Video: Si kuibiwa ni kuzidiwa!

Video: Si kuibiwa ni kuzidiwa!

Status
Not open for further replies.
Wakuu naona kwenye huu mjadala kuna assumptions nyingi ambazo hatuna uhakika nazo na hata mshitaki hana uhakika na madai yake.

Kwanza, Dr. Slaa alimtambulisha huyo mama kama mchumba na siyo mke. Inawezekana wanasubiri huyo mama akamilishe formalities za official divorce ndipo wafunge ndoa.

Pili, nimeona kuna watu wanasema Josephine na Dr. Slaa wamekaa kinyumba, lakini hakuna ambaye ana uhakika na hilo. Ukisoma maelezo ya mume wa Josephine, hata yeye hajui mkewe alikuwa anaishi wapi au sasa hivi mkewe na watoto wanaishi wapi. Ni wapi ambako Dr. Slaa ameishi kinyumba na huyo mama? Hakuna mwenye uhakika au ambaye anajua.

Kutongoza mwanamke ambaye ametengana (separate) na mumewe hakuna kosa, kosa ni kufunga ndoa na mke wa mtu. Tukisema tuingie kwenye mila, huko ndio tunapotea zaidi kwa kuwa hakuna mila inakubaliana na ujinga wa mwanamke kuwa separate na mumewe for more than 6 months halafu bado ahesabike kwamba ni mke.

Cha msingi tusubiri kesi iungurume mahakamani na hukumu itolewe, hapo ndipo tutajua mbivu na mbichi ziko wapi. Alternatively, tusubiri maelezo ya upande wa pili, ambayo kwa sasa hatuwezi kuyapata kwa kuwa aliyekuwa mume wa Josephine kapeleka kesi mahakamani.

Ukiangalia kwa undani sana, sioni kosa la Dr. Slaa iwe ni kimaadili au hata mbele ya sheria, unless kuwe na proof kwamba Slaa kalipa mahari (kafunga ndoa ya kimila), au amekaa kinyumba na huyo mama for atleast 6 months ndani ya nyumba moja au amefunga ndoa kanisani au ofisi ya DC/RC, of which hayo yote hakuna anayejua. Slaa mwenyewe alisema Josephine ni "mchumba".

Pia kuna lugha za kiutu uzima jamani, Mzee Slaa hawezi kusema huyu mama ni mpenzi wangu, lakini kiukweli wanaweza kuwa ni wapenzi na wako kwenye process ya divorce kabla ya kufunga ndoa official..
 
Kiranga,
Wewe ngojea tu!! Walioanzinsha hii vita ya unyumba ni CCM (CCM Strategy); ngoja naye Dr Slaa atakuja na CHADEMA Strategy; have you red a book called ART OF WAR by Sutze?? that is what is going on here; ART of WAR, that is what DR. Slaa is doing all the time! If you are reading well, between the lines you will find that Dr Slaa is a very informed and stragegist; a man who knows the ART of War; what he lacks is; the support of dumb people like you!! WE need to seize time; this is the only time we have!! Look at the big picture first, ECONOMY is our priority!
 
Hivi we Mwanakijiji ni mzee kweli?? hebu tuwekee lirics kwanza ndo tujadili mengine...
 
Hahahahaha................hahahah................
Tanzania bana,
Hi ni sawa na ile hadithi ya Mzungu anakuna kichwa kufikiria jinsi gani atapata mlo wa siki,Lakini mwafrika anakuna sehemu zake za siri kufikiria ni saa ngapi atapata kiburudisho.lol....
Yes,This is Tanzania bana,no probe,anything is possible,behind the scene somebody is taking care,we know what is going on,this is just the start,the end is too far,but the decision is 31 octoba.
Keep in mind,new era is just at the corner,

 
Soma nyongeza niliyoweka kwenye posti ya mwanzo chini kuhusu Sheria ya ndoa inachosema hasa maana naona watu wanazungumza tu kwa kukisia.
 
jamaa anayumiwa na ccm. deep down ndani ya moyo wake anajua kuwa almuacha.

alitegema huyo mama anyanyasike na awe na maisha magumu
imekuwa kinyume chake sasa jamaa anadai hajampa talaka
 
Mimi si support Kiwete au Siraha, wote ni miyeyusho tu kwangu. Especially kwa sababu Siraha kashapewa nafasi na kajionyesha kumbe mtu wa kujali bupe kuliko public service.

Ataweza kazi kweli huyu? Whats the point of taking the change of doing a whole regime change only to replace one fisadi with another ?

Hahahaaaa!!! Karanga = MS = Mugongo Mugongo = Mchambuzi = Fikiri.... You guys you are the same people busy defending your Master's interests. Manafikiri Wadanganyika bado tumelala??? Mwaka huu mpaka kieleweke hata kama mtaleta rafu kama za Kagame kule Rwanda. Tell them (Your Masters) we are not the same peple anymore!!!!
 
Ndoa ya Slaa ndiyo imeleta matatizo ya wa TZ kama kudorora kwa uchumi wetu,wachache kugawana mali asili zetu,ukosefu wa huduma za msingi za jamii,kukithiri kwa rushwa na mengineyo mengi yanayofanya"life expetency"ya MTZ izidi kushuka siku hadi siku?
Yaani tunasahau kuwa uadilifu unaanzia katika maisha binafsi???!!!!!!!. Labda kama tumeamua kukubali kuwa jamii yetu imeoza kiasi kwamba kiwango chetu cha uadilifu sasa kimeshuka kiasi kwamba mtu anayezini na mke wa mtu mwingine bado tunaweza kumuhesabu ni muadilifu anayefaa kuliongoza taifa hili. Hebu angalia hapo kwa waingereza tu John Terry alizini na mwanamke aliyeachika lakini ilikuwa ni kimbembe kiasi cha kuvuliwa unahodha.....Sisi leo hii tunataka kuhalalisha kuwa na marais wazinzi!!!!! Na hapa nina maana yeyote yule awe ni Slaa au Kikwete kama ni wazinzi hawatufai hata kidogo.
 
Kama tunaangalia swala la ndoa, mimi ni bora nimchague mtu ambaye hajaoa (na hakai kunyumba na mke wa mtu) kuwa rais kuliko kumchagua mtu anayekaa na mke wa mtu kindoa, bila mke huyo wa mtu kupata talaka rasmi.
Kiranga naamini by now ulisha make up your mind utamchagua nani.

Wale ambao walishaamua kama wewe, kuwa chaguo lao ni Dr.Slaa, siamini kama watabadilisha msimamo wao kwa sababu kama uliyoitoa wewe.

Uzuri wa demokrasia, ni uhuru wa kuchagua, endelea na kule ulikoamua kupeleka kura yako, ila pia usiutumie ushawishi wako, kujaribu kupunguza kura za Dr. Slaa kwa hizi siasa za maji taka, maana lazima tukubali, bado kuna wengi wetu, hawajaamua na hawajakata shauri, wao sio moto (Dr. Slaa na sio baridi (CCM), ila moto unawaka na unachoma na kuendelea kuunguza kwa kasi, na sasa wanajaribu kuuzima kwa maji taka, ambayo mengine yake yana gesi, hivyo kujikuta, badala ya kuuzima, ndio kwanza wanazidi kuuchochea!.

The wind if Change is sweeping accross!.
 
OK, hii kesi ni ya kisiasa zaidi na pengine vitu kama hivi sijui kwa nini CCM wanaving'ang'ania. Ila Dr. Slaa na huyo Josephine wakikaa kimya, na ofcourse wameshafunguliwa kesi hawatakiwi kuyazungumzia mambo haya wazi wazi. Lakini CCM hawataweza kuvizuia vyombo vyao vya habari kuendelea kuifanya kesi hii kuwa big issue. Lakini katika court of public opinion, Slaa will emerge a winner. Absolutely, nadhani PR machinery ya CCM wanatakiwa hili waliangalie sana ni mojawapo ya vitu vitakavyomfanya Slaa aibuke kidedea kwa kumfanya aonekana victim wa circumstance.

Slaa katangaza uchumba, hata kanisani au kwa mkuu wa wilaya, ukitaka kufunga ndoa na mtu unatoa tangazo. Lengo la Tangazo ni kuwa kama kuna matatizo wenye matatizo na ndoa hiyo wajitokeze. Slaa katangaza uchumba na mwanamke hadharani (anaweza sema alikuwa hajui kama huyu mke wa mtu kwa sababu alimkuta huru ndo maana katangaza hadharani). Then wewe badala ya kutoa pingamizi, unakuja na mashtaka mahakamani, tena mashtaka yanayoonesha kuwa interrest yako si ndoa bali fidia tu ... au mashtaka yenyewe. Hii inathibitisha kuwa haya mashtaka ni ya kutunga na timing yenyewe inawafanya watu wa kawaida waone kama Slaa anaonewa.

Hili ndo PR strategist wa CCM inatakiwa walione. Reaction ya wanawake wengi (majority ya wapiga kura) ni tofauti sana na strategist wa CCM (ambao ni wanaume) wanavyofikiria. CCM has far more options to attack Slaa and Chadema badala ya kung'ang'ania suala hili. Je CCM majibu waliyo nayo kuhusu rundo la tuhuma za ufisadi ni hili la ndoa ya slaa pekee?? Doom!!
 
CCM watakuwa wanafanya kosa sana kufikiri watanzania ni wazungu. Haya mambo ya kumchokoa mtu kwenye privacy yake huwa yanashindwa siku zote hapa Afrika. Privacy tena inayomfanya Slaa kuonekana mwanaume 'macho' si suala litakalombomoa hapa Tanzania na si katika nchi yoyote Afrika. Si kwamba waafrika ni tofauti na watu wengine, ila ushahidi unaonesha kuwa hila hizi Afrika huwa hazifanikiwi.

Hata kama Slaa kura zake hazitatosha, nina uhakika hii kampeni ya ndoa yake itamuongezea kura badala ya kumpunguzia. Tamaduni ni kitu cha ajabu sana, ila hili liko wazi na wanawake wa Tanzania wengi wanamuona Slaa kama shujaa hata kabla ya kujua utetezi wa Josephine ni upi?

Mahakamani ni wazi huyo mme hawezi kushinda. Hata kama atashinda mahakamani, public opinion haiko naye!
 
Huu ushabiki unatupeleka pabaya, let's be serious!!

Tatizo kubwa lililoifikisha nchi hii hapa ilipo ni kulindana na kuwaabudu viongozi ata pale ambapo makosa yao yapo dhahiri.

Nasikitika kuwa katika karne ya 21 bado watanzania wanaelekea kwenye njia hiyo ya ujima.

Hivi sakata la Karamagi kupoka mke wa mtu lliliishia wapi??? Mwenye mke alienda mahakamani??
 
unapinga wenzako kuwa wanajichanganya na kisha unakuja na maswali kibao ambayo unataka majibu toka kwa wataalamu wa sheria. Kwa nini usipate majibu ya maswali hayo kabla ya kuja kuonesha utupu wako hapa?

Wewe ndio mtupu kwa kujifanya kila kitu unajua...Ushauri: mtazamo wako ni mdogo, unaishia kwenye kupigia debe Chadema kwa hiyo huwezi kuona beyond that kama wazako wanaopigia debe CCM blindly...Maswali uleta changamoto, usijifanye wewe ni mtaalamu wa magonjwa ya moyo wakati wewe ni karani
 
hapo ndipo nasema huyu jamaa angemshtaki Josephine halafu tungeona yaliyofichika. Huyu jamaa anajua fika kwamba Kumshtaki Josephine haiwezekani kwa sababu target yao ni Dr. Slaa ili kuonyesha bibie ni victim of circumstance.. alihadaika na Dr - unakumbuka jamaa kasema mwanamke alisema anaondoka ktk kibanda chake anakwenda kuishi ktk nyumba!!?.. hii yote picha imechorwa tayari.... isitokee tu huyu bibie naye akubali kwamba Dr. Slaa alimhadaa hadi kufikia kufanya maamuzi kinyume cha ndoa yake. hapo mkuu wangu itakuwa kibano - dr chupi itambana.

Hapa Mr. Mkandara umenichekesha sana
 
Yaani tunasahau kuwa uadilifu unaanzia katika maisha binafsi???!!!!!!!. Labda kama tumeamua kukubali kuwa jamii yetu imeoza kiasi kwamba kiwango chetu cha uadilifu sasa kimeshuka kiasi kwamba mtu anayezini na mke wa mtu mwingine bado tunaweza kumuhesabu ni muadilifu anayefaa kuliongoza taifa hili. Hebu angalia hapo kwa waingereza tu John Terry alizini na mwanamke aliyeachika lakini ilikuwa ni kimbembe kiasi cha kuvuliwa unahodha.....Sisi leo hii tunataka kuhalalisha kuwa na marais wazinzi!!!!! Na hapa nina maana yeyote yule awe ni Slaa au Kikwete kama ni wazinzi hawatufai hata kidogo.
WAKUU,
Inasikitisha, nani katika dunia hii hazini au hajawahi kuzini. jambo hili linatakiwa lifungwe, haifai kuedelezwa, kwa sababu hakuna jipya. Kinachopaswa kupangaliwa na kupewa umuhimu ni nani yuko makini na uhai na uedelevu wa nchi yetu, badala ya nani anazini au
la. This is immaterial. Let us be serious, tarehe 31 Oktoba iwe ya mafanikio.
 
Japo huwezi kuona tatizo la kulinganisha nilichosema mimi na hawa kuwa ni unnecessarily reckless utatafuta namna ya kuhalalisha kwanini unafikiria nimefanya spin.



Hapa tunatofautiana kwa sababu dhamira ya mtu ni kuu kuliko. Kama huyo mama alijijua kuwa bado ni mke wa mtu na akaamua kumuacha mume wake na akamfuata mtu ambaye naye alikubali moyo wake wewe na mimi ni nani kucondemn kitendo ambacho kimetokana na dhamira na kiko katika suala la binafsi? Hawa ni watu wazima na wamefanya maamuzi yao wao wenyewe na it is none of your business, na wala siyo ya CCM wala mtu mwingine yoyote. Mtu mwenye hoja hapo ni mume wa huyo mama na peke yake anatakiwa kucondemn au kugombania mke wake arudi (siyo arudishwe kwani hajatekwa).
Sasa kama slaa anaweza kuamua kukaa na mke wa mtu kwa sababu tu dhamira yake imemtuma hivyo huku akijua si jambo zuri kimaadili ni mangapi anaweza akafanya atakapokuwa na mamlaka ya uraisi kwa sababu tu dhamira yake itamtuma kufanya hivyo. Btw it is very business of ours kama huyu mtu anataka kuwa raisi wetu.
 
Jamani kwenye ufunguzi wa kampeni za chadema Dr Slaa alimtambulisha Joshiphine kuwa ni Mke wake hata TBC jana kwenye taarifa ya habari wameonyesha tena
 
Jamani kwenye ufunguzi wa kampeni za chadema Dr Slaa alimtambulisha Joshiphine kuwa ni Mke wake hata TBC jana kwenye taarifa ya habari wameonyesha tena

Ile habari kwenye youtube imepotea ghafla...Ni bora wangeiweka hapa watu wajionee wenyewe...
 
Ha ha ha nimependa shairi,bwana tunataka sera sio mambo ya kufuata fuata maisha ya mtu
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom