Vijana Mapenzi Yanawatesa😂😂

Nashukuru nilikutana na mwalimu konki kamoyo kakawa kagumu japo siyo jiwe lakini ubwege mwingi uliondoka
 
Hawa viumbe wanatesa kweli kweli, kuna mmoja hapa amechemsha kichwa changu haswa. Kuna kazi naifanya sehemu, nikiimaliza inatakiwa nitafute sehemu tulivu nikake na kujitafakari upya, huu ni ujinga kwa kweli. Unahangaika na kazi kuanzia asubuhi mpaka jioni, unakosa hata muda wa kwenda kula. Kuna mwehu mmoja anakwambia "kwanini hijanipigia simu" ukimueleza ulikuwa wapi na kwa mazingira yapi anakasirika na kukata simu, yeye akili yake muda wote anaamini unatembea unatafuta wanawake, akipiga simu hataki asikie sauti ya kike, ila wewe ukisikia sauti ya kiume kawaida.
Kama haya ndio mapenzi bora wale tunaoita, Hit and run kuliko kuonesha upendo kwa kiumbe chenye wivu uliopitiliza.
 
Back
Top Bottom