Vifo vya watoto hawa 2 vichunguzwe! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vifo vya watoto hawa 2 vichunguzwe!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Dec 11, 2008.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Dec 11, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Tunabishania vitu visivyo na msingi, tunapingana kwa mambo ya kitoto, na tunabakia kushutumiana kwa visivyo na umaana. Vile vya msingi tunaviacha kimya; hakuna mwenye hasira, hakuna anayekerwa; na wale waliokuwa na haraka ya kuzungumza kwenye mambo yasiyo na msingi wako kimya!

  Tuna tatizo Watanzania; Tuna tatizo kubwa.. hebu angalieni yaliyotokea Ugiriki na usome hiki cha Tanzania!! Maalbino na sasa watoto wadogo!!


  Umma waua watoto wa shule kwa mawe

  2008-12-10 16:16:56
  Na Godfrey Monyo

   
  Last edited by a moderator: Dec 12, 2008
 2. C

  Chuma JF-Expert Member

  #2
  Dec 11, 2008
  Joined: Dec 25, 2006
  Messages: 1,330
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  MKJJ...kwa tukia hili ni vigumu kukoments hadi tupate taarifa za uchunguzi au kama kuna watu walikuwepo ktk Tukio....

  Siku hizi Matukio ya wizi wa kuwatumia watoto umekuwa Mkubwa sana....Maeneo ya Mbagala huwezi kutembea usiku alone...unaweza vamiwa na watoto/vijana wa rika la Std 7 wakakufanya vibaya...
  Wizi Umekuwa vicious cicle...watu hawana kitu....options walizonazo ni kuiba....na mtu alieitafuta mali yake kwa jasho kubwa akija kuibiwa hasira zake sikambii kuiba site mirror..kukaruzwa rangi tu inaweza kuwa kasheshe...

  Kwa itakavyokuwa...kujichukulia hatua Mikononi bila vyombo vya usalama ni jambo linalotakiwa kupigiwa kelele...
   
 3. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #3
  Dec 11, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  hakuna udhuru wa kuwaua watoto wa miaka 14/16 kwa mawe. None whatsoever. Hakuna kuongezeka kwa matukio ya wizi kunakoweza, paswa, au fafanua mauaji haya ambayo ni zaidi ya kinyama; kama kuna matatizo kwenye jamii ni sisi watu wazima we have to deal with!
   
 4. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #4
  Dec 11, 2008
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Ama kweli Mwanakijiji naona tunaanza kufikiria namna moja telepathikali maana baada ya kuhoji kuhusu Dr. Cho, nilikuwa nianzishe thread kuhoji ni lini tutakasirika?

  Umeyaona yanayotokea Ugiriki na Thailand? Sasa najiuliza ni lini Mtanzania ataachana na unafiki wa Amani, Utulivu na Mshikamano?

  Leo hii Serikali inaleta ubabe, viongozi wake wanafuja mali na kuhujumu, lakini Watanzania wanakaa kimywa kazi kusema hewala kasoro siye tunaopiga kelele kwa vidole na machapisho ambao tunaambiwa hatufiki hata theluthi ya asilimia moja!

  Umeme unaposuasua, shurti tumkabe koo waziri wa nishati ati! Maana watu wanafikiri umeme ni taa pekee kuangaza nyumba na kuwasha kiyoyozi, wanasahau kuwa umeme ndio gurudumu la maendeleo yetu na uhai wetu ambao tunaegemea kwenye viwanda na biashara.

  Leo kuvuja kwa mitihani, migomo ya wanafunzi na waalimu, waziri anapeta na VX, hakuna anayemkwida koo au kung'ang'ania afukuzwe kazi kwa uzembe!

  Dege la ATCl limekufa, treni zote TRC na Tazara zinachechemea, barabara ni mbovu, madaraja hayajamalizika ujenzi, nyufa barabarani, ajali barabarani huku njaa inakuja, lakini hatuna ma Dr. Cho waliobobea na wale kina Bulicheka tulionao, wanapukuta ma VX, M5, C350, ES 400 na vijisafari vya kila kona ya dunia.

  Ni lini mtanzania ataachana na upendo wa Kikristo wa kugeuza shavu na kusamehe mara 70? Miaka 47 ya uhuru bado tunaoneana haya na kuogopana?

  Kewli tupo tupo, mambo ni powa, dole, msondo afya!
   
 5. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #5
  Dec 11, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Yawezekana sisi ni miongoni mwa watu wa ajabu zaidi duniani; Kuna kitabu fulani nilikisoma kinachapwa na wale "Onion News" people.. ukikipata angalia wanasema nini kuhusu Tanzania..
   
 6. M

  Mutu JF-Expert Member

  #6
  Dec 11, 2008
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 1,333
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Inasikitisha sana kusikia hili ,ngoja tuone daktari watasemaje maana maelezo kama yanachanganya hizi.Tukisikia kuwa hawana vioungo vya siri basi hawakuwa wezi hawa wamefanyiwa hujuma.

  Ila mashawishika kuwa bongo siku baada ya siku vijana wadogo wanajiingiza kwenye mambo ya hatali kama njia rahisi ya kupata pesa.Sitetei vitendo viovu ila maisha yanakuwa magumu sana .
  Kwa hiyo kujingwamua katika hili imefikia kipindi cha kuangalia jinsi ya kuongeza ajira bongo .Kwa kuwa kipato ni kidogo basi at least member kadhaa wa familia wawe na kazi kisha wanashare ,tujifunze kutumia nishati kwa ufanisi ili tuilipe bill kubwa za umeme na umeme mdogo tulionao ukidhi .Najua maendeleo yana kwamishwa na ufisadi ila tuwe positive let us play our part huku tukipigana na ufisadi pia.
  Kuna swali najiuliza kila siku nakosa jibu kwa kuwa sina utafiti wa kutosha:Hivi kwa nini asitokee mtu ama makampuni makubwa au hata serikali wakawekeza kwenye kilimo.Au serikali itowe taaluma na uwezeshaji katika kilimo naona itatoa ajira kwa wengi na tutaweza kupata mapato kutoka nje kwa kuuza mazao ya biashara.
   
 7. M

  Mama JF-Expert Member

  #7
  Dec 11, 2008
  Joined: Mar 24, 2008
  Messages: 2,858
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 0
  Lau tena.......
   
 8. C

  Chuma JF-Expert Member

  #8
  Dec 11, 2008
  Joined: Dec 25, 2006
  Messages: 1,330
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  MKJJ....mauaji yoyote yawe ya Mtoto au Mtumzima kwa style ile hayafai...

  Sijui kama una kumbukumbu...Polisi waliwapiga Risasi watoto pale Mwembechai(Rejea Mwembecha Killings)...akina Chuki ATHUMAN...wakadai eti waliwakuta na karatasi za uchochezi....Hivi waliwapiga risasi baada ya kuwaona na karatasi hizo...au waliwapiga risasi then wakawakuta na karatasi hizo...

  Hapo Hasira zako hazikuwepo?
   
 9. M

  Mpanda Merikebu Senior Member

  #9
  Dec 11, 2008
  Joined: Dec 27, 2007
  Messages: 170
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Huu ni udhihirisho wa matatizo mawili; wazazi kutokuwa na majukumu ya uzazi na serikali haimtunzi vema raia wake, hasa wale wasiokuwa na nguvu kama watoto, wanawake na walemavu.

  Nikianzia kwa wazazi, kulingana na taarifa iliyoletwa katika habari hii, inaonesha kuwa wazazi wa marehemu wote wawili hawakujua watoto walipo mpaka walipoletewa taarifa (na mzazi/mlezi mmoja akijiuliza mbona mtoto hajarudi nyumbani) kuwa watoto hawa wameuawa. Wazazi wana wajibu wa kuwatunza na kuwalea watoto wajue mazuri na mabaya. Wizi ni mbaya. Hili ni jambo linalojulikana kwa watu wote, bila kujali rangi, dini, kabila au itikadi. Zaidi ya hapo, mzazi anapaswa kujua mtoto wake ana tabia gani, anaenda kucheza wapi, atarudi saa ngapi n.k.

  Simaanishi kuwa wazazi wageuke kuwa polisi kwa watoto wao. Ninamaanisha kuwa, kama mzazi atakuwa na muda kumfahamu mtoto wake, atafahamu tabia zake, marafiki zake, tabia na mahusiano yake shuleni n.k. Ninawasikitikia wafiwa, lakini, nafikiri wazazi wangekuwa makini zaidi, jambo hili la kusikitisha lingeweza kuepukwa.

  Kwa upande mwingine, serikali haiwezi kukwepa lawama. Sijui hata nianzie wapi. Mara nyingi, watu wakiamua kuchukua sheria mkononi ni ishara kubwa kuwa wamechoshwa na tabia ya kutowajibika ya serikali na vyombo vyake vya dola na pia hawaiamini. Ni mara ngapi wezi wamekamatwa hali kukiwa na ushahidi halafu wakaachiliwa kabla hata ya giza kuingia?

  Au labda tuangalie kwa upande mwingine, je serikali imechukua hatua gani kuhakikisha kuwa ustawi wa watoto kwa ajili ya malezi mema unafanikiwa? Hakuna sehemu za watoto kuchezea, hakuna mitaala itakayowawezesha watoto kujishughulisha baada ya saa za shule. Serikali hiyo hiyo inampa wakati mgumu mzazi wa mtoto (mishahara duni) na kusababisha hali ngumu nyumbani. Serikali haiwachukulii hatua na kuwamaliza vibaka, changudoa, wauzaji na watumiaji madawa ya kulevya; hawa ni watu ambao wanakuwa kama mfano mbaya wa kuiga (role models) kwa watoto hawa.

  Ni dhahiri kuwa kama hawa watoto waliiba vioo vya gari, mtu mzima mmoja angeweza kuwaadhibu na kuwapeleka kwa wazazi wao. Lakini, najiuliza, kwanini jamii yetu imefilisika kimaadili kiasi hiki mpaka kwa watu kushabikia kuwaua watoto ambao hawakujua walichokifanya na ni watu ambao walihitaji msaada mkubwa? Kama nilivyosema hapo awali, wanawake, watoto na walemavu ni makundi ambayo yamenyanyasika kwa muda mrefu nchini kwetu. Angalau kuna makundi ya wanawake (kama TAMWA, TAWLA, UMATI, etc) ambayo yanajitoa mhanga kutetea wanawake na haki zao. Na walemavu pia wana makundi yao yenye sauti na yana uwakilishi hata Bungeni.

  Je, ni nani amebaki kutetea watoto? Walikuwa wapi mpaka watoto hawa marehemu wakawa na tabia hizi zisizostahili katika jamii? Hivi watoto hawa wamekufa; ni nani atakayetetea haki zao mbele ya sheria au watazikwa, kusahaulika au kukumbukwa kuwa ni wale watoto vibaka waliouawa? Kipi kitafanyika kwa wale waliowaua?

  Majonzini,

  Mpanda Merikebu
   
 10. I

  Interested Observer JF-Expert Member

  #10
  Dec 11, 2008
  Joined: Mar 27, 2006
  Messages: 1,401
  Likes Received: 433
  Trophy Points: 180
  Mkijiji;
  You have already put it prospectively; society and values are crumbling; the government have failed to mobilize its people; and law enforcement is not there. Nobody respetcs laws of the land from the top man in office and the society at large is taking by laws on their hands. poverty and survival have become our norms of life; anger can no longer be relinguished by love, but by brutal killing. We are all a party to a society on making; think what will be Tanzania in 20 years. WEwe si umeona maalbino wameuawa kikatili wala serikali haijachukua emergency measures; tumebakia kulaumiana, na cha kushangaza mno hata waziri wa mambo ya ndani anaweza kuanza kulaumu society!
   
 11. I

  Interested Observer JF-Expert Member

  #11
  Dec 11, 2008
  Joined: Mar 27, 2006
  Messages: 1,401
  Likes Received: 433
  Trophy Points: 180
  reading your rips/thinking; you want to start the old story; hapa watu wapo kwa taifa la Tanzania is about ourselves, our country and our children!
   
 12. M

  Mutu JF-Expert Member

  #12
  Dec 11, 2008
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 1,333
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Wewe changia hoja ,kwani hii ni kwa manufaa ya mwanakijiji dont make it person.
   
 13. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #13
  Dec 11, 2008
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,659
  Likes Received: 21,878
  Trophy Points: 280
  Si kuwa yawezekana, sisi ni waajabu kwelikweli. Yapo mambo ya msingi kabisa yanayojitokeza hapa TZ na yanahitaji watu kuweka umakini na kukasirika kama alivyosema KUHANI lakini tumekalia ushabiki na malumbano tuu.
  Hata hapa JF ambako tunadhani watu (wengi wao) ni makini kutokana na tunavyoona mpangilio wa michango yao, bado nao wamebobea katika ushabiki na chuki za wazi kabisa. Mtu makini ukimwona anatetea uozo ulio dhahiri ujue kuna jambo nyuma yake limejificha.
  Nakubali kabisa sisi ni watu wa ajabu kabisa.
   
 14. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #14
  Dec 11, 2008
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Theoretically and morally you are quite right. But, in order to understand whay people choose to take laws in their own hands you have to see the reality on the ground. You are being robbed and no one cares, if you go to the police the best they will tell you is 'pole, next time be careful'. You work tirelessly day and night to buy a little TV so as you can watch Ze commedy, you end up being robbed, beaten and no body cares. This kind of event sends a message to the authorities that people are tired of being ignored. Mwizi ni mwizi tu, akiiba sight mirror, kijiko au sahani. Kesho atakuja na SMG au panga akaiba na kuua, kwa hiyo kuchukua hatua mapema namna hii kunaweza kuwa justfied kutokana na hali halisi.
   
 15. Belo

  Belo JF-Expert Member

  #15
  Dec 11, 2008
  Joined: Jun 11, 2007
  Messages: 11,276
  Likes Received: 4,260
  Trophy Points: 280
  Kweli ni wa ajabu mtu anaiba kioo au simu anapigwa mawe hadi kufa but kuna MAFISADI wameiba mabilioni lakini hawaguswi
   
 16. C

  Chuma JF-Expert Member

  #16
  Dec 11, 2008
  Joined: Dec 25, 2006
  Messages: 1,330
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  IO....hio ni Old Story....?Unajua kesi zinavyoendeshwa mahakamani....? Hakimu huwa anakuwepo wakati wa tukio?...unaposema Old....unakusudia nini...miaka? siku? masaa..? dakika?....

  so CHUKI ATHUMANI sio "ourselves"...sio "our children"

  Nimelihusianisha tukio la chuki Athuman kwakuwa wakati Ule Polisi walihusika...ktk Hii Story iliyokuwa pasted na MKJJ....moja ya wazee anasema Polisi wanahusika kwani walikuwa ktk lindo...

  So unachotaka mie nikubali ni nini kaka?
   
 17. I

  Interested Observer JF-Expert Member

  #17
  Dec 11, 2008
  Joined: Mar 27, 2006
  Messages: 1,401
  Likes Received: 433
  Trophy Points: 180
  Chuma, all our children are important they should not be killed; you brought an old story to negate MWJKJJ allegation that our morals have declined and we have reached a pont to kill even our own children by mob justice. We condemn all killings being by police (government) or by individuals. That is what we have to discuss here. And this infact is declining morals in our values in core families. A president or learders in our government is the reflection of our society!
   
 18. Ibrah

  Ibrah JF-Expert Member

  #18
  Dec 11, 2008
  Joined: Mar 22, 2007
  Messages: 2,721
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  You have said it all; na tena hakuna udhuru wa kumuua mtu yoyote kwa kosa lolote la uhalifu, ni sheria tu kuchukua mkondo wake. Nadhani jamii yetu imeanza kuoza na kushindwa hata ku-reason hta kwa kuangalia ukubwa wa kosa na umri wa muhusika.

  Hata hivyo, lazima kuna tatizo katika mfumo mzima wa utawala nchini mwetu kiasi kwamba watu wanaamua kuchukua sheria mkononi. Ama jamii imechoshwa kwa Serikali kushindwa kusimamia sheria au serikali kushindwa kusimamia mgawanyo mdogo wa raslimali tulizo nazo kwa usawa. Kila mtu anafanya lwake ili kumuwezesha kuishi katika msukosuko wa kiuchumi na kijamii.
   
 19. Z

  Zion Train JF-Expert Member

  #19
  Dec 11, 2008
  Joined: Jun 5, 2008
  Messages: 503
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  inasikitisha mno watu kuuwawa na huku vyombo husika vikiangalia, namuomba mh.JK afuatilie kwa makini utendaji wa polisi, mie nasema polisi hawafanyi kazi haswa inavyotakiwa, kuna siku niliibiwa simu mtaani kijana aliyeniibia namjua, nikaenda polisi kutoa taarifa jinsi nilivyoibiwa na ni nani aliyeniibia, wakaandika maelezo na kusema nikimuona niwajulishe, basi narudi mtaani nikamuona,mie mbio mpaka kituoni tena, unajua waliniambiaje hawawezi kutoka, nimkamate mwenyewe nimpeleke. basi toka siku hiyo nilimechoka na kuchoka na polisi, sasa kama mimi namkamata na mimi si polisi anaanza kuniletea za kuleta si tutamalizana. mimi nasema tena kwa sauti ya juu utendaji wa POLISI haulizishi.
   
 20. Mfamaji

  Mfamaji JF-Expert Member

  #20
  Dec 11, 2008
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 6,523
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280

  Tanzania inachekesha mbaya kabisa. Fikiria hata Tampa Sallon ni bora kuliko Tz. Soma Hii.
  Tanzania Loses Name To Tanning-Salon Chain | The Onion - America's Finest News Source.
   
Loading...