Hii ndiyo ilikuwa original story; lakini nadhani ni sahihi kuwa wameachishwa kazi rasmi. Kwanini uamuzi huo haukutangazwa kwenye maazimio ya mwisho, it boggles my mind. Asante Pope.
2007-08-01 08:46:49
Na Mary Edward, PST Dodoma
Kikao cha Halmashauri Kuu (NEC) ya CCM ambacho jana kilitarajiwa kutangaza majina ya wanachama wake watakaowania ujumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya chama hicho, kiliendelea hadi usiku huku kukiwa hakuna taarifa zozote za maana kuhusu walioteuliwa.
Hata hivyo, habari zilisema kuwa baadhi ya mawaziri waliokuwa wakigombea uwakilishi katika NEC majina yao yamekatwa, wakiwemo wenyeviti wa CCM wa mikoa.
`Ninaomba tu msubiri kesho taarifa rasmi, lakini ninachoweza kukudokezea ni kwamba kuna majina ya mawaziri yamekatwa pamoja na baadhi ya wenyeviti (wa CCM) wa mkoa, akiwemo wa Mtwara Lakini subirini tu kesho,` kilisema chanzo chetu.
Kikao hicho ambacho kilitanguliwa na kingine cha Kamati Kuu ya CCM tangu Julai 28, awali kilitarajiwa kumalizika Julai 30, mwaka huu, lakini kilisogezwa mbele hadi jana kutokana na baadhi ya ajenda, ikiwemo ya kuwateua wagombea wa nafasi hiyo, kutokamilika.
Wakati tunakwenda mitamboni jana usiku, wajumbe wa kikao hicho cha Halmashauri Kuu kilichokuwa chini ya Mwenyekiti wake, Rais Jakaya Kikwete, walikuwa wakitoka kuelekea katika viwanja vya Bunge ambako walikuwa na hafla.
Hata walipokuwa nje ya ukumbi huo, maarufu kama White House wa mjini hapa, wajumbe wengi walikataa ama kuwakimbia waandishi ili tu wasitaje majina ya watakaowania nafasi ya NEC ambayo ni ya juu kabisa kwa chama hicho.
Na katika hatua nyingine, hatimaye Kamati Kuu ya?CCM, imethibitisha
kuwasimamisha uongozi viongozi wanne wa Jumuiya ya Wazazi akiwemo Mwenyekiti wa jumuiya hiyo Taifa, Bw. Abihud Maregesi kwa tuhuma za ubadhirifu wa fedha za shule za sekondari za Wazazi na kutumia madaraka yao vibaya.
Uamuzi huo ulichukuliwa kufutia kikao cha Kamati cha siku tatu kilichofanyika mjini hapa chini ya Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Jakaya Kikwete.
Taarifa iliyotolewa mjini hapa jana na kusainiwa na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa, Itikadi na Uenezi, Bw. Aggrey Mwanri, ilisema hatua ya kuwasimamisha viongozi hao imelenga kutoa nafasi kwa vyombo vinavyohusika kufanya uchunguzi juu ya tuhuma zinazowakabili.
Mbali ya Bw. Maregesi, wengine waliotajwa kusimamishwa katika taarifa hiyo ni pamoja na Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi, Bw. Ramadhani Suleimani, Kaimu Katibu Mkuu wa jumuiya hiyo, ?Bw. Cosmas Hinju na Bw. Babilas Mpemba ambaye ni ofisa makao makuu ya jumuiya hiyo.
Aidha, taarifa hiyo ilifafanua kuwa, viongozi hao wamesimamishwa uongozi kwa mujibu wa Katiba ya CCM, toleo la Mei 2005, kifungu cha 110 (7) na kwamba Bw. Mpemba amesimamishwa kwa mujibu wa kanuni za utumishi wa chama na jumuiya zake.
Taarifa iliongeza kuwa, lengo la kuwasimamisha viongozi hao ni kutoa nafasi kwa vyombo? vinavyohusika kufanya uchunguzi ili kubaini ukweli wa tuhuma kabla ya uamuzi kamili juu yao kutolewa.
Na katika hatua nyingine, Kamati Kuu imeridhia uamuzi wa kuwafukuza uanachama madiwani?watano wa CCM wa Wilaya ya Tunduru kwa tuhuma za kukiuka maadili ya CCM.
Taarifa ilisema uamuzi?huo wa Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Ruvuma wa hivi karibuni wa kutoa adhabu ya kuwafukuza uanachama madiwani hao, ulikuwa sahihi.
Halmashauri Kuu ya CCM? Mkoa wa Ruvuma, iliwafukuza uanachama madiwani hao baada ya kuthibitika kuwa walikiuka maadili ya uongozi na ya uanachama ambapo taarifa hiyo ilisema kuwa walifukuzwa kwa mujibu wa kanuni na maadili toleo la Mei,? 2002 kifungu 8.2.9.
Aidha, taarifa hiyo iliwataja waliofukuzwa na kupoteza wadhifa wa uanachama na Udiwani kuwa ni? pamoja na aliyekuwa? Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru, Bw. Burhan Makonje, madiwani Zuhura Mafutari, Suleiman Shaibu, Aindi Bakari na Halima Luambano.
Mbali na hilo, katika siku ya kwanza, Kamati Kuu ya CCM? ilifanya uteuzi wa wana-CCM watatu wa kugombea nafasi ya Meya wa Manispaa ya Arusha.
Walioteuliwa kuwania nafasi hiyo kwa mujibu wa taarifa hiyo ni Bw. Anaelson Ole Joel, Laurence Heddi na Julius Sekayan.
?Madiwani hao watatu walioteuliwa kugombea watapigiwa kura na Kamati ya Madiwani? wote wa CCM? wa Manispaa ya Arusha na atakayeshinda jina lake litawasilishwa kwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Arusha kama mgombea wa?nafasi ya Meya wa Manispaa ya Arusha? kwa tiketi ya CCM, taarifa ilifafanua.
Nafasi ya Meya wa Arusha, imekuwa wazi baada ya aliyekuwa Meya wa Jiji hilo, Bw. Paul Laizer kujiuzulu.
Wakati huo huo, Kamati Kuu ya CCM, imewateua wanachama wake watatu kuwa Makatibu wa CCM wa Wilaya kujaza nafasi zilizokuwa? wazi kutokana na sababu mbalimbali.
Taarifa ya Kamati hiyo iliwataja walioteuliwa kuwa ni Bw. Zabron Msemwa, Bw.Othman Dunga na Bi. Mary Maziku ambapo kabla ya uteuzi huo, Bw. Msemwa alikuwa Kaimu Katibu wa CCM Wilaya ya Kibondo.
Bw. Nduga alikuwa Kaimu Katibu wa CCM Wilaya ya Bukoba Mjini na Bi. Maziku alikuwa Katibu Msaidizi na Mhasibu wa Wilaya ya Ilala.
Hali kadhalika, Kamati hiyo imemvua haki ya kuchaguliwa katika uongozi wa CCM, Bw. Thomas Nyimbo baada ya kuthibitika kuwa tabia na mwenendo wake vinamfanya asistahili kuwa na haki hiyo.
Taarifa ilisema Kamati Kuu?imechukua hatua ya kumpa adhabu? hiyo kwa mujibu wa?kanuni za uongozi? na maadili toleo la 2002, kifungu 8.2.4 na kwamba hatua hiyo? imezingatia ukweli kuwa, Bw. Nyimbo aliwahi kupewa?adhabu ya karipio kwa kuacha tabia na mwenendo huo alionao lakini amerudia tena hivyo atatumikia adhabu hiyo kwa miezi 24.
Original Thread:
http://www.jamboforums.com/showthread.php?t=4124