Shunie
JF-Expert Member
- Aug 14, 2016
- 157,400
- 465,165
- Thread starter
- #181
SEHEMU YA 44
Hakutaka kubaki kimya, alichokifanya ni kumpigia simu Cassian. Mwanaume huyo aliyekuwa ofisini alipoona simu ya mlinzi wa getini ikiingia, akaanza kuogopa, haikuwa kawaida, akili yake ilimwambia kwamba inawezekana kulikuwa na tatizo limetokea nyumbani.
Kabla ya kuipokea akaanza kujiuliza maswali mengi yasiyokuwa na majibu kwamba kabla ya kuondoka nyumbani kulikuwa na jambo baya gani lililokuwa limetokea nyumbani?
Hakuna! Sasa kwa nini mlinzi huyo alikuwa akimpigia simu? Kulikuwa na nini? Akapiga moyo konde na kupokea simu.
“Hamisi! Kuna nini?”
“Eti ulimwambia Sikujua awapeleke hospitalini watoto?” lilikuwa swali la kwanza kabisa, swali ambalo lilimshtua mno Cassian.
“Unasemaje?”
“Sikujua kawapeleka watoto hospitalini. Kachukua gari na kuondoka nalo huku watoto wakiwa humo,” alisema Hamisi maneno ambayo yalimfanya Cassian kuinuka kwenye kiti huku akionekana kuchanganyikiwa.
“Unasemaje?” aliuliza, akasimama, mwili ulikuwa ukimtetemeka na kijasho chembamba kumtoka.
**** Cassian hakuamini alichokuwa amekisikia kutoka kwa mlinzi, alimuuliza tena na tena na jibu lilikuwa lilelile kwamba dada wa kazi za ndani, Sikujua aliyekuwa akimwamini sana aliondoka na watoto nyumbani kwake, na alipokuwa ameelekea, hakukuwa na aliyepafahamu.
Alichanganyikiwa, haraka sana akakata simu na kuwapigia polisi, alipowapa taarifa, wakamwambia kwamba wangefika nyumbani kwake kwa ajili ya kuzungumza, ilikuwa ni lazima wajue ni kitu gani kilitokea mpaka mfanyakazi huyo kuondoka na watoto.
Yeye mwenye akaondoka ofisini, hakutaka kumpigia simu mke wake kwa kuona kwamba angemchanganya, ilikuwa ni lazima apambane yeye kama yeye kuona ingekuwaje ndipo amwambie mkewe kilichokuwa kimetokea.
Njiani, alionekana kuwa na mawazo mengi, alishindwa kabisa kuyazuia machozi kumtoka, moyo wake uliuma na kuchoma, kile kilichokuwa kimetokea kilikuwa kama ndoto kwake, hakuamini kama Sikujua angeweza kufanya kitu kama hicho.
Hakuchukua muda mrefu akafika nyumbani kwake, hakuliingiza gari, akateremka na kumfuata mlinzi, hata kabla hajamfikia tayari polisi wakafika mahali hapo na wote kumfuata mlinzi ambaye alianza kuhadithia kila kitu kilichokuwa kimetokea.