Vimambo na vijimambo safari yangu Mtwara to Singida

Vimambo na vijimambo safari yangu Mtwara to Singida

Pole kwa kuumwa mkuu, umalizie basi.
 
Hebu fanya calcultion ya kufikirika yaani iliyo posible.


Stendi ya mbezi mnaipita saa 10,na bado mnapakia abiria kil stendi na bado mnashusha kila stendi.


Then toa posible time ya kutoka dar hadi moro,kisha uniambie kwanini gari isiingie Msamvu saa nne kasoro.
Story ikiwa na vipicha picha kama hii inaleta uhalisia. Imebidi tuamini LAKINI HILI LA KUTOKA UBUNGO SAA NANE MCHANA NA KUFIKA MSAMVU SAA NNE USIKU NDIO LIMEHARIBU KILA KITU.
 
Nilidamka kongwa asubuhi mapema nikasikilizia tumbo nikaona lipo fresh,nikasogea stendi sasa kuangalia usafiri wa Singida.

Hata hivyo kilichonishangaza katika eneo hili ni wingi wa mbwa wanaorandaranda huku na huko,tena mbwa wenye afya hasa nao walipishana na watu bila hta wasiwasi wala hakukuwa na mtu aliyejali wala kuwabugudhi wanyama hawa.

Kwa mawazo yangu niliamini ni kutokana na jamii iliyopo kuwa ya wafugaji zaidi,kadhalika eneo hili malori na magari madogo yalisimama hapa kwa huduma za vyakula hasa Nyamachoma,mbwa hawa walineemeka sana na mabaki ya vyakula kiasi kwamba walinawiri kwelikweli.

Vilevile nilishangazwa na ufundi wa kuendesha gari la kuvutwa n ng'ombe,kiukwelj sio rahisi kwani mwongozaji aliweza kuwaamuru watembee,wakimbie,wasimame na kukata kona alimwongoza mnyama mmojawapo tu kulingana na wapi anataka kukata kona,ujuzi huu ni muhimu sana hasa kwa barabra iliyo bize kama ya moro-dodoma.

Baada ya kuulizia usafiri nikabaini kwamba ni lazima kusubiri magari toka Morogoro na nilikuwa na haraka basi nikapanda gari ndogo hadi dodoma nilipobahatika kupata basi la Nyehunge,shida ikaja pale kuingia garini na siti hamna,sikujali nilikuwa na haraka nikakaa tu pale mbele.


Safari hii dereva alikuwa ni kichaa haswa,muda wote VTS ilikuwa ikipiga kelele tu,naye alipunguza mwendo kidogo kisha ikizima anakanyaga mafuta basi ni kelele tu na ilikuwa na sauti kubwa kiasi.


Baada ya kuacha mzani hatukwwnda sana trafiki akaipiga mkono wakashuka pamoja na dereva wakaongea kidogo kisha safari ikaendelea,nadhani Rushwa ilifanya kazi yake.

Saa nane tayari tulikuwa ndani ya stendi ya Misuna,hii stendi naipa Kongole halmashauri ya manispaa ya Singida.

USHAURI WANGU.

Kutokula kabisa safarini ni hatari kwa afya,ni rahisi zaidi kupata shida kama vile kuharisha usipokula kuliko ubapokula.

Ni vizuri kumeza dawa za flgil unaposafiri hata kama huumwi,meza tu kwa tahadhari ukizingatia vyakula vingi njiani si salama,ukiweza beba chakula chako toka nyumbani.


Wahusika mtuondolee adha ya kurundika abiria kwani ni hatari kwa usalama vilevile haipendezi kwa sifa za kampuni.

Hizi VTS zinatoa alam mara spidi ifikapo 85+kph waongeze angalau 100kph,hii ni biashara na huu ni uchumi ni kuchelewesha maendeleo tu haiwezekani basi zitembee sawa na lori la mizigo inachosha.


Trafick punguzeni rushwa fanyeni kazi,madhara ya rushwa hizi ni makubwa endapo vyombo hivi vitapata ajali,fanyeni kazi kama ni njaa kila mtu ana njaa jikazeni kizalendo.
 
nikisafiri afu tumbo langu likiwa empya ni kujamba kwa nguvu na ni shida kwangu..niwe mkweli bila msosi wa nguvu sisafiri kabisa..samahani mtoa mada ushauri wako namba 1. hauendani na mm
 
nikisafiri afu tumbo langu likiwa empty ni kujamba kwa nguvu coz tumbo hujaa na ni shida kwangu..niwe mkweli bila msosi wa nguvu sisafiri kabisa.nikiwa nimekula vzr yaani kwenye basi naweza fanya hata vitu vingi vya kujitolea

.samahani mtoa mada ushauri wako namba 1. hauendani na mm
 
Hahaha uwe unameza flgil tu basi inatosha
nikisafiri afu tumbo langu likiwa empya ni kujamba kwa nguvu na ni shida kwangu..niwe mkweli bila msosi wa nguvu sisafiri kabisa..samahani mtoa mada ushauri wako namba 1. hauendani na mm
 
Hatimaye saa saba na nusu tuliwasili mbagala,kwa kweli stendi hii ni mbovu kwelikweli ingawaje kuna matumaini ya uboreshaji wake

Saa nane mchana tuliwasili Ubungo na abiria wanaoishia Dar es salaam walishuka,tulikaa zaidi ya dakika 30 wakijazia abiria wa kuelekea Morogoro.

Ingawaje ilikuwa mchana lakini bado foleni ilikuwa ni kubwa ikichagizwa na ujenzi wa barabara kuu ya Dsm-Morogoro,tulipitia kituo cha mbezi na abiria wakajazwa na kurundikwa hadi kwenye varanda.


Achilia mbali wingi wa Magari yanyofanya safari za Morogoro-DSM bado abiria walikuwa ni wengi mno kiasi kwamba walikua radhi kukaa chini ya varanda.

Kila tuliposimamishwa na trafiki konda alishuka na noti ya elfu tano au elfu kumi naye trafiki hakuwa akiingia garini kusema kwamba huu ni mchezo wao wa kila siku na natumaini wengi wetu huwa tunajionea haya.

Hii inamaan ya kuwa Rushwa haiwezi kuisha leo wala kesho na ni mbaya sana kurundika abiria katika varanda hususani pale inapotokea ajali.


Mnamo saa nne kasoro tuliwasili stendi ya basi Msamvu,kwa stendi hii hongereni Manispaa ya Morogoro ni stendi kubwa na ya kisasa.

Lakini jengo lililopo ghorofani lilionekana kimya kama kwamba halitumiki,ofisi hazijakodishwa na kampuni za mabasi mengi wanakatisha tiketi zao nje kwa mawakala,halmashauri ya Morogoro ijitadthmini kwa kulazimisha makampuni kuwa na ofisi maalumu ili iweze kupata wapangaji wa ofisi zilizo tupu.


Madudu mengine ni maandishi yanayoitambulisha stendi hii KITUO CHA MABASI CHA KISASA MSAMVU,huyu mshauri aliyeyeshauri kiitwe hivyo amekosea sana,je kuna haja gani kuandika neno CHA KISASA?

Eneo la kupumzikia abiria limejaa wafanyabiashara wa vyakula na sikuweza kuona mahali salama kwangu kujipumzisha hadi alfajiri nikaamua tu nitafute Lodge ya bei poa nisije haribu bajeti yangu.


Nikatoa oda kwa bodaboda anipeleke lodge inayotoza chini ya elfu 10 kulingana na bajeti yangu,shughuli ikaja hapa kwani kila mahali chumba ni elfu kumi n tano lakini ukivitazama havina hata hadhi hiyo kabisa.

Lodge zote zimeweka vyoo vya kukaa,hivi nani kawadanganya kuwa kila mtu anapenda aina hii ya vyoo? Mwisho nikakubali lodge mojawapo baada ya kutafuta zisizo na vyoo vya kukaa bila mafanikio,ikabidi niwe naenda kutumia choo cha staff maana sipendi kabisa vyoo hivi labda kiwe changu binafsi.


Inaendelea......View attachment 1222278
Lodge ya 15000 hapo lazima iwe chafu ungelala stand kwa maelezo yako
 
Back
Top Bottom