Ongezeko la wagonjwa wenye Vimelea vya Helicobacter Pylori nini Shida

bryan2

JF-Expert Member
Jun 8, 2016
3,323
4,667
Helicobacter Pylori ni bacteria ambao wanasadikika kusababisha vidonda vya tumbo na pia Kansa ya utumbo/tumbo, njia zake za kuambukizwa ni kupitia matumizi ya vitu vyenye vya H-Pylori kama vile maji au vyakula na pia kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mtu mwingine.

Helicobacter Pylori ni kati ya bacteria ambao zamani hawakuwepo sana ila kwa sasa kati ya wagonjwa kumi wanaofika kwenye vituo vya afya na wenye dalili za kuumwa matumbo, tumbo kujaa gesi, uchovu, kichwa, kuharisha...nk wakipimwa kutumia kipimo cha choo wengi wanakutwa positive kwa huyu bacteria.

Achana na wale wanaotaka kuuza Heligo-kit ila kiuhalisia watu wengi sana wanaopata huduma kwenyevituo rasmi vya afya ni wahanga wa hawa bacteria.

Je shida kubwa ni nini, watu hawana elimu juu ya hawa bacteria au mazingira yetu yamekua machafu au usafi kwenye uandaaji wa vyakula vyetu sio mzuri.
 
Tuanzie hapa kwanza.

H. pylori Infection: Symptoms, Causes, Diagnosis, and Treatment

Medically Reviewed by Jabeen Begum, MD on September 27, 2023 Written by Susan Bernstein, Sarah Gleim
8 min read

Nimecheka sana hapo, kwenye causes:
¤living in a developing country.
 
C7E6D096-D1D5-46A1-B7F6-B409C74EC0C7.jpeg
 
Attachments

  • 1F84746A-16C0-4486-B386-D60E41D212A1.jpeg
    1F84746A-16C0-4486-B386-D60E41D212A1.jpeg
    104.3 KB · Views: 9
  • 7A135EA0-978E-4DD4-80CA-739D981A68A6.jpeg
    7A135EA0-978E-4DD4-80CA-739D981A68A6.jpeg
    38.5 KB · Views: 9
Nimesumbuliwa sana na huyo bacteria. Nimetumia hizo mara tatu mfululizo lakini mara ya mwisho nimehisia shida inaweza ikawa kwenye maji kwa sababu sikuwahi kuwa na imani chanya na haya maji, na kweli yale maji ya mradi wa kijiji walikuwa hawaweki dawa na viongozi wa kamati ya maji ya kijiji walikiri hilo. Kwa hiyo nikaamua kuachana na yale maji katika kusafishia kimya pamoja kunawa kabla ya kula. Nina maendeleo mazuri sana katika afya ya tumbo.
 
Hongera sana ndugu yaa ni kweli ulikua unatibu ugonjwa ila visababishi bado vilikuwepo zingatia sana hygiene.
 
Back
Top Bottom