kinepi_nepi
JF-Expert Member
- Aug 16, 2007
- 869
- 235
Tanzania ninayoipenda ni uwanja wa fujo. Utawala usiofuata sheria haya ndio mambo yake.
Ningefurahi sana kama wangepigwa wezi mafisadi na kufa sio vibaka wa kanda mbili, kwani hawa mafisadi ndio chanzo cha huu wizi. uchumi ukidorora vibaka huongezeka.
Taarifa kweli inasikitisha, ila inamambo mengi na maswali kibao.
Mwili ulioshambuliwa na watu wenye hasira unajulikana, na mwili uliowawa na watawala wasio na huruma unajulikana.
Tukio lilitokea vipi sioni jibu kwenye habari.
Ila swala la wizi na watu kuchukua sheria mikononi hilo ni la siku nyingi wapo wengi sana wameuwa wakiwa sio wezi.
Ni nani wa kulaumiwa, ni serikali. Niliwahi kukaa jirani na polisi Dar, na siku moja walifukuza majambazi wa magari, kisha wakawauwa. nilimuuliza kwanini mmeuwa hao majambazi hamkuwakamata na kuwapeleka polisi.
Alinijibu hawawezi kufanya opereshini ya kukamata jambazi kama hawauwi kwani huwa wakifika polisi wanaachiwa huru kwa kuhonga wakubwa halafu kisasi kinakuwa ni binafsi kati ya jambazi na polisi waliokamata. Na baadhi ya polisi ni majambazi hivyo hufanya uhalifu na majambazi.
Tanzania bila utawala wa sheria tutapiga kelele vizazi na vizazi.
Ni lazima viongozi na watendaji waoogope sheria, bila hivyo vita hii ambayo imeanza siku itakuwa kubwa.
Kama nchi imeshindwa kulinda BOT kweli wataweza kulinda watoto wenye umri wa miaka 14 na 15??
kama mkuu wa usalama wa taifa alishiriki kuibia nchi anayoilinda akishirikiana na mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama hatuoni hapa nchi haina walinzi.
Kama mkuu wa polisi alishirikiana na majmbazi ni nini kinatushangaza??
tatizo kubwa Tanzania hakuna wa kumfunga paka kengele.
Nchi haina utaratibu wala mpangilio. Waziri wa mambo ya ndani kazi yake ni kupanga njama za kufilisi wafanya biashara, Raisi kazi yake kulinda mafisadi, waziri mkuu kazi yake haijui yupo yupo tu..........
Tusipo kuwa tayari kuitetea tanzania kwa vitendo kinachokuja ni kikubwa sana.