Vifo vilivyoniumiza JF

Vifo vilivyoniumiza JF

Ukipewa uzima na siha njema mshukuru sana Mungu
Ukiamka huna miadi na tabibu mshukuru sana Mungu
Ukiamka huna kesi polisi mshukuru sana Mungu

Ukiamka una sehemu ya kwenda na ukirudi una sehemu yako mwenyewe ya kupumzisha fuvu mshukuru sana Mungu
Mengine ni changamoto za kawaida za maisha! Kamwe USIKUFURU

Hivi ndio vifo vilivyoniumiza JF
1. Mwalimu Frank.. Mtu mzima above 50 alikumbwq na changamoto za kifamilia.. Tukawa na mawasiliano ya karibu.. Lakini hatimaye akafa akiwa mpweke

2. Miguu ya kuku.. Kijana aliyekuwa na ndoto za kufanya makubwa maishani.. Akapata changamoto za kiafya zilizompelekea kupata ulemavu wa miguu.. Nilishiriki kwa karibu kwenye kutafuta tiba sahihi na suluhu ya kudumu.. Lakini hatimaye alikufa😪

3. Warumi.. Alitikisa vilivyo jukwaa la celebrity.. Akapata changamoto za figo.. Hakutamani kufa mapema.. Mawasiliano yangu ya mwisho na yeye ni wakati nimemwelekeza aende hospital ya figo Kibaha loliondo.. Hakupona alikufa

4. Valentine.. Apumzike kwa amani😪 .. Pamoja na juhudi nyingi za kuonana lakini mpaka kifo kinamchukua hatukuwahi kuonana!

5. Niah.. Huyu kwangu alikuwa Dada.. Ni mama mtu mzima aliyewahi kushika nyazfa za juu serikali ya mchonga na mzee ruksa.. Alijawa na upendo na amewasaidia wengi hata hapa JF..!

6. Gwapo Mwakatobe.. Nilimuita brother. Tulishaonana na tulikuwa na mawasiliano ya karibu. Mchambuzi mahiri wa bbc meza ya duara
Baada ya hustle za maisha akatamani akaishi maisha ya shamba kwenye utulivu.. Alifanikiwa kuhamia huko .. Lakini hakudumu.. Ajali ya boda ikamtenganisha nasi😭
Jana usiku nilijikuta nawakumbuka wote hawa.. Nikajikuta bado nina mamba zao za simu! Nimezifuta zote maana zimenikumbusha mengi

Naogopa sana maana sijui nitaona kifo cha nani tena tunayefahamiana.. Ama je itakuwa zamu yangu kwao!?🙌🏿🏃🏿😭
Mwenyezi Mungu apokee roho za marehemu wote na aziweke mahali pema peponi. Amina.
 
Hukuogopa kukutana na watu wa humu jamiiforums? Au unawafanyia vetting kwanza ndio mkutane physically? Jamiiforums wewe ni mmoja wa watu tunaokosoa mashetani ya kijani na wewe ni maarufu sana huogopi kumafweliwa na mafwele? Binafsi naogopa sana watu wa humu japo nawapenda sanah hasa wanaharakati wenzangu.
 
Warumi.
Ni zaidi ya rafikii, zaidi ya mtu wa karibu, zaidi ya jiranii, nimekumbuka those days, alikua anakuja Main campus ananichukua ananipeleka maeneo ya kujidai, alikua ananifanya nifurahie uwepo wake kila akiwa karibu yangu, zaidi nilikua napenda mchezo wetu wa kuendesha Gari kwa kufukuzana. Toka aniache mpweke hata road ya Bagamoyo sipiti mara kwa mara tena.

Endelea kupumzika salama Kipenzii. 😭😭😭

Valentine.
Huyu Dada tulijuana humu humu ndani kupitia uzi wa selfika, thou akaja PM tukawa marafiki, kupeana ubuyu na umbea wa hapa na pale, tulikutana siku hiyo alitaka nimsindikize sehemu, tukakutana na nili msindikiza huko, ilikua moment nzuri kwetu, na baada ya hapo tulikua tunakutana mara kwa mara.

Pumzika salama Baby Vals, 😢😢😢
Dah! Basi nishakujua Best.
 
Mimi naulizia walipo hamphrey PolePole na mdude nyagali.
Kama hawajauwawa, basi warejeshwe kwenye familia zao. Na kama wameuwawa kwa sababu tu za kisiasa (ukosoaji) pia miili yao ingerejeshwa kwa familia zao.
Mkuu hata Mimi hawa watu wananiuma sana maana wamechukuliwa tunaona kabisa huu mchezo Sasa sijui ni uoga wetu au lakini kimsingi ilibidi kisasi kilipwe.
 
Daah naukumbuka ule uzi, ndo maana tunaambiwa be kind kwa watu hujui wanapitia nini.
Ila mtu kama una roho nyepesi bora usilete changamoto zako mtandaoni kuna vichaa humu kama wametiwa pili pili kichaa kwenye ubongo!
 
Hukuogopa kukutana na watu wa humu jamiiforums? Au unawafanyia vetting kwanza ndio mkutane physically? Jamiiforums wewe ni mmoja wa watu tunaokosoa mashetani ya kijani na wewe ni maarufu sana huogopi kumafweliwa na mafwele? Binafsi naogopa sana watu wa humu japo nawapenda sanah hasa wanaharakati wenzangu.
Zamani kidogo ushetani huu ulikua haujatamalaki humu jamvini!
Hata mimi najuta kwanini sikua active sana enzi zile huenda ningekutana na watu wa maana wengi sana ☺️
 
Member pekee nafahamiana nae kwa ukaribu sana ni mkwepu jr , nadhani ndio mtu pekee nikiondoka atawapa taarifa au yeye akitangulia Mimi nitawapa taarifa.
Yule jamaa Fork kifo chake kilinihuzunisha sana maana alikuwa anatuambia Hali anayopitia na tukawa tunachukulia poa na kukejeli. Aendee kupumzika kwa amani aisee.
 
4. Valentine.. Apumzike kwa amani😪 .. Pamoja na juhudi nyingi za kuonana lakini mpaka kifo kinamchukua hatukuwahi kuonana!
Valentina au Valentine?
Kama ni Valentina nilikuwa na mawasiliano nae nje na jamiiforum japo ni muda sijawasiliana nae

Mkuu Mshana Jr ebu niweke wazi aiseee!!
 
Hukuogopa kukutana na watu wa humu jamiiforums? Au unawafanyia vetting kwanza ndio mkutane physically? Jamiiforums wewe ni mmoja wa watu tunaokosoa mashetani ya kijani na wewe ni maarufu sana huogopi kumafweliwa na mafwele? Binafsi naogopa sana watu wa humu japo nawapenda sanah hasa wanaharakati wenzangu.
Spiritual protection.. Nakutana na watu weka.. Wale wabaya wanajua tulicheza sindimba na mdumange.. Hata wabaya huwa wema inategemea mazingira..!!!
 
Huyu jamaa nilikuwa karibu nae sana na kifo chake kilinitikisa. Ni miaka mitano sasa nadhani imepita

Wengine sijui hata kama tukifariki kuna wa kuleta taarifa au na sisi tutaishia kama IDs ambazo zinapotea pasipo watu kujua shida ni nini.
Dah usiseme hivyo.. Halafu next week tengeneza ratiba...!
 
Member pekee nafahamiana nae kwa ukaribu sana ni mkwepu jr , nadhani ndio mtu pekee nikiondoka atawapa taarifa au yeye akitangulia Mimi nitawapa taarifa.
Yule jamaa Fork kifo chake kilinihuzunisha sana maana alikuwa anatuambia Hali anayopitia na tukawa tunachukulia poa na kukejeli. Aendee kupumzika kwa amani aisee.
 
Daah naukumbuka ule uzi, ndo maana tunaambiwa be kind kwa watu hujui wanapitia nini.
Ila mtu kama una roho nyepesi bora usilete changamoto zako mtandaoni kuna vichaa humu kama wametiwa pili pili kichaa kwenye ubongo!
Wale waliokuwa wanapondea sijui wanajisikiaje huko.. Baada ya kifo cha jamaa wengi waliukimbia ule uzi
 
  • Thanks
Reactions: naa
Back
Top Bottom