ikuchukue miaka kumi na mbili kuja kusema jamba ambalo umekaa nalo mika 12,totally rubbish na inaonyesha ni kwa jinsi gani kuna machafu hata ya CDM anayo sema anasubiri baadaye aje Kuyasema.


2.Hoja hii ni dhaifu na CCM watatumia Mtu wa karibu wa Mwalimu kwend ahuko kukanusha na kumkana Vicent(hili nalitegemea litatokea)


-Baadaye CDM itaonekana wamezusha hili na litawaharibia..Ugonjwa wowote hautakiwi kusubiri miaka mingi ili utoe dawa yake.


-Mkapa ni Mzoefu na alitumia maneno ya kuwatusi CDM kwa kuwa anawajua watabwatuka na kusahau focus ya kampeni zao....


-Kwa knowledge moja tu ya kipuuzi..Kifo cha Mwalimu kimewapunguzia nini watu wa Arumeru?ukiwaambia alimalizwa na Mkapa et all kinajibu mattatioz waliyo nayo?


Sijui...Ila hili la Mkapa ni kama uzushi tu
Mkuu hayo madai ni maji taka kwako? Hao wazee wakanushe kama mwisho hawajabaki mdomo wazi!! Hata akija madaraka mwenyewe! Kuepusha haya yasiwe makubwa subiri usikie kauli zao!
 
jamaaan jamaan...hapa lazma kuna ukwel ndani yake. Ngoja tusikie watu wakifunguka..
 
Na hii ni nzito kuliko angeambiwa yeye fisadi, hii hata akikana hilo doa kulisafisha mioyoni mwa watu itakuwa kazi. Tulikuwa tunasikia pembeni pembeni sasa imetolewa na mtoto wa familia yenyewe, tutajuaje huko kwenye familia wanavyomsema Mkapa.

Kama haya yalijulikana ilikuwaje baada ya maziko akawa mwanafamilia ya Mwl.?
 
Siasa ndio zilivyo game of chance,huyu mzee ana dharau sana we mwangalie hata siku ccm ilipomaliza kampeni pale jangwani mwaka jana,tambo,kejeli na matusi kwa vyama pinzani akiilenga chadema,mkapa hafai na kombola la vicent ambalo halikufahamika kwa wengi ni saizi yake kabisaaa,ufisadi+kumuua Nyerere kazi kwake haya mkapa chomoa nikuone,mtu anaependa siasa za maji taka dawa yake ni hiyo ili akili yake ikae sawa na arudi kwenye kero za wana arumeru mashariki,lakini hata huko kwenye siasa za kistaarabu atadeliver nini huyo????
 
Ninashauku ya kupata majibu yaliyojitosheleza kutoka kwa Vicent Nyerere kuhusu tuhuma kwamba yeye si mtoto wa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere. Vicent hajajibu hoja hiyo matokeo yake ameishia kumtuhumu Mkapa kwamba ndiye muasisi wa ufisadi na kwamba alimuua Mwalimu bila kueleza kwa kiina uhusiano wake na Mwalimu.
 
Tena wadai genes za kina Nyerere zina chembechembe za CCM, hivyo kitendo cha Vincent kujiuunga Chadema ni uthibitisho dili ilichezwa hivyo kudai anayepinga DNA ifanyike kuthibitisha not only ni mtoto wa nje bali pia wa kusingiziwa!.
Umeshaanza porojo.
 
Imagine huyo MKP ndio wanamwamini chamani! kazi kweli kweli. Ni wapi na lini Vicent alisema yeye ni mtoto wa Nyerere kwa maana ya kuzaliwa naye?
 
Ninashauku ya kupata majibu yaliyojitosheleza kutoka kwa Vicent Nyerere kuhusu tuhuma kwamba yeye si mtoto wa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere. Vicent hajajibu hoja hiyo matokeo yake ameishia kumtuhumu Mkapa kwamba ndiye muasisi wa ufisadi na kwamba alimuua Mwalimu bila kueleza kwa kiina uhusiano wake na Mwalimu.
Soma thread za wenzako ujue majibu yake na sio unafungua thread mpya kama juha! Mbona unakuwa kiazi kama huyo Che Nkapa!
 
duh, nazidi kushangaa kwa nini mtu aliyekupa chakula unamtobolea sufuria lake na misumari??????????
ama kweli wema mtendee mbuzi hata utakunywa mchuzi,
huyu jamaa sasa kwenye mkutano ujao ataanza kubwabwaja kwa kujisafisha, na kama kweli mlimtanguliza the founder wa Tz, basi atakua kawatanguliza wengi hapo jameni...
hiii thread nimeipenda, mods wasijewakaitoa tu
 
Kwani mkapa yeye alipelekwa Arumeru kueleza nani kazaliwa na nani??au kueleza sera za serikali yake na chama chake!!Hiyo ndo stahili yake akuanzaye mmalizie!!
 
Mbona amesema yeye ni mtoto wa Josephat na sio wa Julius lakini hawa wawili ni mtu na kakaake!
 
Ninashauku ya kupata majibu yaliyojitosheleza kutoka kwa Vicent Nyerere kuhusu tuhuma kwamba yeye si mtoto wa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere. Vicent hajajibu hoja hiyo matokeo yake ameishia kumtuhumu Mkapa kwamba ndiye muasisi wa ufisadi na kwamba alimuua Mwalimu bila kueleza kwa kiina uhusiano wake na Mwalimu.
Kweli wewe ni Kamura, unawatia aibu Mamura!
 
Back
Top Bottom