Suip
JF-Expert Member
- Sep 21, 2010
- 1,314
- 760
Nina kuku wakubwa ambao nawatumia kama wazazi,pia nina vifaranga wa takriban miezi 3 na nusu,mara mwisho niliwapa chanjo ya kideri tar. 20.8.2023 na hapa kati nilikuwa na vifaranga wengine wapatao 40 wenye umri wa mwezi moja ambao niliwapa chanjo ya kideri juzi tar. 4.12.2023 ikiwa ni pamoja na hao kuku wakubwa na vifaranga hao wa miezi 3na nusu.Sasa kilichotokea vifaranga hao wa miezi 3 na nusu wamepata kama kuambukizwa kideri na nimeshapoteza vifaranga hao watano,ila kuku wakubwa na hao wa mwezi moja hawana tatizo bado.
Nashindwa kuelewa kwani chanjo imesafirishwa vizuri na ni ile ya kuchanganya kwa maji ya kunywa na nilichanganya kwenye lita 10 ya maji na baada masaa mawili niliondoa na kuosha vyombo kwa maji ya moto na kuwapa maji mengine masafi. Na tangu mwaka 2012 natumia hizi chanjo na sijawahi pata maambukizi ya kideri hadi leo nimewapa chanjo juzi.
Nina mashaka sijui ni uhifadhi kwenye maduka ya wauzaji wa chanjo au kampuni iliyotengeneza ya hapa ndani ya nchi ambayo ndio mara kwanza kutumia nipo njiapanda kupoteza zaidi vifaranga vyangu wakubwa hivyo.Nahangaika kuwapa OTC plus ambayo ni antibiotic na multivitamin kwenye maji ya kunywa