Vijana walio Dar wilaya ya Temeke tukutane

Baraka sheni

JF-Expert Member
Jan 5, 2015
470
193
Habarini wapendwa nina wazo kwa wale vijana wenye nia ya kuthubutu na wenye mawazo au biashara au wamejiajiri tukutane na tuunde kikundi.

Lengo la kikundi kwenda kupata Mkopo wa Halmashauri.

Yawezekana kila mtu akawa na biashara yake au ya pamoja ila kama kila mwanakikundi atakuwa na biashara yake itabidi awe na wadhamini ambao watarejesha hela pale atakapo shindwa kurejesha.

Binafsi licha ya taaluma nilizokuwa nazo pia ni mbunifu na mtengenezaji wa viatu vya kimasai na mikoba.

Karibuni tuchangie mawazo
 
Mkuu hata mimi nipo wilaya fulan nje ya Dar es salaam,hii kitu niliambiwa na rafiki yangu nikambishia nikaona ni ushenzi mtupu.

Bas wao walijiunga wakiwa sita wakasajiliwa na hati ya kikundi wakapewa,wa wilayan walikuja kukagua kikundi (ni kikundi cha bodaboda watu 6)

Huwez amin mwez uliofata waliitwa kila mmoja akapewa pikpik mpya na acc yakikund ikabak inasoma million 5.hadi saiv madogo wanapika kazi.nasikia mnarejesha baada ya mwaka.

Nilivyoona hivyo na mimi nikadandia kikund kingine cha vifaa vifaa vya umeme tukawa 6 tukaanza hatua za usajil hadi mwisho kufungua acc yakikund .kufikia saiv ishanitoka kama elfu 50,ndo tunasubilia tuone kama tutafanikiwa.

Pesa itakayomtoka kila mwanakikundi ipo hivi (kulingana na sehem uliyopo)

Passport 2, 3000
nauli (kuwachangia viongoz kama ni mbali)
acc ya kikundi elfu 30.kila mmoja 5k kwa watu 6.
acc ya maafa ,(sikumbuk ila kila mmoja alitoa elfu 6)
kitambulisho cha mjasiliamal 20k.
mkishamaliza kila kitu ndo mnasubilia wakae kikao .

Kuna kikund kingine cha watu 6 waliingiziwa million 12.
kuna kikundi cha akina mama walipewa cherehan kila mmoja.

NB:Mkianzisha kikund kama akiwemo msichana hata mmoja kuna uwezekano mkubwa wa kupata (gender issues)

Kama kuna sehemu hujaelewa niulize .

Mkumbuke pia hii aliitamka mheshimiwa Jaffo sikumbuk mwaka alisema kila mwisho wa mwaka kila halmashauri iwe inatenga asilimia 5%-10 % ya mapato ya ndani ili kuwasaidia na kuinua vikundi vya vijana pamoja na akina mama.
je kila Halmashauri inatoa hiyo mokopo
 
Habarini wapendwa nina wazo kwa wale vijana wenye nia ya kuthubutu na wenye mawazo au biashara au wamejiajiri tukutane na tuunde kikundi.

Lengo la kikundi kwenda kupata Mkopo wa Halmashauri.

Yawezekana kila mtu akawa na biashara yake au ya pamoja ila kama kila mwanakikundi atakuwa na biashara yake itabidi awe na wadhamini ambao watarejesha hela pale atakapo shindwa kurejesha.

Binafsi licha ya taaluma nilizokuwa nazo pia ni mbunifu na mtengenezaji wa viatu vya kimasai na mikoba.

Karibuni tuchangie mawazo
Njooni huku keko machungwa tufahamiane
 
Back
Top Bottom