Video: Si kuibiwa ni kuzidiwa!

Video: Si kuibiwa ni kuzidiwa!

Status
Not open for further replies.
Tujaribu kujadili huu mjadala, hapa tunazungumzia swala la Slaa na mke wa mtu! Ni jambo la maadili na sheria za ndoa...

Naona umeongeza neno maadili baada ya kuona swali langu kuhusu sheria za ndoa.
Narudia swali langu kwako, sheria ya ndoa inayombana Dr Slaa hapa ni ipi?
 
Ahsante,

Mimi nawaambia wana JF hapa, kama mnasimamia priciple za kupinga uovu, basi pingeni uovu bila kujali kwamba aliyefanya ni Slaa au Kikwete, CCM au CHADEMA.

Uovu wa Slaa hapa ni upi? kwa nini usiwekwe wazi na kisha ionekane kama kuna mtu anautetea au la?

Tatizo watu wanataka kuvaa miwani ya mbao kama matatizo ni ya CHADEMA.

Kuna mkuu alitukumbusha huko juu, kipendacho roho, chongo huita kengeza. Hata Malcolm X alipokuwa katika Nation of Islam alipoanza kupata habari za ubaradhuli wa Elijah Muhammad kuwaingilia vimwana wadogo waumini wake na kuwapa mimba alitaka kumu excuse kwa kila jinsi aliyoweza, hakuweza kuamini ati. Mpaka baadaye alivyoenda Hajj na kurudi Marekani ndipo alipofunguka macho na kuona hila za Elijah Muhammad.

haihusiki kabisa

Najua baadhi yetu tuna shock kuona mtu kama Slaa ambaye tulimuwekea matumaini makubwa sana anakuja kutu dissapoint vibaya hivi.Lakini ukweli - so far- unaonekana kwamba Slaa is just a man na ana matatizo yetu yale yale ya kila siku, na ana matatizo ya integrity kama uongozi wetu wa sasa.

Nasubiria sana kuona pale ambapo Slaa kavunja sheria za nchi ndipo nione ukweli kwenye sentensi hii.
Wewe ni mtu ambaye umepondea kila ambacho chadema wamefanya hapa kabla hii stori yenu ya udaku haijatoka. Hushangazi kwa mtizamo huu.

Kwa hiyo hata kama mnaenda kumchagua Slaa, mumchague huku mnajua hili.Kwamba msitegemee muujiza, na mambo yanaweza kabisa kuwa mabaya zaidi ya CCM.

I am not a CCM fan, but I am just asking myself, kama mtu ana guts za kupiga campaign ya urais huku amemuweka kinyumba mke wa mtu, je akipata urais atakuwa na guts za kufanya nini ?

Wewe ni big fan wa ccm. Unaipigia ccm kampeni kwa default. Unaua chadema ili ccm wakose upinzani na kubaki madarakani kama kagame wa rwanda.

tatizo kwako ni kuwa, wengi hapa tulishakushtukia na tutakushikia bango mpaka utoe kikadi chako cha kijani ulichokificha kwenye begi lako.
 
Kiranga,

katika yote nitaomba hili hapa ulijibu, kama sheria haisemi kuwa kitu fulani ni makosa, ni nini tena kinatambulisha/kupima kosa?

Uongo mwingine hapa, Slaa hajamtambulisha huyu mama kama mke wake.

Utarudia hili mara mia lakini bado ni uzandiki tu.

Hata hizo A, B, C bado hazijaweka kwenye katiba kwa hiyo hakuna cha substitution hapo.

Yes unaweza.....kuhusu ndoa hiyo ni case nyingine lakini uchumba hiyo inaruhusiwa kabisa. Uchumba hauwi bound na sheria za nchi lakini ndoa iko.

All along, hiki ndicho unachotaka kufanya hapa, kumlinganisha Slaa na Kikwete.
Utetezi wako wa kifisadi unakufanya ulinganisha mtu aliyeuza Buzwagi kwa bei ya karanga na mtu aliyechumbia mwanamke aliyeachika.

Trust me, kwa mwendo huu Slaa hana tofauti na Kikwete.Labda uniambie tofauti yao ni kwamba Slaa hajapata madaraka tu.

Tena Slaa anaonekana ana uchu na pupa kumpita hata Kikwete.
 
Naona umeongeza neno maadili baada ya kuona swali langu kuhusu sheria za ndoa.
Narudia swali langu kwako, sheria ya ndoa inayombana Dr Slaa hapa ni ipi?

Nadhani bongo kuna sheria inayofanana na "alienaton of affection". Kuna siku WoS nilimwuliza akasema ipo sheria kama hiyo. Nimeisahau inaitwaje. Lakini sidhani hata hiyo sheria inambana Slaa kwa sababu inavyosemekana huyo Josephine alikuwa keshamtosa huyo "mume" wake....
 
hapo ndipo nasema huyu jamaa angemshtaki Josephine halafu tungeona yaliyofichika. Huyu jamaa anajua fika kwamba Kumshtaki Josephine haiwezekani kwa sababu target yao ni Dr. Slaa ili kuonyesha bibie ni victim of circumstance.. alihadaika na Dr - unakumbuka jamaa kasema mwanamke alisema anaondoka ktk kibanda chake anakwenda kuishi ktk nyumba!!?.. hii yote picha imechorwa tayari.... isitokee tu huyu bibie naye akubali kwamba Dr. Slaa alimhadaa hadi kufikia kufanya maamuzi kinyume cha ndoa yake. hapo mkuu wangu itakuwa kibano - dr chupi itambana.

Of course Dr. Slaa ni target.

My fear ni kwamba Dr. Slaa anakuwa such an easy target. Au alivyokuwa mtawa wanawake walikuwa adimu sana kiasi kwamba anashindwa kutumia busara na kuona midege ya jeshi i wapi na wanawake wa maan wako wapi ?

"Head of state" Slaa anaweza kwenda Davos akasakiziwa ki bodyguard cha Gaddaffi akatoa state secrets zote.
 
Kwani Kikwete kishasakiziwa nyamafu na kuliingiza mkenge Taifa mara ngapi? Usijifanye hujui mikenge ambayo Taifa limeingia kupitia kwa Kikwete.

Unachanganya mambo, ya Kikwete tunayafahamu...you can't justify something just because so and so did this and that...Hapa ni issue ya maadili na sheria za ndoa..Forget that it was Slaa that found himself in this...what do think of this act? what do you know about marriage law of the country? do we have common-law, de factor marriage in Tanzania ? Ingekua vizuri tusikie kutoka kwa wataalamu wa sheria
 
Trust me, kwa mwendo huu Slaa hana tofauti na Kikwete.Labda uniambie tofauti yao ni kwamba Slaa hajapata madaraka tu.

Tena Slaa anaonekana ana uchu na pupa kumpita hata Kikwete.

See, what i have been saying all along.
You are very okay with Kikwete --- ccm supporter at best
 
Nadhani bongo kuna sheria inayofanana na "alienaton of affection". Kuna siku WoS nilimwuliza akasema ipo sheria kama hiyo. Nimeisahau inaitwaje. Lakini sidhani hata hiyo sheria inambana Slaa kwa sababu inavyosemekana huyo Josephine alikuwa keshamtosa huyo "mume" wake....

Kumtosa mume mimi ninakokujua ni talaka, ama sivyo every "girls night out" itakuwa "kumtosa mume" na kumchukua mke aliyeenda "girls night out" itakuwa poa tu.
 
Unachanganya mambo, ya Kikwete tunayafahamu...you can't justify something just because so and so did this and that...Hapa ni issue ya maadili na sheria za ndoa..Forget that it was Slaa that found himself in this...what do think of this act? what do you know about marriage law of the country? do we have common-law, de factor marriage in Tanzania ? Ingekua vizuri tusikie kutoka kwa wataalamu wa sheria

unapinga wenzako kuwa wanajichanganya na kisha unakuja na maswali kibao ambayo unataka majibu toka kwa wataalamu wa sheria. Kwa nini usipate majibu ya maswali hayo kabla ya kuja kuonesha utupu wako hapa?
 
See, what i have been saying all along.
You are very okay with Kikwete --- ccm supporter at best

Mimi si support Kiwete au Siraha, wote ni miyeyusho tu kwangu. Especially kwa sababu Siraha kashapewa nafasi na kajionyesha kumbe mtu wa kujali bupe kuliko public service.

Ataweza kazi kweli huyu? Whats the point of taking the change of doing a whole regime change only to replace one fisadi with another ?
 
Of course Dr. Slaa ni target.

My fear ni kwamba Dr. Slaa anakuwa such an easy target. Au alivyokuwa mtawa wanawake walikuwa adimu sana kiasi kwamba anashindwa kutumia busara na kuona midege ya jeshi i wapi na wanawake wa maan wako wapi ?

"Head of state" Slaa anaweza kwenda Davos akasakiziwa ki bodyguard cha Gaddaffi akatoa state secrets zote.

Tayari kishaanza smear. Slaa kachumbia mwanamke aliyeachana na mmewe. Smear manager wetu keshaenda step zaidi.

Bado nafuatilia kujua unafaidika vipi na system ya kifisadi ya ccm.
 
Mimi si support Kiwete au Siraha, wote ni miyeyusho tu kwangu. Especially kwa sababu Siraha kashapewa nafasi na kajionyesha kumbe mtu wa kujali bupe kuliko public service.

Ataweza kazi kweli huyu? Whats the point of taking the change of doing a whole regime change only to replace one fisadi with another ?

Wewe ni supporter wa ccm (mpondeaji mkuu wa chadema).
Eti anamlinganisha mtu aliyeleta EPA, Buzwagi, richmond, etc na mtu aliyemchumbia mwanamke aliyeseparate toka kwa mme wake
 
Kumtosa mume mimi ninakokujua ni talaka, ama sivyo every "girls night out" itakuwa "kumtosa mume" na kumchukua mke aliyeenda "girls night out" itakuwa poa tu.

Vipi spousal abandonment (desertion)? Huko sio kumtosa mwenzi wako?
 
Kumtosa mume mimi ninakokujua ni talaka, ama sivyo every "girls night out" itakuwa "kumtosa mume" na kumchukua mke aliyeenda "girls night out" itakuwa poa tu.
Mkuu wangu ni miezi saba imepita jamaa hajui mke na watoto wako wapi..

Je unajua Dr.Slaa kachukua lini mali hiyo au unakisia tu kwa sababu leo hii ni mgombea kiti cha Urais. na Dr.Slaa anaweza kula vitu pasipo kumhusisha mwanamke ni hulka ya watu wa kaskazini kutomhusisha mwanamke na kazi za mume. Pili, Dr.Slaa siku zote amepiga vita vitu hivi hadi bungeni toka kina Mwinyi hadi Mkapa kuhusisha wake zao na majukumu yao serikali. Hivyo inaonyesha wazi mke wake atakuwa na kazi zake nje na atapewa sifa zake kwa kazi zake.
 
Kumtosa mume mimi ninakokujua ni talaka, ama sivyo every "girls night out" itakuwa "kumtosa mume" na kumchukua mke aliyeenda "girls night out" itakuwa poa tu.

Swali kwako Kiranga,

Kwanini umeongopa hapa kuwa Dr Slaa hajaongelea hizi habari?
 
Naona umeongeza neno maadili baada ya kuona swali langu kuhusu sheria za ndoa.
Narudia swali langu kwako, sheria ya ndoa inayombana Dr Slaa hapa ni ipi?

Tatizo unakuwa defensive, hapa ndio maana nikasema ni swala la sheria za ndoa, kwa kifupi waliopeleka mashitaka wamedai kuwa kisheria yule bado ni mke wa mtu..sasa hii bado ni kesi, kwa hiyo tunategemea naye Slaa atakuja na hoja zake mahakamani kujibu. Slaa anakesi ya kujibu mahakamani kama wewe hulioni hilo...
 
Ha aha ha defensive my foot!

Mimi nimekuuliza maoni yako na bado nasubiria jibu lako.
Swali la nyongeza kwako, Slaa ameshitakiwa kwa kosa gani?

Slaa ametishiwa mara nyingi sana kushitakiwa na hiyo haikumfanya mvunja sheria.
Kuwa na kesi ya kujibu hakumfanyi yeye mkosaji. Kesi za madai za ajabu na kipuuzi (frivolous lawsuits) zinafika mahakamani mara nyingi sana.
 
Labda hii kidogo itafungua mjadala mwingine, tujadili maadili na sheria za ndoa if it is too sensitive Slaa akitajwa
Source:Makala -Ukomo wa ndoa na aina zake katika sheria za Tanzania

Ukomo wa ndoa na aina zake katika sheria za Tanzania

Lusungu Hemed

Leo hii tuendelee kutazama ukomo wa ndoa na aina za ndoa kwa sheria za Tanzania. Kwanza kabisa, nianze kwa kusema kuwa muungano wa kindoa kati ya mwanamume na mwanamke lazima uwe na kusudio la kudumu maishani.

Tunaposema kwamba muungano wa mwanamke na mwanamume lazima ukusudiwe kuwa wa kudumu kwa muda wa maisha yao, nina maana ya kawaida kabisa ambayo ni kusudio la kutotengana au kuachana.

Sheria inatahadharisha uwezekano wa kuwa na muungano wa muda mfupi tu wa wanandoa. Sehemu fulani za jamii na dunia miongoni mwa jamii ya ‘Khoja Shia Ithna – Asheri' wanatambua kitu kinachoitwa ‘mutaa' au ndoa ya muda fulani unaopangwa.

Sheria ya Tanzania haitambui ndoa ya muda mfupi ambayo inatamkwa rasmi wakati wa kufunga ndoa hiyo. Sheria hiyo ya Ndoa ya mwaka 1971 inasema kwamba ndoa itadumu hadi pale litakapotokea tukio fulani linaloweza kuivunja.

Kufa kwa mume au mke ni mfano mmoja wapo wa tukio ambalo linakomesha kuwepo kwa ndoa. Mume au mke anaweza pia kuyumkinika kuwa amekufa iwapo ametoweka bila kujulikana au kusikia aliko kwa muda mrefu, miaka saba au zaidi na mahakama ikatamka.

Vile vile ndoa itabaki kuwa hivyo mpaka mahakama itoe amri ya kuibatilisha au kwa kutoa amri ya talaka. Kwa mujibu wa Sheria ya Ndoa ya Tanzania kuna aina mbili za ndoa.

Aina hizo ni zile ndoa za mke mmoja au zinazokusudiwa ziwe za mke mmoja na ndoa mitala, yaani zile zinazoweza kuwa za wake wengi.

Zipo pia taratibu tatu za kujenga ndoa, yaani kimila, kidini na kiserikali. Ndoa ya mke mmoja ni muungano wa mwanamume mmoja na mwanamke mmoja tu bila mwingine yeyote.

Muungano ambao unamwezesha mume kuoa mke mwingine au wake wengine, wakati ndoa ya mwanzo ingalipo, huitwa ndoa ya mitala.

Hapa Tanzania ndoa inaweza kugeuzwa. Ndoa inaweza kugeuzwa kutoka kwenye ndoa ya mke mmoja na kuwa ndoa inayoweza kuwa ya mitala.

Vile vile ndoa inaweza kugeuzwa kutoka ndoa inayoweza kuwa ya mitala na kuwa ya mke mmoja. Lakini wakati mabadiliko hayo yanapofanyika itakuwa ni lazima kuzingatia mila, desturi na imani ya wahusika.

Ndoa inaweza kugeuzwa kwa tamko rasmi litakalotolewa na mume pamoja na mkewe kwamba kila mmoja wao kwa hiari yao wenyewe wamekubaliana juu ya mabadiliko hayo.

Pia kwa kuzingatia namna ilivyofungwa, yaani mila, desturi na imani ya wahusika. Tamko hilo lazima litolewe mbele ya jaji, hakimu mkazi au hakimu wa wilaya.

Ni lazima pia tamko hilo lithibitishwe kwa maandishi yatakayosainiwa na mume na mke. Tamko hilo pia itabidi lisainiwe na shahidi ambaye tamko hilo lilitolewa mbele yake.

Ndoa ya Wakristo wawili inayofungwa kanisani kwa mujibu wa dini yao, haiwezi kugeuzwa kutoka ndoa ya mke mmoja na kuwa ndoa ya mitala.

Ndoa hiyo itabaki kuwa ya mke mmoja kwa wakati wote wafunga ndoa hao wanapoendelea kuwa Wakristo. Masharti ya sheria inayoruhusu kugeuzwa ndoa hayahusishi ndoa yoyote ya Kikristo.

Hata kama ndoa ya Kikristo ilitanguliwa au kufuatiwa na ndoa iliyofungwa kiserikali au kwa namna yoyote nyingine, taratibu za kugeuza ndoa hazitaihusu ndoa hiyo.

Iwapo ndoa yake ingalipo, basi mwanamke haruhusiwi kufunga ndoa nyingine. Ni dhahiri kwamba mwanamke akifiwa na mumewe ataruhusiwa kufunga ndoa nyingine.

Kadhalika mwanamke ataruhusiwa kufunga ndoa nyingine baada ya amri ya kubatilisha ndoa yake ya awali au baada ya amri ya talaka.

Tukutane juma lijalo!
 
Mapmbano,
Hivi kweli nyie haiwaingii akilini kwamba kama kuna makosa yoyote yale yamefanywa ni mke ndiye anapaswa kushtakiwa ktk kesi ya madai. Dr.Slaa angeshtakiwa tu kama kaiba huyo mke pasipo hiari yake lakini inaonyesha wazi ni mke aliyekwenda kwa Dr.Slaa na anaishi kwa mapenzi yake mwenyewe tena baada ya kuachwa miezi sita. Ndoa hakuifunga Dr.Slaa na huyo mbabaishaji wala Slaa na huyo mwanamke hivyo unamshtaki kwa makosa yapi?
 
Mapmbano, Hivi kweli nyie haiwaingii akilini kwamba kama kuna makosa yoyote yale yamefanyawa na mke na ndiye anapaswa kushtakiwa ktk kesi ya madai. Dr.Slaa angeshtakiwa tu kama kaiba huyo mke lakini inaonyesha wazi ni mke aliyekwenda kwa Dr.Slaa na anaishi kwa mapenzi yake mwenyewe tena baada ya kuachwa miezi sita. Ndo hakuifunga Dr.Slaa na huyo mbabaishaji hivyo unamshtaki kwa makosa yapi?

Mke hagombei urais. Mimi namuangalia mgombea urais.

Mgombea urais aliyekaa kinyumba na mke wa mtu, akamtambulisha mkwe huyu wa mtu kama mke wake kwa watu.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom