Watumishi 6 wa Wilaya ya Misenyi wasimamishwa kwa Ubadhirifu

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
43,115
49,833
Misenyi: WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameagiza watumishi sita wa Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi wafuatiliwe ili warejeshe fedha za umma na kisha wachukuliwe hatua za kinidhamu.

“Uongozi wa Mkoa uendelee kuwafuatilia na kuisimamia Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi ili warudishe fedha za makusanyo za Julai na Agosti, 2023.”

Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo jioni wakati akizungumza na mamia ya wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Uwanja wa Mashujaa katika tarafa ya Bunazi, wilayani Missenyi, mkoani Kagera.

Amewataja watumishi hao kuwa ni Chrispin Mbuga, Andrephnus Kalisa, Nashrath Buyungilo, Lusiana Irunde, Issack Sadick na Willington Mutabilwa ambao ni watoza ushuru wa Halmashauri na kwa pamoja wanadaiwa Sh. milioni 37.3.

Habari Leo

===

Kazi ya Kufumua mitandao ya kifisadi ambayo Rais aliagiza inaendelea ambapo PM akiwa Misenyi ameagiza kuchukuliwa hatua Kwa Watumishi ambao walikuwa Wanapeleka mapato kiduchu Serikalini huku wao wakigawana Mamilioni Kila siku.

My Take
Msiishie kuwaandama Watumishi wa Halmashauri tuu Bali upigaji uko Kwenye taasisi zote.
 
Hao ni vidagaa tu. Mapapa wapo wanatamba. Mkuu wa Wilaya yupo, Mkurugenzi wa Halmashauri yupo, OCS na OCD wapo, TAKUKURU ipo n.k. lakini dagaa bado wanatoboa nyavu kiulaini. Haiwezekani kabisa. Lazima kuna mtandao mkubwa wa ulaji unaowahusisha wakubwa wengine.
 
Misenyi: WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameagiza watumishi sita wa Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi wafuatiliwe ili warejeshe fedha za umma na kisha wachukuliwe hatua za kinidhamu.

“Uongozi wa Mkoa uendelee kuwafuatilia na kuisimamia Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi ili warudishe fedha za makusanyo za Julai na Agosti, 2023.”

Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo jioni wakati akizungumza na mamia ya wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Uwanja wa Mashujaa katika tarafa ya Bunazi, wilayani Missenyi, mkoani Kagera.

Amewataja watumishi hao kuwa ni Chrispin Mbuga, Andrephnus Kalisa, Nashrath Buyungilo, Lusiana Irunde, Issack Sadick na Willington Mutabilwa ambao ni watoza ushuru wa Halmashauri na kwa pamoja wanadaiwa Sh. milioni 37.3.

Habari Leo

===

Kazi ya Kufumua mitandao ya kifisadi ambayo Rais aliagiza inaendelea ambapo PM akiwa Misenyi ameagiza kuchukuliwa hatua Kwa Watumishi ambao walikuwa Wanapeleka mapato kiduchu Serikalini huku wao wakigawana Mamilioni Kila siku.

My Take
Msiishie kuwaandama Watumishi wa Halmashauri tuu Bali upigaji uko Kwenye taasisi zote.
Naona mpango wenu dhalimu wa kumfitini PM umefeli..sasa mmeamua kumuacha afanye kazi.. wapumbavu nyinyi
 
Back
Top Bottom