Blender
JF-Expert Member
- Mar 5, 2022
- 4,256
- 6,862
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye @Nnauye_Nape amesema baadhi ya Vijana Wabunifu wa TEHAMA imewabidi wakasajili ubunifu wao katika Nchi za jirani sababu ya kutokuwepo kwa Sera ya Kampuni changa za TEHAMA (Startups) nchini.
“Kwa muda kidogo Sekta hii imekuwa haina mfumo mzuri wa kisheria wa kuratibu ubunifu wa Ki-TEHAMA hapa nchini na matokeo yake tunao Vijana wa Kitanzania ambao wanafanya ubunifu lakini wanalazimika kwenda Nchi jirani kusajili ubunifu wao na kuufanya ubunifu wao ufanye kazi na mfano mzuri ni Kijana mmoja wa NALA alifanya ubunifu mkubwa hapa na ikabidi aende kwa majirani zetu kusajili ubunifu wake”
Waziri Nape ameyasema hayo wakati akiongea na Vyombo vya Habari baada ya kufunga Kikao na Wadau Kujadili Ushirikiano wa Maendeleo Juu ya Sera ya Kampuni Changa za TEHAMA (Startups) Tanzania, Jijini Dar es Salaam.
“Kama Serikali tukasema inabidi tuwe na mfumo mzuri utakaotambua bunifu za hawa Vijana lakini pia uweze kuzilinda bunifu hizo ili pia waweze kuvutia uwekezaji nchini, tumekaa tumekubaliana na Wadau mbalimbali kutoka ndani na nje Nchi, tumeweka msingi na sasa tuko tayari kuendelea na hatua inayofuata”
#MillardAyoUPDATES
Kumbuka hiyo nchi jirani ndio wamekubali huduma ya starlink, Huku yeye akimlitea zengwe tajir #1 duniani kwamba afungue ofisi Bongo ili kuwe eti kuwe na usalama wa data Kwa watumiaji.
Na startups nyingi kama costech ni wapiganaji Tu 😂