Hakuna mwanamke aliyeandaliwa kuwa mke siwashauri vijana kukurupukia ndoa

Loading failed

JF-Expert Member
Sep 14, 2023
1,945
5,850
Habari za asubuhi ndugu zangu. ni kweli kuoa na kua na mke wakati mwingine ni jambo la heri na baraka ila kwa upande mwingine linaweza likawa ni jambo hatari, la maangamizo na la kujutia sana siku zote za maisha yako kutokana na mabinti wengi kutokuandaliwa kuwa wake na mama bora tokea enzi za utoto na ukuaji wao.

Ndugu zangu katika mfumo wa maisha ya sasa wanawake na mabinti wengi sana hawajaandaliwa kuwa wake na hii ni kutokana na mfumo wa maisha ya kwao waliolelewa tokea enzi na enzi, mabinti wengi mno wameishi maisha ya kuigiza na kufanyiwa kila kitu ikiwemo na wazazi wao, mashuleni, vyuoni , nyumba za ibada na kwenye taasisi na mashirika mbali mbali kwa namna zake na jinsi zake.

Unakuta binti amelelewa maisha ya kufuliwa,kuoshewa vyombo, kupangiwa nguo na madaftari kabatini na kwenye begi, kupelekwa shule na vigari vya kusubiria au na wazazi wake, kupewa kila kitu pamoja na poketi money ya kutosha, binti amezoeshwa kula vitu vya super market hata kibandani hajawahi kwenda, binti hajazoeshwa kula dagaa mchanga yeye anajua ni dagaa za kupikia chakula cha mbwa wala hajazoeshwa kufagia uwanja, kung'oa majani yanayozunguka nyumba na wakati mwingine hata kutengeneza kabustani cha hapa na pale,

Mbaya kabisa unakuta mwanamke /binti hajawahi tumia jiko la kuni au mkaa, hajawahi kukata hata mboga, kuchambua mchele, kuchambua maharage au kuchambua choroko unategemea hizo kazi akizikuta ndani ya ndoa atawezana nazo, binti hajalelewa maisha ya maji ya kikatika anapaswa kubeba ndoo na kwenda kuyafata mbali huku kajitwika kichwani yeye anajua yakiisha yataletwa na gari au housegirl atafata na atatumia tuu kufulia mpaka nguo zake za ndani ,kuoga na kutumia apendavyo akijua mfataji yupo je unategemea kwenye ndoa atakuwaje.

Binti amelelewa kwenye maisha hajui hata kupika chochote kazoeshwa kupikiwa na kufunuliwa tuu dishi na kujichukulia chakula, hajawahi hata kupika ugali wala kuchemsha chai asububi wazazi wanywe, binti kazoeshwa tokea akiwa chekechea anakuta kila kitu kaandaliwa kwanzia chai ,nguo , madaftari, mswaki, kisahani cha shule na kigari cha kumpeleka shule na kumrudisha, tena mwanamke kazoea alipokua elimu za juu anakula magengeni chochote atakacho unategemea atakua mke

Ndugu zangu vijana binti kazoeshwa akiwa likizo kutoka masomoni yeye ni kuamkia kwenye Tv kwanzia asubuhi ,mchana ,jioni mpaka usiku unategemea utawezana nae isitoshe binti tokea awe kwao hajawahi mbadilisha nepi mdogo wake , kumvisha wala kumuogesha kazoeshwa ni kazi ya housegirl je, unatarajia huyo atakua mke na mama wa watoto

Mbaya kabisa unakuta wazazi na ndugu wanamuambia kabisa binti yetu ukiolewa hapa ni kwako hatujakufukuza, unaweza kurudi muda wowote na tutakupokea je unatarajia nini kwa huyo mwanamke na waambia?

Vijana swala la kuoa sio la mchezo mabinti wa kuoa sasa hivi ni wachache sana kutokana na mfumo wa maisha ya kwao na penginepo katika kaya tofauti tofauti huenda hakuna kabisa , wanawake hawaja lelewa kuwa wake wala kua mama hivyo acheni kukurupuka vijana chezeni kwa akili ndoa inajumuisha mfumo mzima wa maisha aliolelewa binti/mwanamke akiwatokea mdogo mpaka alipofikia kuolewa na kama hawakumkunja akiwa mdogo basi sahau wewe kumkunja ukubwani.

Napia usidanganywe na hawa motivation speker eti mwanamke una muanda wewe kuwa mke unayemtaka hilo sahau wahenga hawakukosea kusema samaki mkunje angali mbichi, binti /mwanamke anaandaliwa kuwa mke na mama bora akiwatokea mdogo na anapovunja uongo wanamuandaa zaidi na zaidi ukiona hajaishi maisha ya kushughulika kuwa mke au mama ndugu kijana jiulize mara mbili sana na ikibidi kimbia moja kwa moja maana wasiwasi ni akili usije ukasema utamfundisha shauri yako.

Mwenye masikio na asikie, mwenye ufahamu na afahamu neno hili
 
Vichaa ni wengi sana siku hizi, unaanzaje kuwapangia Watu Maisha yao, mbona magari kila siku husababisha vifo tokana na ajali za bahati mbaya au sintofahamu lakini bado Watu hununua magari?

Sent from my CPH2387 using JamiiForums mobile app
 
Hao wanawake uliowataja wameandaliwa kuwa wake za waume matajiri. Kwahiyo usiseme hajaandaliwa kuwa mke, sema kaandaliwa kuwa mke wa mwanaume tajiri.

Kupika atapika mfanyakazi, kufua kuna washing machine, kupika kuna gas full time, atafunguliwa kampuni ofisi ina kiyoyozi, tv itakuwa internet connect muda wote kustream.

Ukitaka mke wa kuwasha mkaa, kufua, kupika, asiangalie tv, akakae kibandani basi tafuta mbona wapo tu huko nje ya mji ambako hakuna umeme.
 
Dah! Hatari sana hii
 
Mabinti wa mfumo wa maisha hayo ni wachache sana ukilinganisha na idadi kubwa ya mabinti wanaokulia katika Maisha ya kawaida haya ya changamoto za kuzoeleka.

Kimsingi ndoa ni taasisi kama benki, kama Wizara, kama kampuni na ina misingi yake ila la muhimu zaidi kujua ni kuwa ndoa ndio taasisi ya juu na ya thamani kuliko zote kwenye jamii.

Kiukweli swala la ndoa kwa miaka ya hivi karibuni limelala sana na limechukuliwa poa sana na jamii. Wazazi wamekuwa wazembe sana katika kuwaandaa vijana na mabinti zao.

Mtoto wa kiume hapewi mamlaka anaekezea kumsikiliza mkewe of which automatically ni kuwambia aache kuwa kiuongozi kwa mkewe.

Mwanamke anaagizwa kupanda kichwani mwanaume halafu utegemee matokeo mazuri ya ndoa.

Vijana na mabinti wengi kwasasa wapo autopilot eneo la mahusiano na ndoa hawajielewi sababu hawana muongozo mzuri wa kufuata kutoka kwa wazaz sababu wazazi nao wamewaachia kujiamulia.

Ndio maana binti leo atalalwa na wanaume hata 50 then ndipo ajifunze hasara za kutokuheshimu mwili wake. Mtoto wa kiume anawekwa kando kimamlaka hadi anafika miaka 30+ ndipo kila mtu anamuamuru awe mwanaume kwa kumwambia "wewe ni mwanaume sasa na mwanaume ni kiongozi".

Hatupo serious.
 
Back
Top Bottom