Viganja Mashavuni Mwangu

Viganja Mashavuni Mwangu

Sehemu ya 85

Katika kila njia alizopita kulionekana kuwa na nafuu kwake, na kwa sababu ilikuwa ni siku ya Jumamosi, siku ambayo mashabiki wa timu za mipira, raga na kriketi walikuwa wakienda viwanjani, njiani alikuwa akipishana na watu wengi kiasi kwamba kwa mhalifu kama yeye ilikuwa rahisi sana kwenda bila kukamatwa.

Aliendesha gari mpaka katika kituo cha mafuta cha Shell ambapo haraka sana akateremka na kuchukua kadi yake, akaiingiza katika kitundu kidogo, akaandika lita alizotaka na kuweka mpitra katika mdomo wa gari lake, akajaza, akaichukua gari lake na kuondoka mahali hapo.

Wakati hayo yote yakiendelea, hakujua kama alikuwa akitafutwa na polisi. Wakati akikaribia Bristol ndipo alipoamua kufungua redio kusikiliza kilichokuwa kikiendelea. Katika kila redio taarifa ambayo ilikuwa ikitangazwa sana ilikuwa ni kuhusu tukio lile lililotokea hospitalini.

Alisikiliza kwa makini, alitaka kujua kama mapacha hao walikufa au la. Kila aliposikiliza, alisikia kwamba walikuwa kwenye hali mbaya m,no ambapo muda wowote ule wangefariki dunia.

Hakuhuzunika, ndiyo kwanza akafurahia kwa kuona kwamba alimkomoa na kama kukosa basi wakose wote. Wakati akiendelea kusikiliza ndipo akapokea taarifa kwamba tayari mtu aliyefanya tukio hilo alijulikana, na mpaka jina lake likatajwa.

Hakushangaa kwani hata alipoondoka nyumbani aliwaacha polisi wakiingia hapo. Aliendelea mbele mpaka kufika Bristol huku akiwa amechoka.

Wazo lake kwa kipindi hicho lilikuwa ni kuendelea na safari kwa gari lake mpaka katika kituo cha treni cha Bristol Packway.
 
SEHEMU YA 86

Akalipaki gari lake nje ya kituo hicho katika sehemu husika na kisha kuelekea ndani. Alipoanza kushusha ngazi, kitu cha kwanza kabisa alichokutana nacho kilikuwa ni picha zake nyingi zilizobandikwa kwenye kuta mbalimbali.

Alishtuka, hakuamini kama kwa saa chache angekuwa kwenye kila kona nchini Uingereza.

Haraka sana akafungua begi lake, akatoa kofia yake nyekundu na kuivaa, baada ya hapo akaanza kutembea kwa kujiamini mpaka sehemu kulipokuwa na watu wengi ambapo walikuwa wakiweka sarafu kwenye kifaa kimoja na chuma kujifungua.

Alipofika, naye akaweka, chuma kikapanda na kuingia ndani. Kwa mwendo wa haraka sana akaanza kuelekea kulipokuwa na watu wengi waliokuwa wakisubiri treni na kusimama hapo.

“Treni itafika baada ya dakika chache, ndiyo inaondoka katika kituo cha Reading, baada ya dakika chache itaingia mahali hapa,” ilisikika sauti nyororo ya msichana kwenye spika zilizokuwa humo.

Moyo wake ulikuwa ukimuomba Mungu, alitaka kuondoka mahali hapo salama kwani kama angeendelea kubaki nchini Uingereza ilimaanisha kwamba huo ndiyo ungekuwa mwisho wake.

Wakati akiwa amesimama mahali hapo, akasikia watu waliokuwa nyuma yake wakilizungumzia suala la mapacha wale kupuliziwa gesi ndani ya gari.

Akajificha zaidi lakini ghafla watu wale wakanyamaza kana kwamba waliambiwa wanyamaze, wakati akijiuliza kuhusu ukimya huo wa ghafla, akashtukia akishikwa bega kwa nyuma na kutakiwa kugeuka.

“Turn around, please...” (geuka tafadhali) ilisikika sauti ya mwanaume mmoja nyuma yake.

Je, nini kitaendelea?
 
Wahenga nao tunamsemo kuwa, hakuna marefu yasiyo na ncha!
Edmund mwisho wake u karn mnoo!!

Shunie asanteh sana
 
SEHEMU YA 89

Catherine alikuwa akilia, hakuamini kilichokuwa kimetokea, kitendo cha kuambiwa kwamba rafiki yake, Walter alikuwa amepuliziwa gesi yenye sumu moyo wake ulimuuma mno na kumfanya kulia kila wakati.

Alijiona kuwa yeye ndiye mtu aliyesababisha lile lililotokea, alijihukumu moyoni mwake na muda wote alikuwa akiwaambia wazazi wake kwamba yeye ndiye alikuwa chanzo kwani bila yeye aliamini mapacha hao wasingeweza kupata tatizo walilokuwa wamelipata.

Kwa kuwa alikuwa akijisikia nafuu, hakutaka kubaki katika chumba kile alicholazwa, aliomba sana aende katika chumba walichokuwa mapacha wale ili aone walikuwa wakiendeleaje.

Hilo lilikuwa gumu kuruhusiwa kwa kuwa tangu tukio la kupuliziwa gesi iliyokuwa na sumu hakukuwa na mtu yeyote aliyeruhusiwa kuingia ndani ya chumba kile.

Kila kona duniani ni stori za mapacha hao ndizo zilizokuwa zikisikika. Watu waliichukua picha ya Edmund na kuiweka katika mitandao ya kijamii, Watanzania hawakuwa nyuma, wao ndiyo walikuwa watu wa kwanza kuichukua picha hiyo na kuisambaza kwa nguvu zote kwani hakukuwa na mtu aliyehitajika mikononi mwa polisi kama ilivyokuwa kwa Edmund.

Mbali na mapacha hao, Walter na Walker pia wazazi wao walikuwa hoi kitandani. Tangu walipolazwa, mpaka inaingia siku ya pili hakukuwa na yeyote aliyerudiwa na fahamu.

Mapigo ya mioyo yao ilikuwa ikidunda kwa mbali sana hali iliyoonyesha kwamba muda wowote ule watu hao wanne wangefariki dunia.

Wakati hayo yote yakiendelea, tayari taarifa za kwanza zilionyesha kwamba polisi walikwenda nyumbani kwa Edmund siku ileile lakini hawakufanikiwa kumpata na hivyo kuhitaji msaada wa kamera za CCTV.

Ilikuwa vigumu kumpata kwa siku hiyo kwa kuwa tu mitaani kulikuwa na idadi ya watu wengi kutokana na Jumamosi kuwa siku ya mechi mbalimbali nchini humo.

Picha zilipigwa, gari lake lilionekana sehemu nyingi likipita, hawakujua mahali lilipokuwa likielekea lakini baada ya kufika Bristol, hakukuwa na mtu aliyejua mahali gari hilo lilipokuwa.
“Lilikwenda wapi?” aliuliza jamaa mmoja.
 
SEHEMU YA 90

“Hatujui! Au aliondoka kwenda kwenye kituo cha treni kupanda treni?” aliuliza mwanaume mwingine.

“Ni vigumu! Inawezekanaje ukatafutwa halafu ukaenda kupanda treni? Hakuna kitu kama hicho,” alisema mwanaume mwingine kabisa.

Kila mtu hakujua mahali alipokuwa Edmund, alionekana kama mzimu kwani kwa nchi kama Uingereza ilikuwa vigumu sana kumkosa mtu aliyekuwa akitafutwa kutokana na teknolojia yao kuwa juu sana.

Mpaka inafika wiki ya kwanza, hakukuwa na mtu aliyejua mwanaume huyo alipokuwa. Kila mmoja akajiuliza kwamba kama mwanaume huyo aliondoka nchini Uingereza, alipitia wapi mpaka kwenda kwenye nchi nyingine? Kila walipojiuliza, walikosa majibu.

*** Polisi walikuwa wakihangaika kila kona kumtafuta Edmund ambaye mpaka muda huo hawakujua mahali alipokuwa.

Kwenye kamera zao, waliliona gari lake lakini baada ya muda likawapotea. Wakahakikisha wanaweka ulinzi kila kona kuhakikisha mwanaume huyo hatoki kuelekea sehemu yoyote ile.

Polisi waliokuwa katika Kituo cha Treni cha Bristol walikuwa wametulia kuhakikisha ulinzi unakuwa salama mahali hapo.

Walimwangalia kila mtyu aliyepita ili kuona kwamba ni lazima wahakikishe kwamba ndani ya kituo hicho, mwanaume huyo haingii kabisa kwani kama wangemkosa mahali hapo na kuondoka kuelekea nchi nyingine basi wasingeweza kumpata tena.

Wakiwa hapo, ghafla polisi wawili wakamuona mwanaume ambaye kwa muonekano alifanana kabisa na Edmund japokuwa alijaribu kuvaa kofia ambayo aliamini kwamba ni lazima ajifiche na asionekane kwa watu wengine.

Hawakutaka kuchelewa, wakaanza kumfuata kule alipokuwa. Kwa jinsi alivyokuwa akitembea huku akiangalia huku na kule, ikawapa uhakika kwamba mwanaume huyo alikuwa Edmund, na alipokwenda na kusimama sehemu kwa ajili ya kupanda treni, wakasimama kwa mbali nyuma yake na kuanza kumwangalia vizuri.

“He is the one, let’s arrest him,” (ndiye yeye, tukamuweke chini ya ulinzi) alisema polisi mmoja.

Wakaanza kumfuata, walipomkaribia, mmojawapo akamshika begani kwa lengo la kumtaka ageuke ili kama ni yeye basi wamuweke chini ya ulinzi lakini kama si yeye, wamuombe radhi.
 
SEHEMU YA 91

Edmund alihisi kabisa mtu aliyemshika bega kwa nyuma alikuwa akimfahamu na ndiyo maana aliamua kumfuata na kumtaka ageuke ili atambulike na kukamatwa.

Wakati mapigo ya moyo yakimdunda kwa nguvu tena huku akitetemeka, mara zikaanza kusikika kelele kutoka kwa binti mmoja aliyetoka chooni, alikuwa akikimbia kwa mwendo wa kasi.

“A bomb....a bomb...” (bomu...bomu...) alisema msichana huyo huku akikimbia kutoka chooni.

Vichwa vya Waingereza wengi vilikumbuka tukio ambalo lilitokea mwezi uliopita jijini Manchester ambapo kituo cha treni kililipuliwa kwa bomu lililowekwa na Waarabu kutoka Mashariki ya Kati.

Waliposikia hivyo, hakukuwa na mtu aliyebaki, kila mmoja akaanza kukimbia kwa hofu kuyaokoa maisha yake. Pale polisi wale waliposimama, wakashtukia wakikumbwa na watu waliokuwa wakikimbia, walipoinuka, Edmund hakuwepo, naye aliungana na watu wengine kukimbia.

Ilikuwa ni balaa ndani ya kituo hicho, watu wakatawanyika, si wale wanaosimama kwenye kizuizi, bali kila mtu aliyekuwa ndani ya kituo hicho ambao walikuwa ni zaidi ya elfu tatu, walikimbia kuelekea nje.

Edmund hakutaka kurudi, pale alipofika, akalikuta gari lake lakini hakutaka kulifuata, akahisi kwamba kulikuwa na watu waliokuwa wakilifuatilia na kutaka kuona ni mtu gani ambaye angeingia ndani ya gari hilo.

Alichokifanya ni kutembea kwa mwendo wa kasi huku watu wengine wakiendelea kukimbia hovyo. Alipofika umbali fulani, akasimamisha teksi, akaingia na kuondoka.

“Kuna nini?” aliuliza dereva teksi, alishangaa kuona watu wakikimbia huku na kule.
“Kuna bomu!”
“Kuna bomu! Wapi?”
“Kituoni!”
“Acha utani!”
“Kweli! Kuna bomu humo!”

Edmund akamshukuru Mungu kwa kumuwezesha kuondoka salama katika kituo kile pasipo kugundulika. Safari iliendelea, alipokuwa akielekea, hakupajua, wakati mwingine alijisikia kumwambia dereva kwamba wazunguke tu mpaka pale ambapo giza lingeingia.

Wakati wakiwa wanaendelea kuzunguka ndipo akapata wazo kwamba aondoke mpaka nchini Ireland kwa kutumia gari kwani wangepitia katika daraja kubwa lililokuwa likipita kutoka Uingereza mpaka Wales ambapo huko kusingekuwa na kazi kubwa ya kwenda huko.
 
SEHEMU YA 92

Wazo hilo lilionekana kufaa, akamwambia dereva kwamba walitakiwa kuanza safari ya kuelekea nchini Wales kitu ambacho hakikuwa na ugumu hata kidogo.

“Kwa hiyo twende Wales?”
“Ndiyo! Twende huko!” alijibu Edmund.
Hakukuwa na tatizo lolote lile, katika muunganiko wa Uingereza, pia kulikuwa na nchi nyingine kama Scotland na Wales ambapo kwa Muingereza kwenda huko hakuhitaji viza kwa kuwa ilionekana kama kutoka sehemu moja na kwenda nyingine.

Ilikuwa ni safari ndefu lakini Edmund hakutaka kujali. Muda wote ambao safari ilikuwa ikiendelea, masikio yake yalikuwa katika redio aliyokuwa akiisikiliza humo garini.

Hakutaka kupitwa na wakati, ilikuwa ni lazima kufuatilia kila kitu kilichokuwa kikiendelea ili ajue msako mkubwa wa kumtafuta yeye ulikuwa ukifanyika mahali gani.

Baada ya saa tano, saa mbili usiku wakafika katika eneo ambalo ilikuwa ni lazima magari yaangaliwe kama kulikuwa na kitu cha hatari ambacho kilikuwa kikitoka nchi moja kwenda nyingine.

Hapo kulikuwa na msururu mkubwa wa magari na yote ambayo yalikuwa yakiingia nchini Wales ilikuwa ni lazima kupekuliwa kwanza. Hapo, Edmund akawa na hofu, akahisi kabisa kwamba angeweza kuonekana kitu kilichomfanya kuanza kuzungumza na dereva yule.

“Ninahitaji kupita hapa salama,” alisema Edmund huku akimwangalia dereva huyo.
“Hakuna tatizo! Hatujabeba kitu cha hatari, tunapita bila tatizo lolote lile,” alisema dereva yule kwa kujiamini.

“Najua! Ila hatuwezi kufanya kitu chochote tukapita salama?” aliuliza Edmund.
“Hapa lazima tupite salama! Mbona unakuwa na wasiwasi sana?”
“Yeah! Nataka unifiche.

Unajua ninatoroka nyumbani!”
“Kivipi?”
“Baba yangu kanizingua. Ninakwenda kuonana na mpenzi wangu. Familia yetu ni Wazungu, mchumba wangu ni mtu mweusi.

Baba hataki niwe naye, amenizuia, nimetoroka nyumbani na ninajua tu kwamba ametuma polisi kunitafuta ili wanirudishe nyumbani kwani hapendi kweli ngozi nyeusi,” alidanganya Edmund.
 
Shunie mbona umeruka sana toka sehemu ya 86 umeenda mpaka sehemu ya 89. tunamiss sehemu ya 87 na 88
 
SEHEMU YA 93

“Baba yako nani?”
“Steven Powell.”
“Huyu mkuu wa jeshi la polisi?”
“Ndiyo! Naomba unisaidie nipite salama.

Sitaki kurudi nyumbani, ninampenda Vanessa, naomba unisaidie katika hili nivuke salama,” alisema Edmund huku akionekana kuomba sana. Na kwa sababu dereva alikuwa na roho nzuri kama papa Francis, akakubaliana naye kwamba iwe isiwe ilikuwa ni lazima kumvusha salama mahali hapo.

*** “Mom! Where are we?” (mama! Tupo wapi?) lilikuwa swali la kwanza kabisa alilouliza Walter kwa sauti ya chini kabisa.
Aliyafumbua macho yake, mbele yake alisimama mwanamke mnene, aliyevalia nguo nyeupe ya kinesi, kutokana na kutokuona vizuri, hakujua kama mwanamke huyo hakuwa mama yao, alimfananisha.

Mwanamke huyo hakuzungumza kitu zaidi ya kutoka na kwenda kumuita daktari. Walikuwa wamekaa kwa wiki moja hospitalini hapo na hawakuwa wamerudiwa na fahamu kitu kilichoonekana kuwa kibaya kwa afya yao.

Nesi yule hakuchukua muda mrefu, akarudi chumbani hapo akiwa na daktari ambaye uso wake ulionyesha tabasamu pana kwani hakuamini kama vijana hao wangeweza kuyafumbua macho yao, kila mmoja alikata tamaa na kuhisi kwamba huo ndiyo ungekuwa mwisho wao.

“Where are we?” (tupo wapi?) aliendelea kuuliza Walter huku akiangalia kwa macho yake mazito.
Kwa kuwa bado hali zao hazikuwa nzuri, daktari akaagiza wawekewe dripu iliyokuwa na dawa ya Morphometip ambayo ilikuwa na kazi ya kuyaamsha zaidi mapigo yao ya moyo.

Kidogo baada ya kuwekewa dripu hiyo, wakapata nguvu na hapohapo Walker naye kuyafumbua macho yake na kuanza kuangalia huku na kule.

Kutokana na hali iliyokuwepo mahali pale, wakagundua kwamba walikuwa hospitalini, hawakujua walifikaje mahali hapo, hawakujua mahali walipokuwa wazazi wao, walishangaa lakini baada ya kukaa kwa dakika kadhaa, wakakumbuka kila kitu kilichokuwa kimetokea kwamba walikuwa wakiingia ndani ya gari na ghafla wakahisi wakiishiwa nguvu na kuanguka chini.

Walihitaji kuwaona wazazi wao, hawakujua mahali walipokuwa, walitaka kuwaona kwani wao ndiyo walikuwa watu muhimu katika maisha yao.
 
Back
Top Bottom