Vitabu vya Dini vina Mafumbo kana kwamba ukiwa Kichwa nazi uwezi kuelewa au utaelewa tofauti

Mhaya

JF-Expert Member
Aug 20, 2023
1,658
4,861
Tatizo letu binadamu ni moja, vitabu vya dini tunataka tuvisome kama vitabu vya hadithi vya akina Nyemo, tunataka kuvielewa kama vilivyoandikwa, yaani hatutaki kujua walikuwa na maana gani. Tatizo huwa hapo tu.

Sina uhakika na Kurani kwa kuwa sijaisoma sana, ila kwa Biblia, imeandikwa kimafumbo sana, sasa kwa kuwa sisi akili zetu zipo chini sana, tunaisoma Biblia kama tusoma gazeti, tunataka tuielewe kama tunavyoelewa magazeti.

Ninapopita njiani, nakutana na miadhara, watu wanabishana, mmoja ameshika Biblia, anapinga kwa kusoma maandiko ya Biblia, anayasoma kama gazeti, yaani A inakuwa A lakini Biblia haisomwi hivyo, yaani ukiisoma kama hivyo, utaanza kuona kama inakudanganya sana. Kuna wengine hata kuielewa hawaielewi halafu inawapa maswali ya kipuuzi, kwa nini? Kwa sababu wameisoma kama gazeti.

Ukisoma kitabu cha Mwanzo unaambiwa watu wa Babeli walitengeneza mnara mkubwa ili wakamuone Mungu. Ukisoma kama ilivyoandikwa, unaona kweli ni mnara wa Babeli lakini kiundani si mnara kama unavyoujua wewe, yaani si mnara jengo bali ni mnara kwa maana ya mambo ya kiroho.

Kila kitu kilichokuwepo zamani, sasa hivi kipo. Ukitaka kugundua kama Mnara wa Babeli haukuwa mnara kama mnara, hata picha za mabaki yake hazipo.

Ukiingia Googole, utakutana na safina ya Nuhu, mabaki yake bado yapo huko Mashariki mwa Uturuki, utakutana na mke wa Lutu aliyegeuka na kuwa chumvi. Utakutana na sehemu alizotembelea Yesu, utakutana na hekalu alilolijenga Sulemani, utakutana na mahali ambapo palikuwa na Bustani ya Eden huko Iraq, lakini kamwe hautokutana na sehemu kulipokuwa na mnara wa Babeli.

Kwa namna mnara ulivyo mkubwa, ungekutana hata na mabaki yake, kila kitu wenzetu walikitunza kama kumbukumbu, mnara wa Babeli upo wapi? Hata mabaki yake basi turidhike, hakuna.

Kwa nini kila kitu kilihifadhiwa kwenye kumbukumbu lakini si mnara huu? Hujiulizi? Unataka ufafanuzi gani?

Unanipata!

Sasa ukikutana na mtu anaanza kuzungumza kuhusu mnara, hujiulizi kwa nini siku hizi kuna majengo marefu zaidi ya huo wa Babeli lakini hakuna lolote lile, kwa nini?

Mnara uliozungumziwa Babeli si mnara wa jengo bali nguvu ya kiroho. Watu walitaka kumfikia Mungu si kwa mnara wa jengo bali kiroho. Ngoja nikwambie kitu.

Baada ya Mungu kumtupa shetani kuzimu na malaika wengine, wao wakaja duniani na kuzaa na wanadamu. Wakawa majitu makubwa mno. Wao wakaleta elimu ya uchawi, teknolojia na mengine, nadhani nilishawahi kuyaelezea huko nyuma.

So watu wa Babeli walikuwa wachawi sana, acha na huu uchawi wako wa siku hizi sijui unamloga mtu asifanikiwe, uchawi uliokuwa pale ulikuwa mkubwa sana, kiasi kwamba mtu akifa, watu wanamfufua.

Kupitia uchawi huo, shetani akawapa watu nguvu ya kutaka kukutana na Mungu, waonane naye na kupambana naye. Si kupambana kwa mishale ndugu yangu, ilikuwa ni kupambana kwa uchawi.

Wachawi wakajikusanya na kuanza kuloga, ulikuwa ni moja ya uchawi mkubwa kuwahi kutokea hapa duniani, huo ndiyo mnara uliojengwa, haukuwa jengo kama unavyofikiria, kiasi kwamba Mungu alipoangalia duniani, aliona watu wapo serious na kile walichokitaka.

Akawachanganyia lugha. Watu wakaacha kufanya matunguli.

So ukisoma Biblia kama gazeti, utasema mnara unaozungumziwa na jengo, na Biblia imeandikwa hivyo, kimafumbo, haikuwekwa wazi, na sijui kwa sababu gani imekuwa hivyo.

Watu mnawajua malaika wana mbawa mbili, lakini Biblia imeeleza kuhusu malaika. Shetani alikuwa malaika mzuri tu mbinguni, hakuwa na mbawa mbili, alikuwa na mbawa sita. Hebu vuta picha unakutana na malaika mwenye mbawa sita, yupoje?

Ukisoma kitabu cha Daniel 10:12 unaona kwamba mfalme wa Uajemi alipigana na malaika Mikaeli. Yaani Mikaeli alipigana vita na shetani kumleta kuzimu baada ya kuleta fujo mbinguni, halafu baadaye alipigana naye jangwani wakati anataka mwili wa Musa, sasa ilikuwaje huyu Mikaeli mwenye nguvu kuja kupigana na binadamu? Tena mfalme wa Uajemi?

Ukisoma Biblia kama gazeti utashangaa ni kwa nini binadamu alipigana na malaika mwenye nguvu, ilikuwaje? Kumbe vita ambavyo walikuwa wakipigana vilikuwa ni vya kiroho, yaani malaika Mikaeli alikuwa akipigana na mfalme wa Uajemi kwa uchawi na nguvu za kimungu.

Haikuwa vita ya kawaida, ila kwa kuwa tunasoma Biblia kama gazeti, kwenye miadhara unasikia mtu anasema Mfalme wa Uajemi alipigana na malaika Mikaeli, ilikuwaje binadamu apigane na malaika, si uongo huu umeandikwa kwenye Biblia...unabaki kucheka tu.

Shetani anapigana na Mungu, jiulize hapa. Kwa nini? Jibu ni moja tu, jamaa naye ana nguvu kubwa. Nguvu amezitoa wapi?

Harmonize alikuwa WCB, Diamond akampa kila kitu, akamuonyesha nguvu zake nyingi, siku Harmonize alipoondoka, aliondoka akiwa na siri nyingi sana za Diamond, alijua nguvu ya jamaa ilikuwa wapi, alijua mambo mengi.

Mondi amemtengeneza Harmonize lakini ndiye mtu anayemsumbua. So ni sawa na Mungu na shetani. Shetani anapata wapi nguvu ya kupigana na Mungu? Nguvu ameitoa wapi? Ni kwa sababu alikuwa karibu na Mungu.

Si malaika wote waliokuwa wakimuona Mungu, ila shetani alikuwa akimuona, pamoja na kuwa muovu lakini ana uwezo wa kuzungumza na Mungu uso kwa uso, soma mkasa wa Ayubu.

Nguvu za shetani ni kubwa, ila kuna nguvu nyingine shetani hakujua kama Mungu anazo na hizo ndizo zinazomsumbua. Sasa kwa nguvu ambazo shetani anazo ndizo alizokwenda kuzipandikiza kwa binadamu. Unasoma mfalme wa Uajemi alipigana na malaika, unasoma watu wa Babeli walikuwa wachawi kiasi kwamba walitaka kumuona Mungu na kupambana naye.

Hizo nguvu zake ndizo amewapa akina freemason na illuminati. Leo hii wanatusumbua na kuitawala dunia.

Wakati malaika wa kuzimu waliposhuka duniani na kuzaa na wanadamu, Biblia inasema walikuwa majitu makubwa. Hilo lilikuwa kosa kubwa shetani alilolifanya, sasa hivi hao malaika wamezaa na wanadamu, si majitu makubwa tena, ni binadamu kama tulivyo sisi.

Unasikia familia ya Roshchild ni uzao wa kishetani, ukiwaangalia hao watu, ni kama sisi tu. Shetani hataki agundulike tena, kuna makosa aliyafanya na ameamua kuyarekebisha.

Kuna vita kubwa sana ya rohoni inaendelea kwenye ulimwengu huu ila hatujui tu. Kwa hiyo ndugu zangu, ukisoma Biblia usisome kama gazeti, hakikisha unapata muongozo wa vitabu vingine ili ujue maana iliyomaanishwa.

Ukisoma kitabu cha Mwanzo, sijui ni Esau vile, alipigana na malaika vile, sijui Bwana, alipoona Bwana anashindwa, akamshika uvungu wa paja. Sasa ukisoma kikawaida, wewe utahisi ni vita vya mwili kwa mwili.

Ndugu yanguuuuuuuuuuuuuuuuuuuu!!!!!!!!!!!

1703832263262.jpg
 
Unathibitisha vipi ni vita vya kiroho na si mawazo yako ya kufikirika tu?

Mfano, Waisraeli walipokuwa utumwani Misri hawakuwa kimwili walikuwa kiroho?

Kwamba kila Andiko la biblia ni la kiroho zaidi?

Utajuaje andiko hili ni la kiroho na si kimwili?
Ndio maana nikasema Ukiwa kichwa nazi uwezi kuelewa.... Wapi nimeandika kila Andiko ni la kiroho zaidi... Mimi nimeandika kuwa baadhi ya matukio ni ya Kiroho zaidi, mfano binadamu kupigana na Malaika na akamshinda, wewe binadamu wa kawaida unaweza kupambana na malaika ukamshinda. Biblia ukikurupuka uwezi kuielewa
 
Waislam huparamia na kufakamia biblia kwa lengo la kupotosha huishia kuchanganyikiwa wasijue mafumbo ya biblia, wanadhani biblia husomwa kama qur an na gazeti au novel.
 
Ndio maana nikasema Ukiwa kichwa nazi uwezi kuelewa.... Wapi nimeandika kila Andiko ni la kiroho zaidi... Mimi nimeandika kuwa baadhi ya matukio ni ya Kiroho zaidi, mfano binadamu kupigana na Malaika na akamshinda, wewe binadamu wa kawaida unaweza kupambana na malaika ukamshinda. Biblia ukikurupuka uwezi kuielewa
Ni vigezo gani unatumia kusema hili tukio ni la kiroho zaidi na hili sio la kiroho zaidi liko kama lilivyoandikwa?
 
Waislam huparamia na kufakamia biblia kwa lengo la kupotosha huishia kuchanganyikiwa wasijue mafumbo ya biblia, wanadhani biblia husomwa kama qur an na gazeti au novel.
Usivamie waislamu kwanza. Rekebisheni ndani kwanza, uangalie utofauti mkubwa kuanzia wakatoliki, waanglican, wasabato, walutheran na orthodox na mashahidi wa Yehova. Kila mmoja anaabudu anavyojua yeye.

Hamuelewi mnachokiabudu. Kila mmoja anaelezea kivyake. Biblia mnatumia tofauti, kuna wengine wanachonga masanamu, wengine ibada kukata viuno kanisani kuchanganyika mwanaume na mwanamke, kuna wengine wanakanyaga mafuta.

Bahati nzuri hapa serikali wanajifanya kumonitor haya makanisani. Nina imani kungekuwa tuna uhuru kama Kenya, wangepatikana wakina Mackenzie na Kibwetere wa Uganda kwa sababu waumini wengi mazezeta.
 
Akili na mambo ya kidini ni kulia na kushoto, magharibi na mashiriki. Wewe kama unaamini dini yako amini tu ila ni ujuha kusema unatumia akili katika mambo ya kidini, wengine nimeona wanasema kitabu chao kinathibitishwa hadi na Sayansi!
 
Ndio maana nikasema Ukiwa kichwa nazi uwezi kuelewa.... Wapi nimeandika kila Andiko ni la kiroho zaidi... Mimi nimeandika kuwa baadhi ya matukio ni ya Kiroho zaidi, mfano binadamu kupigana na Malaika na akamshinda,
Wakati binadamu huyo anapigana na huyo malaika alikuwa katika hali ya kimwili au kiroho?

Roho inapigana?


wewe binadamu wa kawaida unaweza kupambana na malaika ukamshinda. Biblia ukikurupuka uwezi kuielewa
Huyo Yakobo wakati anapigana na huyo malaika alikuwa Yakobo roho au Yakobo mwili?
 
Back
Top Bottom