Vinapatikana Wapi Hivi Vitabu?

Vinapatikana Wapi Hivi Vitabu?

King Shaat

JF-Expert Member
Joined
Aug 30, 2013
Posts
863
Reaction score
835
Habarini wanaJF, wadau, na wachangiaji wote humu ndani. Leo nimekumbuka baadhi ya vitabu vya hadithi vya kiswahili nilivyovisomaga enzi zilee.
Vitabu kama vya Someni kwa Furaha, Hadithi za Bulicheka, Kalumekenge, na vingine vingi.
Kwa siku hizi sivisikii tena, labda kwa sababu watoto wa siku hizi elimu yao imebadilishwa sana. Ila yote tisa kumi, vile vilikuwa vitabu vizuri sana vilivyotufanya baadhi yetu (na wengine wengi) kupenda sana kusoma hadithi na vitabu kwa ujumla. Je, vitabu kama hivi naweza kuvipata wapi, wakuu?
Natanguliza shukrani nyingi kwenu.
 
Pale mtaa wa samora karibu na duka la Sapna kuna duka la vitabu jina nimelisahau. Ukienda hapo utavipata vitabu hivyo.
 
Dah, asante sana mkuu. Ntafanya utaratibu wa kuvipata.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom