Vijana msidanganywe, ukiwa na pesa utapata mwanamke umtakaye

Chini ya Jua ,Pesa inaweza kuletea mwanamke yoyote unayemtaka, ila Haitakaa kukuletea mwanamke mwema.

Lkn pia Bado chin ya Jua, Umasikin utakuletea Mwanamke yoyote unayemtaka lkn hautakaa kukuletea Mwanamke mwema.
Mkuu, unamadini Sana, nakuheshimu, kama unataaluma flani niheri ukaandika vitabu, au ukawa mshauri
 
Na huu pia ndo ukweli.

Unajua wanaume masikin hapa Dunian, ndo wanaamin kua wao wanamapenz ya Dhati..nakwamba wao ndio wakipendwa wanapendwa kwa dhati.

Ukweli nikua, Tajiri anaweza kupendwa kwa dhati au akapendwa kuchunwaa km.buzi.

Masikin pia anaweza kupendwa kwa dhati au akapendwa kuchunwa tu nando hapa Masikin anakua na madeni chungu nzima,kila mahali amekopa

Hawa wote wawili hata kama wameoa, bado wake zao wanaweza kuchapwa tuu... Wa tajiri akachapwa na masikin..wamasikin akachapwa na wa Tajiri.

Inshu ni ndogo sana... Wanawake wanaishi kwa kihisia na kuona .

Kuna tuvitu fulan huwa vinawawewusha sana wanawake ukiwa navyo uwe una pesa au hauna..

Utu tuvitu wasipoviona kwako hata kama unapesa au hauna, aisee watakuliza sana.
Nituvitu gani huto mkuu!tupe nondo
 
Mkuu,mada ninzuri Sana,je hyo mipaka nikatika uashareti Tu au namambo mengi,pia,hujaelezea mbinu zipi tuzifanye ili kuweza kumuwekea mipaka, mwanamke,iwe mchumba au mke,or whatever
Mkuu nimekupata, nitaandika kuhusu hayo... Ila kwa kuwaelewa zaidi, usiache pitia nyuzi zangu
 
Kijana, kijana kijana.
Kwanini una roho mbaya namna hiyo we mleta uzi?? Yaani huijali kabisa jinsia ke!!?

Yani yeye ndo aje kuteseka na wewe ili tu kujionesha uwife material kwako, na vipi wewe kama sio mume mwema kwake, ama lah vipi kama usipopata kabisa izo pesa mpaka kufa kwako/kwenu.

Mdada usichezee uzuri wako kwa kudate na maskini wasio na pesa, maskini watadate na hao vigagula, kama unajiona ni mzuri hata kwa kiasi kidogo usitoe nafasi kwa maskini kukumiliki.
Labda itokee janja janja coz janja janja kwetu wanaume ni kawaida na utaliwa tu na wajanja wasio na pesa.
Ila msifate huu ushauri wa huyu mwamba utawapoteza.
 
SUALA LA MWANAMKE MWEMA KAMA MKE MWEMA LINABAKI PALEPALE, MKE MWEMA ANATOKA KWA BWANA.....
Hapa ndipo ukweli ulipo.....kuwa masikini sio sifa ya kupata mke mwema na kuwa na ukwasi sio sifa pia ya kupata mke mwema.

Omba Mungu akupe mwenza sahihi.
 
Nimekua nikisoma thread tofauti humu JF za wanaume wakilalamika kuhusu kutendwa na wanawake zao kisa hawana pesa kisa hawana uwezo wakuwahudumia hao wenza wao, nk

Nimeona wengi kwenye comment wakishauri watu watafute pesa sana na kwa bidiii ili kuepuka hayo yote, kila ushauri mzuri ni vyema ukautendea
Ukweli mtupu. Ukiwa na pesa utapata mwanamke yeyote wa kutumia lakini sio mke sahihi
 
Mapenzi ni pata au potea mambo ya pesa,elimu,malezi na makuzi ni vionjo tu vya mapenzi
Unaweza ukawa na pesa na elimu juu ila bado ukakutana na Pata au Potea bas
Ni matajiri au ni watu wangap wenye pesa na bado mapenzi yanawatesa
Ukiwa huna pesa unaweza zani pesa ndo solution ila hapana utatoa pesa zako wataenda kula wanaume wengne
Mapenzi ni pata potea Mapenzi ni mchezo mchafu
 
Haya mambo ubaya wake kila mtu anatembea kwenye formula tofauti.

Tukikutana wanaume 50 hapa wenye ma wife material utashangaa kuona kila mmoja ananjia yake alivyopata wife.
 
Nimekua nikisoma thread tofauti humu JF za wanaume wakilalamika kuhusu kutendwa na wanawake zao kisa hawana pesa kisa hawana uwezo wakuwahudumia hao wenza wao, nk

Nimeona wengi kwenye comment wakishauri watu watafute pesa sana na kwa bidiii ili kuepuka hayo yote, kila ushauri mzuri ni vyema ukautendea kazi na katika mashauri mengi watu wanayoyatoa mimi niliamuaga kuchukua ule ushauri wa "tafuta pesa kwanza" mengine yote yatakuja.

Vijana wenzangu niwahakikishie muda mzuri wa wewe kutafuta mpenzi/mke/mwenza/mchumba ni kipindi hiki ambacho huna mbele wala huna nyuma huelewi mchana utakula nini wala kesho utatokaje kwenda barabarani, hiki ndio kipindi muafaka kwa jambo lako hilo la kutafuta mwenza wa maisha yako.

Usije ukaacha kunisikiliza mimi mwenzako nasema nina uthibitisho wa asilimia 99.9% kama unataka mke wife material mtafute sasa ukiwa na hali hiyo ngumu hivyo hivyo, wakati unaumiza kichwa usiku ukifika ule nini naomba usisahau kuwaza wapi utapata mke mzuri kwahiyo endelea kutafuta kama ni kutongoza tongoza kama ni kuimbisha imbisha usisubiri upate pesa kama unataka kweli "mke wa maisha yako"

Nyie mnaowaambia wenzenu watafute pesa kwanza kisha mke atafata, mnawadanganya nawahakikishia, wenye pesa hupata wanawake wa kuwachezea na kuwaacha hao wapo wengi, lakini kumpata mke kweli kweli ndugu zangu pesa hai hitajiki.

KWANINI NASEMA HIVI?

Mke kweli hashawishiki na wingi wa pesa zako na tena ukiwa na pesa kumshawishi mwanamke wa kweli kuwa ni kweli unampenda mjomba kibarua chake sio kidogo mama angu mi nawambia.

Real wife material Hashawishiki na magari bro, hashawishiki na hayo mabiashara my brother nawambia hivi kama kweli unataka mke na unataka usije kuchelewa kuoa watu tukakunyooshea kidole, huu muda ambao uko hovyo usisahau msaka wa ubani wako, achana na pesa we msake ataeweza kuishi na wewe ktk hali yako hiyo mbovu kisha msimame pamoja.

Ila ukisimama peke yako, ukawa na pesa ukakamilika kila idara Ishu ya kumpata MKE BORA ni kipengele kitakachokuchukua si chini ya 5yrs, we endelea kuwasikiliza hao wanaokwambia saivi, Tafuta pesa.
Pesa unanunua ngono Ila sio mtu ama huyo wife materials.
Ila wale materialistic,wapenda fursa ama opportunistic girls like Hawa manka huwa wanapatikana ukiwa na pesa zako. Yaani ukiwa na pesa mfano huko kwa waliosoma Moshi unaoa ukoo mzima usikute mpaka mamkwe ukapita naye.
Yaani pesa yako tu wapendwa huko kwa wajanja na wasomi na watafutaji namba moja Tanzania na dunia nzima.
Ujue hata Elon musk anayo damu ya kimangi fuatilia nyuma sana.
So inajulikana kuwa pesa unanunua Ila ukiwa hauna kitu ndo wapata marafiki wenye utu na sio pesa na magari yako
 
Back
Top Bottom