Beatrice Kamugisha
JF-Expert Member
- May 18, 2019
- 762
- 6,980
Maulid Kitenge na Mzee wa Kaliua mmefanya Kubwa sana kutetea uhai wa watoto wa Kimasai. Natambua Binadamu wabinafsi awatawaelewa na Binadamu wanafiki watawaambia na kuwadanganya kwamba Masai anatakiwa kuishi na wanyama Ngorongoro kama kivutio Cha utalii na kwamba Masai ni Moja ya factor iliyochangia Ngorongoro kuingia kwenye maajabu ya Dunia.
Naomba wanaowashambulia na kuwatisha watuambie ni nani Kati Yao anaweza akamwacha mwanaye anachunga ng'ombe ndani ya eneo lenye wanyama wakali kisa anawafurahisha watalii? Ni nani Kati Yao yupo tayari japo kushuka Ngorongoro nakutembea kwenye hifadhi akipishana na wanyama kama tunavyotaka maasai wafanye? Nani baina Yetu angependa kuishi nyumba za tembe ambazo jua na baridi ni Yako?
Mlichokifanya ndicho kilipaswa kufanywa na activists wengi wa nchi na Dunia. Walipaswa kutambua na kueleza Dunia kwamba mambo mawili lazima yafanyike. Moja kumtaftia Masai eneo la ufugaji au kuwawekea mazingira wanyama wasikutane na Maasai Kwa kuongeza eneo la ufugaji na kupunguza eneo la mbuga.
Kwanini nawapongeza Wanahabari hawa?
1. Kwanza wamesimamia kutetea haki ya kuishi ya wanadamu waliopo mbugani. Hii ni haki ya msingi inayotambulika Duniani. Hakuna mwandamu Wala serikali inapaswa kudhulumu haki ya kuishi. Je, Kwa miaka yote ambayo Ngorongoro imekuwepo wamekufa Watu wangapi Kwa kuvamiwa na wanyama?
2. Kitenge na Mzee wa Kaliua wamesimama kuieleza Dunia kwamba watoto Wana haki yakupata elimu. Hii ni haki ya msingi Kwa watoto. Kama serikali n wadau wengine wanathamini haki za Binadamu haki ya elimu Kwa watoto wanaozaliwa mbugani Nani anailinda?
3. Kitenge na Osca wameieleza na kuikumbisha Dunia kwamba iache kutumia ujinga wa fikra na kukosa elimu kwa wamasai kama kigezo Cha kuwasubject kwenye hatari ya wanyama wakali. Leo mchukue masai wa DSM au aliyesafiri kwenda nje then mpeleke akafuge ng'ombe kule mbugani kama atakubali. Lazima tukubali kwamba kinachowasukuma Masai kutoogopa wanyama SIYO Jambo jingine Bali ni ujinga. Hata Sisi wengine mababu zetu walizaliwa maporini Lakini kadri walivyopata uelewa walijitenga na wanyama.
4. Wameikumbusha serikali kuacha siasa na maisha ya Wamasai , waje na Suluhu. Walichukilie suala la loliondo na Longido kwa uzito wake. Wawekeze kulinda uhai wa Masai, wawekeze fedha za utalii kujenga Shule. Inatia simanzi eneo ambalo nikivutio cha utalii linakuwa maskini wakati fedha zinazozalishwa ni nyingi mno. Hakuna Masai anaweza akaondokana na umaskini kwa aiana ya ufugaji wanaofanya Ngorongoro. Hakuna mkulima atatoboa. Serikali ichukue fedha ajenge miundombinu ya kuwakwamua Hawa Binadamu kwenye vifo vinavyoepukika. Tuache kuwafanya wanadamu wenzenu vivutio vya utalii Kwa umaskini na ujinga wao.
Hongera Osca na Kitenge, mtapigwa Mawe Lakini wanaowapiga mawe wakumbuke uhai wa Binadamu ni zaidi ya historia.
Wanaowapiga mawe watambie Masai wana haki ya kuishi salama na kupata elimu pamoja na huduma za afya. Tuache siasa na maisha ya ndugu zetu WASIO na elimu.