Vifurushi vya internet vimepanda bei ghafla, serikali iko wapi?

Vifurushi vya internet vimepanda bei ghafla, serikali iko wapi?

Yaani leo vifurushi vimepanda bei maradufu shilingi 1000 unapata mb 350 hii ni kwenye tigo huko airtel na voda ni majanga serikali iliyochaguliwa na "maskini" iko wapi? Au huku ndio kuisoma namba kwenyewe?
Kwani maskini tunatumia net sisi,acha ipande maana wengine kazi yenu kutukana watu tu mtandaoni.
 
Halotel Mwanachuo kitendo cha kuweka tu vocha ya sh.1000 kabla hujajiunga na kifurushi chochote unapata Mb 100 papo hapo bureeeee.

Ukijiunga na bando ya internet ya sh.1000 hiyo hiyo unapata Mb 1200 kwa hiyo unakuwa na jumla ya Mb 1300 kwa mtonyo wa buku hahahahaha

Halotel ni raha sana kama nanyi hamtachenji huko mbeleni.
 
Mnalonga sana na simu zenu...sasa wanapandisha
 
nenda kwenye maduka yao,utapata mi nilipita kuna ya laki na 20 hii ni kubwa na kuna ya elfu90 ndogo,hkn jinsi ni kuhamia tu Halotel
 
Yaani leo vifurushi vimepanda bei maradufu shilingi 1000 unapata mb 350 hii ni kwenye tigo huko airtel na voda ni majanga serikali iliyochaguliwa na "maskini" iko wapi? Au huku ndio kuisoma namba kwenyewe?
Vifurushi ni offer serekali haiwezi kuwapangia watoa offer watoeje offer yao
 
mkuu line ya chuo halotel unapata 10gb kwa tsh 9999
Duh! Hii ndio haswa inaweza kunifaa manake 10GB unaweza kuibana bana na ukamaliza wiki. Kwahiyo laini zake kuzipata ndo hadi uwe na kitambulisho cha mwanafunzi au mtu unaweza kuipata kiujanja ujanja?
 
Nishasema kila siku ccm ni ile ile nashngaa wanaoshangilia...niseme Hapa ni kunyanyasika tu mpaka watanzania akili ziwaingie!
 
Yaani leo vifurushi vimepanda bei maradufu shilingi 1000 unapata mb 350 hii ni kwenye tigo huko airtel na voda ni majanga serikali iliyochaguliwa na "maskini" iko wapi? Au huku ndio kuisoma namba kwenyewe?
Do not trust a plitician (hasa wale wa kijani) even a dead one
 
Mimi nimeshasahau hata bei ya vifurushi ni kama natumia internet bure tu.

Hii siri nitabaki nayo mwenyewe Wabongo hamna dogo yakifika vyuoni itakuwa shida tupu. Miye kimyaaa.
embu tupe siri mkuu
 
wambea sana na mnafwatilia sana maisha ya watu yasiyowahusu ndo kana mnaona zimepanda...ila kama unataumia mb kwa nidhamu... msingelalamika...mbona beer na condom hamjapiga kelele bei zake
 
Nunueni laini za chuo halotel wanauza kuanzia elfu nne mpaka elfu tano kwa line hio line utapata mb 600 kwa shiling 500 wiki nzima ukiwa na buku unalamba 1.2Gb wiki nzima sasa mpewe nini mbona mnashindwa kujiongeza? au mnaona shida kuha hio mitandao yenu yaki tapeli?
 
Kwa hiyo munataka kusema kuwa TCRA imewekwa mfukoni na makampuni ya simu?
 
Yaani leo vifurushi vimepanda bei maradufu shilingi 1000 unapata mb 350 hii ni kwenye tigo huko airtel na voda ni majanga serikali iliyochaguliwa na "maskini" iko wapi? Au huku ndio kuisoma namba kwenyewe?

Vifurushi vipande tu Mkuu ili Majungu na umbea vipungue humu, watu wafanye kazi.
 
Back
Top Bottom