Viganja Mashavuni Mwangu

Viganja Mashavuni Mwangu

Sio hatupendani huyo ana hasira za kuachwa na acha avune tu alichopanda alifanya dhambi sana kumsingizia baba wa watu bora angemwambia ukweli tatizo lake

Kinacho m-cost Evelyn ni uongo wake wa kutokua mkweli kuhusu tatizo lake la kutozaa... okay... issue ya kumuadabisha mwanamke yoyote atakaye kua na Cassian hapo ndiyo anapokosea...

Ngoja tuone, kama hajafa mdomo wazi...
Na Cassian tayari alishaanza kusifia mwanamke kule Bar alipoenda kula...


Cc: mahondaw
 
Ngoja tuone mbele uko itakavyokuwa
Kinacho m-cost Evelyn ni uongo wake wa kutokua mkweli kuhusu tatizo lake la kutozaa... okay... issue ya kumuadabisha mwanamke yoyote atakaye kua na Cassian hapo ndiyo anapokosea...

Ngoja tuone, kama hajafa mdomo wazi...
Na Cassian tayari alishaanza kusifia mwanamke kule Bar alipoenda kula...


Cc: mahondaw
 
SEHEMU YA 22

Mwajuma alishangaa, ilikuwa ni asubuhi sana hata kutoka ndani hakuwa ametoka, alijiuliza sababu ya msichana huyo kulia namna hiyo, alionekana kuumia, alionekana kuwa na kitu moyoni mwake, ilikuwaje alie kwa uchungu namna ile na wakati siku hiyo ilikuwa ni ysiku ya kufunga ndoa na bilionea mkubwa Afrika Mashariki.

Alijaribu kumbembeleza anyamaze lakini Evelyne hakunyamaza, alikuwa akilia mfululizo, tena kilio kikali kilichojaa kwikwi. Aliendelea kulia kwa dakika ishirini nzima ndipo akanyamaza na kuanza kumwambia Mwajuma kilichokuwa kimetokea.

“Haiwezekani!” alisema Mwajuma huku akimwangalia rafiki yake huyo.
“Ameniacha! Cassian ameniacha,” alisema Evelyne huku kila wakati akiyafuta machozi.

Huo ndiyo ulikuwa ukweli, aliumia mno moyoni mwake, kilichokuwa kimetokea hakukiamini, aliona kila kitu kilichokuwa kikiendelea kama ndoto fulani ambapo baada ya dakika chache angeshtuka kutoka usingizini.

Hawakujua sababu ya Cassian kuchukua uamuzi wa ghafla namna hiyo kwani usiku uliopita tu alikuwa na furaha tele na alimuonyeshea msichana huyo mapenzi yote, sasa iweje abadilike namna hiyo?

“Au ile meseji uliyomtumia ndiyo chanzo?” aliuliza Mwajuma.
“Hapana! Haikumfikia?”
“Una uhakika? Kwako ilionyeshaje? Kama meseji haikwenda inakuonyeshea kwa kuweka kialama chekundu, sasa kama ile ilikwenda, kwa nini kialama hakikuonekana?” aliuliza Mwajuma maswali ambayo yalianza kumpa jibu Evelyne.

“Mmh!”
“Nahisi meseji aliipata ila aliifuta na hakutaka kukuonyeshea dalili zozote zile!” alisema Mwajuma huku akimwangalia msichana huyo.
“Inawezekana!”

“Kwa hiyo utafanyaje?”
“Nimeaibika Mwajuma. Cassian ameniumiza. Kwa pesa nilizokuwa nazo kwenye akaunti yangu, nitazitumia hata zote kumuua mwanamke yeyote atakayekuwa naye, kama kuumia, na yeye aumie kwa kumuua msichana ampendaye!” alisema Evelyne huku akionekana kuwa na hasira kali.

“Wewe tu! Na mimi nitakusaidia. Ukiua kwa kisu, nitaiweka maiti kwenye gunia, sitokuacha ila huyu mbwa lazima tumkomeshe,” alisema Mwajuma huku naye akionekana kuwa na hasira sana kwani mafanikio ambayo angeyapata rafiki yake yangekuwa sawa na mafanikio yake.
 
SEHEMU YA 23

Cassian aliamshwa na alamu ya simu yake, haraka sana akashtuka kutoka usingizini, mwili wake ulikuwa umechoka kwani usiku uliopita alichelewa kulala kutokana na kwenda baa kunywa huku akiwa na rafiki yake, Osman.

Akaanza kuangalia huku na kule, hakuwa sawa, akayapeleka macho yake katika saa yake ya ukutani ambayo ilimuonyesha kwamba tayari ilikuwa ni saa 12:00.

Akapeleka mkono wake pembeni kwa lengo la kumgusa mpenzi wake, Evelyne, alikuwa amesahau kile kilichotokea usiku uliopita, alipomkosa, kumbukumbu zake zikamjia kwamba aliachana na msichana huyo.

Hapo ndipo mawazo juu ya Evelyne yalipoanza kurudi kichwani mwake. Alijiona shujaa, alifanya kitu ambacho kwa wanaume wengine wasingeweza kufanya, alipoteza muda wake, alilia kwa kuwa aliumia sana lakini baadaye, kila kitu kilichokuwa kimetokea hakikuwa kama kile alichokuwa amekifikiria.

Wakati akiwaza hayo, picha ya msichana mmoja ikaja kichwani mwake, hakuwa msichana mwingine zaidi na Naseku. Alimkumbuka binti huyo wa kimasai, jinsi alivyokuwa mrembo, umbo matata ambalo lilitosha kumfanya mwanaume yeyote duniani kuwa kwenye mhemko mkubwa.

Akatoa tabasamu, kwa jinsi alivyokuwa, alihisi kabisa kwamba msichana huyo alistahili kuwa mke wake, alikuwa msichana masikini, aliyetafuta maisha kwa kuwa mhudumu katika mgahawa uliokuwa Kinondoni, hakutaka kujali kwa kuwa alikuwa na pesa, aliamini kwamba angeweza kumbadilisha na kuwa na muonekano mzuri kama ilivyokuwa kwa Kim Kardashian.

Hakuwa amezoeana naye, ila aliamini kwamba kama angemtumia rafiki yake, Osman ingekuwa rahisi kuonana na msichana huyo kisha kuzungumza naye. Hapohapo pasipo kuchelewa akaichukua simu yake na kumpigia rafiki yake huyo.
“Vipi mzee mzima?” ilisikika sauti ya Osman kwenye simu.

“Poa tu! Una nafasi leo?” aliuliza Cassian.
“Yeah! Hasa kwa mtu kama wewe ukiuliza hivyo! Kuna ishu?” aliuliza Osman.
“Ndiyo! Nataka unipeleke kwa yule msichana!”

“Msichana gani?”
“Naseku!”
“Duh! Mpaka jina lake umelikariri! Wewe noma!”
“Hahaha! Itawezekana?”
“Haina shida!”
 
SEHEMU YA 24

Huyo ndiye mtu aliyekuwa akimfikiria muda huo, taswira ya Naseku ilipomjia kichwani, ilimkaa vilivyo. Alitabasamu na muda mwingine kutoa kicheko cha chini.

Aliamini kwamba kama angezungumza na msichana huyo basi angeweza kukubaliana naye na kuwa mpenzi wake.
Akajiandaa, alipomaliza, akaondoka zake kuelekea ofisini. Njiani, alikuwa akiangalia huku na kule, kila alipowaangalia watu aliokuwa akipishana nao, moyo wake ulikuwa na furaha kwani alihisi kila mtu aliyekuwa akimwangalia alijua kilichokuwa kimetokea kati yake na msichana aliyetokea kumchukia mno, Evelyne.

“Bosi! Karibu sana,” alimkaribisha sekretari wake huku akiwa na tabasamu pana.
“Ahsante sana!”
“Na leo kumbe unakuja kazini!”
“Kwa nini nisije sasa?”
“Si unakwenda kwenye harusi!”
“Harusi gani?”
“Jamani! Yaani umesahau?”

Cassian hakujibu kitu zaidi ya kutoa tabasamu na kuingia ofisini kwake. Moyo wake ulikuwa na furaha tele, alijisikia amani kuliko siku nyingine. Alijua kwamba Evelyne alichanganyikiwa lakini hilo hakutaka kujali.

Kila mfanyakazi alishangaa, wengi waliamini kwamba siku hiyo ilikuwa ni siku ya harusi ya bosi wao. Wanakamati walikamilisha ripoti yao, wakatengeneza ratiba lakini kilichowashtua ni kumuona bosi wao akiwa ofisini, ilikuwaje awe mahali hapo na wakati siku hiyo ilikuwa ni ya kufunga ndoa na Evelyne.

Kila mmoja alikuwa na maswali mengi, alilijua hilo, alichokifanya ni kutoka na kuanza kuzungumza nao. Aliwaambia kwamba hakukuwa na harusi, aliahirisha kila kitu baada ya msichana yule kumdanganya.

“Alikudanganya? Kivipi?” aliuliza mfanyakazi mmoja.
“Alinifanya nijue sina nguvu ya kumpa msichana mimba!”
“Kumbe unazo?”

“Tena nyingi! Naweza kujaza hata mbuga ya wanyama!” alisema Cassian na wote kucheka kwa sauti.
Huo ndiyo ulikuwa mwanzo wa kuvujisha kile kilichokuwa kimetokea. Kila mfanyakazi aliyeipata, akachukua picha ya Evelyne na kuiweka mtandaoni, kama alivyokuwa ametamba sana katika mitandao ya kijamii ndiyo hiyohiyo iliyotumika kumchafua.

Waandishi wa habari hawakuwa mbali, baada ya kuipata taarifa hiyo, kitu cha kwanza kilikuwa ni kumpigia simu Evelyne, simu yake iliita bila kupokelewa mpaka pale ilipozima.
 
Back
Top Bottom