Viganja Mashavuni Mwangu

SEHEMU YA 29

Bila Naseku kuingilia kati basi hali ya Cassian ingekuwa mbaya mahali hapo. Oscar alionekana kukasirika, ilikuwa ni afadhali kucheza na maisha yake lakini si kucheza na dada yake huyo aliyeonekana kuwa kila kitu.

Watu waliokuwa pembeni baada ya kuona Naseku amemzuia mwanaume huyo nao ndiyo wakaingilia na kumzuia.

Oscar alikuwa akiongea peke yake huku akiwataka watu hao wamuachie ili amuonyeshee mwanaume huyo kwamba alikuwa mtu hatari aliyekuwa akiheshima katika mtaa huo.

Muda wote huyo Cassian hakuongea kitu, alibaki akiashangaa tu, mambo aliyokuwa akiyafanya mwanaume huyo yalimshangaza lakini akazuia hasira zake kwani kama angeamua kumpoteza kijana huyo, ilikuwa ni kuongea mara moja tu na wasingemuona tena katika dunia hii.

“Mbona mnanishika! Mbona mnagombelezea bhana?” aliuliza Oscar huku akiwa ameshikwa huku na kule.
“Tulia kwanza! Utaua!”

“Mimi nataka niue sasa! Hawa mbung’o ni kuwaua tu! Kwenda kwao kuwapigia misele dada zao hawataki! Jamani si mniache! Mbona mnanishika kama mtoto wenu,” alisema Oscar huku akionekana kuwa na hasira sana.

Naseku ndiye aliyemtuliza zaidi kaka yake na kumwambia kwamba mwanaume huyo hakuwa mtu mbaya, alikuwa mtu mzuri ambaye alifika mahali hapo si kwa lengo la kumtongoza kama walivyokuwa wanaume wengine bali alikuwa hapo kwa ajili ya kumsaidia mama yao.

Kidogo hilo likamfanya Oscar kutulia. Mama yao alikuwa mgonjwa ndani, alikuwa akisumbuliwa na mgonjwa wa miguu kuvimba, alikuwa kitandani mwaka wa pili, kipindi cha nyuma walikuwa wamesumbuka kumpeleka hospitalini lakini kikafika kipindi wakatulia kwani hawakuwa na msaada wowote wa kifedha.

Kidogo Naseku ndiye aliyeonekana kuwa msaada, yeye ndiye aliyekuwa akitafuta pesa kwa ajili ya kumsaidia mama yake na hata kununua chakula cha humo ndani.

Oscar hakuwa akijali, alichokuwa akikiangalia kilikuwa ni ulevi tu. Alikuwa mvuta bhangi na mtafunaji mirungi maarufu hapo Tandale. Maisha yake yaliishia hapo, alijua kabisa kwamba mwisho wa kila kitu ilikuwa ni lazima kufa.
 
SEHEMU YA 30

“Kwa hiyo yupo hapa kumsaidia bi mkubwa?” aliuliza Oscar.
“Ndiyo! Wewe kila mtu unayemuona unadhani kaja kunifuata mimi!” alisema Naseku huku akimwachia kaka yake aliyeonekana kunywea.

Hiyo ndiyo ikawa salama ya Cassian. Mpaka kufikia kipindi hicho hakukuwa na mtu aliyegundua kwamba alikuwa yeye. Pale alipokuwa kulikuwa na giza, alizibwa uso na giza lililokuwepo mahali hapo kwani hata Cassian mwenyewe hakumuona vizuri usoni.

Akachukuliwa na kuingizwa ndani, alishangaa kwamba ni kwa namna gani watu walikuwa wakiweza kuishi katika nyumba mbovu kama hiyo. Alibaki akishangaa kila kitu, kulikuwa na harufu mbaya humo ndani, hakukuwa na sakafu ya simenti, kulikuwa na ndoo za maji zilizotobokatoboka.

Hakutaka kujali sana, akapelekwa mpaka katika chumba alichokuwa amelala mama yake Naseku, alikuwa juu ya kitanda huku akiwa amewekewa chandarua kilichokuwa kimetonokatoboka na sehemu nyingine kilikuwa kimeshonwa.

Alichokiona, akashindwa kuvumilia, machozi ya uchungu yakaanza kutiririka mashavuni mwake. Aliumia mno moyoni mwake, mwanamke yule aliyekuwa kitandani alikuwa akiteseka, pale alipokuwa, hakukuwa na kitu kingine alichokuwa akikisubiria zaidi ya kifo tu.

“Tatizo nini?” aliuliza Cassian ambapo Naseku akaanza kusimulia kila kitu huku machozi ya uchungu yakianza kumtoka.

Ilikuwa ni stori mbaya iliyouchoma mno moyo wake. Hakuamini kama kungekuwa na mwanamke ambaye alikuwa amepitia maisha ya kumuumiza kama alivyokuwa amepitia mama yake Naseku.

Mwaka wa pili mfululizo mwanamke huyo alikuwa akiteseka, hakuwa akisimama, wala kutembea, maisha yake yalikuwa kitandani hapo kitu kilichoonekana kumtesa kila siku.

Walimpeleka hospitali lakini baada ya kuambiwa kwamba matatizo yake yangetibiwa kwa shilingi milioni kumi, wakakata tamaa na mwisho wa siku kumuweka ndani wakisubiri siku ifike na kufariki dunia.

Huruma nyingi ikamuingia Cassian kana kwamba aliyekuwa kitandani akiugua alikuwa mama yake wa kumzaa.

Hakutaka kuona mwanamke huyo akiendelea kuteseka, kwa kuwa alikuwa akimpenda binti yake kwa moyo wa dhati hakuwa na jinsi kumsaidia mwanamke huyo kwa kuamini kwamba ingekuwa rahisi kwa Naseku kuamini kwamba alikuwa akimpenda.
 
SEHEMU YA 32

Maisha yalibadilika haraka sana, hawakuwa wakiamini walichokuwa wakikipitia, wakati mwingine walihisi kama ni ndoto ambapo baada ya muda fulani wangeamka na kujikuta wakiwa kitandani.

Maisha yalikuwa ya raha, hakukuwa na kulia tena, hakukuwa na machozi tena na baada ya miezi miwili, mama Naseku akapona ugonjwa wa miguu na nyumba ile waliyokuwa wakitengenezewa ikamalizika kabisa.

“Naseku!” aliita Cassian baada ya kipindi kirefu kupita, siku hiyo alitaka kumkumbushia msichana huyo juu ya kile alichokuwa amemwambia nyuma.
“Abee!”

“Umependeza sana! Hakika ninauona uzuri wako kwa sasa. Siwezi kujuta kukuchagua wewe,” alisema Cassian huku akitoa tabasamu pana.
“Nashukuru sana!”
“Kuna kitu nahitaji kukwambia!”
“Kitu gani?”

“Kilekile cha siku zote kwamba ninakuhitaji sana! Ninahitaji nikuoe! Nimekaa na kukufanyia haya yote, ulistahili, ulitakiwa kuwa na maisha ya furaha, ufute machozi yako, uondoe maumivu makali moyoni mwako,” alisema Cassian.

Siku hiyo hakutumia nguvu sana, ilikuwa ni kama kumsukuma mlevi katika mteremko wa mlima. Msichana huyo akakubali kuwa mpenzi wake na hatimaye baada ya mwezi mmoja wakafunga ndoa na kuwa mume na mke.

Ilikuwa ni furaha kubwa kwa kila mmoja, Naseku yule, msichana masikini hatimaye maisha yake yalikuwa yamebadilika na kuwa bilionea mkubwa.

Kwa Cassian hicho ndicho kitu alichokuwa akikihitaji, moyo wake ulikuwa na furaha tele, alitaka kuoa na kupata mtoto na mabya zaidi kipindi hicho hakuwa akijua chochote kile kuhusu Evelyne aliyekuwa amemuacha kwa maumivu makali.

“Mume wangu! Sijaziona siku zangu,” alisema Naseku huku akimwangalia Cassian.
“Unasemaje?” “Sijaziona siku zangu!”
“Hebu rudia tena kwanza! Unasemaje?” aliuliza Cassian huku akionekana kutokuamini.

Wiki mbili tu zilitosha kuonyesha kwamba Naseku alikuwa mjauzito. Cassian hakuamini, kila wakati alikuwa akimwangalia mke wake, hakuamini kama kweli hatimaye alikuwa akienda kuitwa baba.

Alikuwa makini, alihitaji kumpenda mke wake kwa mapenzi ya dhati, alihitaji kumpa kila kitu alichokuwa akikiihitaji. Baada ya miezi minne wakaenda kupima ili kuona jinsi ya mtoto aliyekuwa naye Naseku tumboni.
 
SEHEMU YA 33

“Hongereni sana! Mkeo ana mimba ya watoto mapacha,” alisema daktari huku akimwangalia Cassian.
“Unasemaje? Mapacha? Wa kiume wa kike?” aliuliza Cassian huku akionekana kutokuamini.

“Wa kiume.”
“Nashukuru sana!”
Hiyo ndiyo ilikuwa furaha yake, hakuacha kwenda kliniki na mkewe, mara kwa mara walikuwa wakienda huku wakati mwingine wakitumia utra-sound kuangalia jinsi watoto walivyokuwa tumboni mwa mke wake.

Siku ziliendelea, wakati Naseku akiwa amefikisha miezi saba ya ujauzito wake ndiyo hali ya tofauti ikaanza kuonekana kwa mapacha hao.

Siku hiyo walikwenda kupima kama kawaida, kuwaangalia watoto waliokuwa tumboni kuona walikuwa wakiendeleaje.

Baada ya kuwapiga picha, dokta alionekana kuwa tofauti na siku nyingine na hata ile karatasi ngumu ambayo ingeonyesha jinsi watoto walivyokuwa tumboni hakutaka kuwaonyeshea.

“Kuna nini?” aliuliza Cassian.
“Mmh!” aliguna tu daktari.
“Hebu tumabie kuna nini! Hebu nione hiyo karatasi,” alisema Cassian huku akijaribu kuichukua karatasi hiyo ngumu kutoka mkononi mwa daktari.

“Subiri kwanza!”
Cassian hakutaka kukubali, hapohapo akampokonya daktari karatasi ile ngumu na kuanza kuiangalia.

Macho yake yalipotua kwenye karatasi ile hakuamini alichokiona, ghafla tu machozi yakaanza kumtoka, akapiga magoti chini na kuanza kulia kama mtoto.

“Mume wangu kuna nini?” aliuliza Naseku huku akimwangalia mume wake, naye mwenyewe alitaka kuiona karatasi hiyo, cha kushangaza mumewe akamzuia, hakutaka kuiona.

“Hapana! Hebu niambie kuna nini! Watoto wamekufa au? Lakini mbona nawasikia wakichezacheza!

Niambie kuna nini,” alisema Naseku huku akihitaji kuiangalia karatasi hiyo ambayo Cassian hakutaka kabisa kumuonyeshea kwa kuamini kwamba angeumia sana kitu ambacho hakutaka kuona kikitokea.

JE, NINI KITAENDELEA?
 
SEHEMU YA 34

Naseku hakutaka kuelewa kitu, aliamini kabisa kulikuwa na tatizo kwa watoto wake na hivyo kutaka kuangalia kile kilichokuwa kimepigwa tumboni mwake, hali ya watoto wake kwani alichohisi ni kwamba walikuwa wamefariki dunia.

Bado Cassian alikataa, msimamo wake ulikuwa uleule, alijua kwamba kama mke wake angekiona kile kilichokuwa kimetokea kwa mapacha wake basi angeumia kupita kawaida.

Naseku hakukubali, bado alihitaji kuona tena huku akilia kabisa kitu kilichomfanya Cassian kumpa karatasi ile ngumu na kuangalia kilichokuwa kikiendelea.

Hakuamini, watoto wake mapacha waliokuwa tumboni mwake walikuwa na kila dalili za kuungana. Moyo wake ulimuuma mno, hakuamini alichokuwa akikiangalia lakini wakati mwingine alihisi kwamba hata kama wangeungana, bado wangeweza kuwatenganisha kwa kuwa tu walikuwa na pesa.

Hiyo ndiyo hali iliyokuwa imetokea, kila mmoja alihuzunika mno, mioyo yao iliuma, ilichoma kupita kawaida.

Wakakumbatiana na kumshukuru Mungu kwa kuamini kwamba kila kitu kilichokuwa kikitokea, Mungu alikipanga na kamwe hakukuwa na mtu wa kufanya vinginevyo.

Mara kwa mara walikuwa wakifika hospitalini hapo kwa ajili ya kuangalia watoto wao ambao bado hawakuwa wamezaliwa, Cassian alikuwa na muda mwingi wa kuangalia picha za mapacha walioungana kama watoto wake ambao hawakuzaliwa, alitaka kuangalia maisha yao, waliishi vipi na hata mavazi yao yalikuwaje.

Hapo ndipo akaamua kuwafuatilia mapacha wa aina hiyo, Abby na Brittany Hansel waliokuwa wakiishi nchini Marekani. Kila alipoziangalia picha za mapacha hao moyo wake ulimuuma, hakuamini kama kweli Mungu aliamua kumpa watoto wa namna hiyo na wakati alikuwa amemuomba kwa kipindi kirefu mno.

“Mungu! Kama Abby na Brittany wanaishi, nina uhakika hata watoto wangu wataishi pia,” alijisemea Cassian huku akiangalia picha za mapacha hao, hakuishia hapo tu bali aliangalia za wengine wengi ambao wote kwa pamoja walimgusa sana moyoni mwake.

Siku zikaendelea, Naseku hakuonekana kuwa na furaha, muda mwingi alionekana kuwa na huzuni mno. Mama yake alitumia muda mrefu kumtia moyo, hakuataka kumuona akiwa kwenye hali hiyo kila siku.
 
SEHEMU YA 35

Ukiachana na mama yake, pia Cassian alikuwa na kazi kubwa ya kumfariji, alimsisitizia kwamba kila kitu kiilichokuwa kikiendelea ni kwamba Mungu alipanga iwe hivyo, hakutaka kumkatisha tamaa, inawezekana katika mapacha hao kungekuwa na rais wa Tanzania.

“Hutakiwi kulia mpenzi,” alisema Cassian huku akimwangalia mke wake aliyekuwa kwenye maumivu makali.
“Inaniuma sana!”

“Ni bora kupata watoto kuliko kukosa kabisa. Usihuzunike, kuwa na mapacha walioungana si kwamba ndiyo mwisho wa kuishi, bado maisha yanaendelea kama kawaida mke wangu,” alisema Cassian huku akimkumbatia mke wake huyo.

Siku na miezi ziliendelea kukatika mpaka Naseku alipofikisha miezi tisa na hivyo kujisikia uchungu na kwenda kujifungua katika Hospitali ya Ocean Road.

Siku hiyo Cassian alikuwa na presha kubwa, hakuamini kama angekwenda kuwa baba.

Moyo wake ulibadilika, huzuni kubwa aliyokuwa nayo tangu agundue kwamba mke wake angejifungua mapacha walioungana ikatoweka na furaha ya ajabu kumuingia moyoni mwake.

Alikuwa nje ya chumba cha kujifungulia akiwa na wazazi wake, hakukaa chini, alikuwa amesimama huku kila wakati mikono yake ikiwa imekutanishwa kana kwamba alikuwa akisali.

“Dad! I am going to be a father, can you believe that?” (nakwenda kuwa kuwa baba, unaweza kuamini hilo baba?) aliuliza Cassian huku akiwa na tabasamu pana usoni mwake.

“I am so proud of you my son!” (najivunia wewe sana kijana wangu)
“They are conjoined twins. It doesn’t matter, I just want to see them,” (ni mapacha walioungana. Haijalishi, ninataka kuwaona tu) alisema Cassian huku kila wakati akiusogelea mlango wa chumba kile na kutegesha sikio lake.

“Come and give me a hug,” (njoo unikumbatie) alisema mama yake ambaye alisimama na kukumbatiana na kijana wake.

Waliendelea kusubiri mpaka baada ya dakika hamsini ambapo mlango ukafunguliwa na daktari kuwaambia kwamba walishindwa kufanya kazi yao ndani kwani ilishindikana kabisa Naseku kujifungua kwa hali ya kawaida kwani watoto hao walikuwa wawili kwa pamoja na njia ilikuwa ndogo.
 
SEHEMU YA 36

Hawakuwa na jinsi, wakakubaliana na hali iliyokuwepo hivyo Naseku kujifungua kwa njia ya upasuaji kitu ambacho kilifanikiwa kwa asilimia mia moja.

Moyo wa Cassian ukawa na furaha tena, hakuamini kama kweli siku hiyo aliitwa baba baada ya miaka mingi kupita.

Hawakuruhusiwa kumuona Naseku wala watoto siku hiyo, waliambiwa wasubiri mpaka siku mbili zipite ndiyo wangepewa nafasi ya kuwaona watoto hao.

Nyumbani, hakukukalika kwa amani, muda wote Cassian alikuwa akitamani kuwaona watoto wake.

Aliwaita watu wa decoration na kuweka nyumba katika staili ya kitoto na kumkaribisha mke wake, nyumba ilipendeza, kulikuwa na kila kitu ambacho mtoto alitakiwa kuwa nacho, kitanda kikubwa, midoli na vitu vingine vingi.

Hakwenda kazini, muda mwingi alikuwa akishinda hospitalini kuliko hata nyumbani.

Baada ya siku mbili, akaruhusiwa kumuona mke wake, macho yake yalipotua kwa mwanamke huyo tu, uso wake ukawa na tabasamu pana, alimwangalia, alikuwa mwanamke aliyemfanya kujiona mwanaume aliyekamilika, akamsogelea mahali pale na kumshika mkono, hapohapo Naseku akafumbua macho yake na kuangaliana.

“Mke wangu...” aliita Cassian huku akimwangalia mke wake aliyekuwa akitabasamu tu.

Moyo wake ukafarijika, akajisikia amani moyoni mwake kuliko kipindi chochote kile. Hapohapo manesi wakamletea watoto wake waliokuwa katika chumba kingine kabisa, alipowaona, japokuwa walikuwa wameungana maeneo ya kichwani, upande wa kulia kwa mtoto mmoja na kushoto kwa mwingine lakini moyo wake ulisikia furaha ya ajabu ambayo hakuwahi kuisikia kabla.

“Watoto wangu!” alisema Cassian huku akiwachukua, machozi ya furaha yalikuwa yakimtoka.

Walikuwa watoto wazuri wa kiume waliochukua sura yake, walikuwa wadogo lakini aliwaona jinsi alivyokuwa amefanana nao. Alitabasamu, alicheka kwa furaha, akamuinamia mke wake na kumbusu shavuni.

“Nashukuru kwa kunipa watoto na kunifanya niwe mzazi,” alisema Cassian huku akimwangalia mkewe, alishindwa kumshukuru vipi mke wake huyo.

Naseku hakujibu kitu chochote zaidi ya kuachia tabasamu pana.

Moyo wake ulifurahia, aliwapenda watoto wake, hakuangalia namna walivyokuwa, kwake, hao walikuwa kila kitu katika maisha yake.
 
SEHEMU YA 34

Naseku hakutaka kuelewa kitu, aliamini kabisa kulikuwa na tatizo kwa watoto wake na hivyo kutaka kuangalia kile kilichokuwa kimepigwa tumboni mwake, hali ya watoto wake kwani alichohisi ni kwamba walikuwa wamefariki dunia.

Bado Cassian alikataa, msimamo wake ulikuwa uleule, alijua kwamba kama mke wake angekiona kile kilichokuwa kimetokea kwa mapacha wake basi angeumia kupita kawaida.

Naseku hakukubali, bado alihitaji kuona tena huku akilia kabisa kitu kilichomfanya Cassian kumpa karatasi ile ngumu na kuangalia kilichokuwa kikiendelea.

Hakuamini, watoto wake mapacha waliokuwa tumboni mwake walikuwa na kila dalili za kuungana. Moyo wake ulimuuma mno, hakuamini alichokuwa akikiangalia lakini wakati mwingine alihisi kwamba hata kama wangeungana, bado wangeweza kuwatenganisha kwa kuwa tu walikuwa na pesa.

Hiyo ndiyo hali iliyokuwa imetokea, kila mmoja alihuzunika mno, mioyo yao iliuma, ilichoma kupita kawaida.

Wakakumbatiana na kumshukuru Mungu kwa kuamini kwamba kila kitu kilichokuwa kikitokea, Mungu alikipanga na kamwe hakukuwa na mtu wa kufanya vinginevyo.

Mara kwa mara walikuwa wakifika hospitalini hapo kwa ajili ya kuangalia watoto wao ambao bado hawakuwa wamezaliwa, Cassian alikuwa na muda mwingi wa kuangalia picha za mapacha walioungana kama watoto wake ambao hawakuzaliwa, alitaka kuangalia maisha yao, waliishi vipi na hata mavazi yao yalikuwaje.

Hapo ndipo akaamua kuwafuatilia mapacha wa aina hiyo, Abby na Brittany Hansel waliokuwa wakiishi nchini Marekani. Kila alipoziangalia picha za mapacha hao moyo wake ulimuuma, hakuamini kama kweli Mungu aliamua kumpa watoto wa namna hiyo na wakati alikuwa amemuomba kwa kipindi kirefu mno.

“Mungu! Kama Abby na Brittany wanaishi, nina uhakika hata watoto wangu wataishi pia,” alijisemea Cassian huku akiangalia picha za mapacha hao, hakuishia hapo tu bali aliangalia za wengine wengi ambao wote kwa pamoja walimgusa sana moyoni mwake.

Siku zikaendelea, Naseku hakuonekana kuwa na furaha, muda mwingi alionekana kuwa na huzuni mno. Mama yake alitumia muda mrefu kumtia moyo, hakuataka kumuona akiwa kwenye hali hiyo kila siku.
Shunie your back..... Karibu tena na pole kwa ban
 
SEHEMU YA 37

Waliendelea kukaa hospitali hapo kwa siku mbili zaidi na ndipo wakaruhusiwa huku Cassian akiwa amewapa watoto wake majina ya Walter na Walker.

Walikuwa na sura nzuri, kila mtu aliyekuwa akifika nyumbani na kuwaangalia, alidiriki kusema kwamba Walter na Walker walikuwa na sura nzuri mno.

Kila mtu akawapenda, watu wengi wakasikia habari zao na kutaka kwenda huko kuwaona.

Wengine walimfuata Cassian na kumshauri kwamba alitakiwa kutumia kiasi cha fedha kuwapeleka watoto hao nchini India kwa ajili ya kutenganishwa lakini alikataa, katika maisha yake aliamini kitu kimoja tu kwamba Mungu anaporuhusu jambo fulani kutokea, huruhusu kwa kusudi maalumu.

“Kuungana si tatizo! Mungu aliamua iwe hivyo, kwa nini sisi wadamu tupingane naye?” aliuliza Cassian kila alipokuwa akiambiwa mambo ya kuwatenganisha watoto wake.

Walikuwa watoto wenye afya tele ambao waliungana vichwa vyao. Kwa jinsi walivyokuwa wameungana, hata kama Cassian angekubaliana na kila mtu kwenda kuwatenganisha ingeshindikana kabisa kutokana na watoto hao kuchangia ubongo.

Pale walipokuwa wameungana kulikuwa na mishipa mikubwa, mingi iliyokuwa ikipitisha damu, kitendo cha kuwatenganisha kilimaanisha kwamba ni lazima mishipa hiyo ikatwe na sehemu ya ubongo ambao walikuwa wakitumia pamoja iondolewe kitu ambacho kingemaanisha kifo chao.

Lilikuwa jambo gumu mno kuwatenganisha, Cassian alikubaliana na kila kitu, alikuwa tayari kuwaona watoto wake wakiendelea kukua kwenye hali ile kuliko kuwatenganisha au kuwaua wote.

Watoto waliendelea kuwa kwenye uangalizi mkubwa mpaka baada ya kufikisha miezi miwili ambapo wazazi hao wakaamua kuanza kutafuta mfanyakazi kwa ajili ya kuwaangalia watoto hao.

Kitu cha kwanza kabisa walitaka kwenda kijijini kuchukua msichana wa kuwaangalia watoto hao lakini baada ya siku nne, Cassian akapigiwa na mjomba wake, Marcus ambaye alimwambia kwamba angewapa mfanyakazi mzuri kwa ajili ya kukaa na watoto hao.

“Anajua kutunza watoto?” aliuliza Cassian.

“Hilo si swali! Alimtunza Jackson na Careen mpaka walipoanza kuongea,” alijibu mjomba huyo, wakati huo walikuwa wakiongea uso kwa uso.
 
SEHEMU YA 38

“Nashukuru sana! Naomba uniitie huyo msichana, nitamlipa kiasi chochote kile,” alisema Cassian.
“Hakuna shida.”

*** Ilikuwa ni rahisi kwa Evelyne kusahau kila kitu kilichotokea katika maisha yake, kusahau tarehe ya siku yake ya kuzaliwa, kuwasahau watu waliomtendea mabaya kuliko kumsahau Cassia na mambo yote aliyokuwa ameyafanya.

Ilikuwa ni aibu kubwa, hakutoka ndani, kila alipokuwa chumbani kwake alikuwa mtu wa kulia tu, alihuzunika, aliumia moyoni mwake na wakati mwingine alihisi kwamba ilikuwa ni afadhali kujiua kuliko kuendelea kuishi.

Rafiki yake, Mwajuma ndiye aliyekuwa karibu naye, yeye ndiye aliyekuwa akimbembeleza usiku na mchana na hata msichana huyo alipotaka kufanya maamuzi magumu ya kutaka kujiua, Mwajuma alikuwa akimuokoa, alifanya hivyo mara tatu kwa nyakati tofauti.

Alimchukuia Cassian, aliilaani siku aliyokutana na mwanaume huyo, aliwachukia wanaume wote duniani hata kama wengine hawakumfanya kile alichofanyiwa na Cassian.

Alilia sana, alihuzunika mno na moyo wake kuchomwa na kitu cha moto kilichokuwa na ncha kali.

Siku zikakatika, alijiapiza kwamba ilikuwa ni lazima kulipiza kiasi kwa Cassian, kama alikuwa amemuumiza kwa staili ile na yeye ilikuwa ni lazima kumuumiza kwa pigo lenye maumivu kama lile.

Kwa mwaka mzima alikuwa chumbani, ni mara chache tu ndizo alizokuwa akitoka ndani, tena usiku, kila alipokuwa akipita kwenye mitandao ya kijamii, watu walimcheka, walimdhihaki kwa kile kilichokuwa kimetokea na hivyo moyo wake kubaki na kidonda kikubwa ambacho hakudhani kama kuna siku kingekuja kupona.

Mwajuma ndiye aliyekuwa akifuatilia kila kitu kilichokuwa kikiendelea, yeye ndiye aliyemwambia Cassian kwamba alikuwa amepata mwanamke mwingine, wa uswahilini, asiyejua hata thamani ya dola ya Kimarekani kwa pesa ya Kitanzania.
 
Back
Top Bottom