Video: Uchochezi wa Lowassa huu hapa

Video: Uchochezi wa Lowassa huu hapa



Ni kweli kitendo cha kuwatia kizuizini miaka na miaka bila mashitaka mashehe wa Zanzibar wasiotaka Muungano ni kitendo cha kionevu na kifashisti. Wengine tunakubaliana kabisa na Edward Lowassa, tunakemea na kulaani kurudi kwa political prisoners ambao walishatoka magerezani toka JKN anatoka madarakani miaka ya 80.

Lakini katika kutetea mashehe hao, Lowassa amevuka mipaka kwa kiasi cha kutisha. Lowassa ameombea zirudi siku zile za taharuki za siasa za kidini zilizokuwepo enzi za Ally Hassan Mwinyi na Benjamin Mkapa, mpaka ikafikia kudhibiti hali ile kwa kutumia watu wa usalama na askari wenye mbwa kuingia misikitini kusikiliza mawaidha na kukamata watu. Lowassa anataka misikiti na mashehe radical and firebrand wa enzi zile warudi kwa sababu misikiti siku hizi imekuwa baridi.

Lakini uchochezi wa kijahili na mbaya kuliko wote ambao usingeutegemea kutoka kwa Edward Lowassa ni pale aliposema WAISLAMU SASA WAANZE KUONGEA LUGHA AMBAYO SERIKALI INAIELEWA.

Lugha ya Waislamu ambayo serikali itailewa ni ipi, kujilipua? Muhimu tukumbuke hapa pakiwaka hapa sio wewe wala mimi wala Lowassa wala Magufuli wala Shehe wala Kadinari wala polisi wala majeshi yeyote atakaekuwa na hakika ya kubaki salama.

Lugha gani unapoteza muda wako bure. Tanzania ni kubwa kuliko individuals wachache wenye agenda za kutisha
 
Yaani huwa najiuliza kuna sababu gani kwenye nchi yetu kuwa na Mahakama kama zinaonekana hazitendi haki? Maana kuna ule msemo usemao " si tu haki itendeke bali pia ionekane inatendeka". Sasa watu wamo ndani bila ya dhamana na kesi haiendeshwi lakini mahakama iko kimya.

Tunajua kwamba tuna Kaimu Jaji lakini sidhani kama pia tuna Kaimu Mahakama!
Nazi ideology muone aveta yake ila poaa haki ikuje
 


Ni kweli kitendo cha kuwatia kizuizini miaka na miaka bila mashitaka mashehe wa Zanzibar wasiotaka Muungano ni kitendo cha kionevu na kifashisti. Wengine tunakubaliana kabisa na Edward Lowassa, tunakemea na kulaani kurudi kwa political prisoners ambao walishatoka magerezani toka JKN anatoka madarakani miaka ya 80.

Lakini katika kutetea mashehe hao, Lowassa amevuka mipaka kwa kiasi cha kutisha. Lowassa ameombea zirudi siku zile za taharuki za siasa za kidini zilizokuwepo enzi za Ally Hassan Mwinyi na Benjamin Mkapa, mpaka ikafikia kudhibiti hali ile kwa kutumia watu wa usalama na askari wenye mbwa kuingia misikitini kusikiliza mawaidha na kukamata watu. Lowassa anataka misikiti na mashehe radical and firebrand wa enzi zile warudi kwa sababu misikiti siku hizi imekuwa baridi.

Lakini uchochezi wa kijahili na mbaya kuliko wote ambao usingeutegemea kutoka kwa Edward Lowassa ni pale aliposema WAISLAMU SASA WAANZE KUONGEA LUGHA AMBAYO SERIKALI INAIELEWA.

Lugha ya Waislamu ambayo serikali itailewa ni ipi, kujilipua? Muhimu tukumbuke hapa pakiwaka hapa sio wewe wala mimi wala Lowassa wala Magufuli wala Shehe wala Kadinari wala polisi wala majeshi yeyote atakaekuwa na hakika ya kubaki salama.

Lowasa hajaitwa kwa DCI kwajili ya mashekh
Wqngapi wqmetamka Maneno yaashekh wacjiwe huru Na hawajafikishwa hata mahakamani wala police ije kuwa lowasa
Lowasa kahojia kuhusu rechmond sio lingine
 
Hivi kweli kuna gt humu jamvini au kumejaa wanaitikadi wa ccm na wachochezi? Nawashangaeni sana the way mnavyofanya analysis ya kauli za mtu ambaye kazungumza bila uwepo wako ili uweze kufanya vivid comparison kati ya maneno yatokayo na body language yake.
Eti ni maneno ya kichochezi kivipi wakati hakukuwepo mtaalamu wa psychology kubaini moody na feelings za mzungumzaji kama zililandana na maneno ualiyokuwa yanamtoka kinywani pamoja na mkazo wa sauti yake?
Kama haya na mengineyo hayakuwepo hukumu juu yake mnaitoa wapi?
Na mbona mnatilia maneno ya kichochezi kinywani mwake?
Kusema kuwa tuzungumze lugha iyakayoeleweka sioni kama aliashiria uvunjifu wa amani bali uki-perceive kitiikadi utajipeleka huko jasa ukiwa mwinda cheo au kazi kutoka kwa unaojipendekeza!
Kuweni na hekima na walinzi wa amani, umoja na mshikamano wa kitaifa tuliokuwa nao, tuache kuleta na kuaanikiza mifarakano iliyojaa maslahi ya kisiasa.
Mbona sioni mkihangaika na kuinua uchumi wa taifa letu? Au mmeishatajirika?
 
Binafsi sikutegemea mtu aliyefunzwa siasa na CCM ile ya Mwalimu asimame hadharani kuongea maneno yale ...hii ni ya kukemewa na kila mtu bila unafiki ....Lowasa angeacha akina Mwita waseme hayo ....si yeye ....kama Lowasa anaweza kuongea hayo inabidi tuwahoji CCM wamepanda nini kichwani mwa watawala wetu ambacho kina faida kwa Taifa ....tulifikiri CCM imezaa mafisadi tu ....kumbe ni zaidi ya mafisadi ....JPM anayo kazi kubwa sana kama kweli dhamira yake ni ya dhati ....
Kumbe mafunzo ya ccm ya Mwalimu Nyerere yalikuwa kushabikia Masheikh kuweka gerezani miaka minne bila kuhukumiwa na mahakama? Je hilo linaweza kufanyika kwa Cadinali Pengo au Askofu Kilaini? Kama tutaendelea kushabikia injustices hatutaiponya hii nchi
 
Mbona Lukuvi aliposema haya hamkupiga kelele, mungano huu uko kwa faida ya Tanganyika sio ya wazanzibari,huu ndio uchochezi wa kidini kumbuka haya maneno ameongea kanisani

 
Kuna mambo yanaleta ukakasi.

Mashehe wa Zanzibar walikamatwa wakati wa Rais Kikwete, Lowassa hakusema chochote, na kipindi hicho Tanzania haikuwa na tatizo la Kibiti. Watu zaidi ya 30 wameuwawa katika mazingira ya kutatanisha, halafu anaibuka Lowassa ambaye amewahi kuwa Waziri Mkuu anawakusanya Waislam nyumbani kwake na kuwaambia "WAISLAMU SASA WAANZE KUONGEA LUGHA AMBAYO SERIKALI INAIELEWA". Lowassa anakwenda mbele zaidi na kuwakumbusha namna 'watu walivyotumia dini kuleta machafuko wakati wa Rais Mwinyi.

Maswali ya kujiuliza,

1. Mbali na maagizo aliyotoa hadharani, Lowassa amekuwa anafanya nini nyuma ya pazia?
2. Lowassa anajua nini kuhusu Kibiti?
3. Lowassa ana maana gani anapoagiza waislam waongee 'lugha ambayo serikali inaielewa? Hiyo lugha ikoje?
4. Ni kwanini ametolea mfano wa mchafuko ya kidini wakati wa Mzee Mwinyi?
5. 'Shehe' ambaye amekuwa anafuatana na Lowassa kila mahali (hata leo alikuwa naye) ni kwa ajili ya maombi au ndiye msimamizi mkuu wa 'lugha' ambayo Lowassa anataka waislam waitumie.

Kuna tatizo kubwa.
Hivi tatizo ni Lowasa kuwaambia Waislamu 'kuanza kuongea lugha ambayo serikali inaielewa' ndio mnaanza kujaribu kumhusisha na kushindwa kwa polisi na vyombo vya usalama kutegua kitendawili cha Kibiti? Hebu msidhalilishe vyombo vyetu vya ulinzi na usalama, tunaviamini sana!
 
Lowasa hajaitwa kwa DCI kwajili ya mashekh
Wqngapi wqmetamka Maneno yaashekh wacjiwe huru Na hawajafikishwa hata mahakamani wala police ije kuwa lowasa
Lowasa kahojia kuhusu rechmond sio lingine
Hata MEMKWA umeshindwa kujiunga?
 
Kaongea mambo mengi, ni lipi hasa unaona kaongea na kusababisha kukamatwa kwake?
Wewe kule jela umewaona waislam tu ndio wa kuwasemea. Wengine ambao wana matatizo yanayofanana na sio waislam watasemewa na nani unadhani. Ni uhuni tu wa kisiasa hapa. Serikali ichukue hatua hatuwez kubali matamshi ya kipumbaf ambayo yanaweza letea taifa letu machafuko ambayo hayatakuwa na mwisho. Hakuna atakayepona katika issue hii nawaambia
 
I wish wadeal na huyo mchochezi extensively..Nilikuwa najiuliza kibaya gani alichofanya mpaka aitwe kuhojiwa??..Now I see..huwezi kuwaambia waislamu wamekuwa baridi ..na wazungumze lugha ambayo serikali wataielewa na huku wote tukiwa na historia ya matukio ya kidini hapa nchini..
 
Kwa maneno yale watamsumbua tu ila hakuna kesi. ''Waislamu mmekuwa baridi na ongeeni lugha watakayoielewa'' could have 100 meanings na sio lazima yamaanishe kile kamanda Sirro anachokifikiria. Ukisikiliza maneno ya Lowasaa na Lukuvi, unaona kabisa Lukuvi alikuwa direct sana na maneno yake ni ya kichochezi
 
Lowasa hajaitwa kwa DCI kwajili ya mashekh
Wqngapi wqmetamka Maneno yaashekh wacjiwe huru Na hawajafikishwa hata mahakamani wala police ije kuwa lowasa
Lowasa kahojia kuhusu rechmond sio lingine

Lawyer wake mwenyewe Kibatala ndio kasema mashitaka ni matamshi yake kuhusu mashehe aliyowaongelea kwenye futari ya Mbunge wa Ukonga.

Lowassa was booked, akasomewa miranda warning, akaandika cautioned statement, halafu akajidhamini on his own recognizance. Kosa, uchochezi. It is that simple. Hili si suala la Richmond.

Lowassa amekosea kuombea nchi irudi kwenye kipindi ambacho ma spy wa Usalama walikuwa wanashinda misikitini na maaskari wenye mbwa.
 
Natabiri Ipo siku hao mashehe wataachiwa huru.
Na vizuri zaidi ataachiwa na mh. Rais ama aliyepo au ajaye.
Pia natabiri kuwa baada ya kuachiwa CCM watatoa matamko zaidi ya 1000 ya kumuunga mkono mkono mh. Rais na maandamana na ngonjera nyingi za kumpongeza rais kwa hatua hiyo.

Ni vema tukavishauri vyombo vya sheria vikatoa haki kwa hao mashehe.

Na pia naamini kabisa kuwa hao mashehe wakitoka watakuwa wastarabu tu na pia watamuunga mkono mh. Rais kwa kufanya kazi tu.
Hakuna mtu kwa sasa mwenye muda wa kufanya uchochezi kwa kuwa kila mtu anaona juhudi za mh. Rais wa awamu ya tano.
Hata Lowasa hua anamkunali sana Magufuli.
Na nadhani alichokuwa anakisema Lowasa ni moja wapo ya kumkumbusha rais kuwa aingilie kati ili haki itolewa na wale mashehe wahukumiwe au waachiwe huru.
Ni kweli kuwa familia zao zinaumia sana.

Wote tuangalie amani ya nchi yetu lakini pia tuangalie amani na haki ya mtu mmoja mmoja.
Mtu mmoja tu,Yesu Kristo ndiye tunayeamini (sisi wakristo) kuwa alikufa kwa ajili ya dhambi za watu wengine lakini wengine kila mtu atabeba mzigo wake mwenyewe.
Mtu akikosa haki yake anaumia sana na haki za kitaifa hua haziwezi kumfaa mtu huyo. Mtu huyo anakua haoni umuhimu wowote wa haki zinazotamkwa kwa watu wengine.

Pamoja na Lowasa kuhojiwa lakini serikali na vyombo vya kutoa haki vitafakari haki za mahabusu wanaokaa gerezani bila kuhukumiwa kwa muda mrefu.

Kama mtu ni mkosaji basi ahukumiwe hata kifungo cha maisha lakini sio kukaa tu gerezani bila kuhukumiwa.
Na pia kwa mtu aliyefanya makosa chini ya sheria za Zanzibar ni vizuri akabakia kwenye magereza na mahakama za hukoa Zanzibar. Kwa nini tuumize watu wengnie wenye haki sawa na wengine kwa lengo la kufurahisha kundi la watu wachache tena watawala wenye kulipwa na kuishi maisha bora huku jamii kubwa ikiishi kwa hofu ,chuki na uhasama.
Busara itumike kwa hawa mashehe.

Ingetosha kabisa kuwafunga kifungo cha nje wakae na familia zao kwa masharti ya kutokufanya mikutano ya uchochezi badala yake wawe watoa nasaha kama mashehe wengine.


Pia wana CCM sio vyema kushabikia hao mashehe kuendelea kukaa ndani bila sababu za msingi. Siasa za Zanzibar zina mambo yake hivyo ni vizuri tukawa na siasa za kuwaweka pamoja na sio kuzidi kuwagawa Wazanzibari kila kukicha.
 
Back
Top Bottom