KWELI Vidonda vya tumbo(Ulcers) huweza kuambukizwa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine kupitia mate au kinyesi

Taarifa hii imethibitika kuwa ya kweli baada ya kufanya tathmini ya kina
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2
Leo nimesoma mtandaoni kuwa Vidonda vya tumbo(Ulcers) huweza kuambukizwa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine.

Naomba kujua kama ni kweli maana siku zote mie najua vidonda vya tumbo huvipata mtu kutokana na mtindo wake wa maisha(kutokula) au kwa kutumia baadhi ya dawa ambazo zinaweza kuchubua utumbo.

Sasa hii ya kuambukiza kwangu imekuwa mpya sana, tena mwandishi alifafanua zaidi kuwa eti iwapo mwenza wako ana ulcers basi uwezekano wa wewe kuupata ni mkubwa maana anaweza kukuambukiza.

1710569707751.jpeg

 
Tunachokijua
Vidonda vya tumbo hutokea katika ukuta wa tumbo. Vidonda hivi hufahamika kitaalam kama peptic ulcers. Vidonda hivi hutokea kutokana na mashambulizi ya bakteria wanaoitwa Helicobacter pylori (H.pylori) au kulika kwa ukuta wa tumbo kutokanana na athari za tindikali zilizopo tumboni (stomach acids) kama vile tindikali ya hydrocloric yaani hydrocloric acid.
images
Vidonda hivi vimegawanyika katika makundi makuu matatu ambayo ni:-
1.Gastric ulcers hivi hutokea ndani ya tumbo la chakula
2.Esophageal ulcers hivi hutokea ndani ya esophagus. Hii ni sehemu inayounganisha kati ya koo la chakula na tumbo la chakula.
3.Duodenal ulcers hivi hutokea kwenye sehemu ya juu ya utumbo mdogo inayoitwa duodenum

Sababu za vidonda vya tumbo ni maambukizi ya bakteria Helicobacter pylori (H. pylori) na utumiaji wa dawa za muda mrefu za aspirini na aina za dawa ziitwazo nonsteroidal anti-inflammatory drugs (NSAIDs) ni kama (Advil, Aleve, na nyingine). Stress (msongo wa mawazo) na vyakula vyenye viungo havisababishi vidonda vya tumbo. Walakini, vinaweza kufanya dalili zako kuwa mbaya zaidi.

Baadhi ya Dalili za vidonda vya tumbo
1. Maumivu ya tumbo kutokea kitovuni mpaka kifuani
2. Kukosa hamu ya kula
3. Kutoka na damu na kupata choo cheusi sana au chenye damu

Baada ya Mdau wa JamiiCheck kutaka kufahamu iwapo vidonda vya tumbo vinaweza kuambukizwa kutoka kwa mtu moja kwenda kwa mwingine Jamiicheck ilifuatilia suala hilo kwa kusoma machapisho mbalimbali na kuzungumza na mtaalam wa afya ambapo walieleza kuwa:-

Chuo kikuu cha Arizona kimechapisha kuwa H. pylori huweza kusambazwa kutoka kwa mtu hadi mtu kupitia mate.

Bakteria hawa pia wanaweza kuambukizwa kwa uchafuzi wa mazingira kupitia kinyesi cha mtu mwenye bacteria hawa ambapo chembe chembe zitaingia kwenye chakula au maji ambayo hayajatibiwa na kuwa safi na salama. Watu wengi huambukizwa wakiwa watoto.

Pia JamiiCheck imezungumza na Dkt. Norman Jonas ambaye ni Daktari na Mkufunzi ambaye amefafanua kuwa

Ugonjwa wa vidonda vya tumbo husababishwa na bakteria aitwaye Helicobacter pylori (H. pylori) kwa kiasi kikubwa.

Kuna njia mbili kuu za maambukizi

  • Fecal-oral: Hii hutokea wakati Mtu anaambukizwa kwa kula au kunywa chakula au maji yaliyochafuliwa na kinyesi chenye H. Pylori.
  • Oro-oral: Hii hutokea wakati mtu anaambukizwa kupitia mate au majimaji mengine ya mdomo kutoka kwa mtu aliyeambukizwa, hii inaweza kutokea kwa njia ya kumbusu, kushiriki chakula kilichotafunwa au kutumia vyombo sawa vya kula.
Maambukizi kwa njia ya kubusu
  • Uchunguzi wa Epidemiologia: Baadhi ya tafiti zimeonyesha Watu wanaoishi pamoja na wenzi wao walioambukizwa H.Pylori wana uwezekano mkubwa wa kuwa na aina sawa ya bakteria.
  • Uchunguzi wa Maabara: Tafiti zingine zimegundua H.Pylori kwenye mate ya watu walioambukizwa.
Pamoja na hiyo, hilo halijawa wazi kwa sababu hii
Kiasi cha H.Pylori kwenye mate kinaweza kuwa kidogo sana kusababisha maambukizi. Ingawa tafiti zingine zinaonyesha uwezekano wa kuambukizwa H.Pylori kwa njia ya kumbusu, ushahidi bado haujaisha. Utafiti zaidi unahitajika ili kuthibitisha au kukanusha nadharia hii.

Mapendekezo
Ili kupunguza hatari ya kuambukizwa kwa H.Pylori kwa ujumla, ni muhimu kuosha mikono mara kwa mara, hasa baada ya kutumia choo na kabla ya kula.

  • Kunywa maji safi na salama
  • Kula chakula cha moto
  • Ikiwa una wasiwasi juu ya kuambukizwa H.Pylori, zungumza na daktari
Kutokana na uchambuzi wa wataalamu wa afya na machapisho ambayo Jamiicheck imepitia ni kweli kuwa uwezekano wa mtu kuambukizwa vidonda vya tumbo kutoka kwa mwingine upo na hivyo hoja hiyo ni kweli.

Similar Discussions

2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom