Serikali yazuia vifaranga 62,730 vilivyoingizwa nchini kutoka Ubelgiji

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,308
5,462
Mkurugenzi wa Huduma za Mifugo wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Profesa Hezron Nonga amesema wamezuia vifaranga 62, 730 vya kuku wa mayai kuingia nchini baada ya kubainika kutokuwa na vibali pamoja na cheti cha afya.

Vifaranga hivyo ambavyo ni mali ya kampuni ya Phoenix Farms Limited ya Mkuranga mkoani Pwani vilivyohifadhiwa katika makasha 697 vilikuwa vinatokea Ubelgiji na vimezuiliwa katika uwanja ndege wa Julius Nyerere eneo la mizigo.

Profesa Nonga amewaambia wanahabari leo Jumamosi Desemba 24, 2022 vifaranga hivyo viliwasili Desemba 22 saa 4 usiku ndipo wakaguzi wa mifugo na mazao yake walipovibaini kwamba vimeingia bila kufuata taratibu na kanuni.

“Kulingana na kifungu cha 54 (2) cha sheria ya magonjwa ya wanyama, sura 156 inakataza kuingiza mifugo na mazao yake nchini bila kuwa na vibali. Kitendo cha Phoenix kutaka kuingiza kuku wa mayai 62,730 ni kukiuka sheria.

“Kanuni ya 26 ya Udhibiti wa Usafirishaji wa Wanyama na Mazao yake GN namba 28/2007 inabainisha kuwa ikiwa wanyama au mazao ya wanyama yatafika nchini bila kibali au cheti cha afya ya wanyama au mazao ya wanyama, mkaguzi aliyeko kituoni azuie uingizaji,” amesema Profesa Nonga.

Profesa Nonga amebainisha kuwa kutokana tafsiri ya vifungu hivyo vifaranga vya kuku wa mayai 62,730 walioletwa na Phoenix Farms Limited wamezuiliwa kuingizwa nchini kwa sababu ni hatarishi.

“Wizara inautaka uongozi wa kampuni hii kuvirudisha vifaranga hivyo Ubelgiji kwa sababu vinaweza kuhatarisha usalama wa kuku nchini, pia waviondoshe katika maeneo ya uwanja wa ndege.

“Zamani vilikuwa vinachomwa moto, lakini sasa hapana bali aliyevileta avirudishe alikovitoa kwa gharama zake,” amesema Profesa Nonga.

Chanzo: Mwananchi
 
2017 USA ilikamata trei 300, 000/= za mayai toka Brazil zilizoyakinishwa zilikuwa na virusi vya kansa.

Hongera Prof. Mkurugenzi kwa uthubutu na uwezo mzuri kuzuia hivyo vifaranga.
 
Mkurugenzi wa Huduma za Mifugo wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Profesa Hezron Nonga amesema wamezuia vifaranga 62, 730 vya kuku wa mayai kuingia nchini baada ya kubainika kutokuwa na vibali pamoja na cheti cha afya.

Vifaranga hivyo ambavyo ni mali ya kampuni ya Phoenix Farms Limited ya Mkuranga mkoani Pwani vilivyohifadhiwa katika makasha 697 vilikuwa vinatokea Ubelgiji na vimezuiliwa katika uwanja ndege wa Julius Nyerere eneo la mizigo.

Profesa Nonga amewaambia wanahabari leo Jumamosi Desemba 24, 2022 vifaranga hivyo viliwasili Desemba 22 saa 4 usiku ndipo wakaguzi wa mifugo na mazao yake walipovibaini kwamba vimeingia bila kufuata taratibu na kanuni.

“Kulingana na kifungu cha 54 (2) cha sheria ya magonjwa ya wanyama, sura 156 inakataza kuingiza mifugo na mazao yake nchini bila kuwa na vibali. Kitendo cha Phoenix kutaka kuingiza kuku wa mayai 62,730 ni kukiuka sheria.

“Kanuni ya 26 ya Udhibiti wa Usafirishaji wa Wanyama na Mazao yake GN namba 28/2007 inabainisha kuwa ikiwa wanyama au mazao ya wanyama yatafika nchini bila kibali au cheti cha afya ya wanyama au mazao ya wanyama, mkaguzi aliyeko kituoni azuie uingizaji,” amesema Profesa Nonga.

Profesa Nonga amebainisha kuwa kutokana tafsiri ya vifungu hivyo vifaranga vya kuku wa mayai 62,730 walioletwa na Phoenix Farms Limited wamezuiliwa kuingizwa nchini kwa sababu ni hatarishi.

“Wizara inautaka uongozi wa kampuni hii kuvirudisha vifaranga hivyo Ubelgiji kwa sababu vinaweza kuhatarisha usalama wa kuku nchini, pia waviondoshe katika maeneo ya uwanja wa ndege.

“Zamani vilikuwa vinachomwa moto, lakini sasa hapana bali aliyevileta avirudishe alikovitoa kwa gharama zake,” amesema Profesa Nonga.
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Dar es Salaam, Desemba 24, 2022

KUZUILIWA KUINGIA NCHINI KWA VIFARANGA 62,730 VYA KAMPUNI YA PHOENIX FARMS LIMITED VILIVYOFIKISHWA AIRPORT KUTOKA NCHI YA UBELIGIJI
Ndugu wanahabari,

Tarehe 22/12/2022 saa nne usiku Wakaguzi wa Mifugo na Mazao yake walio katika kituo cha Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) walikamata vifaranga wa kuku wa mayai 62,730 mali ya Kampuni ya Phoenix Farms Limited ya Mkuranga, Pwani vilivyofikishwa uwanjani hapo vikitokea nchini Ubeligiji bila ya kuwa na vibali vya kuingiza nchini vifaranga (Import permit) pamoja na cheti cha afya (animal health certificate). Vifaranga hivyo viko kwenye makasha (crates) 697 na stakabadhi ya mauziano (Invoice) ya mzigo inaonesha vina gharama ya shilingi 200,262,706 ambayo ni sawa na Euro 80,828.80 (Cost Insurance and Freight – CIF). Mkurugenzi wa Kampuni pamoja na Wakala wa Mmiliki wa vifaranga (clearing agent) hivyo walikiri kutokuwa na kibali hivyo kuwa amevunja Sheria ya Magonjwa ya Wanyama Sura ya 156 na Kanuni za Udhibiti wa Usafirishaji wa Wanyama na Mazao yake ya GN. Na. 28/2007.

Ndugu wanahabari,

Kulingana na kifungu cha 54(2) cha Sheria ya Magonjwa ya Wanyama Sura ya 156 kinakataza kuingiza nchini mifugo na mazao yake bila kuwa na kibali nanukuu; “No person shall bring or cause or permit allow to be brought into the country any animal product, contrary to any order or regulation prescribing the introduction of animal products into the country or without animal products inspected and certified in the prescribed manner.” Hivyo kwa kitendo cha Kampuni ya Phoenix Farms kutaka kuingiza nchini vifaranga wa kuku wa mayai 62,730 ni kukiuka Sheria hii.
Ndugu wanahabari,

Aidha, Kanuni ya 26 ya Kanuni za Udhibiti wa Usafirishaji wa Wanyama na Mazao yake ya GN. Na. 28/2007 inabainisha kuwa, “Ikiwa wanyama au mazao ya wanyama yatafika nchini bila kibali na cheti cha afya ya wanyama au mazao ya wanyama, Mkaguzi aliyeko kwenye kituo cha ukaguzi azuie uingizaji wa wanyama au mazao ya wanyama husika nchini. In the event, of any animal or animal products intended for importation arriving without the certificate required as aforesaid, an Inspector shall refuse to allow such animal or animal products to enter Tanzania ….”.

Ndugu wanahabari,

Hivyo, kutokana na tafsiri ya vifungu hivyo viwili hapo juu, vifaranga wa kuku wa mayai 62,730 walioletwa na Kampuni ya Phoenix Farms Limited waliopo katika Uwanja wa Julius Nyerere International Airport (JNIA) upande wa mizigo (cargo) wamezuiliwa kuingizwa nchini kwa kuwa ni mzigo hatarishi. Aidha, Wizara ya Mifugo na Uvuvi imeutaka uongozi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania Tawi la Uwanja wa Ndege wa Dar es Salaam kuielekeza Kampuni ya Phoenix Farms Limited kuvirudisha vifaranga hivyo nchini Ubeligiji kwa sababu wanaweza kuhatarisha usalama wa kuku nchini. Vilevile, Mkurugenzi wa Kampuni ya Kampuni ya Phoenix Farms Limited ameelekezwa kuviondosha vifaranga hivyo katika maeneo ya uwanja wa ndege na kuvirudisha alikovitoa.

Ndugu wanahabari,
  • Kama mtakumbuka, Mwaka 2006 Tanzania iliweka zuio (karantini) la uingizaji wa kuku na mazao yake kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa Mafua Makali ya Ndege duniani (HPAI). Kutokana na zuio hilo (karantini), nchi yetu imeendelea kuwa salama dhidi ya ugonjwa huo ambao umeathiri nchi nyingi duniani. Ugonjwa wa Mafua Makali ya Ndege huambukiza wanyama na binadamu na hutokea kwa njia ya mlipuko na kusababisha madhara makubwa ikiwemo vifo vingi vya kuku na ndege wa porini. Njia za kudhibiti ugonjwa huu ni pamoja na kuzingatia usafi kwenye mabanda ya kuku (biosecurity measures) na karantini ya kuzuia kuingiza kuku, ndege wengine na mazao yao. Nitoe wito kwa watanzania wote hususan wadau wa kuku kuzingatia Sheria, Kanuni na Miongozo iliyopo ya kudhibiti kuingia na kuenea kwa magonjwa ya kuku nchini hususan Ugonjwa wa Mafua Makali ya Ndege ili kulinda usalama wa kuku, na ndege wengine pamoja na afya ya jamii ya watanzania kwa ujumla.
Asanteni kwa kunisikiliza
Imetolewa na
Profesa Hezron E. Nonga
Mkurugenzi wa Huduma za Mifugo
WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI
24 DESEMBA 2022
 
Attachments

  • TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI VIFARANGA PHOENIX 2022.pdf
    355.1 KB · Views: 3
Kwanini vitoke mbali kote huko! Vina maslahi gani hata wauze 5000 mathalani, ukijumlisha uandaaji wa mzigo, usafiri from origin to port to tanzania bado port charges bila kusahau insurence! Wana maslahi gani hata wakiuza mmoja elfu10
JamiiForums2073952431.jpg
 
Viongozi wetu kuwaelewa ni kazi sawa kampuni imevunja sheria lakini kwanini wasivipime hivo vifaranga then kodi ikatwe na viruhusiwe kama vipo salama
Sheria haisemi hivyo... haitaki hilo unalotaka... tii sheria, fata sheria... kama tuna taka mabadiliko basi tufanye mabadiliko ya sheria na kanuni zake

Juzi yule mzungu mwenye kiwanda cha kuzalisha vifaranga vya kuku pale moshi alivitia moto au teketeza kwa moto vifaranga vingi sana kwa sababu ya kukosa soko

Leo nashangaa kuna mtu ana ingiza vifaranga takribani 60k, yani mwezi mmoja nazani baada ya yule mwanamama mzungu kuteketeza vifaranga vyake

Na alilalamikia kukosa soko na hasa uingizwaji wa vifaranga kutoka nje...

Hivi vifaranga vipatavyo 62,730 vina gharama ya Tsh. 200,262,706 ambapo kila kimoja ni Tsh. 3,192.4551

Wakati kwetu hapa tuna vifaranga vina uzwa mpaka 800/- na bei ya juu nazani ni 2,500/-

Uingizwaji wa hivyo vifaranga bago vina kodi zake hivyo tutegemee gharama zake kuongezeka kulingana na kodi atakayo chajiwa mnunuzi/muingizaji

SERIKALI YASITISHA UTOAJI WA VIBALI VYA KUINGIZA VIFARANGA VYA KUKU KUTOKA NJE... soma hapo chini...

NAIBU Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega amesema baada ya tarehe 30 mwezi huu, hakuna vifaranga vya kuku vitakavyoingizwa hapa nchini na kwamba serikali haitoi tena vibali vya kuingiza vifaranga hivyo.

Naibu Waziri Ulega amebainisha hayo (22.07.2022) jijini Dodoma wakati wa kikao cha wizara na wadau wa tasnia ya kuku, kujadili namna ya kukuza tasnia hiyo ambapo lengo la hatua hiyo ni utekelezaji wa sheria ya mwaka 2006 ambapo serikali imekuwa ikizuia uingizaji wa vifaranga nchini kutoka nje ya nchi ili kudhibiti ugonjwa wa mafua ya ndege kwa mifugo jamii ya ndege na kulinda wazalishaji wa kuku ndani ya nchi.

Akizungumza wakati akifunga kikao hicho kilichojadili ajenda mbalimbali zikiwemo za upatikanaji wa vifaranga vya kuku, chakula cha kuku na bei ya kuku sokoni, Mhe. Ulega amesema ni mategemeo kuwa serikali haitaona vifaranga vinaingizwa nchini kutoka nje ya nchi na kutaka kuwepo kwa mfumo wa taarifa zinazohusu wazalishaji wa vifaranga vya kuku kuanzia wazalishaji wakubwa hadi wadogo ambao wamesajiliwa na kutoa taarifa serikalini ili kuiwezesha kujua kiwango cha uzalishaji na kuwa na takwimu sahihi juu ya mahitaji ya vifaranga nchini.

“Ni mategemeo yetu ni kutokuona baada ya tarehe 30 mtu anaingiza vifaranga hapa nchini kutoka mahali popote pale, jambo la pili kuwepo na mfumo ambao utasaidia serikali kujua ni kiasi gani cha uzalishaji vifaranga ndani ya nchi yetu ili kujipima uwezo wetu na mahitaji yetu ndani ya nchi.” Amesema Mhe. Ulega

Awali Naibu Waziri Ulega akizungumza wakati akifungua kikao hicho cha wizara na wadau wa tasnia ya kuku amesema tasnia hiyo imekua kwa kasi miaka ya hivi karibuni kutokana na kuwepo kwa soko linalotokana na ongezeko la watu na kipato, ongezeko la uwekezaji na uwepo wa mazingira bora ya uwekezaji katika tasnia ya kuku, urahisi wa kufuga kuku na uwezekano mkubwa wa kuwamiliki kuliko wanyama wakubwa.

Kwa upande wake Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Mifugo Bw. Stephen Michael akizungumza kwenye kikao hicho amesema kutokana na umuhimu wa tasnia ya kuku katika Mpango Kabambe wa Sekta ya Mifugo wa Mwaka 2016 umefanya tathmini na kubainisha kuwa hadi kufikia Mwaka 2031 kutakuwa na upungufu wa nyama kwa tani milioni 1.8 hivyo tasnia ya kuku ni rahisi ikitiliwa mkazo itasaidia katika kuongeza uzalishaji wa nyama nchini.

Bw. Michael ambaye pia ni Mkurugenzi wa Idara ya Uzalishaji na Masoko katika Wizara ya Mifugo na Uvuvi, amesema ufugaji wa kuku ni njia rahisi na ambayo haihitaji maeneo makubwa na miundombinu mingi tofauti na mifugo mingine hivyo kikao hicho ni muhimu kwa kuwa kimeunganisha wadau wa tasnia hiyo pamoja na kutatua changamoto zilizopo kwa kuzingatia uwepo wa taasisi mbalimbali zinazotoa mikopo kwa vijana na akina mama na vikundi mbalimbali ambao wengi wamejizatiti katika biashara ya kuku.

Naye Katibu wa Chama cha Wadau wa Kuku Tanzania (PAT) Bw. Manase Mrindwa amebainisha changamoto za chakula cha kuku kuwa kimefikia hadi Shilingi Elfu 80 kwa mfuko mmoja kwa mwezi wa Julai ambapo kunatokana hasa na ongezeko la bei ya mahindi na mashudu ya soya kwenye soko la Tanzania.

Bw. Mrindwa amebainisha pia changamoto ya kutokea kwa uhaba wa vifaranga kwa wakati fulani wa mwaka, huku mitaani bado viko vifaranga visivyo bora ambavyo vinawafikia wafugaji hususan wafugaji wadogo.

Kikao cha wadau wa tasnia ya kuku kilichoandaliwa na Wizara ya Mifugo na Uvuvi kimejumuisha menejimenti ya wizara Sekta ya Mifugo, wazalishaji wa vifaranga vya kuku, chakula cha kuku na wafugaji wa kuku ambapo wametoa maoni mbalimbali ya namna ya kuboresha tasnia hiyo na kuomba kuwepo kwa vikao vya namna hiyo mara kwa mara lengo likiwa ni kukuza tasnia hiyo kwa kuirasimisha na kuwepo kwa machinjio maalum kwa ajili ya kuku na bei elekezi ya kuku sokoni.
 
Sheria haisemi hivyo... haitaki ilo unalo taka... tiisheria, fata sheria... kama tuna taka mabadiliko basi tufanye mabadiliko ya sheria na kanuni zake

Juzi yule mzungu mwenye kiwanda cha kuzalisha vifaranga vya kuku pale moshi alivitia moto au teketeza kwa moto vifaranga vingi sana kwa sababu ya kukosa soko

Leo nashangaa kuna mtu ana ingiza vifaranga takribani 60k, yani mwezi mmoja nazani baada ya yule mwanamama mzungu kuteketeza vifaranga vyake

Na alilalamikia kukosa soko na hasa uingizwaji wa vifaranga kutoka nje...

Hivi vifaranga vipatavyo 62,730 vina gharama ya Tsh. 200,262,706 ambapo kila kimoja ni Tsh. 3,192.4551

Wakati kwetu hapa tuna vifaranga vina uzwa mpaka 800/- na bei ya juu nazani ni 2,500/-

Uingizwaji wa hivyo vifaranga bago vina kodi zake hivyo tutegemee gharama zake kuongezeka kulingana na kodi atakayo chajiwa mnunuzi/muingizaji
Mbali ya Mama Fey kufanya alivyofanya (BUT) She had a valid concern.
 
Urasimu umerudi... Kwani Si tunanunua mchele kilo 3000 sababu mchele mwingi umeuzaaa nje?? Mahindi kama yote yameenda kenyaaa... Leo wananchi wanapambana na kupanda na bei za mazao ila kuna viongozi wakubwa aana maghala ya vyakulaaa wanatuuzia bei juuu.. Urasimuu urasimuuuu...
 
Back
Top Bottom