Kiranga sidhani kuna anayetetea infidelity hapa.
Inanisumbua sana kuona Mkatoliki anayeelwa "The Sacred Permanence of Matrimony" anatetea common infidelity.
Taratibu ndugu, Mwanakijiji anatetea infidelity kwa mbwembwe zote. Anasema infidelity si kuibiwa ni kuzidiwa.Kwa maneno mengine wanaume wafanye mashindano ya kuiba wake wa wenzao, wakiiba wake wengi watakuwa "wamezidi" na hilo ni jambo la fahari. Mwanakijiji kaleta ushabiki na kumtetea Slaa katika jambo la aibu kwa sababu ni Slaa tu. Slaa huyu aliyejua nini maana ya utawa, leo kawa si tu mtu aliyekuja kuoa na kuvunja utawa, bali kaja kuwa nyang'au anayenyemelea na kukwapua wake za watu na kuharibu ndoa za watu.
Kama anafanya hivi kabla ya kuwa rais akiwa rais si ndio itakuwa balaa ?
Namshukuru sana MMJ maana hainiingii akilini mwenzio amekuaga, amekukimbia kwa zaidi ya miezi sita na hujafuatilia hata mara moja, leo unaibuka na madai umenyanganywa mke.
Inawezekana kabisa kwamba kuna mambo ya siasa yameingizwa hapa. Lakini ninachojali mimi ni kwamba, Slaa kachukua mke wa mtu au hajachukua ?
Unaweza kuibiwa kitu na mtu wa kawaida kabisa, ukawa hata hujali kwamba umeibiwa kitu ingawa mwizi wako unamjua. Baada ya miezi sita, mwizi wako kaja kushinda bahati nasibu ya mamilioni. Wanasheria wakakushawishi kwamba mwizi wako ana mihela, twende kuanzisha kesi ya kumdai kitu chako. Je, ukweli kwamba umeanza kutaka kurejeshewa chako baada ya miezi sita, au umeanza kutaka kurejeshewa chako baada ya mwizi wako kupata hela za bahati nasibu, au kwamba umetaka kurejeshew chako baada ya kushawishiwa na wanasheria, mambo haya yanapunguza haki yako ya kudai chako ? Kwangu mimi hayapunguzi kabisa.
Kwa desturi zetu za kiafrika, kama amekutoroka, unakwenda kwao kutoa taarifa, na aghalabu unarudishiwa mahari.
Afrika ina desturi nyingi sana, desturi hizi za Afrika wapi? Tanzania pekee tuna makabila 120, desturi hizi ziko kwa watanzania wote? Sheria ya nchi inasemaje? Mimi sijali sana nini kitatokea baada ya hapa, ninachojali zaidi ni kwamba huyu Slaa si mtu wa Slaa, ni muhuni tu, ni mtu anayekwenda na kutembea na kina mama wenye ndoa zao. Kama ameshindwa kujiheshimu kwa hili ataweza kuheshimu madaraka ya umma? Au ndio akiwa rais atakuwa anafanya magwaride kama ya Mfalme Mswati na kuchagua kinamama atakavyo, hata kama wameolewa ? Aogope nini na mfano kashaanza kuonyuesha hata kabla ya urais?
Pili, naona hao waliochonga ngoma hii wameharakisha mno kama walivyokwisha sema wengine hapa, Mh ametoa taarifa tu kuwa yeye ni Mchumba wake; hawajaoona bado.
Wewe unafahamu mchumba ni nini? Je huyu mama ametalikiwa na mumewe? Kama ahajatalikiwa utawezaje kumchumbia mtu ambaye yupo katika ndoa ?
Mh Slaa ni mvunjandoa ?
Shida ya Slaa ni kusema mno! Na hata huyo Josephine! Ingetosha kubaki pale kwamba wao ni wachumba,
Wachumba kwa minajili gani wakati huyu mwanamke anadaiwa ameolewa na hajatalikiwa bado? Ukiwa na mahusiano ya kinyumba na mwanamke aliye katika ndoa, ambaye bado hajatalikiwa, hii ni infidelity. Kuna madhehebu mengine kama hao wakatoliki hawaamini hata katika divorce, unless imepitwa machoni kwa baba mtakatifu. Sasa Dr. Slaa ni mtu wa dini gani? Kama bado Mkatoliki, na anataka kumuoa huyu mama atapeleka swla kwa baba mtakatifu ili talaka ipate kubarikiwa? Kama sivyo anaweza kutengwa na kanisa katoliki kwa kuoa mke wa mtu. Maana kanisa katoliki haliamini katika talaka, na talaka pekee inayoeleweka ni ile inayopata baraka za baba mtakatifu. Angalia
"The Permanence of Matrimony"
lakini kusema kwamba wameishi tena kinyumba sasa hii wapi na wapi, bwana. Si sahihi na siwezi nikaacha kulikemea hili. Lakini nisipoambiwa kama nilivyoambiwa nitabaki nasema lakini washenzi hawa wameshaonjana, lakini sitaenda mbali, maana kwa namna fulani ni kama jamii yetu ya sasa imeshakubali kama desturi kwamba huwezi ukawa na mchumba bila ya kumfanya hawara(concubine). Hii ni bahati mbaya sana.
Kwa hiyo unataka mtu kama Slaa ndiye aje kuhalalisha habari hizi ? Slaa ni Mkatoliki na anajua haya mambo kwa sababu yeye alishakuwa mtawa.Hofu yangu ni kwamba Slaa ana unafiki wa kutaka kujidai ni Mkatoliki, huku wakati huo huo ni mvunja nyumba. Kama Slaa anaweza kuwa mnafiki katika hili kuna mengine mangapi anaweza kuwa mnafiki?
Kila siku tunamsema Kikwete kwa ufisadi na unafiki, tunataka kumtoa mnafiki mmoja na kumuingiza mnafiki mwingine ?
Mimi nadhani twendelee na kile tulichotaka kufanya, uchaguzi, haya ni mambo yameletwa kututoa kwenye mstari na wamefanikiwa kweli!!!! na inauma
Kwa hiyo Mwanakijiji ndiye anayetaka kututoa katika mstari? Aliyeleta hii mada hapa ni Mwanakijiji.