Vijana njooni Ughaibuni mtafute mitaji bongo ngumu

Vijana njooni Ughaibuni mtafute mitaji bongo ngumu

Status
Not open for further replies.
Najua wazee wakutuponda team box FC wazee wakago a.k.a wabeba boksi mpo na mmejipanga vyema kushambulia Uzi huu kwa makombora mazito Kama bwana Hamza Mzee wa salenda bridge.

Lakini ukweli utabaki kuwa hapo bongo kwa sasa hivi pamekuwa kama tanuru la moto kwa vijana na Cha ajabu jitu Lina miaka 28-35 utakuta limemaliza midigrii yake na mi masters na job ni za hovyo afu bado Lina ndoto za kutoboa kirahisi hapo ukweli mchungu ni kwamba hizo ni ndoto za abunuwazi sababu kutoboa bongo sahiv imekua bahati na sio kwa kutegemea mipango na maarifa havita tusaidia Chochote ndani ya Tz

Mama Hana huruma na tawala za kiafrika hazinaga huruma kwa raia katika kutekeleza maazimia Yao.

Imagine mtu ndani ya miezi mitatu minne naweza save 80k SEK baada ya mahitaji yangu muhimu na bills zote,

UGHAIBUNI pesa ipo nyie endeleeni kuleta ubishi wa kung'ang'ania msipopendwa.

View attachment 1911080View attachment 1911081
Hii hela ya kupewa bure hujaifanyia kazi. Kwa viwango vya Sweden, hiyo siyo hela nyingi ndiyo maana wamekupa bure. Leo unaringa lkn ujue kazi itaanza baadaye ukiacha kuwa tegemezi wa pesa za bure. Utaishia kuwa maskini tu huko unamiliki nguo na viatu
 
Mbona hujatoa hatau za kufika uko?tunaona tu mafanikio.
 
Ifike kipindi wa Tanzania tuwe kama wezetu wa Naingeria tubebane tupeane michongo...mwisho wasiku tuje tulisaidie Taifa letu...
Tatizo kubwa hapa ukitaka kuwapa michongo watu; wanadhani unataka kuwapiga.
 
kwa hiyo mwanangu ndani ya miez mitatu una zaidi ya 20M na hapo ushatoa xpenditure zote? kweli ughaibuni patamu.
 
We tafuta tu, siku ukirudi na hiyo mjihela utarundikiwa mikodi kibao au ukutane wa wazee wa kung'ang'ania wakuchomoe zote kama Hamza
 
😏😏😏 kweli Tanzania ngumu sana ukiweza kuishi Tanzania hata sweeden utaishi na hata jehanamu. Maana nauli ya kwenda huko tu ni mtihani plus vibali vya huko.
Je unaruhusiwa kukaa muda gani mpaka visa kuexpire,na je? Unafikia wapi.
Mwisho una work permit.
Oredhesheni hivi ajibu mtoa mada?

Maana mtoa mada anaturingishia tu wala hatupi channel ya kupita🚶🚶🚶🚶🚶🚶
 
Hongera mkuu mzigo ushatema nn (ISS)...?

Ntakucheki wkend hii
 
aliwahi kuweka uzi hum,huko sweden maisha magumu bora arudi bongo .....wadau wakawa wanampa maneno ya kijasiri akomae huko huko,aliweka hadi picha ya passpoti na mihuri ya visa.
Kumbeee aisee mkuu umenifungua masikio
 
Sawa mkuu , ndio maana tukafunguwa uzi huu hapa... ili tuweze kupeana taarifa nzuri tunaotaka kusaka maisha nje... karibu ufnguke na sisi tunufaike kupitia wewe kwa michango na mawazo yako!!

Karibu tuweze kushare fursa mbali mbali zinazopatikana nje ya mipaka ya nchi yetu ya TANZANIA.

Uzi huu ni maalumu kwa wote wenye roho nyeupe na mawazo chanya yatakayotuwezasha kuleta maendeleo katika nchi yetu..

kwa kuzifukuzia fursa nje ya nchi.

Tatizo... Fursa za Nje ya Nchi: Scholarship(Kusoma), Ajira/kujiajirina Biashara/kuwekeza
 
Ifike kipindi wa Tanzania tuwe kama wezetu wa Naingeria tubebane tupeane michongo...mwisho wasiku tuje tulisaidie Taifa letu...
Tuanze na wewe mkuu toa mwongozo
 
Sa mbona unatufokea na kutuita jitu, si useme tu kistaarabu! Bongo kugumu njooni huku kuna a,b,c uwape na mbinu za kufika huko.

Huyo hawezi kutoa ABC halafu kutoka muhimu lakini sio kila aliebaki ni fala hapana, asidharau waliobaki Bongo kwa kuhisi wote wanawaza sawa ni kosa kwa baharia mpambanaji kuwadharau watafutaji,
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom