Intelligence Justice
JF-Expert Member
- Oct 23, 2020
- 3,105
- 3,556
Aliyebuni jina sio Julius Kambarage Burito Nyerere au Abeid Aman Karume bali ni huyu hapa chini:Kwa hiyo shida ya "kutojitambua" iko upande wetu wa pili yaani Tanganyika..
Tanganyika na Watanganyika wako wapi?
Jina halisi la nchi hii kumbe linapaswa kuwa ni
"Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar"
na siyo
"Jamhuri ya Muungano wa Tanzania"
Hili jina la "Tanzania" ilitoka wapi? Shida iko kweye jina hili. Uchawi uko humu ndani ya jina hili. Inawezekana vipi kiongozi mmoja anayeitwa "Julius Kambarage Nyerere" abadili jina la nchi na uraia wetu bila ya ridhaa ya wananchi wenyewe??
Huu ni wakati wa kuhoji maamuzi ya huyu aitwaye baba wa taifa hili Mwl Julius K. Nyerere..
Kuna maamuzi yake mengine mengi yalikuwa very fatal na ya hovyo sana na yanahitaji kurekebishwa sasa au kuachana nayo kabisa maana ni mitego ya mauti na kikwazo cha ustawi wetu kama taifa na nchi..
Jina la Tanzania lilibuniwa na mmoja wa wananchi walioshiriki mchakato wa kutafuta jina la nchi hii, baadaya muungano wa Tanganyika na Zanzibar mwaka 1964.Mohammed Iqbal Dar ndiye aliyebuni jina la Tanzania, wakati huo akiwa na umri wa miaka 18 akiwa mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Mzumbe.Mwandishi huyo baada ya kuonana na Mohammed Iqbal Dar akamuuliza:MWANDISHI: Uliingiaje katika shindano la kubuni jina la nchi?IQBAR DAR: Siku moja nilikuwa maktaba nikijisoma Gazeti la Tanganyika Standard ambalo siku hizi linaitwa Daily News, mikaona tangazo lililosema: "Muungano wa Tanganyika na Zanzibar unafahamika kama Republic of Tanganyika and Zanzibar jina likaonekana refu sana. Kwa hiyo wananchi wote mnaombwa kushiriki kwenye shindano la kupendekeza jina moja litakalozitaja nchi zote mbili yaani Tanganyika na Zanzibar."
IQBAR DAR: Nilichukua karatasi nikaandika kwanza Bismillah Raahman Rahimu hii ni kutokana na imani ya dini yangu. Baada ya hapo nikaandika jina la Tanganyika kisha nikaandika Zanzibar halafu nikaandika jina langu la Iqbal halafu nikaandika jina la Jumuiya yangu ya kidini ya Ahmadiya. Baada ya hapo nikamrudia tena MwenyeziMungu, nikamuomba anisaidie ili nipate jina zuri kutoka katika majina hayo niliyokuwa nimeandika. Baada ya hapo nilichukua herufi tatu kutoka jina la nchi ya Tanganyika yaani TAN na kwa upande wa Zanzibar nikachukua herufi tatu za mwanzo ZAN, kisha anikaunganisha nikapata jina TANZAN.
IQBAR DAR: Kabla ya kulipeleka kunakohusika serikalini nilifanya utafiti mdogo na kugundua kuwa nchi nyingi za Afrika majina yao yanaishIA na IA kwa mfano EthiopIA, ZambIA, NigerIA, TunisIA, SomalIA, GambIA, NamibIA, LiberIA, MauritanIA.
Baada ya utafiti huo nikapendekeza na kuamua kwamba jina TANZANIA ndilo litumike kuwakilisha nchi hizi mbili yaani Tanganyika na Zanzibar. Kwa maana hiyo jina TANZANIA limezaliwa kutoka katika majina manne ambayo ni Tanganyika, Zanzibar, Iqbal na Ahmadiyya.
TAN-Tanganyika
ZAN-Zanzibar
IA-IQBAR AHMADIYYA
TAN-ZAN-IA