vijimambo vya vyoo vya master bedroom

vijimambo vya vyoo vya master bedroom

Hii ni hadithi au! Yani choo jamaa hakuflash mwezi mzima? Sasa sink mbona linge overflow!
 
Ni hulka ya mtu binafsi kuwa mchafu na mwenye kiburi na dharau. Ni wale wanaodhani kuwa mwanamke yupo kufanya kila kitu cha nyumbani!!!!!!!!
 
Kusikiliza mazungumzo ya watu kwa hila ni tabia mbaya.

sorry kweli nimefanya tabia mbaya nilijitahidi kujizuia nikiwa nimekonsentreti na kitabu changu lakini kadiri walivyokuwa wakiongea ndipo masikio yangu yakawa wazi kwao kuwasikiliza, ingekuwa macho ningefumba.........sasa maskio hayana kifunikio........
 
Yeah,

Hilo ni jambo la jakamoyo lenye kizungumkuti, kwani si kama umetaka kuingilia ila mambo yametokea yenyewe, kwa kadiri ya maelezo.

Sasa basi, maadam yameshatokea na wewe mshawasha wako haukuishia kusikiza tu, bali kama binadamu mwenye utashi umetaka kuwasilisha, na mimi kama binadamu mwenye utashi nawasilisha.

1. Mashoga mnapendana sana, lakini mambo mengine ya ndoa kuwasilisha kwa mashoga mwiko. Mume ni mwandani na msiri wako. Kama mna matatizo kuna namna za kuyamaliza na vikao vyake, na watu maalum wa kuwashirikisha. Kutoa habari za ndani kwa mashoga sijui mume wangu ha flashi choo kunamshusha hadhi mumeo. Mumeo akishuka hadhi na wewe mwanamke umeshuka hadhi kwani mume ni luba la maisha. Hata mkiachana atabaki "alikuwa mume wako". Utamuhadithia shoga mapungufu ya mumeo mangapi? Kesho keshokutwa ukikwaruzana na shoga akaenda kukutolea siri zako za ndani "mumeo mchafu hajui hata ku flashi" utasemaje?

2. Sijaona maelezo yoyote kama mke kamuuliza mume. Na kwa kweli umesema kwamba kwa kadiri ya habari ilivyo mke hajamwambia mume kuhusu kero hii. Hapa kuna tatizo kubwa kuliko ku flush vyoo na lisipotatuliwa ndoa hii haina mustakabali mzuri. Kwa nini mke ajisikie huru kumueleza habari shoga yake na asijisikie huru kumueleza mume wake? Nani kala viapo vya ndoa hapa? Shoga au mume? Kwa nini mke hamuamini mume? Mana hili ni suala la kuaminiana. Ina maana mke akimuambia mume kwamba "Bwana, umesahau kuflush". Halafu aangalie kama atasahau tena itakuwa tusi? Kuna tatizo la mawasiliano? Mke anamuogopa mume? Mke anajishtukia kwamba yule mume aliyemchagua wakati wa uchumba si huyu wa wakati wa ndoa?

Ni muhimu kuwa wazi. Mke asipokuwa muwazi atajulikana. Na hatimaye mwanamme anaweza kuona kitu hakiko sawa akafikiri mke kapata bwana nje tatizo likawa kubwa zaidi.

Kumbe kisa ku flashi choo tu!

Wakati hatujui hata kwa nini mume ha flashi choo. Inawezekana ni mwanamazingira kama Hugo Chavez au "mashikolo mageni" tu!
 
Nauliza tuu wanajamvi pengine kunawanajamvi wanapitia tatizo kama hili je ni sawa kuflash ukimaliza haja zako flash uziache kwa anayekuja aone mmeng'enyo wa vyakula ulioushusha?

sakapal
sidhani kama jibu la hili swali ni gumu. Jibu lake ni simple na straight.

Anayetumia choo kiwe cha kuflash au cha shimo lazima akiache katika hali ya usafi.

Lalamiko kubwa hasa kutoka kwa wanawake ni wanaume kujisaidia haja ndogo kwenye choo cha ku-flash bila kuinua kiti cha choo.

Again tatizo kama hili linaweza kutatuliwa na wahusika.
 
Sasa ukutane na mie, nimekulia Sangabuye, hatukuwa na choo ni mwendo wa kukata gogo porini afu unaji-'shenena chini'

Unaniambia nikisaidia haja ndogo ni-flush? si nitakushangaa? Ila ukinifundisha taratibu nitaelewa tu, kuwa mkojo unaleta harufu mbaya chumbani.

Kuna wengine kutokana na shida ya maji, wanaflash tuu pale wanapokitumia choo kwa haja kubwa. Unajua flash moja inatumia lita ngapi za maji?

Halafu kuna mtindo wa baadhi ya akina dada wanajifanya eti wanaenda chooni kumbe anaenda kujiangalia tuu kwenye kioo au kusoma message kwenye simu yake, halafu anaflash choo as if amekitumia.

Bora nibaki na choo changu mie. Mkija kwangu haja ndogo mkajisadie kwenye shina la mgomba.

wachawi%2Bbugaboo%2B006.jpg
 
Sakapal mwanaume kama huyo pengine ni mwendawazimu!!! Utawezaje hata kutaka mwenzio aone uchafua wako wa ndani? Yaani mtu kuona kimba changu huwa najisikia aibu sana na hakika wife hajawahi kukiona kwa miaka yote hii nimeishi naye!! Nipigieni makofi waaawaaaaa!!! Nasafisha choo kwa kuwa choo kulingana na mama yangu miaka hiyo alikuwa anakiheshimu sana!! Na alitufundisha kuheshimu sana chooni, bafuni na jikoni!! Watoto wote (kike na kiume ni usafi kwa zamu chooni, bafuni na jikoni ikiwemo vyombo kuosha na kufagia uwanja na kudeki). Nimekuwa na hiyo tabia hata nilipokuwa sina mwenzi nilikuwa msafi anzia chumbani hadi jikoni!! Mwenzangu angekuwa member hapa na angeeleza mazuri sana kutetea baadhi ya wanaume!!! Kwa mantiki hii mtu kama kweli unampenda mwenzio hutakubali akereke kwa uchafu wako wa ndani na mambo mengine!! Wanawake ni maua si punda wa kukufanyia kila kitu!!! Ndoa zitadumuje kwa hali hii, je mtakaa muwe na bronze, silver na golden jubilee au mtasikia kwa wenzenu tu? This is so sad, eti mwenzio anaenda kwa mwenzake kuelezea ushuzi wako huu wanaume!!! Aibu sana!! Mwishowe, mtoto umleavyo ndivyo akuavyo na pia achana na mob justice, maana vijiwe navyo kwa upande mwingine vinaponja!! Achana na makudi mabaya kama tabia yake si njema!! Maana ukikutana na watano ambao hawasafisi vijesi vyao na wakikusomesha basi na wewe unaweza fanya!! Kata tawi lilotaka kuangamiza nyumba yako!! Kumbuka mkeo ni mtu wa pekee mtaishi pamoja hata uzee wenu kama mtajaliwa!! Marafiki na vijiwe vitapita tu!!
 
Wote hawako sawa upstairs. Asiyeflush baada ya haja zake na huyo anayeshindwa kumwambia mwenzake akumbuke kuflusoh. Kila mtu kakimbia majukumu. Kuhadithia shosti zake hakumsaidii zaidi ya kumdhalilisha mumewe
 
Yeah,

Hilo ni jambo la jakamoyo lenye kizungumkuti, kwani si kama umetaka kuingilia ila mambo yametokea yenyewe, kwa kadiri ya maelezo.

Sasa basi, maadam yameshatokea na wewe mshawasha wako haukuishia kusikiza tu, bali kama binadamu mwenye utashi umetaka kuwasilisha, na mimi kama binadamu mwenye utashi nawasilisha.

1. Mashoga mnapendana sana, lakini mambo mengine ya ndoa kuwasilisha kwa mashoga mwiko. Mume ni mwandani na msiri wako. Kama mna matatizo kuna namna za kuyamaliza na vikao vyake, na watu maalum wa kuwashirikisha. Kutoa habari za ndani kwa mashoga sijui mume wangu ha flashi choo kunamshusha hadhi mumeo. Mumeo akishuka hadhi na wewe mwanamke umeshuka hadhi kwani mume ni luba la maisha. Hata mkiachana atabaki "alikuwa mume wako". Utamuhadithia shoga mapungufu ya mumeo mangapi? Kesho keshokutwa ukikwaruzana na shoga akaenda kukutolea siri zako za ndani "mumeo mchafu hajui hata ku flashi" utasemaje?

2. Sijaona maelezo yoyote kama mke kamuuliza mume. Na kwa kweli umesema kwamba kwa kadiri ya habari ilivyo mke hajamwambia mume kuhusu kero hii. Hapa kuna tatizo kubwa kuliko ku flush vyoo na lisipotatuliwa ndoa hii haina mustakabali mzuri. Kwa nini mke ajisikie huru kumueleza habari shoga yake na asijisikie huru kumueleza mume wake? Nani kala viapo vya ndoa hapa? Shoga au mume? Kwa nini mke hamuamini mume? Mana hili ni suala la kuaminiana. Ina maana mke akimuambia mume kwamba "Bwana, umesahau kuflush". Halafu aangalie kama atasahau tena itakuwa tusi? Kuna tatizo la mawasiliano? Mke anamuogopa mume? Mke anajishtukia kwamba yule mume aliyemchagua wakati wa uchumba si huyu wa wakati wa ndoa?

Ni muhimu kuwa wazi. Mke asipokuwa muwazi atajulikana. Na hatimaye mwanamme anaweza kuona kitu hakiko sawa akafikiri mke kapata bwana nje tatizo likawa kubwa zaidi.

Kumbe kisa ku flashi choo tu!

Wakati hatujui hata kwa nini mume ha flashi choo. Inawezekana ni mwanamazingira kama Hugo Chavez au "mashikolo mageni" tu!
Kiranga umechangia vizuri sana kwenye 1 na 2 ila hapo nilipoweka green umeniacha hoooiii kwa kucheka hahahahahaaaaa, usishangae inawezakuwa havichekeshi ila mie napenda kucheka kuliko kula loooh. Thanks.
 
Last edited by a moderator:
Kuna wengine kutokana na shida ya maji, wanaflash tuu pale wanapokitumia choo kwa haja kubwa. Unajua flash moja inatumia lita ngapi za maji?

Halafu kuna mtindo wa baadhi ya akina dada wanajifanya eti wanaenda chooni kumbe anaenda kujiangalia tuu kwenye kioo au kusoma message kwenye simu yake, halafu anaflash choo as if amekitumia.

Bora nibaki na choo changu mie. Mkija kwangu haja ndogo mkajisadie kwenye shina la mgomba.

wachawi%2Bbugaboo%2B006.jpg

Khaaaa jamani!!! sasa hapo si mambo hadharani? hapo ndo unaweza ng'atwa na mdudu ukajikuta unakata haja na kukimbia wazi bila nguo looh.
 
hawo ndiyo ananunua chupi ikichafuka anatupata ananunua nyingine
 
Unaweza ukaikuta kwenye choo sasa hii ni mara moja lbda kwa muuuda, but hii ya mtu ndio tabia yake na ndio unaishi naye 7 days a week, 12 months a year x miaka utakayoishi naye mh! si unyanyasaji wa kisaikologia huu !

Maamuzi ya busara ni kwenda kumpima akili, wajua tunatembea na vichaa halisi. Note "Kila binadamu ni kichaa ila aliyezidi ukichaa ndie tunaemwona tofauti na sisi" Ukitaka kuamini angalia watu wakimpiga mwizi hadi kufa, kuna akili timamu hapo?
 
wenzio tulifanikiwa..siyo kila mtu kafika saa 12 kama wewe hadi huoni

Loooooooooooooooh!!!!!!!!!!!!!!!! sijacomment hukufanikiwa ila ni wazi mwanamke akishafikisha 30+ ni wazi anatafuta mme na sio wa aina gani, same same kwa mwanamme akishafikisha 40+ anatafuta mke na wala sio wa namna gani. Ni muhimu kufanya maamuzi ya kuoa/kuolewa ikiwa mapema kwani wengi walidanganyika na starehe za ujana leo wanajutia. ILa pia sikuchelewa mie by saa 6 adhuhuri nilikuwa nimemaliza machaguo. Sorry kama ulikwazika my comment was GENERAL.
 
Maamuzi ya busara ni kwenda kumpima akili, wajua tunatembea na vichaa halisi. Note "Kila binadamu ni kichaa ila aliyezidi ukichaa ndie tunaemwona tofauti na sisi" Ukitaka kuamini angalia watu wakimpiga mwizi hadi kufa, kuna akili timamu hapo?

Mimi nilishasema ukipata mchumba pima ukimwi, malizia na kupima akili
 
Mimi nilishasema ukipata mchumba pima ukimwi, malizia na kupima akili

Tena wakati huu wa vuguvugu la katiba mpya ndio wakati muafaka ili tuliweke kisheria kabisa, ili huyu jamaa yetu awe sample baada ya katiba kupitishwa.
 
Tena wakati huu wa vuguvugu la katiba mpya ndio wakati muafaka ili tuliweke kisheria kabisa, ili huyu jamaa yetu awe sample baada ya katiba kupitishwa.
Ha ha we Tamatheo sasa unataka kuanzisha mandamano ya wababa hapa nchini, yaani katiba itamke wazi kuwa wa baba wapimwe akili kabla ya ndoa
 
Last edited by a moderator:
nyumba kuta nne jamani lol!na bati lake juu!
Yaaaani, Hakuna USIRI wa NDOA!! siku hizi , kila kitu wanawake tunahadithiana, kwani angesafisha halafu akamwambia kuwa kitendo hicho alichofanya hakipendi ingekuwaje? na akumbuke huyo amwambiaye ataenda kuyasambaza mtaa wooote , so itajulikana kuwa mumewe ni mchafu huwa akisha PUU " haflash. KIFUA Mungu alikiumba kusitiri vitu vikubwa vya ndani ya NDOA na si upambo! TUWE NA USIRI WA NDOA ZETU JAMANI!!!! Loh!
 
Kwanza mi mwenyewe naona aibu mtu kuona uchafu niliotoa.....
 
Back
Top Bottom