Vijana msidanganywe, ukiwa na pesa utapata mwanamke umtakaye

Hamna kila kitu ni kujifariji kulingana na na Hali ya maisha uliyo nayo , Mwenyezi Mungu amebarki kila level inakuwa satisfied , Kama huna hela kuna type ya wanawake utawapata na ni wife material Kwa level hyo ya kutokuwa na hela, kama Una hela za Kati pia kuna wanawake level hyo na..
Na huu pia ndo ukweli.

Unajua wanaume masikin hapa Dunian, ndo wanaamin kua wao wanamapenz ya Dhati..nakwamba wao ndio wakipendwa wanapendwa kwa dhati.

Ukweli nikua, Tajiri anaweza kupendwa kwa dhati au akapendwa kuchunwaa km.buzi.

Masikin pia anaweza kupendwa kwa dhati au akapendwa kuchunwa tu nando hapa Masikin anakua na madeni chungu nzima,kila mahali amekopa

Hawa wote wawili hata kama wameoa, bado wake zao wanaweza kuchapwa tuu... Wa tajiri akachapwa na masikin..wamasikin akachapwa na wa Tajiri.

Inshu ni ndogo sana... Wanawake wanaishi kwa kihisia na kuona .

Kuna tuvitu fulan huwa vinawawewusha sana wanawake ukiwa navyo uwe una pesa au hauna..

Utu tuvitu wasipoviona kwako hata kama unapesa au hauna, aisee watakuliza sana.
 
Wewe uko kinyume na wanawake wengi unaowasema.
Nampenda YYY yuko diploma 2 chuo kingine ila anadai hataki tena mwanaume wa kuanza nae kwa vile aliyekuwa nae waliachana baada ya kupata hela wakiwa wote na akamuacha. So huyu YYY ananambia kabisa nitafute demu wa kuzuga nae ili nikifikia wakati wa kuoa nimtafute maybe atakuwa tiyari. Huyu ananililia shida zake ndogo namsaidia siku zote

Hapa napo kuna RRR huyu anadai hawezi kuwa na mimi kwa vile sijawa stable, mambo yakichangamka nitamkimbia. Outing zangu anakubali, dinner nights na zawadi nikijitakia ingawa hadai hela.

Ex wangu aliniacha kwa vile nilikuwa bahiri kwake ila bora hela ningempa maana alikuwa ananipa amani ya nafsi na hakutaka hela nyingi, cha ajabu za kwake nilitumia. Badae nikamfidia hela zake zote kwa namna tofauti. Baada ya huyu sahivi naweza toa hela kwa girlfriend

Sasa nimeamua hivi: Mapenzi ya kweli niliyoishi nayo nyuma yashapotea na sasa nakutana na majambazi. Na kwa vile mimi ni bepari sio mjamaa nitawapa hizo hela wanazotaka. Naona advancement kwenye mapenzi pia na kwa vile tuna globalization mimi nitaishi nayo tu. Upepo unakovuma ndio naelekea sitaki vunjika kushindana nao
 
Chini ya Jua ,Pesa inaweza kuletea mwanamke yoyote unayemtaka, ila Haitakaa kukuletea mwanamke mwema.

Lkn pia Bado chin ya Jua, Umasikin utakuletea Mwanamke yoyote unayemtaka lkn hautakaa kukuletea Mwanamke mwema...

Nina gari, nina pesa, nina maisha lkn mbona Yule demu ananikwepa sana?
Big mind
 
....aisee....haya mapenzi sio hesabu hivyo hayana kanuni, yeyote anaweza pendwa awe na pesa au asiwe nazo.

...Kusema masikini atapendwa na tajiri atachunwa ni kukariri kwani yeyote anaweza pendwa na yeyote anaweza kuchunwa.
 
Uzi mtamu nitaurudia kesho
Ila wanawake hakika mnachanganya sana akili zetu sisi watawala wenu
 
Mnajichanganya tu.
Huwa sipend kucomment bali huwa nawaquote wenzangu ila leo nitacomment kuwakumbusha mnachosahau au msichokijua kwa baadhi yenu Mwangalie mwanamke anaetoka kwa tajiri na kuliwa na masikini sio yule ambae masikini analala akiota siku moja kummiliki bali ni ile tu simva kakosa nyama kala majani rudi umtazame mwanamke anaemzingua muhuni kabwela kitaa hampi mzigo ni pisi kali tena mbichi ikifika kwa papa mimoney inapanua mpaka hata ukishuhudia hautaamini.
Duu kweli ugonjwa haupon kizembe bado nimekuquote mkuu shumee mm!
 
Nimekua nikisoma thread tofauti humu JF za wanaume wakilalamika kuhusu kutendwa na wanawake zao kisa hawana pesa kisa hawana uwezo wakuwahudumia hao wenza wao,nk

nimeona wengi kwenye comment wakishauri watu watafute pesa sana na kwa bidiii ili kuepuka hayo yote,kila ushauri mzuri ni vyema ukautendea kazi na katka mashauri mengi watu wanayoyatoa mimi niliamuaga kuchukua ule ushauri wa "tafuta pesa kwanza" mengine yote yatakuja.

Vijana wenzangu niwahakikishie muda mzuri wa wewe kutafuta mpenzi/mke/mwenza/mchumba ni kipindi hiki ambacho huna mbele wala huna nyuma huelewi mchana utakula nini wala kesho utatokaje kwenda barabarani,hiki ndo kipindi muafaka kwa jambo lako hilo lakutafuta mwenza wa maisha yako.

usije ukaacha kunisikiliza mimi mwenzako nasema nina uthibitisho wa asilimia 99.9% kama unataka mke wife material mtafute sasa ukiwa na hali hiyo ngumu hivyo hivyo,wakati unaumiza kichwa usiku ukifika ule nini naomba usisahau kuwaza wapi utapata mke mzuri kwahiyo endelea kutafuta kama n kutongoza tongoza kama n kuimbisha imbisha usisubiri upate pesa kama unataka kweli "mke wa maisha yako"

nyie mnaowambia wenzenu watafute pesa kwanza kisha mke atafata,mnawadanganya nawahakikishia,wenye pesa hupata wanawake wakuwachezea na kuwaacha hao wapo wengi,lakini kumpata mke kweli kweli ndugu zangu pesa hai hitajiki.

KWANINI NASEMA HIVI ?

Mke kweli hashawishiki na wingi wa pesa zako na tena ukiwa na pesa kumshawishi mwanamke wa kweli kuwa ni kweli unampenda mjomba kibarua chake sio kidogo mama angu mi nawambia.

Real wife material Hashawishiki na magari bro,hashawishiki na hayo mabiashara my brother nawambia hivi kama kweli unataka mke na unataka usije kuchelewa kuoa watu tukakunyooshea kidole,huu muda ambao uko hovyo usisahau msaka wa ubani wako,achana na pesa we msake atae weza kuishi na wewe ktk hali yako hiyo mbovu kisha msimame pamoja.

ila ukisimama peke yako,ukawa na pesa ukakamilika kila idara Ishu ya kumpata MKE BORA ni kipengele kitakachokuchukua si chini ya 5yrs,we endelea kuwasikiliza hao wanaokwambia saivi,Tafuta pesa.

SEASON 5 wife material hashawishiki na pesa wala magari, ila anashawishika na mwanaume makini anayeweza kubeba majukumu ya mume/ubaba. Mwanaume anayeweza kusimamia ustawi wa mke na mali kwa gharama yoyteyoyte ile iwe ya hali au mali.

Ushauri wako utawasaidia sana vijana kama utawaambia watafute pesa na watafute mali lakini wasivitumie kama zana au kishawishi wanapotafuta mke. Tena hata pale wanapota mke waendelee kutafuta mali ili kuweza kuendelea kuboresha familia zao.

Sijasema kama huna mali usitafute au huwezi kupata mke aliye bora. Ila unapotafuta mke wewe kama mwanaume ujue kabisa unaingia kwenye jukumu zito la kusimama kama kiongozi wa familia. Na kama kiongozi na kichwa cha familia na mlinzi wa familia yako lazima uwe mwanaume unayeweza kuiendesha familia kijamii na kiuchumi. Na ili uweze kuwa kiongozi bora lazima uweze kufanya maamuzi yahusuyo maendeleo ya familia yako na mengi ya hayo maamuzi huwezi yafanya bila kuwa na uwezo wa kifedha.

Wadogo zangu wa kiume, kaka zangu na wanangu tafuteni pesa, tafuteni mali kwa bidii. Unaweza kupata mke anakupenda kweli ananiheshimu kweli, anafanya majukumu yake kama mke sawasawa lakini utakaposhindwa kufanya majukumu yako ukambadilisha huyo mwanamke kabisa na mkashia kushindwana.

Tafuta pesa kabla hujaoa, tafuta pesa ukiwa umeshaoa. Usitumie pesa kumpata mwanamke unayemtaka maana utapata hata wale wasiofaa ila tumia pesa kumaintain mwanamke sahihi uliyempata. Mtunze, muongoze, mlinde, mfundishe, endelea kumpa sababu ya kuona wewe ni mwanaume bora dunia kuliko mtu mwingine yoyote

mrangi East Wind
 
Mimi pesa ninayo( angalau kidogo) lakin sijawahi pata mpenzi wala kuexprience love Tangu nimezaliwa.

It's very sad indeed.
May be siko lucky nawasichana
 
Back
Top Bottom