Kwa mizania ya kiuchumi miji hii miwili bado Mtwara na Singida zina upinzani mkali lakini Mtwara itatwaa kombe kwakuwa shughuli za kiuchumi ni nyingi na zina pato kubwa kuliko zile za singida...kwa mfano.
SHUGHULI ZA USAFIRISHAJI,wakati Singida in airport na barabar,mtwara ina airport,bandari na barabara.
VIWANDA,,Singida in viwanda kdhaa vya mafuta y alizeti n sabuni,viwanda vya unga wa mahindi na maji ya kunywa,Mtwara in viwanda zaidi ya vitano vya Simenti vikiongozwa na kiwanda kikubwa zaidi cha Dangote,viwanda vya korosho,ufuta na vipuri vya pikpiki achilia mbali vile vya maji ya kunywa na chumvi.
NISHATI,Mtwara inatumia umeme wa gesi zaidi na hupata umeme ht kama sehemu nyingi za nchi hazina umeme,umeme ni wa uhakika na hauktiki hovyo,kdhalika nishati ya gesi inzalishwa hapa na kuuzwa,kusafirishwa sehemu mbalimbali nchini,Singida intumia umeme toka Gridi ya taifa pamoja na vyanzo vidogo vidogo kama jua.
BIASHARA NA UCHUMI,mzunguko wa fedha Singida ni mdogo sana,wannchi wake hufunga maduka mapema saa ttu hadi nne usiku,kadhalika huchelewa kuyafungua hufunguliwa saa tatu au nne asubuhi,tofauti na Mtwara ambapo mzunguko wa fedha ni mkubwa muda wa huduma za maduka ni asubuhi mpema saa 11 hadi saa saba usiku,vilevile usafiri katikati ya mji ni bajaji na pikpiki zaidi kutokana na kukosekana kwa idadi kubwa ya wasafiri hivyo daladala hzitumiki,mtwara daladala ni nyingi na coster pia huhudumu katikati ya mji.
MANDHARI ,mtwara iko vizuri sana,Barabra za kuvutia zenye mata ingawaje wakti mwingine haziwashwi,fukwe za bahari na ile hali y kuzungukwa na maji pnde zote tatu huvutia zaidi,Hoteli nyingi za hadhi ya nyota 2 hadi 4,hoteli za kitalii,maeneo ya kihistoria kama vile Mikindani haya yanaiacha mbali sana Singida ambyo ina Hoteli kubwa ya nyota 2 ya Regency pekee,pia kuna hoteli mpya ambayo haizidi nyota 2 nimeisahau jin lake,Singida maeneo ya kuvutia ni Regency hotel na kituo cha basi misuna(mnisamehe wanyaturu)
Kadhalika makazi ya Mtwara ni ya kisasa na ya kuvutia yanyotofutisha mjini na pembezoni mwa mji,tofuti n Singida ambapo hakuna msawazo wa mji wala pembezoni kwani hata mjini kbisa nyumba duni ni nyingi sana na mjengo binafsi ya kuishi mazuri ni machche sana kulinganisha na yale ya kawaida na kienyeji.
UWEZO WA KUCHNGIA PATO LA TAIFA mtwara nitiweka juu kutokana na sababu zinazoonekana,mf bandari utrii na viwanda kama nilivyofafanua hapo juu.
ZIADA,mambo mengi sana yanaiacha Singida nyuma kwa wakazi wake kutobadilika kielimu na kimtazamo,kwa mfano English medium schools ni chache sana hzizidi nne au tano mjini na suala la School bus wanashngaa sana vilevile ni kawaida shule za bweni kutumia mtaala wa kiswahili badala ya English medium.
Je kwa mandhari,upi mji ambao uko vizuri kati ya Singida na Mtwara,hali ya Biashara,uwezo wa mji kutoa pato ghafi kwa Taifa na mizania mingine kama Hotel/Lodge za kisasa,Attractive Destination,Recreation nk