Viganja Mashavuni Mwangu

Viganja Mashavuni Mwangu

SEHEMU YA 38

“Nashukuru sana! Naomba uniitie huyo msichana, nitamlipa kiasi chochote kile,” alisema Cassian.
“Hakuna shida.”

*** Ilikuwa ni rahisi kwa Evelyne kusahau kila kitu kilichotokea katika maisha yake, kusahau tarehe ya siku yake ya kuzaliwa, kuwasahau watu waliomtendea mabaya kuliko kumsahau Cassia na mambo yote aliyokuwa ameyafanya.

Ilikuwa ni aibu kubwa, hakutoka ndani, kila alipokuwa chumbani kwake alikuwa mtu wa kulia tu, alihuzunika, aliumia moyoni mwake na wakati mwingine alihisi kwamba ilikuwa ni afadhali kujiua kuliko kuendelea kuishi.

Rafiki yake, Mwajuma ndiye aliyekuwa karibu naye, yeye ndiye aliyekuwa akimbembeleza usiku na mchana na hata msichana huyo alipotaka kufanya maamuzi magumu ya kutaka kujiua, Mwajuma alikuwa akimuokoa, alifanya hivyo mara tatu kwa nyakati tofauti.

Alimchukuia Cassian, aliilaani siku aliyokutana na mwanaume huyo, aliwachukia wanaume wote duniani hata kama wengine hawakumfanya kile alichofanyiwa na Cassian.

Alilia sana, alihuzunika mno na moyo wake kuchomwa na kitu cha moto kilichokuwa na ncha kali.

Siku zikakatika, alijiapiza kwamba ilikuwa ni lazima kulipiza kiasi kwa Cassian, kama alikuwa amemuumiza kwa staili ile na yeye ilikuwa ni lazima kumuumiza kwa pigo lenye maumivu kama lile.

Kwa mwaka mzima alikuwa chumbani, ni mara chache tu ndizo alizokuwa akitoka ndani, tena usiku, kila alipokuwa akipita kwenye mitandao ya kijamii, watu walimcheka, walimdhihaki kwa kile kilichokuwa kimetokea na hivyo moyo wake kubaki na kidonda kikubwa ambacho hakudhani kama kuna siku kingekuja kupona.

Mwajuma ndiye aliyekuwa akifuatilia kila kitu kilichokuwa kikiendelea, yeye ndiye aliyemwambia Cassian kwamba alikuwa amepata mwanamke mwingine, wa uswahilini, asiyejua hata thamani ya dola ya Kimarekani kwa pesa ya Kitanzania.
Mwishowe nmewafikia
Asanteh Shunnie!!!
 
SEHEMU YA 39

Moyo wake ulichoma zaidi, kidonda kikatoneshwa, maumivu yakaongezeka, alizidi kulia na kuomboleza kila siku.

Siku zikaendelea kukatika huku Mwajuma akimletea kila kitu kilichokuwa kikiendelea, mpaka aliposikia kwamba mke wa Cassian, Naseku alikuwa amejifungua mapacha walioungana, kidogo moyo wake ukajisikia nafuu kwa kuona kwamba machozi aliyokuwa amemwaga kwa ajili ya mwanaume huyo hatimaye Mungu alikuwa amemlipia.

“Mungu amenilipia, na bado ataendelea kunilipia,” alimwambia rafiki yake, Mwajuma pasipo kujua kwamba huo ulikuwa ni mpango wa Mungu kwa watoto hao kuwa katika hali hiyo.

“Tena sana. Chozi la mwanamke haliendi bure,” alisema Mwajuma pasipo kujua kwamba siku zote machozi ya mwanamke malaya kama walivyokuwa yalikuwa yakienda bure, yaani kama kumwaga maji mtaroni kutoka kwenye ndoo chafu.

Wakajifariji sana, wakazungumza maneno yao ya kujipa nguvu na kujiaminisha kwamba kila kitu kilichokuwa kimetokea kilikuwa ni mpango wa Mungu.

Baada ya siku miezi miwili watoto kuzaliwa, Evelyne akapata wazo jingine kwamba hata kama Mungu alikuwa amemlipizia kwa mwanaume huyo kupata watoto walioungana ilikuwa ni lazima kufanya jambo, kuwateka na kuwaua ili Cassian aumie, alie kama alivyokuwa akilia.

Hakujua ni kwa namna gani angeweza kuwapata watoto hao.

Cassian alikuwa bilionea, mwenye ulinzi mkubwa ambaye kila kona nyumbani kwake kulikuwa na walinzi waliokuwa na bunduki, alijifikiria sana na baada ya kumtuma Mwajuma kumchunguza kwa undani zaidi, akagundua kwamba familia hiyo ilikuwa ikitafuta mfanyakazi wa ndani wa kukaa na watoto.

“Unasema kweli?” aliuliza Evelyne huku akionekana kutokuamini.
“Ndiyo shoga yangu!”

“Hii ndiyo nafasi yangu!” alijisemea.
Alikuwa na pesa, akaunti yake ilikuwa na milioni tisini, alichuma pesa hizo kwa Cassian, zilikuwa ni zaidi ya milioni mia moja na ishirini ila kwa matumizi ya mwaka mzima zikabaki hizo.

Alitaka kutumia sehemu ya pesa hizo kumuumiza Cassian, kitu alichokifanya ni kuwatafuta vijana watatu kutoka katika Kundi la Fogo lililokuwa na maskani yake Tandale na kuwaambia kwamba alitaka kuona watoto wa mzee mmoja wakitekwa.
 
SEHEMU YA 40

“Mzee gani?”
“Anaitwa Marcus!”
“Anaishi wapi?”
“Mbezi Beach.”
“Hakuna shida.”

Akawaelekeza namna ya kuwapata watoto hao, haikuwa kazi kubwa, akawaelekeza shule waliyokuwa wakiishi, gari lililokuwa likielekea shuleni kuwachukua, gari hilohilo lilitakiwa kutekwa.

Ilikuwa ni kazi ndogo sana, watu hao waliokuwa na bastola ambao walitumwa kufanya kazi hiyo kwa malipo ya shilingi milioni kumi wakaanza kufuatilia, ni ndani ya siku mbili tu, tayari watoto wake, Jackson na Careen wakatekwa na hivyo kupigiwa simu.

“Jamani naomba msiwaue,” alisema Mzee Marcus huku akionekana kuogopa.
“Wala usijali! Ukifanya tunachokitaka, hawatokufa, ila usipokifanya, tutaviweka vichwa vyao kwenye boksi na kukutumia,” alisikika mwanaume upande wa pili wa simu.

“Jamani naomba msifanye hivyo! Nitawapendi kiasi chochote cha pesa,” alisema Mzee Marcus.

“Hatuhitaji pesa, tunahitaji kuonana na wewe. Ukishindwa, tunawaua, au ukiwapa taarifa polisi, ndiyo kabisa tunawatumbukiza kwenye pipa la tindikali na hutoona hata maiti zao,” aliskika mwanaume huyo.

“Basi sawa. Tuonane, tuyapange na tutakuachia watoto wako wakiwa wazima wa afya,” alisema mwanaume huyo.
“Wapi?”

“Tandale Sokoni, kesho saa saba mchana, pembeni ya kijana anayeuza mihogo, utamuona amevaa fulana iliyoandikwa Big Man kifuani. Zingatia muda, ukichelewa, tusilaumiane.

Saa saba mchana kumbuka,” alisema mwanaume huyo na kukata simu.

Itaendelea
 
Yaani evelyn bhana eti machozi yake hayaendi bure amesahau yale aliyomtendea cassian??
Hovyo kabisa
 
SEHEMU YA 41

Mzee Marcus alikuwa kwenye mawazo mengi, hakujua ni kitu gani alitakiwa kufanya.

Alihisi kwamba watu hao walihitaji pesa lakini wazo hilo lilifutika kichwani mwake kwani kama kweli walikuwa wakihitaji pesa ilikuwa ni lazima wamwambie kwamba alitakiwa kwenda na pesa zao kabisa.

Siku iliyofuata mapema tu alifika Tandale Sokoni, kulikuwa na watu wengi na ilikuwa vigumu kwa mtu kama yeye kugundua ni mahali gani walipokuwa wakiuza mihogo.

Akaulizia mahali kulipokuwa kukiuzwa mihogo, akaambiwa na kwenda huko.
Macho yake yalikuwa yakiangalia huku na kule, aliogopa, kulikuwa na watu wengi kiasi kwamba hakujua mwema alikuwa yupi na mbaya yupi.

Alipoendelea kuangalia huku na kule macho yake yakatua kwa mwanaume aliyekuwa akiuza mihogo ambaye alivalia fulana ya Bluu iliyoandikwa Big Man kifuani.

“Yule pale.”
Akaanza kumsogelea kijana yule na kumsalimia. Ilionekana kama kijana yule hafahamu kitu chochote kile, kwani baada ya kuitikia salamu ile, akaendelea na mambo yake kama kawaida.

Mzee huyo alisimama kwa dakika kadhaa, mara mwanaume mmoja akafika mahali hapo akiwa na pikipiki, akaisimamisha na kumwambia apande ili aondoke naye.

“Watoto wangu wapo wapi?” aliuliza hata kabla ya kupanda kwenye pikipiki ile.
“Wewe twende! Au hutaki?” aliuliza mwanaume huyo, haraka sana mzee huyo akapanda na kuondoka mahali hapo.

Mwendo ulikuwa ni wa kasi, wakaondoka kwa kupitia barabara iliyokuwa ikielekea Kwa Mtogole, walipofika kwenye msikiti wa Bi Mtumwa, wakachukua njia upande wa kulia na kwenda sehemu ambayo ilikuwa na kibanda cha wauza mkaa.

Walikwenda kwa mwendo wa kawaida mpaka wakaingia kwenye kichochoro ambacho ilikuwa ni vigumu sana kuona kama pikipiki ingeweza kupenya,

wakaingia na kwenda mbele ambapo ikasimama mbele ya nyumba moja chakavu, wakateremka.

Akaingizwa ndani ya nyumba hiyo, akakutana na vijana watatu waliokuwa na bastola, wakamuamrisha kukaa chini na kumwambia kwamba kulikuwa na kitu alichotakiwa kufanya.
 
SEHEMU YA 42

Wakamwambia kwamba watoto wake walikuwa wazima kabisa na ili kumridhisha wakamuonyeshea picha za watoto hao ambao walikuwa wamefungwa vitambaa.

“Naomba msiwaue,” alisema mzee huyo huku akitetemeka.
“Hilo si tatizo! Unachotakiwa ni kufanya tunachotaka ukifanye,” alisema mwanaume mmoja.

Wakaanza kumwambia kile walichokuwa wakikihitaji. Alihitajika kumwambia Cassian kwamba atafute dada wa kufanya kazi za ndani ambaye huyo ndiye angekaa na watoto aliokuwa amewapata na msichana huyo hakuwa na sababu ya kumtafuta kwani walitaka kumpa wao wenyewe.

“Jamaniiii!”
“Kama hutaki basi tuwaue!”
“Naomba msiwaue!”
“Basi fanya tulichokwambia!”

Wakamwambia zaidi jinsi hali ilivyotakiwa kufanywa. Hakutakiwa kubisha, ili watoto wake wawe salama ilikuwa ni lazima kufanya kile ambacho watu hao walimtaka kukifanya. Wakakubaliana na kuondoka huku akiacha namba ya simu.

Siku iliyofuata, akapata ugeni, alikuwa msichana mwenye sura mbaya ambaye ndiye huyo aliyetakiwa kutumwa kwa Cassian kwa ajili ya kufanya kazi za ndani kumbe lengo kubwa likiwa ni kuwateka watoto hao na kwenda kuwaua.

Akampigia simu Cassian, aliongea naye kwa kirefu, akamsifia msichana huyo kwamba alikuwa mtu safi, aliyewalea watoto wake mpaka kukua.

Cassian hakuwa na hofu, alimwamini Mzee Marcus na hivyo kuhitaji kuonana na msichana huyo.

Alipomuona tu, kwa jinsi alivyokuwa, akahisi kwamba kweli huyo alikuwa mfanyakazi wa ndani na hivyo kumkaribisha kwa mikono miwili. “Unaitwa nani?”

“Sikujua!”
“Ooh! Sawa. Karibu sana mama!” alimkaribisha Cassian.
Hakukuwa na mtu aliyegundua kwamba mwanamke huyo alikuwa mbaya, wakatokea kumwamini, kila siku ilikuwa ni lazima wampe majukumu yote ya kuwalea watoto hao kitendo kilichomfanya kuwa karibu na watoto hao.

Kila siku asubuhi walikuwa wakiondoka kuelekea katika majukumu yao, nyumbani alikuwa akibaki msichana huyo na watoto hao tu pamoja na walinzi waliokuwa wakilinda mahali hapo.

Siku zilikatika, watoto wao walikuwa furaha yao kubwa, waliendelea kuwapenda, na kila siku walipokuwa wakirudi, kitu cha kwanza kilikuwa ni kuwajulia hali.
 
Lisiwafike baya lolote tu watoto hawa!!!!
SEHEMU YA 42

Wakamwambia kwamba watoto wake walikuwa wazima kabisa na ili kumridhisha wakamuonyeshea picha za watoto hao ambao walikuwa wamefungwa vitambaa.

“Naomba msiwaue,” alisema mzee huyo huku akitetemeka.
“Hilo si tatizo! Unachotakiwa ni kufanya tunachotaka ukifanye,” alisema mwanaume mmoja.

Wakaanza kumwambia kile walichokuwa wakikihitaji. Alihitajika kumwambia Cassian kwamba atafute dada wa kufanya kazi za ndani ambaye huyo ndiye angekaa na watoto aliokuwa amewapata na msichana huyo hakuwa na sababu ya kumtafuta kwani walitaka kumpa wao wenyewe.

“Jamaniiii!”
“Kama hutaki basi tuwaue!”
“Naomba msiwaue!”
“Basi fanya tulichokwambia!”

Wakamwambia zaidi jinsi hali ilivyotakiwa kufanywa. Hakutakiwa kubisha, ili watoto wake wawe salama ilikuwa ni lazima kufanya kile ambacho watu hao walimtaka kukifanya. Wakakubaliana na kuondoka huku akiacha namba ya simu.

Siku iliyofuata, akapata ugeni, alikuwa msichana mwenye sura mbaya ambaye ndiye huyo aliyetakiwa kutumwa kwa Cassian kwa ajili ya kufanya kazi za ndani kumbe lengo kubwa likiwa ni kuwateka watoto hao na kwenda kuwaua.

Akampigia simu Cassian, aliongea naye kwa kirefu, akamsifia msichana huyo kwamba alikuwa mtu safi, aliyewalea watoto wake mpaka kukua.

Cassian hakuwa na hofu, alimwamini Mzee Marcus na hivyo kuhitaji kuonana na msichana huyo.

Alipomuona tu, kwa jinsi alivyokuwa, akahisi kwamba kweli huyo alikuwa mfanyakazi wa ndani na hivyo kumkaribisha kwa mikono miwili. “Unaitwa nani?”

“Sikujua!”
“Ooh! Sawa. Karibu sana mama!” alimkaribisha Cassian.
Hakukuwa na mtu aliyegundua kwamba mwanamke huyo alikuwa mbaya, wakatokea kumwamini, kila siku ilikuwa ni lazima wampe majukumu yote ya kuwalea watoto hao kitendo kilichomfanya kuwa karibu na watoto hao.

Kila siku asubuhi walikuwa wakiondoka kuelekea katika majukumu yao, nyumbani alikuwa akibaki msichana huyo na watoto hao tu pamoja na walinzi waliokuwa wakilinda mahali hapo.

Siku zilikatika, watoto wao walikuwa furaha yao kubwa, waliendelea kuwapenda, na kila siku walipokuwa wakirudi, kitu cha kwanza kilikuwa ni kuwajulia hali.
 
SEHEMU YA 43

“Oh! My kings!” (Oh! Wafalme wangu) alisema Cassian huku akiwaangalia, hapohapo akaanza kuwamwagia mabusu mfululizo.

Wakati hayo yote yakiendelea Evelyne alikuwa akifuatilia kwa karibu, mara kwa mara alikuwa akiwapigia simu watu hao na kuwauliza ni kitu gani kilichokuwa kikiendelea. Aliwalipa pesa zote na kilichokuwa kikisubiriwa ni kimoja tu, watoto hao watekwe na kuwaua kwa mikono yake.

“Mmefikia wapi?” aliuliza Evelyne.
“Hadija yupo ndani ya nyumba!”
“Sawa. Amekwishawateka?”
“Wewe unataka watekwe lini?”
“Hata kesho!”
“Haina shida!”

Kule ndani alipokuwa, msichana yule alikuwa na simu yake ndogo ambayo hakukuwa na mtu yeyote aliyekuwa akiiona, hiyo ndiyo aliyokuwa akifanya mawasiliano na wenzake waliokuwa wamempa kazi hiyo.

Aliambiwa kitu gani alitakiwa kufanya. Mipango ilikuwa imekamilika na kilichokuwa kikisubiriwa ni yeye kuwateka watoto hao na kuondoka nao.

Siku ambayo alitaka kufanya tukio hilo, akasubiri mpaka Cassian na mkewe waondoke nyumbani, walipofanya hivyo, saa 3:00 asubuhi akaelekea chumbani kwao, akachukua ufunguo wa gari aina ya Range SUV nyekundu na kwenda kufungua.

Mlinzi mmoja aliyekuwa mahali hapo alishangaa, haikuwa kawaida kwa mfanyakazi huyo kufungua mlango wa gari lolote lile, hakutaka kusubiri kuambiwa, akamfuata msichana huyo kwa lengo la kuzungumza naye.

“Sikujua!” aliita mlinzi huku akimsogelea.
“Naam kaka!”
“Vipi tena?”
“Vipi kuhusu nini?”

“Mbona unafungua gari. Kuna lolote?” aliuliza mlinzi huku akimwangalia msichana huyo.

“Nataka niwapeleke hospitali. Mama aliniachia maagizo nifanye hivyo!” alisema Sikujua.

“Uwapeleke hospitali! Eeh! Tangu lini umeanza kuwapeleka hospitali?” aliuliza mlinzi huyo huku akionekana kushangaa sana.

Sikujua hakutaka kujibu hilo, akatoka hapo, akaingia ndani ambapo akawachukua watoto hao, akawaingiza ndani ya gari na kuondoka nao.

Mlinzi alibaki akiashangaa. Kwanza hakuamini kama msichana huyo alikuwa akiwapelekea hospitalini lakini kilichomshangaza kabisa, iliwezekanaje msichana kama Sikujua ambaye kwa muonekano tu hakuonekana hata kujua kupiga honi ya gari awe anaendesha gari?
“Mmh!” aliguna mlinzi.
 
Back
Top Bottom