peno hasegawa
JF-Expert Member
- Feb 24, 2016
- 12,830
- 21,460
Mkurugenzi wa Huduma za Mifugo,Herzon Nonga akionesha Vifaranga vya kuku wa mayai vilivyozuiwa kuingia nchini,kutokuwa na vibali na cheti cha afya katika kago ya mizigo ya uwanja wa ndege wa Juliasi Nyerere,jijini Dar es Salaam jana.
Kukamatwa kwa vifaranga vilivyokuwa vikiingizwa nchini kumeibua masuala ya uwajibikaji na kutofuata sheria miongoni mwa viongozi wa Serikali na wadau wa sekta ya ufugaji wa kuku.
Vifaranga vilivyozuiliwa kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Desemba 22, 2022, ni mali ya Kampuni ya Phoenix Farms Limited iliyopo Mkuranga mkoani Pwani.
Vifaranga hivyo vilivyofungwa kwenye maboksi 697 yenye thamani ya Sh200.262 milioni, vilikamatwa wakati wa ukaguzi walipokuwa wakiingizwa nchini kutoka Ubelgiji.
Mwananchi imebaini kuwa Kampuni ya Phoenix Farms Limited iliwasilisha barua ya maombi kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi kuomba kibali cha kuagiza vifaranga kutoka nchi hiyo ya Ulaya.
Pia, imethibitishwa kuwa waagizaji walikuwa wamepewa cheti cha mifugo na mamlaka ya Ubelgiji.
Baadhi ya wadau katika sekta hiyo wameishutumu wizara hiyo kwa kushindwa kutoa leseni za uagizaji bidhaa kutoka nje na kuchukua hatua za ziada kuwalinda wawekezaji wa ndani.
“Mamlaka zimeshughulikia suala hilo kwa njia isiyo ya haki. Walitakiwa kutoa kibali hicho kwa kuzingatia kwamba nchi haina uwezo wa kuzalisha kuku wa kukidhi mahitaji yake,” alisema mdau kwa sharti la kutotajwa jina.
“Vifaranga hivyo vingeweza kupelekwa kwenye shamba la kampuni hiyo na kuwekwa karantini humo. Vingegundulika kuwa na afya njema mwekezaji angeweza kuadhibiwa na vifaranga virudi kwake,” kiliongeza chanzo hicho.
Alipotafutwa, Ofisa Mkuu wa Phoenix Farms Limited, Irfan Mitha alikataa kutoa maoni yake kuhusu uhalali wa hati mbili zilizotajwa hapo juu.
“Niko busy leo; nipigie simu kesho, nitakuwa kwenye nafasi ya kutoa maoni yangu,” aliliambia gazeti hili.
Mkurugenzi wa Huduma za Mifugo (DVS) katika Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Profesa Hezron Nonga alisema ombi la kibali cha kuagiza cha Desemba Mosi, 2022, halijafika ofisini kwake wala wizarani.
“Tuliona barua ya maombi ya vibali kutoka nje ya nchi, muda mfupi baada ya vifaranga kukamatwa JNIA. Kadhalika, cheti cha mifugo kilichoandikwa na Shirikisho la Ubelgiji la Usalama wa Mnyororo wa Chakula (FACFAS),” alisema Profesa Nonga.
Akitoa taarifa ya vifaranga hivyo, Profesa Nonga alisema vyote 62,730 vimekufa baada ya kutelekezwa kwenye uwanja wa ndege.
“Mwagizaji ana kesi nyingine ya kujibu mbele ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa kuwa mipango ya uteketezaji wa kuku inaendelea,” alisema.
Chanzo: Mwananchi