Vifo vilivyoniumiza JF

Mwenyezi Mungu apokee roho za marehemu wote na aziweke mahali pema peponi. Amina.
 
Hukuogopa kukutana na watu wa humu jamiiforums? Au unawafanyia vetting kwanza ndio mkutane physically? Jamiiforums wewe ni mmoja wa watu tunaokosoa mashetani ya kijani na wewe ni maarufu sana huogopi kumafweliwa na mafwele? Binafsi naogopa sana watu wa humu japo nawapenda sanah hasa wanaharakati wenzangu.
 
Dah! Basi nishakujua Best.
 
Mimi naulizia walipo hamphrey PolePole na mdude nyagali.
Kama hawajauwawa, basi warejeshwe kwenye familia zao. Na kama wameuwawa kwa sababu tu za kisiasa (ukosoaji) pia miili yao ingerejeshwa kwa familia zao.
Mkuu hata Mimi hawa watu wananiuma sana maana wamechukuliwa tunaona kabisa huu mchezo Sasa sijui ni uoga wetu au lakini kimsingi ilibidi kisasi kilipwe.
 
Daah naukumbuka ule uzi, ndo maana tunaambiwa be kind kwa watu hujui wanapitia nini.
Ila mtu kama una roho nyepesi bora usilete changamoto zako mtandaoni kuna vichaa humu kama wametiwa pili pili kichaa kwenye ubongo!
 
Zamani kidogo ushetani huu ulikua haujatamalaki humu jamvini!
Hata mimi najuta kwanini sikua active sana enzi zile huenda ningekutana na watu wa maana wengi sana ☺️
 
Member pekee nafahamiana nae kwa ukaribu sana ni mkwepu jr , nadhani ndio mtu pekee nikiondoka atawapa taarifa au yeye akitangulia Mimi nitawapa taarifa.
Yule jamaa Fork kifo chake kilinihuzunisha sana maana alikuwa anatuambia Hali anayopitia na tukawa tunachukulia poa na kukejeli. Aendee kupumzika kwa amani aisee.
 
4. Valentine.. Apumzike kwa amani😪 .. Pamoja na juhudi nyingi za kuonana lakini mpaka kifo kinamchukua hatukuwahi kuonana!
Valentina au Valentine?
Kama ni Valentina nilikuwa na mawasiliano nae nje na jamiiforum japo ni muda sijawasiliana nae

Mkuu Mshana Jr ebu niweke wazi aiseee!!
 
Spiritual protection.. Nakutana na watu weka.. Wale wabaya wanajua tulicheza sindimba na mdumange.. Hata wabaya huwa wema inategemea mazingira..!!!
 
Huyu jamaa nilikuwa karibu nae sana na kifo chake kilinitikisa. Ni miaka mitano sasa nadhani imepita

Wengine sijui hata kama tukifariki kuna wa kuleta taarifa au na sisi tutaishia kama IDs ambazo zinapotea pasipo watu kujua shida ni nini.
Dah usiseme hivyo.. Halafu next week tengeneza ratiba...!
 
Your browser is not able to display this video.
 
Daah naukumbuka ule uzi, ndo maana tunaambiwa be kind kwa watu hujui wanapitia nini.
Ila mtu kama una roho nyepesi bora usilete changamoto zako mtandaoni kuna vichaa humu kama wametiwa pili pili kichaa kwenye ubongo!
Wale waliokuwa wanapondea sijui wanajisikiaje huko.. Baada ya kifo cha jamaa wengi waliukimbia ule uzi
 
Reactions: naa
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…