Video: Uchochezi wa Lowassa huu hapa

Video: Uchochezi wa Lowassa huu hapa

Kuna mambo yanaleta ukakasi.

Mashehe wa Zanzibar walikamatwa wakati wa Rais Kikwete, Lowassa hakusema chochote, na kipindi hicho Tanzania haikuwa na tatizo la Kibiti. Watu zaidi ya 30 wameuwawa katika mazingira ya kutatanisha, halafu anaibuka Lowassa ambaye amewahi kuwa Waziri Mkuu anawakusanya Waislam nyumbani kwake na kuwaambia "WAISLAMU SASA WAANZE KUONGEA LUGHA AMBAYO SERIKALI INAIELEWA". Lowassa anakwenda mbele zaidi na kuwakumbusha namna 'watu walivyotumia dini kuleta machafuko wakati wa Rais Mwinyi.

Maswali ya kujiuliza,

1. Mbali na maagizo aliyotoa hadharani, Lowassa amekuwa anafanya nini nyuma ya pazia?
2. Lowassa anajua nini kuhusu Kibiti?
3. Lowassa ana maana gani anapoagiza waislam waongee 'lugha ambayo serikali inaielewa? Hiyo lugha ikoje?
4. Ni kwanini ametolea mfano wa mchafuko ya kidini wakati wa Mzee Mwinyi?
5. 'Shehe' ambaye amekuwa anafuatana na Lowassa kila mahali (hata leo alikuwa naye) ni kwa ajili ya maombi au ndiye msimamizi mkuu wa 'lugha' ambayo Lowassa anataka waislam waitumie.

Kuna tatizo kubwa.
Sasa unapouliza hayo maswali nani ayajibu?
 
sioni tofaut kat ya BAKWATA na UVCCM,...nilitegemea BAKWATA wawasaidie mashekhe hawa lakini wameziba masikio
 
Masheikh wameonewa. Detention without trial. Upuuzi hadi lini?
 
Mtaenda kuthibitisha mahakama pasi na shaka kama kuwa moto ni kutaka waislamu wajilipue au!
Binafsi silioni kosa la lowasa
 
Maneno "waombe waachiwe" yanapunguza uchochezi.
Hapo anaonesha kuwa mamlaka ya kuwatoa kifungoni ipo kwa Rais na aombwe kufanya hivyo.
 
Acha uzwazwa kijana...unamtia maneno lowasa..kwani akisema waongee lugha ambayo serikali itawasikia kawaambia wavunje sheria???
 
Niwape Ushauri wa bure watumiaji Mitandao swala lolote linaloonekana linashughulikiwa na Vyombo vya Ulinzi na Usalama kwa nini lisababishe malumbano kwenu watumiaji wa Mitandao sioni maana ya kulumbana na kutukanana au kutumia lugha mbaya hata ni tofauti za fikira na mlengo wa kivyama vya Siasa tujifunze kutoa mda Wetu kwa kufikiria uzalendo upendo na Amani kwa mama Tanzania yetu na tusiingilie Mambo yaliokatika mahojiano au yanayo chunguzwa kisheria Maadam mkilumbana au mkikaa kimya hukuwezi kuleta ufumbuzi wa jambo husika ukipenda dharau Ushauri huu au uufanyie Kazi ila ukiguswa tusijibizane kwa jaziba
 
  • Thanks
Reactions: Oxx
mimi ni muislam na nina watu karibu ishirini ninaowafahamu wanaoshikiliwa kwa kuchochea uga?idi na kama kuna kitu ambacho seri,, kali ya jk ilifanya cha maana ni kuwatia kizuiz?ini hawa watu make nashindwa kupata picha devastation ambayo wangeshaisababisha kama wangekua uraiani.. alichoongea lowassa sio cha kuungwa mkono na mtu yeyote responsible
 
Ya kujilipua ni mawazo yako. Lugha inaweza kuwa ya kwenda UN, AU kutoa malalamiko. Mahakamani kudai wafikishwa mahakamani/ kesi ifutwe etc! Kwa nini mnakimbilia kwenye upuuzi wa kujilipua. Unadhani Lowasa anaweza kuwa na mawazo ya kujilipua?
Lowassa kasema kila mtu atafsiri vile anavyoweza kutafsiri. Kwa lugha nyepesi ametoa kauli tata. Kiongozi mkubwa kama yeye anapotoa kauli tata maanake mara zote huwa zinalenga uvunjifu wa Amani
 
Ni kweli kitendo cha kuwatia kizuizini miaka na miaka bila mashitaka mashehe wa Zanzibar wasiotaka Muungano ni kitendo cha kionevu na kifashisti. Wengine tunakubaliana kabisa na Edward Lowassa, tunakemea na kulaani kurudi kwa political prisoners ambao walishatoka magerezani toka JKN anatoka madarakani miaka ya 80.

Lakini katika kutetea mashehe hao, Lowassa amevuka mipaka kwa kiasi cha kutisha. Lowassa ameombea zirudi siku zile za taharuki za siasa za kidini zilizokuwepo enzi za Ally Hassan Mwinyi na Benjamin Mkapa, mpaka ikafikia kudhibiti hali ile kwa kutumia watu wa usalama na askari wenye mbwa kuingia misikitini kusikiliza mawaidha na kukamata watu. Lowassa anataka misikiti na mashehe radical and firebrand wa enzi zile warudi kwa sababu misikiti siku hizi imekuwa baridi.

Lakini uchochezi wa kijahili na mbaya kuliko wote ambao usingeutegemea kutoka kwa Edward Lowassa ni pale aliposema WAISLAMU SASA WAANZE KUONGEA LUGHA AMBAYO SERIKALI INAIELEWA.

Lugha ya Waislamu ambayo serikali itailewa ni ipi, kujilipua? Muhimu tukumbuke hapa pakiwaka hapa sio wewe wala mimi wala Lowassa wala Magufuli wala Shehe wala Kadinari wala polisi wala majeshi yeyote atakaekuwa na hakika ya kubaki salama.

TANZABASHITE wewe mnapenda kufikiria uchafu kwa kuwa mmezoea kuonea....sasa mnaogopa maneno mkianza kupigwa risasi km kibiti mtasema mmeshindwa
 
Lowassa kasema kila mtu atafsiri vile anavyoweza kutafsiri. Kwa lugha nyepesi ametoa kauli tata. Kiongozi mkubwa kama yeye anapotoa kauli tata maanake mara zote huwa zinalenga uvunjifu wa Amani

Hakuna utata.

Amesema mbona Waislam siku hizi mmelegea?

Zimeenda wapi zile tashtishi za marehemu Shekhe Kassim bin Jumaa? Sasa ni wangapi hapa wanakumbuka siku zile za Shekhe Kassim?

Hayo maneno hayana ambiguity, yako wazi kabisa, anawachochea Waislamu wadai lolote kwa njia zozote.

Lowassa analindwa na Usalama wa Taifa, hawezi kuja mtaani zikianza mshike-mshike za raia na polisi. Na akija kwenye street violence, vyombo vya dola haviwezi kum target kwa sababu watakwaana na walinzi wa Lowassa ambao ni maafisa wa ofisi ya Rais, Usalama. Sasa kwa nini udanganye wenzio wakavunjwe miguu, wapigwe risasi wakati wewe uko Oysterbay unasubiri kuangalia matokeo kwenye BBC Swahili? Ni makosa makubwa kwa mtu mwenye caliber ya Edward Lowassa kutamka uchochezi ule wa kidini.
 
Ni kweli kitendo cha kuwatia kizuizini miaka na miaka bila mashitaka mashehe wa Zanzibar wasiotaka Muungano ni kitendo cha kionevu na kifashisti. Wengine tunakubaliana kabisa na Edward Lowassa, tunakemea na kulaani kurudi kwa political prisoners ambao walishatoka magerezani toka JKN anatoka madarakani miaka ya 80.

Lakini katika kutetea mashehe hao, Lowassa amevuka mipaka kwa kiasi cha kutisha. Lowassa ameombea zirudi siku zile za taharuki za siasa za kidini zilizokuwepo enzi za Ally Hassan Mwinyi na Benjamin Mkapa, mpaka ikafikia kudhibiti hali ile kwa kutumia watu wa usalama na askari wenye mbwa kuingia misikitini kusikiliza mawaidha na kukamata watu. Lowassa anataka misikiti na mashehe radical and firebrand wa enzi zile warudi kwa sababu misikiti siku hizi imekuwa baridi.

Lakini uchochezi wa kijahili na mbaya kuliko wote ambao usingeutegemea kutoka kwa Edward Lowassa ni pale aliposema WAISLAMU SASA WAANZE KUONGEA LUGHA AMBAYO SERIKALI INAIELEWA.

Lugha ya Waislamu ambayo serikali itailewa ni ipi, kujilipua? Muhimu tukumbuke hapa pakiwaka hapa sio wewe wala mimi wala Lowassa wala Magufuli wala Shehe wala Kadinari wala polisi wala majeshi yeyote atakaekuwa na hakika ya kubaki salama.

Kwa Haya yanaoendelea dhidi ya Masheikh,nitashangaa sana kama kuna muislam anayejielewa ataipa kura ccm!!!Gwajima karopoka haswa lakini hajaguswa.Wazanzibar wameshaikataa ccm siku nyingi
 
Back
Top Bottom