Fundi Mchundo
Platinum Member
- Nov 9, 2007
- 12,303
- 10,410
Somo kwetu kutokana na uchaguzi huu ni kuwa:
1. Hauwezi kulazumisha upendezwe siku zote. Iko siku utatoka. Huyu jamaa alibadili Katiba ili iwe vigumu chama chake kushindwa. Ametawala kibabe lakini wananchi walipomchoka wakamtema.
2. Hauwezi kuung'oa utawala uliokuwepo kwa amani kwa kususia uchaguzi. Hapa kwetu ACT wanalijua hilo lakini Chadema waliamini inawezekana. Wapinzani Hungary waliingia katika uchaguzi huku wakijua thika kwamba mazingira ya uchaguzi si rafiki. Na kuwa mpinzani wao anapendwa anapendwa na watawala wa Marekani na Urusi. Yote hayo hayakusaidia kitu. Tuliona hilo pia Zambia.
3. Lilikuwa kosa kubwa kwa Chadema kutoshiriki uchaguzi. Wangeshiriki wangekuwa katika nafasi nzuri sana kwa ajili ya chaguzi za 2029 na 2030. Wote tunajua kuwa wabunge wachache wa Chadema wanatosha sana kuwapeleka puta wabunge wa chama tawala.
4. Utawala mpya wa Hungary sasa unaweza kurekebisha uchafu wote wa utawala uliopita kwa sababu wameshika mpini. Hapa kwetu hiyo nafasi haipo.
Amandla...