Uzima Tele
JF-Expert Member
- Jan 20, 2023
- 1,198
- 2,618
Ndugu wana JF - Jukwaa la Siasa;
Mjadala wa muungano tata wa Tanganyika na Zanzibar (1964) unaendelea tena leo....
Na kwa kweli mjadala huu haupaswi kuishia njiani isipokuwa tu wote tumeelewana na kukubali kuwa lipo tatizo ktk muungano huu linalostahili kutatuliwa sasa na sio kesho kama tunataka kuendelea nao...
Leo katika video hiyo☝🏻☝🏻 ni makala ya uchambuzi toka kwa mchambuzi nguli wa maswala ya kisiasa, kijamii na kiuchumi ndugu Ansbert Ngurumo kupitia YouTube channel yake [SK Media Online TV] anayeishi uhamishoni Uingereza
Katika uchambuzi huu, Ansbert Ngurumo anazimulika kauli za watu watatu juu muungano wa Tanganyika na Zanzibar (1964) ambao ni;
1. Mzee Steven Wassira a.k.a Tyson (CCM)
2. Rais Samia Suluhu Hassan (CCM)
3. Tundu Antipasy Lissu (CHADEMA)
Hawa wote wanajibu maswali mawili muhimu yafuatayo ambayo ndiyo msingi mkuu wa ubishani unaoendelea sasa ktk muungano huu;
1. KWAMBA, Zanzibar ni nchi au sio nchi?
2. KWAMBA, Watu au wananchi wa nchi ya Zanzibar ni Watanzania au Wazanzibari?
Nani mkweli kati ya hawa watu watatu kuhusu muungano wetu? Nini maoni yako? Tatizo liko wapi? Ni kitu gani kinafichwa kupitia muungano huu?
Tazama na sikiliza video hiyo ya dakika 14 tu hadi mwisho kisha tumia akili yako kupima mwenyewe halafu sema kitu.
Na bila shaka kasi ya internet imeboreka kiasi chake na hivyo kila mtu ataifungua video hii bila kuhangaika sana..
==========================================