Anaweza kubisha lakini ukweli ndiyo huodar moro siku hizi ni masaa matano
Wilaya ya kilwaHapana nimekosea n ihalmashuri
Kutoka ubungo kufika Kibaha tu ni masaa 2 foleniIlikuaje ukafika msamvu saa nne usiku wakati ulikuwa ubungo mida ya saa nane?
InawezekanaStory ikiwa na vipicha picha kama hii inaleta uhalisia. Imebidi tuamini LAKINI HILI LA KUTOKA UBUNGO SAA NANE MCHANA NA KUFIKA MSAMVU SAA NNE USIKU NDIO LIMEHARIBU KILA KITU.
Habari za leo!
Leo ach nishare safari yangu from Mtwara to Singida tujifunze na kujuzana mengi.
TAREHE 26/09/2019 SAA 11:37.
mnamo saa 11:37 alfajiri niliwasili kituo cha basi Chipuputa Mtwara mjini tayari kwa safari yangu kutoka Mtwara kwenda Morogoro.
Kituo cha basi Chipuputa ni kipya hakina hata miezi mitano tangu kianze kutumika,ni kama hakijakamilika kwani ni vumbi tupu,kadhalika kituo hiki hakina hata hadhi kwani kina jengo dogo tu la kupumzikia abiria kama kinvyoonekana pichani.
Nilibahatika kupata siti ya mbele kabisa katika basi la Maningnice (kampuni pekee inyofanya safari za Mtwara to Morogoro) naamini tupo wengi tunaopenda hizi siti za mbele kabisa.
Saa 12:00 magari yalianza kuondoka kwa fujo tulitanguliwa na basi za Machinga high class(sunlong),Buti la zungu (yutong F12+) na sisi Maningnice (zhongtong climber new model) safari ikaanza na dakika chache mbele tulikuwa tukiitafuta Mikindani.
Kabla ya kufika mikindani tuliipita basi la Machinga high class ikiwa imesimama katikati ya barabara na tuliipita kupitia upande usioruhusiwa (kushoto).
Baada ya dakika zisizozidi mbili basi hilo lilitupita kwa fujo katika eneo lenye kona kali,hii ilinifanya nimuone dereva wake kuwa mpenda ligi na asiye makini na maisha ya abiria pamoja na chombo cha mbunge mstaafu (Hasnan Murji,CCM)
Safari ilipamba moto hatimaye sasa tulikipita kiwanda cha simenti cha Dangote huku usalama wa watumiaji wa barabara hii ukihatarishwa na malori yaliyoegeshwa hovyo pembezoni mwa barabara.
Mwendo ni wa wastani na dereva akiwa mtu wa makamo ya miaka 34 hadi 38 hivi hivi kijana mdogo lakini makini sana,palipo na kibao cha 30 alitembelea 30 na palipo na 50 alitembelea 50.
Kipande cha Mtwara hadi Mingoyo weight bridge Mnazi mmoja kimejaa viraka na manundu yanayopunguza hata hamu ya safari yenyewe,nyakati zingine dereva alibaki kurukaruka ajabu kutokana na muundo wa kiti cha dereva kuwa na mneso zaidi lakini hakuwa ananesa tena bali alikuwa anarukaruka kabisa.
Saa 1:49 tuliwasili Mingoyo weight bridge ambapo tulikutana na basi za Maningnice(zhongtong climber),Navil exspress(yutong F11),Buti la zungu(yutong F12+),Baraka classic (yutong F11) zote zikitokea Masasi,saa 2:30 tuliwasili Lindi.
Safari ya kutoka Lindi ilikuwa ni nzuri sana kutokana na barabara kuwa nzuri ingawaje bado kipande cha Mtwara to Lindi kilikuwa na mvuto wake kutokana n mandhari za kuvutia sana.
Majengo ya kihistoria Mikindani huonekana vizuri na kwa ukaribu sana,kadhalika barabara hupita pembeni mwa bahari ya Hindi hii inavutia sana.
Pia mashamba ya chumvi yaliyotamalki pembezoni mwa bahari ya hindi yalizidisha mvuto hususani kwa wale wasiofahamu jinsi chumvi inavyotengenezwa kwa kutegemea jua tu hii ni nafasi yao kujionea sasa.
Hatimaye saa 10:13 tuliwasiliNangurukuru,hapa ndipo abiria hujipatia chakula na huduma za maliwato ipo mkoa wa Kilwa.
Huduma za choo ni nzuri lakini bei za vyakula ni maumivu kwa abiria,bei za vyakula,ubora wa vyakula na ujazo ni vitu viwili tofauti,kutokana na uwepo wa sehemu hii moja pekee ndiko kubakowatia jeuri wafanyabiashara wa sehemu hii.
Nilinunua maji y tshs 1000 na ndizi tatu na kutulia zangu nikienjoi kifungua kinywa.
Inaendelea......
View attachment 1222269View attachment 1222270View attachment 1222271View attachment 1222272
Acha ubishi wewe kwa masaa yako mawili hata mlandizi hufiki kwa kipindi hiki.Piga hesabu mwenyewe 190.7km ni sawa na masaa mangapi?
hii ni nini? soko la samaki au
Mkuu, nikurekebishe kidogo hapo kuwa Nangurukuru haipo mkoa was Kilwa, Bali ipo wilaya ya Kilwa ndani ya Mkoa was Lindi.. But stori nimeipenda nasubiri muendelezo
Asante..
Naunga mkono hilo suala la kuongeza VTS kutoka 85kph hadi 100kphNilidamka kongwa asubuhi mapema nikasikilizia tumbo nikaona lipo fresh,nikasogea stendi sasa kuangalia usafiri wa Singida.
Hata hivyo kilichonishangaza katika eneo hili ni wingi wa mbwa wanaorandaranda huku na huko,tena mbwa wenye afya hasa nao walipishana na watu bila hta wasiwasi wala hakukuwa na mtu aliyejali wala kuwabugudhi wanyama hawa.
Kwa mawazo yangu niliamini ni kutokana na jamii iliyopo kuwa ya wafugaji zaidi,kadhalika eneo hili malori na magari madogo yalisimama hapa kwa huduma za vyakula hasa Nyamachoma,mbwa hawa walineemeka sana na mabaki ya vyakula kiasi kwamba walinawiri kwelikweli.
Vilevile nilishangazwa na ufundi wa kuendesha gari la kuvutwa n ng'ombe,kiukwelj sio rahisi kwani mwongozaji aliweza kuwaamuru watembee,wakimbie,wasimame na kukata kona alimwongoza mnyama mmojawapo tu kulingana na wapi anataka kukata kona,ujuzi huu ni muhimu sana hasa kwa barabra iliyo bize kama ya moro-dodoma.
Baada ya kuulizia usafiri nikabaini kwamba ni lazima kusubiri magari toka Morogoro na nilikuwa na haraka basi nikapanda gari ndogo hadi dodoma nilipobahatika kupata basi la Nyehunge,shida ikaja pale kuingia garini na siti hamna,sikujali nilikuwa na haraka nikakaa tu pale mbele.
Safari hii dereva alikuwa ni kichaa haswa,muda wote VTS ilikuwa ikipiga kelele tu,naye alipunguza mwendo kidogo kisha ikizima anakanyaga mafuta basi ni kelele tu na ilikuwa na sauti kubwa kiasi.
Baada ya kuacha mzani hatukwwnda sana trafiki akaipiga mkono wakashuka pamoja na dereva wakaongea kidogo kisha safari ikaendelea,nadhani Rushwa ilifanya kazi yake.
Saa nane tayari tulikuwa ndani ya stendi ya Misuna,hii stendi naipa Kongole halmashauri ya manispaa ya Singida.
USHAURI WANGU.
Kutokula kabisa safarini ni hatari kwa afya,ni rahisi zaidi kupata shida kama vile kuharisha usipokula kuliko ubapokula.
Ni vizuri kumeza dawa za flgil unaposafiri hata kama huumwi,meza tu kwa tahadhari ukizingatia vyakula vingi njiani si salama,ukiweza beba chakula chako toka nyumbani.
Wahusika mtuondolee adha ya kurundika abiria kwani ni hatari kwa usalama vilevile haipendezi kwa sifa za kampuni.
Hizi VTS zinatoa alam mara spidi ifikapo 85+kph waongeze angalau 100kph,hii ni biashara na huu ni uchumi ni kuchelewesha maendeleo tu haiwezekani basi zitembee sawa na lori la mizigo inachosha.
Trafick punguzeni rushwa fanyeni kazi,madhara ya rushwa hizi ni makubwa endapo vyombo hivi vitapata ajali,fanyeni kazi kama ni njaa kila mtu ana njaa jikazeni kizalendo.
Aahaaa. !!! Jamaa muongo sn ww.Mimi jamaa nawashangaa sana nyie jamaa..!!
Nimepanda bus flani (•••) tukapitia Bagamoyo, msata mpaka kufika moro ni masaa 2:45, sasa sijui ulazima mnaotumia wa masaa 6-8 ni wa nini?
Huku foleni utaikuta wapi ?.
Yawezekana nabishana na mwanangu ambaye anajifanya anajua kumbe hajui mimi ndiye sababu ya yeye kujua.
Pole.
Usibishe, nilitoka Dar saa kumi na moja jioni na abood tukaingia Moro saa sita usiku. Siku ukikuta foleni hata masaa 10 dar moro inawezekana tuu.Story ikiwa na vipicha picha kama hii inaleta uhalisia. Imebidi tuamini LAKINI HILI LA KUTOKA UBUNGO SAA NANE MCHANA NA KUFIKA MSAMVU SAA NNE USIKU NDIO LIMEHARIBU KILA KITU.
Kutoka Mtwara hadi stand ya Ubungo always ni kuanzia saa 8 Mchana ndo unafika hapo....
Nahisi harakati za hapo na kila kitu wanaweza kutoka saa 9 Alasiri, SAWA
Niliwahi panda hiyohiyo Maning Nice kutoka Morogoro niliisubiri Ubungo ikafika saa 6 kasoro... hadi kutoka stand ya Mbagala ni saa 9 Kasoro Mchana, then Mtwara lazima uingie by saa 3 Usiku na Kuendelea....
Ko jamaa yuko sawa kwa kipande cha Mtwara to Morogoro
Usibishe, nilitoka Dar saa kumi na moja jioni na abood tukaingia Moro saa sita usiku. Siku ukikuta foleni hata masaa 10 dar moro inawezekana tuu.