Video: Si kuibiwa ni kuzidiwa!

Video: Si kuibiwa ni kuzidiwa!

Status
Not open for further replies.
Kikwete hana kesi mahakamani inayohusu yeye kumuingilia mtu katika ndoa yake. Mtu kachukua mke wa mtu mwingine na mwanamke katoka kusema, Slaa hajajibu maswali, na wewe bado unaita hii smear ?

Hebu acha hizoo weye! Nadhani unamkumbuka Monica Lewinsky na Bill Clinton. Jamaa pamoja na kufanya aliyoyafanya bado alishinda katika uchaguzi wa 1996. Mmeshindwa hoja sasa mnaleta viroja na chama chenu cha mafisadi.
 
Kiranga,
isiwe poa kivipi? maanake mke ni yule unayeishi naye sio maswala ya Mengi kumwacvha yule mama pale halafu wajomba wachangamkie aanze kudai ni mkewe hali yeye anapeta. Huyu jamaa nakuhakikishia ana mke au kinyumba pia. Kosa lake mwenyewe halioni isipokuwa la mkewe na kwa sababu Dr rais kachukua vitu jumla.
Na kichwa kama wewe nilitarajia kwamba utaunganisha 2+3 vizuri tu kumbe nawe unatupa hesabu za Kingwendu..

Amegundua kuwa hakuna kosa kisheria na sasa ameanza pumba kuwa hili sio jambo zuri kwake so kila mtanzania sasa inabidi aishi kwa standard za Kiranga (na sio katiba ya Tanzania).
 
Kikwete hana kesi mahakamani inayohusu yeye kumuingilia mtu katika ndoa yake. Mtu kachukua mke wa mtu mwingine na mwanamke katoka kusema, Slaa hajajibu maswali, na wewe bado unaita hii smear ?

iko mahakamani ajibu nn?
unajua ww uko onaongea emetional ndugu unasahau kuna sheria.
Mkandara kauliza una weza prove ulichosema " Slaa kakaa kinyumba na mke mtu" hujajibu ni bora ukawa una respond on issue kuliko ku react na kuwa emotional.
 
Hebu acha hizoo weye! Nadhani unamkumbuka Monica Lewinsky na Bill Clinton. Jamaa pamoja na kufanya aliyoyafanya bado alishinda katika uchaguzi wa 1996. Mmeshindwa hoja sasa mnaleta viroja na chama chenu cha mafisadi.

Ujengele,

Angalau hata Clinton alikuwa ana mke at the time, unaweza kuweka uzito kidogo hapo. Slaa sio kwamba amecheat on his wife, amekutana na mwanamke aliyeikimbia ndoa yake (asiye na uhusiano) na akaingia uhusiano naye (wa uchumba).

Kiranga anataka kuleta mambo ya fanatics wa kidini wanaopinga divorce.
 
Kwa hiyo unataka standard zako (kama kiranga) zitumike kuendesha nchi yetu.
Yaani kwa vile fanatics kama wewe mna matatizo na watu wanaofurahia maisha yao ya utu uzima basi kila mtu hilo liwe tatizo.

kiranga umeanza kuishiwa sasa.

Fanatics ni wale wanao suspend rules of engagement ikiwa zinamhusisha mgombea wao. Kwa mfano mgombea wao akituhumiwa kumuweka kinyumba mke wa mtu, bila kujibu tuhuma hizo, wanamtungia mashairi ya urijali na ushujaa kama amefanya jambo la kujivunia.

Fanatics ni wale wanaosema tuhuma za kumuweka mke wa mtu kinyumba ni "standard zako (kama Kiranga)" na hazifai kuendesha nchi yetu.

Mimi naona watu wasiofaa kuendesha nchi yetu ni wale wanaoweka mbele mahusiano ya kinyumba na wake za watu zaidi ya kazi zao za umma.

Slaa anajua kwamba kachemsha hapa, ndiyo maana haongei kuhusu hili.

Angekuwa Kikwete ndiye kachukua mke wa mtu na kuna accusations hizi mngekuwa mna scream bloody murder, mimi na scream bloody murder same way, whether it is Kikwete or Slaa. While some of you are just screaming on partisan basis.

That is the difference between me and you.
 
iko mahakamani ajibu nn?
unajua ww uko onaongea emetional ndugu unasahau kuna sheria.
Mkandara kauliza una weza prove ulichosema " Slaa kakaa kinyumba na mke mtu" hujajibu ni bora ukawa una respond on issue kuliko ku react na kuwa emotional.

Slaa kaongelea hii habari....na hajajificha nyuma ya pazia la kesi iko mahakamani. Yeye ndiye alifungua hizi habari kwa interview kuhusu mchumba wake. Kiranga anajua hili ila anaendeleza smear na uongo kama kawaida yake.
 
Fanatics ni wale wanao suspend rules of engagement ikiwa zinamhusisha mgombea wao. Kwa mfano mgombea wao akituhumiwa kumuweka kinyumba mke wa mtu, bila kujibu tuhuma hizo, wanamtungia mashairi ya urijali na ushuijaa kama amefanya jambo la kujivunia.

Kiranga,

Slaa hajatuhumiwa kumweka kinyumba mke wa mtu. Slaa anakubali kuwa ana uhusiano (wa uchumba) na huyu mama. Hakuna siri hapa.

Fanatics ni wale wanaosema tuhuma za kumuweka mke wa mtu kinyumba ni "standard zako (kama Kiranga)" na hazifai kuendesha nchi yetu.

Kwa standards zipi? hakuna sheria ya nchi iliyovujwa. Mimi nafuata katiba, wewe hufuati katiba, nani fanatic hapa?

Mimi naona watu wasiofaa kuendesha nchi yetu ni wale wanaoweka mbele mahusiano ya kinyumba na wake za watu zaidi ya kazi zao za umma.

Watu wasiofaa kuendesha nchi ni wanaccm wenzako waliofilisi nchi.

Slaa anajua kwamba kachemsha hapa, ndiyo maana haongei kuhusu hili.

Acha uongo kiranga, Slaa ameliongelea sana hili jambo. Amemtambulisha mchumba wake kwenye mikutano yake ya kampeni.

Umeishiwa hadi unaanza kuongopa?! bado unataka kwenda toe to toe na uongo wako huu?
 
Kiranga,
Mkuu wangu weee Dr.Slaa angekuwa hana la kujitetea asingemtoa mbele za watu na kuuafahamisha Umma pamoja na mhusika mwenyewe kujua. hata katika ustaarabu wetu mtu anapotaka kuona hutolewa wakati wa kupinga ndoa hiyo na hata ikitokea mtu akapinga ndoa na kuonyesha yule ni mke wa mtu au wake kwa ushahidi tosha ndipo ndoa huvunjika. Na mtu wa kulaumiwa na kupelekwa hata mbele ya sheria ni Mke aliyetaka kufunga ndoa akiwa bado ndani ya ndoa.. Think whatever U wonna put it, huyu jamaa hakuoana na Dr Slaa, labda angemshtaki mkewe ingeleta maana kidogo kwa sababu ndiye mwenye ushahidi tosha wa kupinga au kukataa ndoa iliyopo huko mahakamani. Kinyume cha hapo Dr Slaa aseme nini?
 
Kiranga,
Mkuu wangu weee Dr.Slaa angekuwa hana la kujitetea asingemtoa mbele za watu na kuuafahamisha Umma pamoja na mhusika mwenyewe kujua. hata katika ustaarabu wetu mtu anapotaka kuona hutolewa wakati wa kupinga ndoa hiyo na hata ikitokea mtu akapinga ndoa na kuonyesha yule ni mke wa mtu kwa ushahidi tosha mtu wa kulaumiwa na kupelekwa hata mbele ya shjeria ni Mke aliyetaka kufunga ndoa akiwa bado ndani ya ndoa.. Think whatever U wonna put it huyu jamaa hakuoana na Dr Slaa, labda angemshtaki mkewe ingeleta maana kidogo kwa sababu ndiye mwenye ushahidi tosha wa kupinga au kukataa ndoa iliyopo.

Exactly,

Kiranga anataka kuendeleza uongo wa ccm kuwa Slaa analikwepa hili jambo.
Slaa ndiye alimtambulisha huyu mama kwenye kampeni zake. Slaa alitoa interview kuhusu huyu mama.

Slaa hajaficha chochote kuhusu uhusiano wake na huyu mama. Kiranga anacholeta hapa ni uongo na uzandiki tu wa kutaka kutumia mitizamo badala ya sheria za nchi kuendesha nchi yetu.
 
Fanatics ni wale wanao suspend rules of engagement ikiwa zinamhusisha mgombea wao. Kwa mfano mgombea wao akituhumiwa kumuweka kinyumba mke wa mtu, bila kujibu tuhuma hizo, wanamtungia mashairi ya urijali na ushujaa kama amefanya jambo la kujivunia.

Fanatics ni wale wanaosema tuhuma za kumuweka mke wa mtu kinyumba ni "standard zako (kama Kiranga)" na hazifai kuendesha nchi yetu.

Mimi naona watu wasiofaa kuendesha nchi yetu ni wale wanaoweka mbele mahusiano ya kinyumba na wake za watu zaidi ya kazi zao za umma.

Slaa anajua kwamba kachemsha hapa, ndiyo maana haongei kuhusu hili.

Angekuwa Kikwete ndiye kachukua mke wa mtu na kuna accusations hizi mngekuwa mna scream bloody murder, mimi na scream bloody murder same way, whether it is Kikwete or Slaa. While some of you are just screaming on partisan basis.

That is the difference between me and you
.

You think you're so much smarter than everybody else, don't you? We've seen many of your type before. Unapenda sana kuwa centre of attention by going against the grain in almost everything just for the heck of it. Always bringing attention to your self and shit...your conceited mindset deludes you into believing you can counter-argue everyone in here on whatever issue under the sun.
 
Kiranga hakuna spin hapa,

Kosa la Slaa kikatiba ni lipi?
BTW - ameshtakiwa kwa kosa gani?

Kama tusipofuata katiba then hatuna understanding yoyote ya kuendesha huu mjadala (kivitabu kwa msemo wako). Unaweza tu kuleta kitabu kingine unachopenda na tukakitumia.

Kwa sasa swali kwako ni kuwa, Slaa kosa lake ni lipi?

Katiba ni sheria mama, just because haijaandikwa kwamba huwezi kuuchana mkono wa mwezako vipande saba katika katiba, haimaanishi kufanya hivyo ni poa.

Katiba ina guarantee haki ya usalama kwa kila mtanzania, na kumuingilia mtu katika maisha ya ndoa ni kumvunjia usalama wa maisha yake kwa namna moja au nyingine, unaondoa amani ya maisha yake.

Si llazima katiba isema "mgombea Slaa huwezi kumchukua Josephine kutokakwa Mahimbo" ili ujue kwamba kufanya hivvyo ni vibaya.
 
Yah kama alivyosema Mkandara kwa nn jamaa asimshtaki mkewe?maana yeye ndiye mwenye knowledge ya ndoa yake
 
Kiranga,
isiwe poa kivipi? maanake mke ni yule unayeishi naye sio maswala ya Mengi kumwacha yule mama halafu wajomba wachangamkie aanze kudai ni mkewe hali yeye anapeta.

Huyu jamaa nakuhakikishia ana mke au kinyumba pia. Kosa lake mwenyewe halioni isipokuwa la mkewe na kwa sababu Dr rais mtarajiwa kachukua vitu jumla imekuwa nongwa.
Na kichwa kama wewe nilitarajia kwamba utaunganisha 2+3 vizuri tu kumbe nawe unatupa hesabu za Kingwendu..

Slaa sio smart kabisa.

Anaweza kusakiziwa nyamafu akaliingiza taifa mkenge. Unless he comes out with a better story, hapa anajionyesha kuwa sawa - if not even worse than- na Kikwete.
 
Slaa kajibu swali. Yeye ndiye alitoa interview kwenye media kuhusu mchumba wake. Alimleta mchumba wake kwenye kampeni zake na kumtambulisha.

Maswali yapi hayo unayotaka ayajibu?

Swali langu la msingi kwako, kosa la Slaa ni lipi?

Unaweza kumchumbia mtu ambaye kaolewa bado ?
 
Katiba ni sheria mama, just because haijaandikwa kwamba huwezi kuuchana mkono wa mwezako vipande saba katika katiba, haimaanishi kufanya hivyo ni poa.

Slaa hajachana mkono wa yeyote hapa

Katiba ina guarantee haki ya usalama kwa kila mtanzania, na kumuingilia mtu katika maisha ya ndoa ni kumvunjia usalama wa maisha yake kwa namna moja au nyingine, unaondoa amani ya maisha yake.

Utavuta hili hadi kesho lakini bado unachofanya hapa ni uzandiki. Unataka kuleta morals zako ziwe standard ya kila mtu. Slaa hajavunja sheria yoyote ya nchi na ili unalijua vizuri.

Si llazima katiba isema "mgombea Slaa huwezi kumchukua Josephine kutokakwa Mahimbo" ili ujue kwamba kufanya hivvyo ni vibaya.

No katiba haitasema chochote specific kuhusu slaa, katiba itasema kuwa ni makosa kwa mwanamume A kuwa na uhusiano na mwanamke B (ambaye inasemekana kuwa aliachana na mwanamme C miaka kibao iliyopita).

Uongo mwingine unaotaka kuuleta hapa - Slaa hajachukua mwanamke toka kwa mwanamme mwingine, Slaa kaanzisha uhusiano (wa uchumba) na mwanamke aliyeachana na mme wake.
 
MGOMBEA urais kwa tiketi ya CHADEMA, Dk. Willbrod Slaa , amefunguliwa kesi katika Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaami, akidaiwa fidia y ash. bilioni moja kwa madai ya kunyang’anya mke wa mtu.

Kesi hiyo namba 122 ya mwaka 2010, ilifunguliwa leo mahakamani hapo na Aminiel Mahimbo kwa kupitia ofisi ya mawakili ya Amicus.

Mahimbo anadai kuwa, Dk. Slaa kamnyang’anya mkewe wa ndoa Josephine Mushumbusi.

Kwa kupitia nakala ya hati ya madai, Mahimbo anadai fidia ya sh. milioni 200 kutokana na hasara alizozipata baada ya mdaiwa huyo, kumtangaza mkewe wa ndoa Josephine kuwa mchumba wake na sh. milioni 800 ikiwa ni hasara ya jumla aliyopata.

Mlalamikaji huyo, anadai Septemba 7, 2002 alifunga ndoa na mwanamke huyo katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Ushirika wa Kijitonyama na kuishi maeneo mbalimbali ikiwemo Kimara, Baruti, Dar es Salaam.

Pia anadai katika maisha yao ya ndoa wamebahatika kuwa na watoto wawili ambao ni Upendo aliyezaliwa Mei Mosi, 2003 na Precious aliyezaliwa Machi 14, 2007.

Mahimbo alidai, ndoa kati yake na Josephine haijavunjwa na chombo chochote na kwamba, bado ni mke wake halali.

Kwa mujibu wa hati hiyo, Mahimbo alidai hivi karibuni, mkewe alikuwa na safari za mara kwa mara na aliamini ni za kikazi. Josephine ni mfanyabiashara ambaye anaendesha kampuni iitwayo Green World Clinic.

Alidai katika tarehe na mahali tofauti, Dk. Slaa alimtambulisha mwanamke huyo kuwa ni mkewe, suala ambalo si kweli.

Mlalamikaji huyo alidai, uhusiano uliopo kati ya watu hao wawili umemfanya adhalilike na kunyanyasika katika jamii na anaiomba mahakama kumzuia Dk. Slaa kuendelea kujihusisha kimahusiano na mkewe.

Anaiomba mahakama kumwamuru Dk. Slaa kumlipa bilioni moja na kulipa gharama za kuendeshea kesi.

Mahimbo amedai ameambatanisha na cheti cha ndoa na Josephine, picha za harusi, vyeti vya kuzaliwa vya watoto na nakala za vipande vya magazeti zilizopigwa wakati Dk. Slaa akimtambulisha mwanamke huyo kuwa ni mkewe.

Source: Michuzi

Hizi ni njama za ccm kumuwekea visiki Dr. Slaa asiendelee vizuri na kampeni za uraisi. Watanzania tufungue macho, tuone hila za CCM kung'ang'ania kutawala ili kuendeleza ufisadi na utawala mbovu. Watanzania wazalendo wote tuwe pamoja na Dr. Slaa wakati huu kumuunga mkono, na kulaani njama za CCM.

Kwa pamoja, hakika tutashinda kwa vile juhudi zetu ni za haki mbele ya Mwenyesi Mungu na wanadamu. Juhudi za CCM zimejaa uovu uliokithiri, na hakika watashindwa.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom