Video: Ubishani ni Zanzibar ni nchi au siyo? Wenzenu upande wa Zanzibar ni Wazanzibari au Watanzania? Wasira, Rais Samia vs Tundu Lissu: Nani mkweli?

P vuka maji nenda Zanzibar kayaongee haya.
Tanzania ni nchi moja ya JMT yenye sehemu mbili, Tanzania Bara na Tanzania Visiwani au Tanzania Zanzibar.

Zanzibar ina utawala wake wa ndani, hivyo ina haki ya kujiita vyovyote ndani kwake hata mimi ndani kwangu najiita rais wa taifa la PPR, najiita amiri jeshi mkuu, nimeweka picha yangu ukutani, na bendera ya PPR, nina wimbo wangu wa taifa langu, ila mwisho ni ndani ya geti langu!.

Hiyo katiba ya Zanzibar, ni ya mambo yao ya ndani, mwisho Chumbe!. Katiba ya JMT haiitambui katiba ya Zanzibar.

Japo Zanzibar sio nchi, lakini huwezi kwenda Zanzibar kusemea kule kuwa Zanzibar sio nchi kama ambavyo huwezi kuja home kwangu kuniambia mimi sio rais wa nchi ya PPR.
P
 
Sio ubatili, hakuna raia wa Zanzibar kwasababu Zanzibar sio nchi, haina raia, nchi ni Tanzania na uraia ni mmoja tuu, uraia wa Tanzania.

Ila Zanzibar ni eneo halali lenye utawala wake wa ndani na eneo hilo lina wakaazi, hivyo kile kitambulisho cha ukaazi wa Zanzibar ni kitambulisho cha ukaazi wa eneo la Zanzibar na sio kitambulisho cha uraia wa Zanzibar, hakuna raia wa Zanzibar, raia wote ni raia wa Tanzania na wana haki zote za uraia sawa sawa ikiwemo kumiliki ardhi na ajira ndani ya JMT!.
P
Nakuelewa ndugu Paschal Ila huu Muungano ni kana kwamba Tanganyika wanaulazimisha. Wazanzibari wako proud kujitambulisha kama wazanzibari. Watanganyika mna lenu jambo kwenye huu Muungano.
 
Tanzania ni nchi moja ya JMT yenye sehemu mbili, Tanzania Bara na Tanzania Visiwani au Tanzania Zanzibar.

Zanzibar ina utawala wake wa ndani, hivyo ina haki ya kujiita vyovyote!.
P
Utasemaje una Tanzania wakati huo huo unaikataa Tanganyika na unaipa uhalali Zanzibar mbona wasomi wetu nanyi ni kama sisi tu.
 
Nakuelewa ndugu Paschal Ila huu Muungano ni kana kwamba Tanganyika wanaulazimisha. Wazanzibari wako proud kujitambulisha kama wazanzibari. Watanganyika mna lenu jambo kwenye huu Muungano.
Tumependa, tumekufa, tumeoza, ndio maana tutaulinda kwa gharama yoyote.
P
 
Sasa nakuuliza kuna Siri gani Serikali ya Muungano kuzuia upinzani kushinda uchaguzi Zanzibar?
Hili nimewahi kukizungumza humu, Iwapo CCM itashindwa Zanzibar, Nini Majaaliwa ya Muungano?

Na nikashauri, Kumuepushia aibu ya Kushindwa, CCM isimsimamishe Dr. Shein CCM haikusikia!, ule uchaguzi CCM ili... Elections 2015 - Imethibitishwa pasi na shaka kuwa ni kweli kabisa, Zanzibar, Maalim Seif na CUF ndio walioshinda

Ukisikia kuulinda Muungano kwa gharama yoyote, ndiko huko!.
P
 
For sure, ila kama ni kusubiri huu Muungano wetu adhimu uvunjike..., then utasubiri sana!.
P
Hakuna aliyefikiria kuvunjika Soviet Union nchi iliyokuwa na nguvu kiuchumi na kijeshi na ilivunjika kiulaini tu ghafla. Viashiria vya kuvunjika huu uvamizi uitwao Muungano vipo kila upande , vingi tu , ni suala la muda tu, utakuja kuniambia tukiwa hai. Wåatu wamechoka nao , ni wezi wachache tu wanaotumia nguvu ndio hulazimisha kuwepo
 

Sasa huoni kuwa hapo Wazanzibari hawautaki? Ni Watanganyika ndio wanaolazimisha chini ya mwamvuli wa muungano ?
 
Watanganyika ni watu wa ajabu sana! Inakuwaje Mtanganyika unaona aibu na kuogopa kujitambulisha kwa jina la nchi yako ya asili na unabaki kung'ang'ana kujiita Mtanzania wakati mshirika mwenzako kwenye huo Muungano anajitambulisha kwa Uasili wake! Tena ajabu zaidi kuna majinga yanajiita wasomi yanajifanya majuaji sana kumbe mabichwa box.
 
Katiba ya Zanzibar ni kwa ajili ya mambo ya ndani ya Zanzibar, Katiba ya JMT haitambui katiba ya Zanzibar. Tanzania ni nchi moja ya JMT, Zanzibar sio nchi ni sehemu ya JMT. Hivyo haijalishi katiba ya Zanzibar inasema nini kuhusu Zanzibar, hayo ni mambo yao, hayatuhusu!.
P
Kaka p.
Mfano mimi kwetu nachingwea
Katiba ya Zanzibar ni kwa ajili ya mambo ya ndani ya Zanzibar, Katiba ya JMT haitambui katiba ya Zanzibar. Tanzania ni nchi moja ya JMT, Zanzibar sio nchi ni sehemu ya JMT. Hivyo haijalishi katiba ya Zanzibar inasema nini kuhusu Zanzibar, hayo ni mambo yao, hayatuhusu!.
P
Ukishasema hayo ni mambo yao,hayatuhusu!

Tayari zanzibar ina mamlaka yake ambayo hayaingiliwi na tanzania bara kwa mantiki hiyo huoni Zanzibar ni nchi?

Unsema Zanzibar si nchi ni sehemu ya JMT? sasa nini maana ya neno jamhuri ya Muungano? Muungano wa nini sasa?

Mbona unakuwa mpotoshaji namna hii mkuu?
 
Mimi nimezaliwa Tanzania, na wengi wetu tumezaliwa Tanzania, waliozaliwa Tanganyika wote by now ni wastaafu, wako over 60 years, na walipopata akili, walikuwa tayari Tanzania, ni Watanganyika gani hao wa kuililia Tanganyika na kujivunia Tanganyika?.

Muungano ni kama ndoa, Zanzibar ni kama mwenza, sasa wewe kama mwenza wako anajipodoa, na wewe utataka kujipodoa ili mlingane?. Hebu acheni hizi kitu!.
P
Hahahaaa...
Code nimeielewa japo umejificha ili chachu yako isije kuharibika kupitia chachu za wengine itunzwe hivyo!.

Ila ukweli mbunge yule kashusha komwe lililokuwa linamsumbua na meseji deliver ila wabunge wa Tanganyika wangetumia hii (ile) fulsa kidogo tungepata kitu ila hofu ndiyo iliwajaa.

Mke mrembo akikuona umezeeka na kutaka kuondoka usimlazimishe abaki kwako kamarada anaweza kukuua, muache aende!.
 
Wale wabunge wa G55 walikuwa sahihi sana hata hivyo bado hatujachelewa kurudisha serikali yetu ya Tanganyika hizi blah blah za haya majinga yanayotoa mifano sijui ya mke na mume hayatusaidii chochote kwa sababu kati ya nchi na nchi hakuna mume wala mke kwahiyo sio sahihi kutoa mfano wa mume na mke kwenye muungano na kuendelea kutoa mifano kama hiyo ni udhalilishaji tu.
 
View attachment 2991056
Ndugu wana JF - Jukwaa la Siasa;

Mjadala wa muungano tata wa Tanganyika na Zanzibar (1964) unaendelea tena leo....

Na kwa kweli mjadala huu haupaswi kuishia njiani isipokuwa tu wote tumeelewana na kukubali kuwa lipo tatizo ktk muungano huu linalostahili kutatuliwa sasa na sio kesho kama tunataka kuendelea nao...

Leo katika video hiyo☝🏻☝🏻 ni makala ya uchambuzi toka kwa mchambuzi nguli wa maswala ya kisiasa, kijamii na kiuchumi ndugu Ansbert Ngurumo kupitia YouTube channel yake [SK Media Online TV] anayeishi uhamishoni Uingereza

Katika uchambuzi huu, Ansbert Ngurumo anazimulika kauli za watu watatu juu muungano wa Tanganyika na Zanzibar (1964) ambao ni;

1. Mzee Steven Wassira a.k.a Tyson (CCM)
2. Rais Samia Suluhu Hassan (CCM)

3. Tundu Antipasy Lissu (CHADEMA)

Hawa wote wanajibu maswali mawili muhimu yafuatayo ambayo ndiyo msingi mkuu wa ubishani unaoendelea sasa ktk muungano huu;

1. KWAMBA, Zanzibar ni nchi au sio nchi?

2. KWAMBA, Watu au wananchi wa nchi ya Zanzibar ni Watanzania au Wazanzibari?

Nani mkweli kati ya hawa watu watatu kuhusu muungano wetu? Nini maoni yako? Tatizo liko wapi? Ni kitu gani kinafichwa kupitia muungano huu?

Tazama na sikiliza video hiyo ya dakika 14 tu hadi mwisho kisha tumia akili yako kupima mwenyewe halafu sema kitu.

Na bila shaka kasi ya internet imeboreka kiasi chake na hivyo kila mtu ataifungua video hii bila kuhangaika sana..
==========================================
Ile nyara toka hifadhi ya Gombe imechanganyikiwa kabisa
 
.
.
Mkuu zanzibar Ni nchi kulingana na Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984

Hata hivyo kwa Mujibu Wa Katiba ya zanzibar

HUWEZI kwenda kwenye shauri la mgogoro wa kiwanja umebeba vielelezo ulivyoviandika mwenyewe nyumbani kwako! Havina nguvu.

Katiba ya Zanzibar walijiandikia wenyewe 1984, miaka 20 baada ya Muungano.

Katiba ya Zanzibar haiwezi kutumika ku define U-taifa na U-nchi wao wenyewe bila kujali Katiba inasema nini.
 
.
.


HUWEZI kwenda kwenye shauri la mgogoro wa kiwanja umebeba vielelezo ulivyoviandika mwenyewe nyumbani kwako! Havina nguvu.

Katiba ya Zanzibar walijiandikia wenyewe 1984, miaka 20 baada ya Muungano.

Katiba ya Zanzibar haiwezi kutumika ku define U-taifa na U-nchi wao wenyewe bila kujali Katiba inasema nini.
Walijiandikia kwa Nguvu ya Nani??
Unajua maana ya Katiba??
Vipi kuhsu sheria ya Uzanzibari ya mwaka 1985??

Je unafahamu CCM imezaliwa baada ya Kuungana kwa ASP (Zanzibar) na TANU (Tanganyika) mwaka 1977?

Katiba ya Tanganyika ndo ilibadilishwa na kuwa katiba ya Muungano..

Je Umesoma Decree 3 za Muungano wa Tanganyika na zanzibar??
Unakumbuka katiba ya Muungano wa Tanganyika na zanzibar Ya mwaka 1964 (ambayo ndo updated version yake ni ya 1977) ilitoka kwenye katiba gani??
 
Hata kama wazanzibari hawaukubali ?? Performance ipi ya kuwauwa wazanzibari kila uchaguzi ili kuweka vibaraka vya Tanganyika ??

..sisi tunadai Tanganyika ili watoto / vijana wetu wasitumwe Zanzibar kufanya mauaji kila kunapofanyika uchaguzi.

..Wazanzibar wanaotaka kuingia madarakani kwa kupora na kuua wafanye hivyo wenyewe na sio kutumikisha vijana wa Kitanganyika.
 
Back
Top Bottom