Vimambo na vijimambo safari yangu Mtwara to Singida

Vimambo na vijimambo safari yangu Mtwara to Singida

Mkuu DAR - MORO ni Kilometa 200. Hata bajaji haiwezi kutumia masaa zaidi ya 8.
Mkuu mbona kasema walifika ubungo saa nane na nusu na ikawalazimu kujazia abiria. Pia mbezi walisimama kuongeza abiria sasa hapo cha kushangaza nini?Pia kasema foleni waliyokutana nayo kutokea ubungo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kumbe kutoka ntwara kuchele mpaka singida ni safari ya siku mbil? Ndo najua Leo. Kama ni hivyo Tanzania tuna safari ndefu sana
Mkuu, usichukulie poa. Mtwr-Dsm(562km)
Dar-Moro( 198km say 200km)
Moro-Dom(260km)
Dom-Singida (244km)
Jumla: 562+200+260+244 zaidi ya kilometa 1250, sawa na DSM Mpanda au Dar-Magu(mbele ya Mwanza)
Sasa kwa sababu hakuna basi la moja kwa moja(ingawa kwa sasa kuna Baraka Classic-Mtrwa to Dom), lakini kwa mwaka 2019 wakati thread hii inaandikwa, hakukua na hii route.
 
Nilidamka kongwa asubuhi mapema nikasikilizia tumbo nikaona lipo fresh,nikasogea stendi sasa kuangalia usafiri wa Singida.

Hata hivyo kilichonishangaza katika eneo hili ni wingi wa mbwa wanaorandaranda huku na huko,tena mbwa wenye afya hasa nao walipishana na watu bila hta wasiwasi wala hakukuwa na mtu aliyejali wala kuwabugudhi wanyama hawa.

Kwa mawazo yangu niliamini ni kutokana na jamii iliyopo kuwa ya wafugaji zaidi,kadhalika eneo hili malori na magari madogo yalisimama hapa kwa huduma za vyakula hasa Nyamachoma,mbwa hawa walineemeka sana na mabaki ya vyakula kiasi kwamba walinawiri kwelikweli.

Vilevile nilishangazwa na ufundi wa kuendesha gari la kuvutwa n ng'ombe,kiukwelj sio rahisi kwani mwongozaji aliweza kuwaamuru watembee,wakimbie,wasimame na kukata kona alimwongoza mnyama mmojawapo tu kulingana na wapi anataka kukata kona,ujuzi huu ni muhimu sana hasa kwa barabra iliyo bize kama ya moro-dodoma.

Baada ya kuulizia usafiri nikabaini kwamba ni lazima kusubiri magari toka Morogoro na nilikuwa na haraka basi nikapanda gari ndogo hadi dodoma nilipobahatika kupata basi la Nyehunge,shida ikaja pale kuingia garini na siti hamna,sikujali nilikuwa na haraka nikakaa tu pale mbele.


Safari hii dereva alikuwa ni kichaa haswa,muda wote VTS ilikuwa ikipiga kelele tu,naye alipunguza mwendo kidogo kisha ikizima anakanyaga mafuta basi ni kelele tu na ilikuwa na sauti kubwa kiasi.


Baada ya kuacha mzani hatukwwnda sana trafiki akaipiga mkono wakashuka pamoja na dereva wakaongea kidogo kisha safari ikaendelea,nadhani Rushwa ilifanya kazi yake.

Saa nane tayari tulikuwa ndani ya stendi ya Misuna,hii stendi naipa Kongole halmashauri ya manispaa ya Singida.

USHAURI WANGU.

Kutokula kabisa safarini ni hatari kwa afya,ni rahisi zaidi kupata shida kama vile kuharisha usipokula kuliko ubapokula.

Ni vizuri kumeza dawa za flgil unaposafiri hata kama huumwi,meza tu kwa tahadhari ukizingatia vyakula vingi njiani si salama,ukiweza beba chakula chako toka nyumbani.


Wahusika mtuondolee adha ya kurundika abiria kwani ni hatari kwa usalama vilevile haipendezi kwa sifa za kampuni.

Hizi VTS zinatoa alam mara spidi ifikapo 85+kph waongeze angalau 100kph,hii ni biashara na huu ni uchumi ni kuchelewesha maendeleo tu haiwezekani basi zitembee sawa na lori la mizigo inachosha.


Trafick punguzeni rushwa fanyeni kazi,madhara ya rushwa hizi ni makubwa endapo vyombo hivi vitapata ajali,fanyeni kazi kama ni njaa kila mtu ana njaa jikazeni kizalendo.
Kosa la kiufundi ulilolifanya mtembezi(mtoa mada) ni kusubiri gari la kutoka Dar pale Moro eti uende Singida.
Mabasi ya kampuni ya Nyehunge ya Moro-Mwanza yako pale tena yako mawili. Ulitakiwa ulivyolala Moro, uchukue basi la Nyehunge linaloanzia Morogoro kuelekea Mwanza, ungefika Singida muda mzuri, ungepata siti pia.
 
Bado masaa nane Dar to Moro haipenyi akilini asilani, hata uondoke Dar saa 1usiku huwezi fika moro saa 4!!!
Kwa hali ya sasa ya Morogoro road, nakupa challenge, panda saa basi 12 asubuhi uone kama huingii Moro saa4 au 5 asubuhi, na ikitokea kama kuna ajali au jambo lolote mbele, masaa hayo yataongezeka.
 
Bus gani hilo LA
Kwa hali ya sasa ya Morogoro road, nakupa challenge, panda saa basi 12 asubuhi uone kama huingii Moro saa4 au 5 asubuhi, na ikitokea kama kuna ajali au jambo lolote mbele, masaa hayo yataongezeka.
Bus gani hilo linalotumia masaa 4-5 Dar Moro? Kijana labda kama ulipanda coaster
 
Kosa la kiufundi ulilolifanya mtembezi(mtoa mada) ni kusubiri gari la kutoka Dar pale Moro eti uende Singida.
Mabasi ya kampuni ya Nyehunge ya Moro-Mwanza yako pale tena yako mawili. Ulitakiwa ulivyolala Moro, uchukue basi la Nyehunge linaloanzia Morogoro kuelekea Mwanza, ungefika Singida muda mzuri, ungepata siti pia.
Acha kumsumbua marehemu.
 
Nawaangalia tu mnavyomsumbua marehemu
 
Back
Top Bottom