Vigogo wa CCM waachishwa kazi kwa Ubadhirifu.

Pope

Senior Member
Dec 3, 2007
117
0
HALMASHAURI Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (NEC) imewaachisha uongozi rasmi viongozi wa Jumuiya ya Wazazi Taifa ambao ni Mwenyekiti Abiud Maregesi, makamu wake Ramadhan Nzori na aliyekuwa Kaimu Katibu Mkuu, Cosmas Hinju. Maregesi ameachishwa uongozi kutokana na ubadhirifu wa fedha za jumuiya hiyo Sh milioni 63.3 na kutumia vibaya madaraka yake.
Nzori ameachishwa kazi kutokana na kosa la ubadhirifu wa Sh milioni 7.5, wakati Hinju anatuhumiwa kutafuna Sh milioni tano na matumizi mabaya ya madaraka. NEC imeagiza kuwa viongozi hao wa wazazi warejeshe fedha za jumuiya hiyo walizochukua kinyume cha kanuni za fedha za jumuiya hiyo. Halmashauri Kuu pia imemteua Badru Bushako kuwa Kaimu Katibu Mkuu.
 
Jamani mnakula hadi MBEGU????
Huyu MAregesi kaingia juzi tuu tayari kesha CHUKUA CHAKE MAPEMA!!!!
 
Typical of CCM,

Hii ni swa na kumpiga kibaka wakati mifisadi kina Lowassa, Aziz, Yona na Mkapa inapeta.

It does nothing for me.
 
Kwa nini wasifunguliwe mashitaka??? Hawa wanatakiwa kupelekwa segerea. Toka lini mwizi huwa anaombwa kurudisha alichokwiba???Tukiamua kufuata utaratibu huu, basi tusianze kubagua. Wezi wote waliofungwa katika magereza waachiwe huru ili warejeshe walichokwiba. Hii itasaidia kupunguza mlundikano wa wafungwa magerezani
 
Nakubaliana na wewe Mheshimiwa!!
 
really..? Kikao cha Kamati Kuu ipi hiyo na kilifanyika lini? maana tusije kuwa tunazungusha habari za mwaka jana mwaka huu.. niko tayari kusahihishwa lakini naamini haya siyo maamuzi mapya..
 
hawa waliachishwa lini? source ya hii habari ni nini na ni wapi na lini? Hii habari ya Maregesi imekuwa kwenye mzunguko for a long time na inatoka tena leo?

Nani hajui kuwa Malegesi alikuwa kambi tofauti na wanamtandao kwa hiyo anavuna alichopanda!!??!!! come on guys you can do better than this!
 
Kwa nini wasifunguliwe mashitaka??? Hawa wanatakiwa kupelekwa segerea. Toka lini mwizi huwa anaombwa kurudisha alichokwiba???Tukiamua kufuata utaratibu huu, basi tusianze kubagua. Wezi wote waliofungwa katika magereza waachiwe huru ili warejeshe walichokwiba. Hii itasaidia kupunguza mlundikano wa wafungwa magerezani

Hii ni ishara kama alivyo tamka JK kwamba hawana mpango wa kuwashitaki wezi wao wala kutaifisha so the same goes for Hinju and co.
 
sasa nakumbuka walisimamishwa kazi na NEC yeye na Kataraiya lakini sijui kama walifukuzwa au la. Najua wiki iliyopita Maregesi aliibuka na kudai kuwa CCM ina makundi (kitu kilichopingwa muda mfupi baadaye na Makamba).

Sasa yawezekana kulikuwa maamuzi mengine nje ya yale waliyoaambiwa waandishi Juzi. Labda kama article ilivyoanza kuwa wamefukuzwa kazi "rasmi".

Pope, tusaidie hii ni habari mpya?
 
http://haki-hakingowi.blogspot.com/

Kama ifuatavyo:

CCM yateua makatibu wanne
wapya wa mikoa..
ccc.jpg

Wajumbe wa Mkutano wa Halmashauri Kuu wa Chama cha Mapinduzi(CCM) wakiwa kwenye ukumbi wa mikutano wa kumbukumbu ya Joseph Kizurira Nyerere katika Kijiji cha Butiama Musoma mkoani mara hivi karibuni.
ccc.jpg

-----------
HALMASHAURI Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi, imeteua makatibu wanne wa mikoa kujaza nafasi zilizo wazi katika baadhi ya mikoa. Mikoa ambayo makatibu hao watafanya kazi ni Mbeya, Dodoma, Kigoma na Kaskazini Unguja. Taarifa ya CCM ilisema walioteuliwa ni Emmanuel Mteming'ombe, Salum Msabaha Mbarouk, Mary Tesha na Moudline Castico, ambao hawajaelezwa watakwenda mikoa ipi.
NEC pia imewaachisha uongozi rasmi viongozi wa Jumuiya ya Wazazi Taifa ambao ni Mwenyekiti Abiud Maregesi, makamu wake Ramadhan Nzori na aliyekuwa Kaimu Katibu Mkuu, Cosmas Hinju. Maregesi ameachishwa uongozi kutokana na ubadhirifu wa fedha za jumuiya hiyo Sh milioni 63.3 na kutumia vibaya madaraka yake.
Nzori ameachishwa kazi kutokana na kosa la ubadhirifu wa Sh milioni 7.5, wakati Hinju anatuhumiwa kutafuna Sh milioni tano na matumizi mabaya ya madaraka. NEC imeagiza kuwa viongozi hao wa wazazi warejeshe fedha za jumuiya hiyo walizochukua kinyume cha kanuni za fedha za jumuiya hiyo. Halmashauri Kuu pia imemteua Badru Bushako kuwa Kaimu Katibu Mkuu.
Anachukua nafasi ya Yasmin Aloo ambaye amerejeshwa katika nafasi yake ya Naibu Katibu Mkuu Zanzibar.
Catherine Nao aliyekuwa anakaimu nafasi ya Naibu Katibu Mkuu Zanzibar atapangiwa kazi nyingine. Taarifa ya NEC ilieleza kuwa imepokea kwa masikitiko taarifa ya ubomoaji wa nyumba Tabata Dampo ambao ulikuwa wa kikatili na ambao haukuzingatia sheria na maadili ya kazi ya maofisa waliosimamia ubomoaji huo ambao umewaacha watu 500 bila makazi. Imeipongeza serikali kwa kuchukua hatua za haraka na sahihi katika kushughulikia mgogoro huo ikiwamo kusimamisha kazi maofisa waliohusika.
 
Tofauti ya utendaji huko ccm ni kuwa ukifuja milioni basi wewe jiandae kushikiwa bango ila ukifuja mabilioni basi wewe ni kupeta tu kama una akili nzuri vile!

Hii issue ya Maregesi imekuwepo hapa zaidi ya mwaka na leo ndiyo inaletwa kwenye spotlight! Ni vizuri kuwa wamefukuzwa kazi, the next step wapelewekwe mahakamani!
 
Hii ndiyo ilikuwa original story; lakini nadhani ni sahihi kuwa wameachishwa kazi rasmi. Kwanini uamuzi huo haukutangazwa kwenye maazimio ya mwisho, it boggles my mind. Asante Pope.

2007-08-01 08:46:49
Na Mary Edward, PST Dodoma

Kikao cha Halmashauri Kuu (NEC) ya CCM ambacho jana kilitarajiwa kutangaza majina ya wanachama wake watakaowania ujumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya chama hicho, kiliendelea hadi usiku huku kukiwa hakuna taarifa zozote za maana kuhusu walioteuliwa.

Hata hivyo, habari zilisema kuwa baadhi ya mawaziri waliokuwa wakigombea uwakilishi katika NEC majina yao yamekatwa, wakiwemo wenyeviti wa CCM wa mikoa.

`Ninaomba tu msubiri kesho taarifa rasmi, lakini ninachoweza kukudokezea ni kwamba kuna majina ya mawaziri yamekatwa pamoja na baadhi ya wenyeviti (wa CCM) wa mkoa, akiwemo wa Mtwara Lakini subirini tu kesho,` kilisema chanzo chetu.

Kikao hicho ambacho kilitanguliwa na kingine cha Kamati Kuu ya CCM tangu Julai 28, awali kilitarajiwa kumalizika Julai 30, mwaka huu, lakini kilisogezwa mbele hadi jana kutokana na baadhi ya ajenda, ikiwemo ya kuwateua wagombea wa nafasi hiyo, kutokamilika.

Wakati tunakwenda mitamboni jana usiku, wajumbe wa kikao hicho cha Halmashauri Kuu kilichokuwa chini ya Mwenyekiti wake, Rais Jakaya Kikwete, walikuwa wakitoka kuelekea katika viwanja vya Bunge ambako walikuwa na hafla.

Hata walipokuwa nje ya ukumbi huo, maarufu kama White House wa mjini hapa, wajumbe wengi walikataa ama kuwakimbia waandishi ili tu wasitaje majina ya watakaowania nafasi ya NEC ambayo ni ya juu kabisa kwa chama hicho.

Na katika hatua nyingine, hatimaye Kamati Kuu ya?CCM, imethibitisha kuwasimamisha uongozi viongozi wanne wa Jumuiya ya Wazazi akiwemo Mwenyekiti wa jumuiya hiyo Taifa, Bw. Abihud Maregesi kwa tuhuma za ubadhirifu wa fedha za shule za sekondari za Wazazi na kutumia madaraka yao vibaya.
Uamuzi huo ulichukuliwa kufutia kikao cha Kamati cha siku tatu kilichofanyika mjini hapa chini ya Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Jakaya Kikwete.

Taarifa iliyotolewa mjini hapa jana na kusainiwa na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa, Itikadi na Uenezi, Bw. Aggrey Mwanri, ilisema hatua ya kuwasimamisha viongozi hao imelenga kutoa nafasi kwa vyombo vinavyohusika kufanya uchunguzi juu ya tuhuma zinazowakabili.

Mbali ya Bw. Maregesi, wengine waliotajwa kusimamishwa katika taarifa hiyo ni pamoja na Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi, Bw. Ramadhani Suleimani, Kaimu Katibu Mkuu wa jumuiya hiyo, ?Bw. Cosmas Hinju na Bw. Babilas Mpemba ambaye ni ofisa makao makuu ya jumuiya hiyo.

Aidha, taarifa hiyo ilifafanua kuwa, viongozi hao wamesimamishwa uongozi kwa mujibu wa Katiba ya CCM, toleo la Mei 2005, kifungu cha 110 (7) na kwamba Bw. Mpemba amesimamishwa kwa mujibu wa kanuni za utumishi wa chama na jumuiya zake.

Taarifa iliongeza kuwa, lengo la kuwasimamisha viongozi hao ni kutoa nafasi kwa vyombo? vinavyohusika kufanya uchunguzi ili kubaini ukweli wa tuhuma kabla ya uamuzi kamili juu yao kutolewa.

Na katika hatua nyingine, Kamati Kuu imeridhia uamuzi wa kuwafukuza uanachama madiwani?watano wa CCM wa Wilaya ya Tunduru kwa tuhuma za kukiuka maadili ya CCM.

Taarifa ilisema uamuzi?huo wa Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Ruvuma wa hivi karibuni wa kutoa adhabu ya kuwafukuza uanachama madiwani hao, ulikuwa sahihi.

Halmashauri Kuu ya CCM? Mkoa wa Ruvuma, iliwafukuza uanachama madiwani hao baada ya kuthibitika kuwa walikiuka maadili ya uongozi na ya uanachama ambapo taarifa hiyo ilisema kuwa walifukuzwa kwa mujibu wa kanuni na maadili toleo la Mei,? 2002 kifungu 8.2.9.

Aidha, taarifa hiyo iliwataja waliofukuzwa na kupoteza wadhifa wa uanachama na Udiwani kuwa ni? pamoja na aliyekuwa? Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru, Bw. Burhan Makonje, madiwani Zuhura Mafutari, Suleiman Shaibu, Aindi Bakari na Halima Luambano.

Mbali na hilo, katika siku ya kwanza, Kamati Kuu ya CCM? ilifanya uteuzi wa wana-CCM watatu wa kugombea nafasi ya Meya wa Manispaa ya Arusha.

Walioteuliwa kuwania nafasi hiyo kwa mujibu wa taarifa hiyo ni Bw. Anaelson Ole Joel, Laurence Heddi na Julius Sekayan.

?Madiwani hao watatu walioteuliwa kugombea watapigiwa kura na Kamati ya Madiwani? wote wa CCM? wa Manispaa ya Arusha na atakayeshinda jina lake litawasilishwa kwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Arusha kama mgombea wa?nafasi ya Meya wa Manispaa ya Arusha? kwa tiketi ya CCM, taarifa ilifafanua.

Nafasi ya Meya wa Arusha, imekuwa wazi baada ya aliyekuwa Meya wa Jiji hilo, Bw. Paul Laizer kujiuzulu.

Wakati huo huo, Kamati Kuu ya CCM, imewateua wanachama wake watatu kuwa Makatibu wa CCM wa Wilaya kujaza nafasi zilizokuwa? wazi kutokana na sababu mbalimbali.

Taarifa ya Kamati hiyo iliwataja walioteuliwa kuwa ni Bw. Zabron Msemwa, Bw.Othman Dunga na Bi. Mary Maziku ambapo kabla ya uteuzi huo, Bw. Msemwa alikuwa Kaimu Katibu wa CCM Wilaya ya Kibondo.

Bw. Nduga alikuwa Kaimu Katibu wa CCM Wilaya ya Bukoba Mjini na Bi. Maziku alikuwa Katibu Msaidizi na Mhasibu wa Wilaya ya Ilala.

Hali kadhalika, Kamati hiyo imemvua haki ya kuchaguliwa katika uongozi wa CCM, Bw. Thomas Nyimbo baada ya kuthibitika kuwa tabia na mwenendo wake vinamfanya asistahili kuwa na haki hiyo.

Taarifa ilisema Kamati Kuu?imechukua hatua ya kumpa adhabu? hiyo kwa mujibu wa?kanuni za uongozi? na maadili toleo la 2002, kifungu 8.2.4 na kwamba hatua hiyo? imezingatia ukweli kuwa, Bw. Nyimbo aliwahi kupewa?adhabu ya karipio kwa kuacha tabia na mwenendo huo alionao lakini amerudia tena hivyo atatumikia adhabu hiyo kwa miezi 24.

Original Thread:

http://www.jamboforums.com/showthread.php?t=4124
 
Wabheja mwanawane MWanakijiji.
Unajua ninachoshangaani kuwa kama mtu anatuhumiwa kwa wizi si polisi wafanye kazi yao?
Inakuwaje au hata wao wana Diplomatic Immunities?
 
Wabheja mwanawane MWanakijiji.
Unajua ninachoshangaani kuwa kama mtu anatuhumiwa kwa wizi si polisi wafanye kazi yao?
Inakuwaje au hata wao wana Diplomatic Immunities?

Huko ccm kuna different standard za kufanya kazi na ndio maana Ditto anapeta tu kama hana akili nzuri pamoja na kuua mtu kwa makusudi yote yanayofahamika hapa duniani.
 
Utaratibu huu wa wezi kuambiwa 'warudishe yaishe' ukiendelea, muda si mrefu askari polisi na magereza watakufa njaa!
 
Usanii wa CCM! walioiba milioni wanafukuzwa kazi lakini walioiba bilioni wanaendelea kupeta! Labda kwa hesabu za CCM milioni ni kubwa kuliko bilioni! acheni unafiki CCM.
 
Mhh inatia uchungu ila chenye mwanzo kinamwisho.
Ilikuwa Kanu na Sasa Zimbabwe... NEEEEEEEEEEEEEEXT!!!
 
Angalieni ibara ya 15:1 na 2 ya Katiba ya CCM mtapa "clue" ya kwanini fedha za CCM zinauma mno kuliko za Serikali. Kwenye yahoo search for "Kataraiya, mwanakijiji"... utapata jibu pia.
 
Angalieni ibara ya 15:1 na 2 ya Katiba ya CCM mtapa "clue" ya kwanini fedha za CCM zinauma mno kuliko za Serikali. Kwenye yahoo search for "Kataraiya, mwanakijiji"... utapata jibu pia.

Ndiyo yale yale ya CCM kutoa kipaumbele kwa CCM kuliko Tanzania.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom