Vifaranga vya Ubelgiji vilivyokamatwa Airport Dar bado havijaondolewa

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,383
8,132
Licha ya Serikali kuagiza vifaranga vya kuku 62,730 wa mayai vilivyoingizwa nchini virudishwe Ubelgiji, inadaiwa hadi sasa bado havijaondolewa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA).

Vifaranga hivyo vilivyoingizwa nchini Desemba 22 na kampuni ya Phoenix Farms Limited, vilizuiliwa na Wizara ya Mifugo na Uvuvi baada ya kubainika kutokuwa na vibali wala cheti cha afya kama utaratibu unavyotaka.

Kutokana na hilo, wizara iliitaka kampuni hiyo kuviondoa eneo la mizigo la uwanja wa ndege na kuvirudisha vilikotoka, lakini hadi jana, taarifa zinasema bado vifaranga hivyo vyenye thamani ya zaidi ya Sh200 milioni havijaondolewa uwanjani hapo.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Huduma za Mifugo wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Profesa Hezron Nonga, kifaranga kikishatotolewa katika yai kinatakiwa kikae siku zisizozidi tatu kabla ya kupelekwa katika chumba maalumu chenye virutubisho vinavyohitajika.

Mpaka jana, vifaranga hivyo vilikuwa vimetimiza siku saba tangu vizuiwe na Mwananchi lilipomtafuta zaidi ya mara tano mmoja wa viongozi wa kampuni ya Phoenix Farms Limited, Irfan Mitha hakutoa ushirikiano baada ya mara ya kwanza, saa 3:59 asubuhi kupokea simu na kumtaka mwandishi ampigie baada ya nusu saa.

Alipopigiwa baadaye alijibu “nipo kikaoni kushughulikia suala hilo” na baada ya hapo hakupokea tena simu.

Juzi, Profesa Nonga alisema baada ya wizara kutimiza majukumu yake, wenye dhamana sasa ni watu wa viwanja vya ndege, forodha na kampuni ya Phoenix.

“Vifaranga havikutumwa Wizara ya Mifugo, tulichokifanya ni kuvinyima uwezekano wa kuingia nchini, sasa taratibu zinazofuata zipo nje ya uwezo wetu. Ukurasa tulishaufunga, kwani hatuna dhamana tena,” alisema Profesa Nonga.

Hata hivyo, taarifa kutoka Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) zinasema hilo ni suala la Wizara ya Mifugo na Uvuvi.

Lakini, kilichosemwa na Profesa Nonga kinafanana na msimamo wa Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mashimba Ndaki aliyesema “tumeshafanya kazi yetu, sasa hatujui kama vimerejeshwa au la na tulisema mzigo hatupokei kwa sababu hauna vibali, ndio utaratibu huo.”

Kanuni ya 26 ya Udhibiti wa Usafirishaji wa Wanyama na Mazao inaeleza wanyama watakaofika nchini bila kibali au cheti cha afya, mkaguzi aliyeko kituoni aizuie kuingia.

MWANANCHI
 
Hili sakata la vifaranga hutajua limeishaje ......kinachoendelea sasahivi ni kuwekwa kapuni tu
 
Hivi haya mambo hayanaga mazungumzo ya kibinadamu? Hayanaga warning ⚠️ ni amri moja tu? Naomba Mungu wasivi chome moto tu...m 200 !! Jamani?!
 
Kama hawafuati utaratibu ni no way, unaona ml200 nyingi ukizuka ugonjwa ,mafua ya ndege gharama ya kuumanage ni mabilioni,fuata taratibu za nchi husika peleka sample ifanyiewe uchunguzi , Magu ndo alikuwa anawaweza piga kiberiti
 
Kwa
Licha ya Serikali kuagiza vifaranga vya kuku 62,730 wa mayai vilivyoingizwa nchini virudishwe Ubelgiji, inadaiwa hadi sasa bado havijaondolewa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA).

Vifaranga hivyo vilivyoingizwa nchini Desemba 22 na kampuni ya Phoenix Farms Limited, vilizuiliwa na Wizara ya Mifugo na Uvuvi baada ya kubainika kutokuwa na vibali wala cheti cha afya kama utaratibu unavyotaka.

Kutokana na hilo, wizara iliitaka kampuni hiyo kuviondoa eneo la mizigo la uwanja wa ndege na kuvirudisha vilikotoka, lakini hadi jana, taarifa zinasema bado vifaranga hivyo vyenye thamani ya zaidi ya Sh200 milioni havijaondolewa uwanjani hapo.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Huduma za Mifugo wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Profesa Hezron Nonga, kifaranga kikishatotolewa katika yai kinatakiwa kikae siku zisizozidi tatu kabla ya kupelekwa katika chumba maalumu chenye virutubisho vinavyohitajika.

Mpaka jana, vifaranga hivyo vilikuwa vimetimiza siku saba tangu vizuiwe na Mwananchi lilipomtafuta zaidi ya mara tano mmoja wa viongozi wa kampuni ya Phoenix Farms Limited, Irfan Mitha hakutoa ushirikiano baada ya mara ya kwanza, saa 3:59 asubuhi kupokea simu na kumtaka mwandishi ampigie baada ya nusu saa.

Alipopigiwa baadaye alijibu “nipo kikaoni kushughulikia suala hilo” na baada ya hapo hakupokea tena simu.

Juzi, Profesa Nonga alisema baada ya wizara kutimiza majukumu yake, wenye dhamana sasa ni watu wa viwanja vya ndege, forodha na kampuni ya Phoenix.

“Vifaranga havikutumwa Wizara ya Mifugo, tulichokifanya ni kuvinyima uwezekano wa kuingia nchini, sasa taratibu zinazofuata zipo nje ya uwezo wetu. Ukurasa tulishaufunga, kwani hatuna dhamana tena,” alisema Profesa Nonga.

Hata hivyo, taarifa kutoka Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) zinasema hilo ni suala la Wizara ya Mifugo na Uvuvi.

Lakini, kilichosemwa na Profesa Nonga kinafanana na msimamo wa Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mashimba Ndaki aliyesema “tumeshafanya kazi yetu, sasa hatujui kama vimerejeshwa au la na tulisema mzigo hatupokei kwa sababu hauna vibali, ndio utaratibu huo.”

Kanuni ya 26 ya Udhibiti wa Usafirishaji wa Wanyama na Mazao inaeleza wanyama watakaofika nchini bila kibali au cheti cha afya, mkaguzi aliyeko kituoni aizuie kuingia.

MWANANCHI
Kwa hizi siku saba- kama wana magonjwa 1. Vingekuwa vimeshaanza kupukutika 2. Upepo na watu ingia toka hapo airport Kitunda na maeneo Jirani wafugaji wangeshakuwa kwenye hot soup na kuku wao. Ushauri Serikali ifanye random sampling ya vifanga wakikuta avina madhara waviruhusu wapelekwe shambani wakafugike as planned
 
Back
Top Bottom