Daniel Mbega
JF-Expert Member
- Mar 20, 2013
- 338
- 180
VIDONDA vya Kinywa ni michubuko inayotokea kwenye mdomo na ulimi. Vidonda hivi katika kinywa husababisha mhusika kupata maumivu kwa maana kinywa ni moja ya sehemu ya mwili yenye mishipa mingi ya fahamu na wakati mwingine vidonda katika kinywa husababisha kushindwa kuongea vizuri.
Ingawa vidonda hukufanya ujisikie vibaya, huwa vinapona vyenyewe ndani ya wiki moja au mbili. Vidonda vya Kinywa hutokea kwenye au ndani ya mashavu, midomo (lips), ulimi, kingo na kuta za meno pia huweza kusambaa mpaka kwenye koromeo ikiwa havitatibiwa kwa wakati.
Aina za Vidonda vya Kinywa
Vidonda vya mdomo huwa vya duara na hutokea ndani ya kinywa, kwenye ulimi na midomo. Vinaweza kuvimba na kuwa vyeupe, vyekundu au vya kijivu. Inawezekana kuwa na kidonda kimoja au zaidi wakati mmoja na kusambaa ndani ya kinywa.
Soma zaidi hapa=> Chanzo na Jinsi ya Kuzuia Vidonda vya Kinywa! | Fikra Pevu