vijimambo vya vyoo vya master bedroom

vijimambo vya vyoo vya master bedroom

sakapal

JF-Expert Member
Joined
Apr 11, 2011
Posts
1,804
Reaction score
1,425
Habari zenu wana MMU,
Naombeni niwasimulie kisa hiki nilichokisikia live..................

.............baada ya kuona mazungumzo yanaendelea nikawa nimeshikilia kitabu tuu huku nikiwasikiliza kwa makini na kufuatilia maongezi yao. Walikuwa wadada wawili wa makamu ya 25-28 wakiongea(kwa maongezi yao na pete vidoleni, wanaonesha wameolewa). Mdada mmoja ndie alikuwa akilalamika kuwa anakerwa na tabia ya mumewe kutosafisha choo mara baada ya kukitumia choo chao cha master bed room. Kwa maelezo yake wakati wako wachumba akienda kwa mchumbawake anakuta toilet safi ila tangu waoane usafi wa nyumba yao nzima ni yeye mwanamke pamoja na usafi wa master room yao. Sasa akagundua tabia aliyoianzisha mumewe ya kujisaidia bila kuflash wakati choo ni cha kuflash na maji yapo muda wote, kiufupi akitoka bafuni au chooni basi ujue hadi usafishe ndo panafaa kutumika tena.
Sasa akawa anajiuliza inamaana mumewe anafurahia hali ya uchafu? anajiuliza je mumewe akiwa anataka kujisaidia na kukuta choo kichafu atachukuliaje? Kwa kadiri ya maongezi yao hajamwambia mumewe juu ya kinachomkera kwani hataki mumewe afanye usafi au wapangiane zamu ila anataka atleast awe anaflash tuu kila baada ya kujisaidia haja zote. Mdada mwenzie akamwambia mmmh ndo umvumilie mumeo ndo kwanza mna mwaka mmoja wa ndoa.

Nilijikuta nimewasikiliza maongezi yao huku nikigelesha kusoma kitabu nikakumbuka tena hapa job kuna dada mmoja alishanisimulia kisa cha ndoa moja anayoifaham tena hata harusi yake alihudhuria hiyo ndoa ilibaki almanusura ivunjike. Kisa ilikuwa hii hii choo cha master, mke aliumwa akalazwa hospitali mwezi mzima kumbe huku nyuma mumewe alikuwa akiingia chooni haflash, mkewe aliporuhusiwa na kukuta hali ile akagoma kukisafisha na akakifunga kisitumike ikabidi wahamie choo cha public kwenye nyumba yao kwani hicho kilikuwa kinasafishwa na house girl. Nilishangaa mno sasa niliposkia haya mazungumzo jana ninasema inamana hili ni tatizo na nikajiuliza kwani wanaume waliooa hawawezi kuflash baada ya kujisaidia ilhali maji yapo basi haja ashushe mwanaume ila kuflash choo aje aflash mkewe?

Mie na kwangu tangu nimeolewa miaka 14 iliyopita tunakaa kajumba ketu kadogo vyumba viwili choo kimoja hamna master na usafi nasimamia mwenyewe wala sijawahi pata hii kadhaa. Nauliza tuu wanajamvi pengine kunawanajamvi wanapitia tatizo kama hili je ni sawa kuflash ukimaliza haja zako flash uziache kwa anayekuja aone mmeng'enyo wa vyakula ulioushusha?
 
Hapana hiyo sio haki kabisa uchafu wako ni wako na hakuna aliye na jukumu la kusafisha uchafu wako hata kama umeoa labda uwe mgonjwa mahututi ila uchafu hasa vyooni ni jukumu la kila mmoja kuhakikisha anaacha choo ikiwa safi ili mwingine atumei kwa amani,choo ni sehemu ya starehe sema wengi hatujui hilo sasa ukiacha uchafu wako starehe ya mwenzio itatoka wapi?nafikiri tunapaswa kufikiria watu wengine pindi tutumiapo vyoo hasa vya halaiki,tujiulize je ingekuwa ndio mimi nakuta uchafu chooni ningejisikiaje?tukifanya hivyo tutaepuka kufanya mambo ya ajabu.
 
Aisee nyumba zina issues, l would never imagine kitu kama hicho.
Wakati nakuwa nilifundishwa mchafu ni yule anayekaa na uchafu na wala sio anayeshika uchafu!
 
Na hii nayo ni kali hadi kuflash hataki hii balaa au ndio mfumo dume!!!
 
Hapana hiyo sio haki kabisa uchafu wako ni wako na hakuna aliye na jukumu la kusafisha uchafu wako hata kama umeoa labda uwe mgonjwa mahututi ila uchafu hasa vyooni ni jukumu la kila mmoja kuhakikisha anaacha choo ikiwa safi ili mwingine atumei kwa amani,choo ni sehemu ya starehe sema wengi hatujui hilo sasa ukiacha uchafu wako starehe ya mwenzio itatoka wapi?nafikiri tunapaswa kufikiria watu wengine pindi tutumiapo vyoo hasa vya halaiki,tujiulize je ingekuwa ndio mimi nakuta uchafu chooni ningejisikiaje?tukifanya hivyo tutaepuka kufanya mambo ya ajabu.

ni kweli kabisa ukiwaza mie nikikuta choo kimeachwa kichafu ntajiskiaje lazima ukimaliza haja yako unasafisha ili wakati ujao ukute mazingira safi. Haja ni starehe mahala pakiwa safi, utakuta hata maofisini au vyoo vya mahoteli mtu akimaliza haja anaacha wazi kilakitu hajui hata kusafisha looh, kweli ustaarabu kitu cha bure.
 
Kumbe kuta za nyumba zinaficha mengi na makubwa zaidi
 
Aisee nyumba zina issues, l would never imagine kitu kama hicho.
Wakati nakuwa nilifundishwa mchafu ni yule anayekaa na uchafu na wala sio anayeshika uchafu!

umenikumbusha maneno ya mama yangu alikuwa akisema hivi akitupangia kufanya usafi kwenye banda la kuku, ila emagine unakutana barabarani au kazini na mkaka au mdada katokelezea ananukia marashi ya safiii ikitokea unaenda mtembelea au imetokea mmeenda mtembelea anaumwa ukaingia ndani kwake au toilet utashangaa, waweza sema hakai hapo ila watu wa namna hiyo tunao kwenye jamii yetu.
 
Mume wa hivyo unamuachia choo cha bedroom anatumia mwenyewe. Wewe unatumia cha public. Akikuta puu yake imekaukia siku mbili, ukisafisha hatokaa achafue.

Kwani si tunaambiwa mwanaume kama mtoto? Mlelee lakini mfundishie in a hard way, atajifunza tu!
 
ni kweli wee ila skuhizi watu uzalendo hawana yaani kidogo tuu keshampigia shoste ake amsimulie hajui yule anayemwambia anaenda yasambaza maneno mtaa mzima.
sijui kwanini my wee!hiyo story yako mi nimeiangalia kwa jicho lingne kabisaaaa!
beyond tht mizigo ndani ya choo!
KIFUA!JAMANI!KIFUA!KIFUA!KIFUA!
Mungu katuma nundu hiz kifuani ana sababu zake basi tu hatujui!
 
Ha ha ha,,, nahisi ni kufurahisha baraza haiwezekani.. Kuflush kunatumia nguvu gani zaidi ya button au kuvuta kamba...

Japokua wanaume tupo disorganised sometime but hii ya kuto flash Hakunaga
MKATA KIU hata sifurahishi baraza mimi binafsi sijashuhudia live wenye ndoa wanaotegeana kuflash haja zao ila kwa habari hizi mbili nilizozisikia nikaona nishee na wana mmu japo lisemwalo lipo kama halipo linakuja. Pia kama habari hizo hapo juu kama hao wadada niliowasikia watakuwa wamenidanganya na huyu dada wa ofisini kanidanganya basi.
 
Last edited by a moderator:
Mume wa hivyo unamuachia choo cha bedroom anatumia mwenyewe. Wewe unatumia cha public. Akikuta puu yake imekaukia siku mbili, ukisafisha hatokaa achafue.

Kwani si tunaambiwa mwanaume kama mtoto? Mlelee lakini mfundishie in a hard way, atajifunza tu!

hahahahahaaaaa kumuachia choo ya master hiko chumba si kitanuka uvundo looh mie siwezi ntasafisha tuu labda na kumueleza ukweli kwamba ningefurahi angekuwa anaflash haja yake. Vinginevyo atachafua hiko cha master ikifika hatua hakiingiliki tena na yeye anahamia cha public jamani hahahahahaaaaaa. Minafikiri kumuambia kwa upole na upendo itafaa ila si kwa kebehi au dharau waweza kula kipondo na bado asiflash tena akafanya mama nanihii njoo hapa simamahapo na usizibe pua, yaani uwe umesimama akiwa anajisaidia na akimaliza umnawishe kisha uflash kisa tu akukomoe nashukuru mie sina hiyo master maana mmmh
 
MKATA KIU hii ipo mimi nimeshawahi lishudia,ni mshikaji wangu na nilpomuuliza reason akasema ni sehemu ya mapenzi inachochea penzi kunoga.
 
Last edited by a moderator:
sijui kwanini my wee!hiyo story yako mi nimeiangalia kwa jicho lingne kabisaaaa!
beyond tht mizigo ndani ya choo!
KIFUA!JAMANI!KIFUA!KIFUA!KIFUA!
Mungu katuma nundu hiz kifuani ana sababu zake basi tu hatujui!

unamaanisha kuficha siri za ndani kwako, nimekuelewa ndo maana nasema watu sku hz uvumilivu hawana tena wanamwaga mambo yao ya chumbani kwa mashoste wao ilhali hawajui mashoste haohao ndo wanarusha habari zao mitaani, kweli si kila kitu cha kumwaga hadharani na hizo kichen party now days wanagwa vyombo na kukata mauno tuu hamna mafunzo ya kutunza nyumba.
 
Back
Top Bottom