Video: Mwanafunzi mwingine akipigwa na Waalimu

Video: Mwanafunzi mwingine akipigwa na Waalimu

Napata feeling huenda hii ni misheni imepangwa ili kuihabarisha serikali kwamba walimu wameamua kuharibu kazi.
Haya matukio mbona kama yanarekodiwa na waalimu wenyewe?
Jamaa amesema hajaribiwi,kuwatimueni wote nchi nzima hashindwi yule,ohoo,shauri yenu!
 
Mishahara pia....inachangia

Yaani kabisa mkuu una support hii insanity eti sababu ni mishahara midogo? mbona kuna wafanyakazi wa kada zingine wanapokea mishahara midogo kuliko walimu lakini hawafanyi brutality kwa ma co worker au watu wengine? Hapana hii haiwezi kuwa justification kuyafanya haya tunayoyashuhudia,hii ni kukosa busara za kiutu na kutambua wajibu wake wa kazi na kujisahau kwamba wao au yeye ni mtu anayepaswa kuinyoosha jamii katika njia iliyonyooka kupitia taaluma aliyosomea,tusipende kurahisisha mambo kwa sababu dhaifu ya mishahara eti ndio sababu, la !hasha tupinge hii kitu kabisa, Japo na sisi jamii tusiwahukumu walimu kwa hasira kutokana na haya tunayoyashuhudia sasa ikafikia tukawa demonise walimu wote.
 
Hawa walimu watatuulia watoto aisee jamani walimu wanakula bangi ndiyo waingie kazini au nini maana yake.. Naona hawatoi onyo ila wanataka kuuwa sio kwa kupiga kwa style hizi za mwendo kasi..[emoji35]
 
Eeee au kuna kitu serikali inataka kukifanya kwa walimu wanatafuta uchochoro wa kupitia ,mbona mwanzo hizi video hazikuwepo ?
 
Hivi ndio tumefikia huku kweli jamani!!
Mwili unanitetemeka kwa hasira,

Khaaaah!!!!
 
Huyu mtoto anashida huenda hajala, anamatatizo lukuki unaanzaje kumpiga. Kama ni jeuri kwanini usikae na wazazi wake.
 
Ni kweli mkuu,yan huyo mwl kapiga bakora mpk kichwani!so sad,hlf mwanafunzi akuwa akionyesha ukaidi wwt ule!
Yaani nimejikuta mnyonge aisee, angalia hata hali ya yule mtoto mpole, lkn jamaa anaanzaje kumpiga hata kichwani!!?
 
Huu ni mwaka wa wanafunzi. Waliitwa viraza, sasa wanapigwa kama Majambazi Mungu wanusuru wanafunzi wa Tanzania.
 
Back
Top Bottom