Habari zenu wana MMU,
Naombeni niwasimulie kisa hiki nilichokisikia live..................
.............baada ya kuona mazungumzo yanaendelea nikawa nimeshikilia kitabu tuu huku nikiwasikiliza kwa makini na kufuatilia maongezi yao. Walikuwa wadada wawili wa makamu ya 25-28 wakiongea(kwa maongezi yao na pete vidoleni, wanaonesha wameolewa). Mdada mmoja ndie alikuwa akilalamika kuwa anakerwa na tabia ya mumewe kutosafisha choo mara baada ya kukitumia choo chao cha master bed room. Kwa maelezo yake wakati wako wachumba akienda kwa mchumbawake anakuta toilet safi ila tangu waoane usafi wa nyumba yao nzima ni yeye mwanamke pamoja na usafi wa master room yao. Sasa akagundua tabia aliyoianzisha mumewe ya kujisaidia bila kuflash wakati choo ni cha kuflash na maji yapo muda wote, kiufupi akitoka bafuni au chooni basi ujue hadi usafishe ndo panafaa kutumika tena.
Sasa akawa anajiuliza inamaana mumewe anafurahia hali ya uchafu? anajiuliza je mumewe akiwa anataka kujisaidia na kukuta choo kichafu atachukuliaje? Kwa kadiri ya maongezi yao hajamwambia mumewe juu ya kinachomkera kwani hataki mumewe afanye usafi au wapangiane zamu ila anataka atleast awe anaflash tuu kila baada ya kujisaidia haja zote. Mdada mwenzie akamwambia mmmh ndo umvumilie mumeo ndo kwanza mna mwaka mmoja wa ndoa.
Nilijikuta nimewasikiliza maongezi yao huku nikigelesha kusoma kitabu nikakumbuka tena hapa job kuna dada mmoja alishanisimulia kisa cha ndoa moja anayoifaham tena hata harusi yake alihudhuria hiyo ndoa ilibaki almanusura ivunjike. Kisa ilikuwa hii hii choo cha master, mke aliumwa akalazwa hospitali mwezi mzima kumbe huku nyuma mumewe alikuwa akiingia chooni haflash, mkewe aliporuhusiwa na kukuta hali ile akagoma kukisafisha na akakifunga kisitumike ikabidi wahamie choo cha public kwenye nyumba yao kwani hicho kilikuwa kinasafishwa na house girl. Nilishangaa mno sasa niliposkia haya mazungumzo jana ninasema inamana hili ni tatizo na nikajiuliza kwani wanaume waliooa hawawezi kuflash baada ya kujisaidia ilhali maji yapo basi haja ashushe mwanaume ila kuflash choo aje aflash mkewe?
Mie na kwangu tangu nimeolewa miaka 14 iliyopita tunakaa kajumba ketu kadogo vyumba viwili choo kimoja hamna master na usafi nasimamia mwenyewe wala sijawahi pata hii kadhaa. Nauliza tuu wanajamvi pengine kunawanajamvi wanapitia tatizo kama hili je ni sawa kuflash ukimaliza haja zako flash uziache kwa anayekuja aone mmeng'enyo wa vyakula ulioushusha?